Habari

Jengo la skuli litaabani , wananchi : PAZA yawa msaada mkubwa

Jengo la skuli litaabani , wananchi : PAZA yawa msaada mkubwa

Imeandikwa na Salmin Juma , Zanzibar

Kufuatia shida ya uchakavu wa jengo la kituo cha skuli kwa muda mrefu katika shehia ya Umbuji wilaya ya kati Unguja hatimae wananchi wameamua kupaza sauti kwa serikali na wadau wengine kuwafanyia ukarabati jengo hilo ili wanafunzi wasome katika mazingira mazuri na salama.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wananchi hao walisema, jengo hilo ni la kabla ya mapinduzi ya 1964 hivyo limeshaanza kuharibika hasa kuvujisha wakati wa mvua jambo linalowafanya wananfunzi kuwa katika mazingira mabaya.

Mmoja kati ya wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Patima Vuai Hassan alisema, tokea kuingia kwa mradi wa kukuza uwajibikaji Zanzibar – PAZA (Promoting Accountability of Zanzibar) kumesaidia kuwafnaya wananchi waweze kuzungumzia shida na changamoto zinazowakabili hivyo waliamua kupaza sauti kuhusiana na jengo hilo wakiamini kutapatikana suluhisho.
“Mradi ulitusaidia sana kutufunua namna ya kuzisemea shida zetu, kwakua banda lilikua linavuja chini ya ukuta, tulihamasishana nyumba kwa nyumba kuchangia kila mmoja Tsh elfu 10 , ili tukazibe na tukafanikiwa kulinusuru banda hilo , tukakaa tena tufanye nini, hapo ndio tukaandaa mipango ya kufikisha kilio chetu kwa serikali” alisema mwananchuyo.

Aidha, aliendelea kueleza kuwa, katika hatua za kufikisha kilio chao serikalini, waliandaa maghafali ya wanafunzi kwa kuwaalika viongozi wakubwa wa serikali kwa shabaha ya kuwaelezea changamoto hiyo.

“tuliyaeleza yote, baada ya siku chache tukapokea ujumbe kutoka halmashauri ya wilaya ya kati kuwa, ombi letu wamelisikia na watarekebisha katika sehemu zenye mapungufu ili Watoto wawe katika mazingira mazuri na hadi sasa wameshaanza marekebisho ” alisema mama huyo.

Mwananchi mwengine Haji Shauri Issa alisema, anatamani kuona mradi wa PAZA haumaliziki, kwa sababu umewafunza mambo tofauti.

“kwanza umetufunza , kujua taratibu za wapi tunaweza kupeleka malalamiko yetu, yaani hatua za awali za kufatilia jambo mfano katika jengo la skuli na tupo katika hatua nzuri” alisema Issa

Kwa upande wake Makame Haji Steni afisa elimu na mafunzo ya amali kutoka halmashauri ya wilaya ya kati Unguja alisema, amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na wengi wao wanalalamikia kuhusu uchakavu wa mabati, vyoo kuwa kidogo katika majengo ya skuli pamoja na uhaba wa mabanda wenyewe.

Alisema , imeyapokea malalamiko hayo na imeshaanza kuyafanyia kazi kwa kwadiri ya hali ikatavyokuwa inaruhusu.

Akigusia kuhusu mradi wa PAZA afisa huyo alisema, watu wengi wanashindwa kujua mambo kwa kukosa elimu lakini sasa wameanza kujua majukumu yao na kuyafatilia kutokana na elimu iliyopatikana kutoka katika mradio huo , hivyo kubakia ndioa mzizi wa maendeleo.

Mradi wa PAZA ulianza Novemba 2017 na unatarajiwa kumalizika Febuari 2019 mradi ambao unatekelezwa katika wilaya tatu za nguja (wilaya ya kaskazini A, wilaya ya kati na wilaya ya kusini ) na Pemba pia upo katika wilaya tatu ( Wilaya ya chakechake, wilaya ya Wete na wilaya na Micheweni)

Mradi unasimamiwa na kutekelezwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzaniab-Zanzibar – TAMWA, Jumuiya ya waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar – WAHAMAZA pamoja na NGENAREKO kisiwani Pemba.

PembaToday

Share: