Habari

Hali ni mbaya Zanzibar.

Na B.OLE,
Wale Wazanzibar ambao mko nje hivi sasa, hali ya hapa Zanzibar imekuwa mbaya kwani vurugu zimetawala, bado mapambano kati ya vikosi vya Serikali na Wananchi zinazidi kuchukua sura mpya. Tayari vurugu hizi ambazo zilikuwa zimetanda maeneo ya Mjini, hivi sasa zimezidi kuenea maeneo ya nje ya mji.

Akina Mama nao pia hawako nyuma katika mapambano hayo, moshi na risasi zinasikika kila kona mchana huu, huku maduka yakiwa yamefungwa na baadhi ya watu wakiwa wanakimbia huku na kule, kuhofia usalama wao.

Pia kuna tetesi kwamba baadhi ya meli zenye askari kutoka Tanganyika huenda zikawasili wakati wowote kutoka sasa, ili kuja kutuliza hali ya usalama Zanzibar. Kwa kweli wamesikika baadhi ya watu wakisema lazima kiongozi wao atolewe ndani, kinyume chake Zanzibar patakuwa hapatoshi.

Share: