Habari

Jee wana wa Donge mutampenda Shamuhuna au mutaipenda Zanzibar yenu kwa hatma ya vizazi vyenu?

Hakuna shaka kuwa Mh Ali Juma Shamuhuna Waziri wa Ardhi Makazi Maji na Nishati (Prences wa Donge) kacheza deal na kashatuuwa Wazanzibar, kwa kumnukuu tu kauli yake ya kinafiki katika mashwala na majibu kwenye Baraza letu la Uwakilishi anasema hivi.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho ameitaka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kutoa taarifa katika baraza la mawaziri suala la TANGANYIKA kuwasilisha ombi la nyongeza masafa ya bahari kuu kwenye Umoja wa Mataifa. Kificho alisema hivyo baada ya Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna kusema kwamba yeye kama wizara taarifa anayo hiyo lakini katika baraza la mawaziri hakuna taarifa ya jambo hilo iliyowasilishwa.

alisema kwamba wizara yake inayo taarifa kamili ya suala hilo ambapo alitakiwa yeye kufunga safari kwenda umoja wa mataifa kuwasilisha ombi hilo pamoja na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi wa jamhuri ya muungano Bi Anna Tibaijuka.
Hata hivyo Shamuhuna alisema kwamba kutokana na kutingwa na kazi nyingi alimtuma afisa wake kufuatana na ujumbe huo kwenda katika safari hiyo.“Ujumbe huo kwa sasa upo katika umoja wa mataifa na tayari unatarajiwa kuwasilisha ombi hilo ambapo TANGANYIKA baadaye itapangiwa tarehe kwenda kusikiliza shauri lao”.

Kwa hio ndugu Wazanzibar Ali Juma Shamuhuna tayari ameshaiuza Zanzibar na rasilimali zake zote, nah ii ilikuwa ni deal ya siri siri , kipindi cha nyuma nyuma niliandika mada yangu katika ukumbi huu kuwa safari ya Joji W Bush sio bure ni mikakati maalum ya uchimbaji mafuta wa Zanzibar ,badhi ya ndugu zangu wengi walinikebehi na zarau kama kawaida yetu na utamaduni wetu tulionao Wazanzibar.

Mimi sikusema vile tu kichwa mchungwa asilimia %80 kuhusu mchakato wa mafuta hupata kutokana na kuna rafiki yangu kaowa M-Norway na yuko top katika serekali ya Norway.

Sasa baada ya kuona Tanganyika kuwa mafuta ya Zanzibar yamekuwa tabu kuyapata kutokana na marekebisha ya katiba ya Zanzibar kuhusu mibaka na mikowa yake , wenzetu wa Tanganyika wanatumia ujanja wakumwaga mamilioni kwa badhi ya viongozi wa Smz ili kuweza kuiza Zanzibar na kuitowa kwa mlango wa nyuma kama vile mali ya urisi wao wa familia.

Sasa na huyu Mh Ali Juma Shamuhuna Allahu yalam kuwa simiongoni mwa wabaya wa Zanzibar ambao M/mungu hutubainishia ili kuweza kuwajua, sasa dalili na ishara zote za marazi zimeshajibainisha lililo baki ni M/mungu kutuangalia tutayatibu vipi maradhi haya?.

Kama tutamshukulia Mh Shamuhuna kuwa ana sifa za ukereketwa kwa chama a. au ni Kada mpevu b. au ni Mwana wa Donge (Prences of Donge) basi Wazanzibar tusubiri azabu zenye kuumiza na maangamizo ya nchi yetu Zanzibar kwa maslahi binafsi za watu wa aina hii (Wanafiki).

Hivi sasa Jumuia za Ulaya zinatupima ukakamavu wetu Wzanzibar, ikiwa tutazembea na kuzarau kuzani kila mtu halimuhusu hili basi wenzetu wa Tanganyika watatumia advantage hii ili wajipendekeze katika mataifa ya kigeni na kutia mrija ili kuyafyonza mafuta ya Watu wa Zanzibar na sisi kutuona mabarazuli hatuna maana.

Kama walivyozowea kusema kuwa watoto wa viozi vya ulojo, tatizo la Zanzibar tunalo Wazanzibar wenyewe tunalilea na kulikuza na hili limekuja kutokana na kujigawa mafungu mawili .

Kuna wazalendo a. na b. kuna watapia mloo ambao wako tayari kuiuza Zanzibar kwa maslahi yao binafsi, ambao hawajuwi kuwa kidogo wapatacho asari yake nikubwa mbeleni.

Nikukuangamiza na kukipoteza kizazi cha Wazanzibar kuja kuwa Homeless(Mayadima kama Palestin) hivyo kweli viongozi wetu wa Smz hawalioni hilo?.

Hawa wenzetu wanajuwa kuwa Muungano ni chumo lakujinufaisha wao kama kweli walikuwa na zamira njema ya Muungano basi tungebakia na kuwa na Tangayika ambae ndio mchirika mkuu wa Muungano, na wangeweza kulinda mikataba ya Muungano ikiwemo kila nchi na mipaka yake.

Vipi leo bahari haimo katika mikataba ya Muungano wao wabiruke tena upande wa pili kudai Bahari kuwa ingizwe kwenye Muungano kwakuwa tu wapate kuiba rasilimali za Wazanzibar?.

Maana naskia hivi sasa Serekali ya Tanganyika imetenga pesa specel ili kuzitumia kwa kuinunua Zanzibar kupitia viongozi zaifu ambao wao wenyewe wamesha waramli kuwa ni nani na nani wanaweza kuwanunua kipesa au kuwa tongoza kimadaraka.

Kuna wengine hupenda wenyewao kujipendekeza kwa viongozi wa Tanganyika na kutumiliwa kuwa vishihata wa kuiangamiza Zanzibar.

Mungu ibariki nchi yetu Zanzibar na watu wake.

Share: