Habari

Hili ndilo ambalo CCM na serikali zake walilikataa katakata! leo wanatapatapa !!

Hili ndilo ambalo CCM na serikali zake walilikataa katakata! leo wanatapatapa !!

Ndipo niliposema kuwa pressure hii ina sababu zake !! kwanza ni lazima CCM na serikali zake ihakikishe yakuwa kura hii ya maoni lazima ipigwe!! kwa kuwa wafadhili wametowa pesa kukamilisha jambo hili, tena tasliim!! kura hii haikwepeki imekuwa jambo la lazima. sasa nionavyo mie mwiba unawachoma wenyewe!! na si wapinzani.

Na la pili yakuwa kura hii haitokuwa na maslaha na CCM na serikali zake zote mbili, ya tanzania bara na Zanzibar !! maana itawaumbuwa!! tena saana!!

kwanza kuhusu kuandikishwa Watanzania katika daftari hili kumekusanya chaguzi mbili si moja!! huu ubabaifu utawafanya CCM na serikali zake kubabaika zaidi!!

Amma kuandikisha wapiga kura au kuwakataa kwa khofu ya kukipigia kura chama pinzani!! huku wanaogopa uchaguzi wa mwaka huu, na huku wanahimiza uandikishaji wa kura ya maoni ili ionekane kuwa wamefaulu katika kuipitisha katiba yao!! unaona mambo hayoo?

hapa ndipo wapinzani watakapopata mwanya wa kujiandikisha khasa kwa wale ambao masheha wakiwazuwia kwa nguvu zote!!

Na kuna suala huwa kila mara najiuliza!!

kuna wana siasa wengi sana upande wa CCM na serikali zake wametoweka, huwa hawaonekani hata katika mikutano yao ya hadhara!! hili limenishangaza mie sana!! aliebakia ni Mtumwa Borafia,,,,,,,, mtefle yule, ndio kwa msemo wao ndio mgeni wa heshima!! lakini kabla ya hali hii kuwageukia, tulikuwa tunawaona wanasiasa na viongozi kutoka bara kuja hutubia Zanzibar. sasa wameufyata!!
tukiuliza tutawauliza wengi tu!! kwanza Enzi talib katika siasa za Zanzibar katoweka!! kuna Mbaraka Shamte siku hizi pia haonekani na wala hahudhurii mikutano yao ya hadhara, kaufyata!! na ukipeleleza sana utaona hata mawaziri wa upande wa CCM Zanzibar kama Shamhuna, Mohamed Aboud na wenginewe hawahudhurii mikutano yao hii ya matusi kabisaa!! wanaohudhuria ni wahuni wenzao tu!! vijana wa CCM maskani, na huwaweka mbele vijana wao na kuwavisha unifomu kukata viuno na mipasho!! sasa tunajiuliza kunaniii CCM????

Kinana ametembea Tanzania nzima, kutuliza mambo, naona yamemshinda. mwisho anatowa kauli ya kufukuzana viongozi wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama ili kukinusuru. wallahi mwaka huu tutayaona mengi sana ya ajabu!! lakini kwa ufupi CCM haiko salama na si shwari mwaka huu !!!

V99!!

Share: