HabariMatangazo

Harambee ya Mzalendo – #Hosting

Assalamu alaykum,

Wanachama na wapenzi wa mzalendo.net, ningependa kuwafahamisha na kuwaomba mchango wa kuendesha forum yetu hii ya mzalendo.net.

Kama mnavyoo kuwa mzalendo.net haitegemei matangazo ya biashara kuendesha mtandao wetu mara zote michango yenu ya hali na mali ndio inayofanya mtandao huu kujiendesha. Na gharama za kuendesha ni $347.88 USD kwa mwaka, na tarehe ya mwisho ni 12/02/2014, waswahili husema nguo ya ijumaa hufuliwa alkhamis, hivyo kwa wale ambao watakaokuwa na uwezo wa kuchangia basi tunawaomba kufanya hivyo kupitia kwenye account yetu ya paypal.

Tunatanguliza shukran zet kwenu nyote.

Ahsanteni

Share: