Habari

Hawa hapa ndio wanaoendesha operesheni ya mazombi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu

Ni wazi sasa kwamba kuna viongozi wakubwa ndani ya serikali ya Dk. Ali Mohamed Shein walioamua wazi kutumia vikosi vyake kuwahujumu wanasiasa wa CUF na hata wananchi wa kawaida, lengo likitajwa kuwa ni kujenga mazingira ya hofu na wasiwasi katika wakati huu ambapo hamasa ya kisiasa inaonekana kurudi upya visiwani.

Mpasha taarifa wetu ameiambia Mzalendo.Net kuwa kikosi maalum cha mashambulizi kilicho nje ya utaratibu wa kawaida wa vyombo vya dola sasa kimo kazini kutekeleza operesheni kubwa kabisa, ambayo inasimamiwa kikamilifu na viongozi wakubwa kwenye baraza la mawaziri la serikali ya Shein na mkuu wa mkoa mmoja anayejijengea sifa ya kuwakilisha kundi la vijana.

“Nina hakika kuwa operesheni hii inaendeshwa na inafanyika hivi ninavyokwambia”, alisema mpasha habari wetu wakati akizungumza nasi kwa ujumbe wa simu akiwa ndani ya mojawapo ya makambi yanayotumika kuweka makundi yanayotumwa kutekeleza hujuma hizo.

“Hata kama nyinyi Mzalendo mmeonekana kujuwa yanayoendelea na kuyaweka wazi, bado hawa jamaa hamjawazuia. Ile habari yenu ya juzi kuwa viongozi 70 wa CUF wanapangiwa kushambuliwa iliwashtua kidogo, lakini hivi nnavyokwambia wamo mbioni kuendelea na mipango yao,” aliongeza mpashaji taarifa huyo.

Majuzi Mzalendo.Net iliripoti kuwapo kwa njama zilizopangwa kufanyika usiku wa Alhamisi iliyopita na makundi hayo yanayofahamika kama mazombi. Baadhi ya wachangiaji wa ripoti hiyo walioonekana kuwa ama ni sehemu ya makundi hayo au ni mashushushu wa serikali walieleza wazi kuwa hawashughulishwi na chochote kinachoandikwa hapa na kwamba wangeliweza kufanya chochote.

Chanzo chengine kutoka ndani ya serikali ya Shein kimewataja kwa majina watu wanne kinachosema ndio waliokabidhiwa operesheni za mazombi ndani ya kisiwa cha Unguja kwa sasa, wakiwa wanapokea maagizo moja kwa moja kutoka kwa viongozi wawili wakubwa, mmoja waziri na mwengine mkuu wa mkoa.

Waliotajwa ni Bakari Khamis Juma, mkaazi wa Kijichi, Juma Said anayeishi Karakana, Ibrahim Maabadi wa Makadara (wote maafisa kwenye Jeshi la Kujenga Uchumi, JKU) na wa mwisho aliyetajwa kwa jina moja la Mwinyi, afisa wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) anayesishi Mwanyanya, Unguja.

“Hawa ndio wanaosimamia makundi hayo kwa hapa Unguja. Wanao wenzao, lakini wao ndio wanaopokea amri ya moja kwa moja kutoka kwa waziri (anamtaja jina kiongozi huyo kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja), kisha na wao wanawakusanya watu wao kwenda kufanya mashambulizi,” kinasema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa kijana mmoja ambaye anasema kuwa yumo kwenye kikosi hicho, wameamriwa kuwalenga wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha CUF ambao walishinda kwenye uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015, uchaguzi ambao matokeo yake yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na kada mkubwa wa chama cha CCM, Jecha Salim Jecha.

Mmoja wa wawakilishi hao kutoka jimbo moja la mkoa wa Kusini Pemba na ambaye ana nyumba yake katika wilaya ya Magharibi B Unguja ameiambia Mzalendo.Net kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita, watu wenye gari nyeupe Toyota Hilux walikwenda kwenye mtaa wake na kuulizia nyumba anayoishi yeye.

Gari kama hiyo ndiyo pia iliyotajwa na Marehemu Ali Juma Suleiman, aliyekuwa mkurugenzi wa habari wa CUF Wilaya ya Magharibi A Unguja, na ambaye alitekwa na kundi hilo, kupigwa na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupoteza maisha katika hospitali ya Mnazi Mmoja hapo Alhamisi ya tarehe 28 Septemba.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka makambi mawili ya kikosi hicho cha wauaji yaliyopo Hanyegwa Mchana na kile kikosi kinachosimamiwa na mkuu wa mkoa kijana, wana silaha za kutosha za moto, yakiwemo mabomu ya kurusha kwa mkono.

“Hawa watu bwana sasa wameamua kushambulia hata mchana na sio tena kuja usiku usiku kama walivyofanya kwa Ali Juma. Na wameamua kuwa hawatumia tena silaha za kienyeji kama mapanga na bisibisi na vyuma. Hapana, sasa ni kitu cha moto tu kwenda mbele,” anasema mpasha habari wetu akikusudia bunduki, bastola na maguruneti.

Tagsslider
Share:

2 comments

 1. shawnjr24 9 Oktoba, 2017 at 01:22

  Wazanzibari zidisheni dua na muwe watulivu jamani si mnaona hata kule Palestina kupo shwari kwa dua zao. Yaani hichi chama cha cuf wapole sijapatapo kuona dunia hii. Kwa ufupi sisi Wazanzibari tuna nini jamani?? Masheikh wapo ndani wana najisiwa, Tunapiga kura tunanyanganywa haki yetu. Bado tuuuu tumetulia kama maji ya mtungini eti watatumaliza hivi nani ataishi milele? ? Hata ukiwa jangwani umeruhusiwa kula ng’uruwe na hawa mazombi ng’uruwe wahed tunatakiwa tuwale jamaniiii.

 2. chatumpevu chatumpevu 9 Oktoba, 2017 at 21:06

  At least waliotajwa ktk andiko hili wawili nawafahamu. Ni watu wa kaskazini ya unguja ( chaani na mkwajuni). Nikiungana na sheikh shwanjr 24 kuwa kuna kitu sio bure wazanzibar tumekaa kimya kama maji ya mtungini. mazombie watuuwe, , watudhalilishe wawaumizie wake zetu / dada zetu/ na kuwauwa viongozi wetu wa CUF halafu tunawaangalia tu kama xxxxx Nafikiri wakati umefika wa kusema liwalo na liwe. Wakiingia kwenye 18 wasitoke jamani. hawa tukikusudia tunawaweza kwa sababu sauti na nguvu za wengi ni silaha tosha kabisa.

  Masheikh wetu wanaumia na kuteseka jela za T/ bara na bado tumekaa kama vile tumeridhika kabisa na kushindwa. Viongozi wa dini wa znz wameshonwa midomo kabisa hawasemi lolote. wameufyata angalau basi wasome dua ili masheikh wetu watolewe.? Naamini kama hakuna harakati zinazoendelea wataendelea kusota jela maisha. viongozi wa dini znz Hawana ujasiri wa kukemea maovu yanayofanywa dhidi ya masheikh wetu wa UAMSHO. Ni aibu jamani. ifike wakati mazombi tuwape mtihani coz na wao ni waoga kama si ujasiri wanaoupata kwa kuwa wamepewa bunduki na dola.

  Ili kuepuka kuendelea kuonewa vijana tumieni akili zenu kwa sababu haitatokea hata siku mjoja viongozi wetu watasema sasa ngoma imenoga kwa hiyo,,,,,,,,,,, . Haki siku haitowwi kama andazi . Lazima upiganie haki yako ikiwemo haki ya kuishi.

  Kokote duniani hakuna mtu atakayewatetea wananchi wanaopata madhila ya mazombie kama sio wananchi wenyewe?

  Inakera na inatosha. Rafiki yangu jino kwa jino upo?

Leave a reply