Habari

Jee dhana ya Uongozi katika Afrika ni kuwatumikia wananchi au ni kuwafanya wananchi watumwa?

Hawa ndio viongozi na dhana ya Uongozi kwa nchi za Kiafrika. Ukiangalia nchi zetu ni maskini sana ukilinganisha na nchi za magharibi, lakini mambo tunayofanya sisi hayaingii akilini kwa wenzetu.
Natoa Mfano Kanzela wa Ujerumani analipwa karibuni 250000€ kwa mezi. Wengi watasema ni nyingi lakini mimi nasema sio nyingi kwa sababu tatu.
1. Kutokana na pato la Nchi kwa ujumla ni kiasi kidogo sana hata Manager Benki kampuni kubwa za ujerumani wanamzidi mara mbili Kanzela wa Ujerumani kwa Mshahara.
2. Kwa vile Pato lake linazidi 50,000 kwa mwaka wanachukuliwa ni watu wenye kipato kikubwa kwa hiyo Tax wanayokatwa inafikia 50% ya mshahara wake wakati watu wa kawaida wanakatwa 14% na ukiwa na watoto wengi hukati kabisa na Pengine Serikali wakulipe wewe.
3. Viongozi wote wa Ujerumani (Mawaziri na Wengineo) hawatembei na na Gari za Serikali wanakuwa na Deinstwagen. Kimsingi zinamilikiwa na Serikali (registration) lakini bei ya gari unalipia mwenyewe yaani unakatwa katika mshara wako kila mwezi. Unapomaliza utumishi wa Serikali gari unaachiwa mwenyewe unalipa difference ya bei ya gari kwa wakati ule tu.
Sisi viongozi wetu wakiwa madarakani kila kitu ni bure
Utashangaa wabunge wa Bunge la katiba wanalipwa Posho la 300000 kwa siku bila kukatwa kodi lákini mfanyakazi wa kawaida anayelipwa 150000 kwa mwezi anakatwa kodi!!
Jee dhana ya Uongozi kwa Afrika ni kuwatumikia wananchi au ni kuwafanya wananchi ni watumwa wao?

Share: