Habari

HALI YA ZANZIBAR, KAMA NI UCHAGUZI …TUMUOMBE MUNGU TU.

Bado naona giza nene mbele. Demokrasia kwa hapa kwetu ina mipaka hasa katika uchaguzi wa Zanzibar.Yaliyofanyika wote mnayajuwa. Kumbe KATIBA na SHERIA zinatafsiriwa kwa matakwa ya WATAWALA. Tokea kadhia hii ya uchaguzi na maamuzi ya Jecha yafanyike Zanzibar inazidi kuwa na hali mbaya na bado giza linainyemelea zaidi.

Tukubaliane kuwa suala la uchaguzi Zanzibar tokea kuja kwa vyama vingi linakuwa tete na jibu ni moja kuwa Walioshika madaraka hawataki kuachia. Hili liko wazi. Leo sitaki kuelezea yaliyotokea naangaza hayo yajayo tu.

Jecha katangaza uchaguzi ndio. Yaani tumerejeshewa tufani wenyewe. Kwamba hatuna hiyari tukitaka CCM itatawala hata kama hatutaki. Naiona Chuki inakuja kwa kasi, Watu kubaguwana na kufukuzwa makazini, Uhasama na visasi.

Ikiwa uchaguzi umekamilika na walioshinda(wawakilishi, wabunge, madiwani na Uraisi wa Jamuhuiri)walishakabidhiwa vyeti lakini Jecha alithubutu kusema kaufuta na leo kutangaziwa uchaguzi mwengine basi hayo ni maangamizi na lazima waliotowa BARAKA HIZI wameshajikubalisha kwa lolote.Haiwezekani uthubutu huu unyamaziwe hivi na hadi kufikia kutangazwa tena tarehe haiwezekani kuna Baraka zote.

Ni mauaji tu, hakuna lengine, hebu jalia huo uchaguzi ufanyike itakuwaje wakati CCM imejiridhisha ilishindwa kwa kura zaidi ya 25,000 na lengo la uchaguzi huu ni kuwa iwe isiwe LAZIMA CCM ishinde itakuwaje?

Katika hali hio wazanzibari ndio wako mashakani. Hatuwezi kupona ila kwa kadari ya MOLA, tuombe Dua sana.

MSIMAMO WA CUF UTAAMUWA.
Ni dhahiri CUf ndio wameshikilia hali ya Zanzibar kwa sasa. Ama washiriki Uchaguzi CCM ijichukulie ushindi na wazanzibari wapone na umwagaji damu wa makusudi ulioandaliwa na watawala au igome na kudai haki zao na damu iendelee kumwaga zaidi. Nasikitika kwa hali hizi zote mbili kuwa sioni Nafuu ya WAZANZIBARI ni muumba pekee anajuwa hili.

Ikiwa CCM italazimisha uchaguzi na ushindi itakuwa dhiki tu vile vile kwa Wazanzibari na uhasama utarudi mwanzo, watataka kuwatia adabu wana mageuzi wote na kutaanza awamu mpya ya ubaguzi na ubabe, watu kufukuzwa kazi na kila aina ya uhasama.

Ikiwa CUF itagoma ni vile vile nguruwe kumuachia shamba la mihogo hapo ndio naona giza.

JUMUIYA YA KIMATAIFA.
Mimi ni mmoja ambao huwa siiamini jumuiya ya Kimataifa hasa linapokuja suala la Zanzibar ingawa sikati tamaaa najuwa wakiamuwa lao wanaweza. Hili la mara hii tulisikia wakisema wameshtushwa na kufutwa uchaguzi hatujasikia tena lolote mpaka muda huu Jecha keshatangaza tarehe bado kimya.

Wasomi hasa wa Bara wamekaa kimya mpaka tumewasikia Akina mzee Butiku, Salim na baadhi ya wanasiasa wachace LAKINI kuna SHAKA? Walikuwa wapi hawa mpaka Jecha kutangaza Uchaguzi? itawezekana hio inayoitwa HAKI YA WAZANZIBARI KUHESHIMIWA? wakati utaambiwa MAAMUZI YA TUME HAYAPINGWI? YAANI HATA HAKI YA WANANCHI HAINA MAANA ILIMRADI JECHA KAAMUWA SIO KWA KISINGIZIO CHA TUME? bado tumuombe MUNGU

MSIMAMO
Inakuwa ni vigumu kubashiri lakini uamuzi wowote utakaokuja uwe wa manufaa, kwa Mfano ikiwa utakuwa wa kushiriki uchaguzi uhakikishe malengo ya kuiondowa CCM kama Adui namba moja wa wazanzibari kwa sasa basi ufanikiwe iwe isiwe iwe ni lazima wangoke au ikiwa ni wa kususia na kudai haki ya Wazanzibari ya Oktoba, 2015 basi tuhakikishe huo mkakati utafanikiwa na kuondowa utawala huu wa kidikteta.

Tumuombe Mungu, kwa pamoja.

Mungu ibariki Zanzibar

Share: