Habari

JESHI LA (JWTZ) KUADHIMISHA MIAKA 54 TANGU KUANZISHWA KWA KUFANYA USAFI

JESHI LA (JWTZ) KUADHIMISHA MIAKA 54 TANGU KUANZISHWA KWA KUFANYA USAFI

Na Fatma Ally

Jeshi la Wananchi Tanzania ( JWTZ) limesema linajivunia kuendelea kulinda amani ya watanzania kwa nidhamu ya hali ya juu kwa muda wa miaka 54 sasa tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo mwaka 1964.

Kauli hiyo,imetolewa mapema leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa habari na uhusiano wa Jeshi hilo Kanali Ramadhani Dogoli, wakati alipokua akitoa taarifa ya maadhimisho ya kutimiza miaka 54 kwa jeshi hilo.

Amesema kuwa,kutokana na uwezo huo jeshi hilo limekuwa likitumiwa na Umoja wa Mataifa( UN) katika kutuliza ghasia kwa nchi zenye machafuko ya amani ikiwemo nchi ya DRC Kongo,na nchi ya Sudan.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya usafi katika maeneo yao siku ya septemba mosi mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya maadhimisho ya miaka 54 tangu kuanzishwa kwake.

“Nawaomba wannchi wajijitokeze kwa winging ufanyaji usafi katika maeneo yao, kwa upande wa jeshi la limeanza tangu Agosti 27 mwaka huu, kushiriki shughuli mbalimbali za usafi kwenye maeneo ya kambi zote za jeshi pamoja na kufanya michezo mbalimbali Vikosini”amesema Dogoli.

Ikumbukwe kuwa Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ huazimisha kumbukumbu ya kuanzishwa kwake mwaka1964 baada ya kubadilishwa jina kutoka Tanganyika Rifle (TR) ambalo lilikua jeshi la wakoloni.

Tagsslider
Share: