Habari

Jeshi Kutumika tena Zanzibar

Kama mujuwavyo, Tanzania imo kwenye matayarisho ya uchaguzi mkuu wa 2020 na wa serikalli za mitaa wa mwishoni mwa mwaka huu. Lakini kutokana na tabia mbovu za kiutawala za Rais Magufuli, hali ya nchi ni tete. Ukosefu wa ajira ni mkubwa, umasikini umezidi, haki za binaadamu zinavunjwa vibaya na mtawala anajenga tabaka lake tu na kuliimarisha. Sasa watawala wameuona ukweli kuwa hakuna uchaguzi hata mmoja watakaoufanya kwa haki wakashinda na wanauogopa kwelikweli uchaguzi wa aina hiyo. Sasa ili kuidhibiti hali na kuendelea kuwapo madarakani, wameanza uharamia wao kwa Zanzibar ambako wameshathibitisha kwa utafiti wao wenyewe kuwa hata kama watakwanga wakiwa uchi wa mnyama hawawezi kushinda kwa kura.

TanzaLeaks tuna taarifa za uhakika kuwa mtawala ameamuu wanajeshi mchanganyiko laki moja na nusu (150,000) waingizwe kwenye daftari la wapigakura la Zanzibar linalotegemewa kuanza kuboreshwa hivi karibuni kwa mabavu. Kura zao bandia ndizo zitatumika kwenye uchaguzi mkuu. Tayari baadhi ya maafisa wa juu jeshini wameona kuwa mpango huom unahatarisha zaidi amani, kwani Wazanzibari wameshaapa kuwa mwaka 2020 hawatakubali tena kuwekewa mtu wasiyemchaguwa wenyewe. TanzaLeaks imezungumza na baadhi ya wanaoujuwa mpango huo wanasema kuwa hata baadhi ya fedha ambazo Mkaguzi Mkuu Profesa Assad amedai kutokuziona kwenye mahesabu ya ukaguzi wake ni zile zilizohamishiwa Fungu la 20 la Ikulu ya Magogoni na zinatumika kwa mpango huo. Dunia inatakiwa kujuwa kuwa mtawala anaipeleka nchi kwenye machafuko na mauaji.

Tagsslider
Share: