HabariHabari-Picha

Harambee ya Salma Said

ASSALAMU ALAKUM

Kutokana na kuwa Salma Said Muandishi wa Habari tuliemzowea anaumwa: Nimeipokea hii taarifa kwa mwenzangu, ambayo imeandikwa na Bwana Hamza Rijaal. Inawezekana na wewe ukavutiwa na habari hii na kuchukua hatua zifaazo:

Suala la Bi Salmah linahitajia tafakuri ya kutosha ili kuweza kulitatua. Mwanaharakati Salmah tangu kumjua inakaribia miongo miwili tulianza kufahimiana pale kwenye NGO ya JAZ sio JAZZ ya kina Miles Davis na John Coltrane, JAZ ni Journalist Association of Zanzibar ikiongozwa na kina Ali bin Saleh, Ali Rashid, Mwitawi, Chunda na wengineo, kwa kiasi fulani kujiunga kwangu mie na JAZ kulinisaidia kwani nilikuwa nikiongoza Gazeti la Ki-Islamu ambalo tukilitoa kwa mwezi, likiitwa Maarifa, kukuweko kwangu huko nilijifunza mengi katika uandishi na Salmah kuwa naye pamoja.

Salmah ni binti wa aina yake na nimwenye juhudi kubwa ya kufanya kazi nilipokuwa , nafanya kazi naye kwenye gazeti fulani, ikiwa tulikuwa hatulipwi kwa kawaida tukilipwa pale tu panopatikana fedha za ziada. Siku mbili kabla ya kulitoa hilo gazeti tena la wiki ilikuwa tunaweza kukutana Saa 12 ya Jioni na kama tumetoka namapema basi 8 ya usiku, mara nyengine tukitoka Alfajiri ikiwa mie nakimbilia kazini, Salmah tupo naye kikazi bila ya kujali.

Salmah anamoyo wa kujitolea ambao wengi kwa waandishi na wasomi mambo leo hapa nyumbani ni kitu gharibu kukipata. Safari mmoja DW wanataka kunifanyia Interview juu ya GMO nikawaeleza kuwa hio sio line yangu, wasiliane na jamaa fulani, basi huyo jamaa la mwanzo aliloniuliza “Jee wanalipa hao?” nilipomjibu hawalipi akanambia hawezi kufanya mahojiano, DW wakafanya mahojiano na mie kwa kadri nilivyoweza, matokeo wakaja kunilipa baadaye. Salmah unapomualika kuja kuchukua habari hakuulizi kama kuna kulipana (mshiko) au laa, na kama akiwa hatoweza kufika atataka umsidie kumpatia taarifa ya huo mkutano, na hayo hubwagwa na sampuli ya watu tulivyo hivi sasa.

Salmah ana moyo wa kizalendo na anaipenda kazi yake. Katika kipindi cha miaka kama 3 hivi kama kumbukumbu zangu zipo sawa isiwe kama Kumbukumbu zilizohajiri Kitabu cha Gurnah (Memory of Departure) Salmah hali yake ya kiafya imekuwa inapanda na kushuka, na amelazwa hospitali na kutumia dawa katika nyakati mbalimbali. Kubwa kati ya yote ni kuwa ingawa yeye ni mgonjwa lakini wakati huo huo yeye anafanyisha HARAMBE za kusaidiwa wengine, la kujiuliza Jee na yeye hahitajii kufanyiwa Harambee?

Kunavipimo hivi ECG, City Scan, X-Ray vyote ni gharama na Salmah anatumia fedha zake nyingi kwa matibabu, ili aweze kupata hayo matibabu, Salmah nimjuae nakwambieni fika hata siku mmoja hatosema jamani nichangieni fedha kiasi kadhaa.

Wana ZIRP, ZANZINET, MZALENDO kama tutaweza kumchangia kiasi cha $1,000 naamini utakuwa ni mchango mkubwa wa kuweza kufanikisha sehemu ya matibabu yake, basi hizi Baraza zianze kwa alichonacho mtu kwa kupeyana wiki mbili kuanzia leo na mweledi Hassan Khamis aliopo UK (Rancho wa UK) aratibu huu mchango wakuweza kumchangia Ndugu yetu na Mwanaharakati.

Anaanza kuona dalili “aaah, haya yote ndio haya yanavyokuwa?” Siku hizi kuna mtindo uliokuwa maarufu nao nikuwa huonekani ulilolifanya ukiwa hasa mdogo pale ulipokua hai watu watakuja na Jazba na ukumbukwe pale ushafukiwa kaburini halafu utasikia risala inasomwa yenye Istilahi ambazo hutumika “Alikuwa mchapa kazi, akipenda watu, hakujali wakati, rushwa kwake ilikuwa mwiko n.k. ” Kibwagizo cha kukamilisha hio risala utasikia na Wizara yangu inachangia 200,000, suala apelekewe Kaburini? Alipokuwa anazihitaji ilikuwa tupo hamnazo na kujitia pambani za mtonga kuosha kidonda kwa maji ya dafu, leo mtu hayupo duniani hisia tele na majonzi.

Nimekuja na ushauri hebu tuendeleze kuangalia jinsi mwenzetu huyu tutavyoweza kumsaidia katika matibabu yake.

Aonavyo
Hamza Rijal

Assalamu Alaykum

Leo nimebatika kumuona mwandishi Salma Said….Usoni ana furaha na bashasha…machoni machofu na maumivu…moyoni mapenzi na matumaini..mwilini vita vikubwa kuyashinda maradhi aina yanayomuelewa…Tumuombee Mungu ampunguzie Mzigo alionao na apate uzima wake tuwe nae…tunamuhitajia mno…hasa kipindi hiki.

Ally Saleh
BBC

Maoni yangu

Kwa wale ambao watakaopenda kutoa harambee kwa Dada yetu salma said kutokana na maradhi yalio msibu mwenzetu ambayo ni Moyo, Mafigo na Mgongo kwa Muda mrefu sasa tunaomba tunaomba michango yenu kwa njia tofauti. Aidha kwa kutumia huduma za Simu wakiwa huko nyumbani ama kwa Paypal na hata kwa njia za Bank.

Simu: 07774 77101 Salma Said Zantel 07674 77101 Salma Said Vodafone 06575 70000 Sheikh Amour.
Paypal tembelea www.mzalendo.net Na kwa wale waliopo UK huduma za Bank unaweza kuni Inbox mimi.

Hassan Mussa Khamis

Tagsslider
Share: