Habari

Hotuba ya Karume ndiyo thabiti zaidi na yenye manufaa kwa ccm cuf uamsho kwani wao wote ni wazanzibar

Mheshimiwa Amani karume anataka wazibar wanaotaka serikali tatu nao wasikilizwe. – nakubaliana naye 100%. Hotuba ya Amani karume ya jana ambayo ninaamini iliwakera wanaccm wengi, japokuwa hakukuwa na aliyeweza kukanusha hadharani hotuba hiyo kutokana na ugumu wa mazingira ya siasa za Zanzibar, nitafafanua.

Karume alisema, namnukuu, Kuhusu katiba mpya watanzania wote na wazanzibar pia wasikilizwe na watoe maoni yao hata yale tusiyoyapenda. Akaendelea, kuhusu Muungano wapo wanaotaka serikali mbili – wasikilizwe, wapo wanaotaka muungano wa mkataba wa serikali mbili- wasikilizwe na wapo wanaotaka serikali tatu — wote wasikilizwe. Aliposema muungano wa mkataba kelele zilianza, aliposema serikali tatu kelele ziliongezeka. Wapiga kelele hawakuwa na ujasiri wa kumzomea lakini walionekana kupiga kelele za kutokubaliana naye – kwa kuwa hawakufanya hivyo kwa wasemaji wengine ni dalili za wazi kwamba aliwakera wengi.

Japokuwa magazeti ya leo hayakuandika kwa upana habari hiyo, hotuba ile imefungua ukurasa mpya kuelekea serikali tatu ambayo ni Sera ya Chadema na CUF – muungano wa serikali mbili sasa ni njia panda.

Kabla ya kufikia hoja hiyo, Amani Karume aliwakubusha wajumbe kuhusu Chama cha ASP, akawaonesha wajumbe kadi yake ya uanachama wa ASP na kuwasomea malengo ya ASP yaliyoko ktk kadi ikiwepo kupigania mustakabali wa wazanzibar. Indirectly, anataka Zanzibar yake.

Ukiunganisha dots ktk hotuba ya Mh Amani karume utagundua kwamba anataka wazanzibar wasikilizwe na kama wanataka serikali tatu nao wasikilizwe. maana yake wakichagua serikali 3 waruhusiwe kama ilivyokuwa kwa serikali ya umoja wa Kitaifa waliyoichagua wenyewe.

Ukiinganisha hotuba ya jana na kitendo chake kusimamia uundaji wa serikali ya umoja wa kitaitaifa akishirikiana na Maalim Seif ili kuwaunganisha wazanzibar – utagundua kuwa Karume anataka Zanzibar huru – kwa maoni yangu at least.

Katika hotuba yake ya Jana, alizungumzia watu kutishana Zanzibar na kuipinga jambo hilo. Na kusema mtu akiwa na maoni tofauti anapewa jina lile ( Hakulitaja ila alimaanisha uamsho). Hii ina maana kwamba Amani karume anawatetea kwa kwa namna isiyo ya moja kwa moja (Indirectly) viongozi wanaotaka muundo tofauti wa Muungano wa sasa (waziri aliyetimuliwa na Shain?). Na ukiunganisha dots hapa anazunguzia kauli kwamba wanaotaka muundo wa serikali ambao hauendani na sera ya ccm wajiondoe ccm- yeye anataka wazanzibar wasikilizwe siyo wanaccm. Na hataki wanaccm kufukuzwa hata kama ni kiongozi kwa kutoa maoni tofauti.
Na kwa maana hiyo, kwa kumsikiliza mantiki ya Amani Karume anawatetea pia wanaUAMSHO ambao ndio wanainijinia muungano wa Mkataba, serikali tatu au kuuvunja kabisa – nao wasikilizwe.

Ifahamike, Uamsho ni kundi la wazanzibar wasiotaka Muungano. Karume kaongea vizuri kabisa kwa niaba yao- kawatetea.
Kwa lugha nyingine, uamsho jana ulitoa hotuba yao ndani ya mkutano mkuu wa CCM wakiwakiliwalishwa na Mwanachama wao – kimtazamo, mkiti mstaafu wa ccm – AMANI KARUME.

Ikumbukwe, CUF wanahusishwa na UAMSHO. Na wakati huo huo injinia wa kuinganisha CUF wanaohusishwa na UAMSHO ni karume huyu huyu aliwatetea UAMSHO jana akitaka wasikilizwe.

Na ikumbukwe pia kuwa , Maalim Seif wa CUF inayohusishwa na Uamsho ambaye ni katibu mkuu wa CUF, alishawahi kupendekeza kwamba Karume wa ccm aliyetetea hoja ya UAMSHO jana aongezewe Muda wa Urais Zanzibar hata baada ya mwaka 2010- karumu na Maalim Seif Hawakufanikiwa.

Nahitimisha kwa kusema, japokuwa Karume alipinga vurugu na uvunjifu wa Amani Zanzibar na kusema kwamba wahalifu washtakiwe, ni wazi kwamba hakubaliani na wazanzibar kulazimishiwa Muungano kwa staili ya sera ya ccm na kutaka wazanzibar wapewe uhuru wao wa kuchagua. Na wakichagua serikali tatu ambayo ni mhogo mchungu kwa ccm na iwe hivyo na wakichagua kuuvunjwa kwa muungano kama wanavyotaka wanauamsho na iwe hivyo.

Na kwa mantiki hiyo, tusitarajie kwamba uamsho utaisha Zanzibar kirahisi na tusitarajie Muungano wa staili ya ccm utaendelea kulazimishwa Zanzibar – Hapana – naktaaa. Uamsho ni mtazamo kuhusu Mustakabali wa Zanzibar kwa macho ya baadhi ya wazanzibar, muafaka kuhusu Muungano kwa mtazamo wao – karume yumo.

Kwa hiyo, hoja ya uamsho ya kubadilisha muundo wa Muungano ingalipo na ndo kwanza inapata wanachama wenye status kubwa – KARUME akiwemo. Hapa tulipofika, njia ya ccm kukwepa at least Serikali tatu ambayo pia ndiyo sera ya Chadema imefika mwisho.
Nawasilisha.Sera ya ccm ya kugawa na kutawala wazanzibari ni muflis. Generation Z wanajitambua cannot be swayed easily na cheap propaganda. Karume a lone dove in flock of crows, you have won the hearts and minds of Zanzibaris

Share: