Kimataifa

Njama za Wamagharibi ya kuzidhibiti nchi za Kiislamu

Arthur C. Olivier ‘Art’ Meya wa zamani wa mji wa Bellflower nchini Marekani amesema kuwa, mpango wa kuleta chuki dhidi ya Uislamu unafanywa kwa minajili ya kurahisisha udhibiti wa nchi za Kiislamu. Olivier amesema kuwa, mlipuko uliotokea kwenye Kituo cha Kimataifa cha Biashara nchini Marekani na hata milipuko ya mabomu ya hivi karibuni huko Boston, ni matukio yaliyopangwa kwa makusudi kwa lengo la kuzidisha chuki dhidi ya Uislamu, njama ambayo ilipangwa kwa shabaha ya kurahisisha zaidi udhibiti wa utajiri na maliasili za nchi za Kiislamu

Meya wa zamani wa mji wa Bellflower ameongeza kuwa, mlipuko wa Boston ulikuwa ni mkakati uliopangwa, kwani wakati wa kufanyika mbio hizo za marathon, Gadi ya Taifa ilikuwa ikifanya doria kwenye barabara zilizokuwa zikitumiwa kwenye mbio hizo.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/31849-njama-za-wamagharibi-ya-kuzidhibiti-nchi-za-kiislamu

Share: