Habari

HARAKATI YA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR YAKANUSHA TAARIFA YA KIFO CHA SHEIKH MSELLEM ALI

ZANZIBAR.

HARAKATI YA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR IMEKANUSHA TAARIFA ZAKUFARIKI DUNIA KWA AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISKAM ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH MSELLEM BIN ALI ZILIZOSAMBAZWA NA WATU WASIOJUILIKANA HAPA NCHINI.

AKIZUNGUMZIA UVUMI HUO MLEZI WA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR AMIRI HAJJI KHAMIS HAJI AMEWATAKA WAISLAM KUONDOA KHOFU WALIYONAYO BAADA YAKUPOKEA TAARIFA HIYO.

AMIRI HUYO AMEONGEZA KUWA SHEIKH MSELLEM BADO YUKO HAI AKIWA NA HALI YA AFYA NJEMA PAMOJA NA VIONGOZI WENZAKE WALIOKO KIZUIZINI KATIKA RUMANDE YA SEGEREA MJINI DAR-ES-SALAAM KUFUATIA TUHUMA ZA UGAIDI NAKUHATARISHA AMANI YA NCHI ZINAZOWAKABILI .

HATA HIVYO AMIRI HAJJI AMEWASISITIZA WAISLAM KUENDELEA KUWA NA SUBRA SAMBAMBA NAKUWAOMBEA DUA MASHEIKH WA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR ILI KUPATA WEPESI WAKUACHILIWA HURU NAKUENDELEA NA HARAKATI ZAO ZAKUELIMISHA JAMII YAKIISLAM.

Share: