Habari

HONGERA MH. MBOWE Kwa Uzalendo Wako

Imeandikwa na P. Mbaga

Habari za kijiweni ndugu  Watanganyika na ware Wa Zanzibari watakao isoma makala hii. Ama mimi sina budu ila kupeleka salamu zangu za rambi rambi kwa Watu wa Mkoa wa vijiji vya UKEREWE ambako imetokea ajali ya Feri ya MV Nyerere na kupoteza maisha ya Watu wasiopungua 200. CC tuliohai tunatakiwa tuseme Innalah Waina-ilaihi Rajiuun. Hakika kila NAFSI (Roho) itaonja mauti. Mungu awape subira wazanzi na ndugu wa marehemu hao na Mungu awalaze mahali wanapostahiki maiti hao Amiin.

HONGERA Mh. MBOWE:

Sina budi ila kumpa pongezi za dhati ndugu yetu na mwana harakati mwenzetu Mh. Mbowe kwakuchukua nafasi yake ya Kiraia kufika katika Eneo la ajali nakuweza kuingia katika harakati za Uokozi. Huku Serikali ya CCM na baadhi ya Viongozi wengine TAWALA na wa Vyama vya Upinzani wakikaa Maofisini nakuangalia habari hizi  au kulaumu wale ambao wamejitokeza na kutoa Hisia zao.

Hakika ajali za Meli zimekuwa zinatia uchungu hasa ukiona kwamba ajali hizo zinafanywa kwauzembe wa makusudi. Tumeweza kuona kule Zanzibar ajali nyingi zikitokea na fedha nyingi kukusanywa lakini Serikali ya SMZ kule Zanzibar walitumia Fedha hizo Kisiasa na nyengine Zilinunuliwa Meli Mbovu ambayo Wazanzibari walio wengi wamegoma kuitumia hadi leo.

Kwa upande wa kwetu huku Tanganyika vile vile hatuna vyombo au TOOLS zakutusaidia tunapopatwa na majanga yoyote yare. Na hiri linazungumzwa sana sana na Viongozi wa Upinzani kwa miaka mingi sasa.  Lakini Serikali ya CCM kwa makusudu inapuuza Ushauri wowote ure unaotolewa na Vyama vya Upinzani. Kama alivosema Mh. Mbowe na hili waliwahi kulisema mara nyingi wakati nchi yetu inapokumbwa na majanga mbari mbari. Lakini hakuna tumeona mabadiliko yoyote, sio kwa Utawala wa Magufuli wala wa hao viogozi waliopita.

Badara yake tumeona fedha nyingi za waripa kodi zikitumika KISIASA badara ya kimaendeleo ya kijamii. Serikali ya MAGUFULI inauwezo wakununua Helcopter za Kijeshi na Kuzituma kure Zanzibar kusimamia na Uchaguzi wao Halamu wa Marudio MaRCH 2016. Rakini Inashindwa kutoa Helcopter hizo kuja kuokoa watu wanapofikwa na majanga yakuzama na Meli au Feri.

Serikali ya MAGUFULI ina fedha zakununua WATU WASIOJULIKANA na kuwateka Raia wasio na hatia na kuwauwa, lakini inashindwa Kununua au Kujenga Vyombo vya Uokoaji katika Mikoa ilioko Kwenye Maziwa Nyasa na kwengineko.

Serikali ya MAGUFULI inauwezo wakureta Makontena ya Mizigo na kupata fedha zakununulia Risasi za Moto na Ndege za Bombadmet huku Raia wa Tanganyika wanakosa maji safi, barabara nzuri na umeme kure Vijijini.

Ametokea Kiongozi mtetezi wa Jami Mh. Mbowe akisimama kama Raia wa Tanganyika mwenye Uchungu na Raia wenzake. Leo Raisi Magufuli na Viongozi wengine wa Upinzani kama Mh. Mbatia wanaanza kumlaumu Mbowe. Mh. Mbowe alilosema ji kweli tupu na hakuna wakuyasema haya kwasababu waandishi wa Habari tunaogopa kusema ukweli. Hivo ametumia haki yake yakusema ukweli na sio Kasumba au propeganda za Kisiasa.

Mh. Mbatia, kama kweli wewe nimsemaji wa watu kwanini umejifungia ofisini kwako nakuongea. Kwanini usimfuate Mh. Mbowe na watu wengine kule Kisarawe?.

Tunaiomba Serikali ya Magufuli ituambie nini kitatokea baada ya kukamatwa waliohusika kuzama kwa meli ya MV Nyerere? MV Nyerere imezama kwa Uzembe wa wafanyakazi pamoja na Serikali yao ya CCM kufeli. Jana usiku tayari tulipata Vijana wanaotumiliwa na Chama chako cha CCM wakitaka majina na Vitambulisho vya Mtanzania vya watu hao Waliopoteza maisha yao. Kwanini Munataka kutumia vitambulisho vya Watu waliopoteza maisha yao na muvihaulishe? Hivo milishapanga hii ajari itokea ili mupate vitamburisho au Jee?

Share: