HabariUjumbe maalum

Hali ya kifedha ndani ya mtandao wa MZALENDO

Asalaam – aleyukum,

Kwa haraka mno ningependa kwanza kueka data zote (account details) za mtandao wetu ili kila mmoja ajue tuko kwenye hatua gani.

Jumla ya fedha zote zilipo wakati wa kuandika:

Jumla : $293.42 USD

Maelekezo zaidi kwa wale waliokuwa hawakuliona hili, kipindi kidogo kilichopita kulikuwa na michango ya familia za masheik wa UAMSHO.Michango iliotolewa kwa kupitia account ya mtandao huu ilikuwa na ujumla wa fedha taslim:
Kiasi ~ $35 USD

Gharama za hosting zinazotukabili:

Dynamic VPS – server.mzalendo.net (12/02/2016 – 12/01/2017) $407.88 USD
Operating System: Gentoo 2011
Disk Space: 20 GB
CPU: 1 Core
Memory: 2 GB
cPanel License: None
Turbo Boost: None
——————————————————
Sub Total: $407.88 USD
21.00% VAT: $85.65 USD
Credit: $0.00 USD
Total: $493.53 USD

P:S
Tutajaribu kufuatilia zaidi juu ya hizo tarehe, inanichanganya hata mie sijuwi kama deadline ni december au februari nikisoma hii 12/02/2016.

Tungeomba ushauri juu ya masuala muhimu yakiwamo:

1)MZALENDO.NET bado ina umuhimu katika jamii ya kizanzibari au tumefikia hatua nzuri nyumbani kwenye suala zima la kupashana habari kiasi ya kwamba tunaweza kutegemea vyanzo vyengine vya habari kama magazeti, radio na tv.
2)Kuna michango ya UAMSHO ambayo ni kidogo mno kusema fedha hizo zifikishwe kwa wahusika.

Wasalaam,
UONGOZI WA MTANDAO WETU

Share: