Kimataifa

Kenya yakataa urundikaji taka kutoka Uingereza

Halmashauri ya Mazingira Kenya NEMA imeamuru taka zilizokuwa zimepangwa kurundikwa nchini humo kurejeshwa Uingereza zilikotoka.

Hii ni baada ya wakaguzi wa halmashauri hiyo kugundua kashfa katika bandari ya Mombasa kuhusu uingizwaji wa kontena ya futi 40 iliyokuwa imesheheni taka kutoka Uingereza. Mkurugenzi wa NEMA Geoffrey Wahungu amesema waagizaji taka hizo zinazojumuisha mabaki ya vifaa vya tiba, elektroniki na plastiki wametakiwa kurejesha shehena hiyo Uingereza kwani uingizaji wake Kenya ni kinyume cha sheria. Halmashauri ya Mazingira Kenya imesema imeimarisha ukaguzi katika bandari ya Mombasa ili kuzuia nchi nchi hiyo kugeuzwa kuwa jalala la taka.

Hivi karibuni Zambia ilisitisha uagizaji wa nyama ya ng’ombe kutoka Uingereza baada ya kubainika ina kemikali inayosababisha ugonjwa hatari wa saratani.

Katika miaka ya hivi karibuni nchi za Ulaya zimelaumiwa kuwa zinazitumia nchi za Afrika kama jalala la bidhaa ambazo zimepigwa marufuku barani humo.

Share: