Habari

JMP na Amri yake: Yamnusuru kijana aliebandikizwa kesi ya Uuwaji.

Asalamu aleikhum Warahmatullah ( Rehema na Amani ziwe juu yenu) ndugu zangu wa  Wazanzibari na Watanganyika wa ndani na nje vi Visiwa/ nchi  zetu adhimu. Sina budi ila kumshukurui Mwenyeenzi mungu SW kwa wingi wa rehma na afya alionijaalia nao wakuweza kuandika makala hii. Na bila yakupoteza muda ni bora nielekee katika kichwa cha habari niliokusudia ambacho nitakichambua katika point 4 kubwa muhimu

Polisi

DPP

Media Intelligence:

Raisi awe baba bila upendeleo.

 

# POLISI:

Ndugu zangu tumeweza kuona kwamba ni jambo la mazoea kuona jinsi jeshi la Polisi linavovunja sheria za nchi na haki za kiraia pale ambapo linamkamata mtu kwa makosa haya na yale. Matatizo haya yamekuwa yakisemewa sana na vyama vikuu vya upinzani, lakini hatujawahi hata siku moja kukisikia chama tawala au kiongozi wa CCM chama tawala kinazungumzia makosa na matatizo haya. Mimi naweza kusewma sababu moja kubwa ya Ukimya wa chama tawala kutokuikemea Polisi pale wanapofanya kazi zao kwa uonevu, nikwamba Polisi huwa ni muhimili wa mfumo wa utawala wa Siasa. Haya ni makosa makubwa sana kuliona Jeshi la Polisi au Ulinzi na usalama linajishuhulisha na Siasa au kufanya upendeleo na kuwatia hatiani watu watu wasiokuwa na hatia na kuwaachia huru wale walio na hatia.

Kwa muda wa miaka mingi sasa ipatayo 25-30 tumeshuhudia huduma za polisi zikiwa zina upendeleo au kutumia madaraka yao vibaya. Polisi hao wamepata vichwa vyakufanya maovu zaidi au kuchukua rushwa tokea JMP aingie madarakani. Kwa Mfano kumbandikiza mtu kesi bila ya sababu yoyote na kumueka ndani bila yakushatakiwa. Hili ndilo lilotokea kwa ndugu zetu wa Muansho na yule kijana wa Kigoma aliesingiziwa kesi ya Uuaji. Polisi wamekuwa wala rushwa wakubwa na mara nyengine huwafanyia Ngono watuhumiwa wakati wakiwaweka rumande. Ingekuwa Polisi wanatumia Utawala wa Sheria na kujuwa Sheria za Nchi na raia basi haya yasingetokea.

Sio hivo tu, ingekuwa kama chama tawala CCm watu wao wanakumbwa na matatizo kama haya naamini wasinge kaa kimya au wangefanya juu chini ili kesi ya mtuhumiwa idhoofishwe. Kama vile ilivo dhoofishwa kesi ya yule mtoto wa Abdul Talib Kilango kule Zanzibar baada yakuwalawiti kwa nyuma wato wadogo wa kiume. Kwavile yeye ni CCM na dada yake yuko katika mfumo wa Serikali basi ilikuwa sio kosa. Pale tunapopata kiongozi wa juu akawa anaangalia kadhia hizi bila ya upendeleo naamini tusingekuwapo hapa tulipofikishwa. Ningemuomba JMP kama yeye i raisi wa haki na wa watu Maskini basi angeuangalia mfumo mzima wa Polisi na makosa ya jinai.

#DPP:

Huu ni muhili mwengine wenye kuchukua fungu kubwa la dhambi pale wanapochelewa kufanya uchunguzi wa kesi katika kipindi kilicho ainishwa na Katiba.. Kuna watu wanasota rumande kwa miaka zaidi ya 7 sasahivi huku DPP ati bado hajamaliza uchunguzi. Mfano ni kesi ya Ndugu zetu wa UAMSHO, nduguzetu hawa wamesukumiziwa kesi za kigaidi nakupelekwa Jela bila yakuhukumiwa . Na kesi yao kila mwezi hupigwa Dana Dana nakuambiwa uchunguzi hauja kamilika. Ni nchi gani au kiongozi gani mwenye haki anaependa kuona raia wake wanabandikiziwa kesi nakutiwa ndani bila sababu?

Kwanini JMP aliamuwa kuingilia kati kesi ya yule kijana wa Kigoma aliesingiziwa mauaji na kuwaacha UAMSHO ambao wamesingiziwa kesi za Ugaidi.. Uamsho kosa lao kubwa la ugaidi nikutoa Elimu ya Katiba ya Muungano na ku-ukosoa mfumo huu wa Muungano ambao umeshakosolewa na Tume nyingi zilizopita hapo awali kabla hata ya tume ya Warioba kuja. Kama kweli Raisi JMP anawatetea wanyonge na Uaamsho ni viongozi wa Dini ambao walikuwa na haki kama asasi ya kirai kutoa elimu juu ya muungano. Kwanini Viongozi wa Dini ya kikristo waliotaka muungano wa Serikali 3 hawakutiwa ndani? Kama Raisi Magufuli ni muungwana kweli na hapendelei baina ya mkristo na muislamu au Mzanzibari na Mtanganyika basi angeliangalia hili suali letu la Mashekhe wa Uamsho. Ni wazee wangapi wanaomwaga machozi juu ya watoto wao? Ni watoto wangapi wanaokosa school fee na nguo au chakula juu yakuwa wazazi wao wako Jela wanasota kwa miaka 7 sasa na kesi bado inambiwa haijakamilika kufanyiwa uchunguzi?

#MEDIA :

Tumeweza kuziona media za Kiafrica au za Kitanganyika na kizanzibar zikijiingiza katika makundi ya vyama vya Siasa na kutoa taarifa za uongo au kutokuwa wabunifu wakuuliza masuali pale wanapoona kwamba Haki haijatendeka. Mfano mdogo ni ule wakufutwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar 2015. Media nyingi za Tanganyika ( Claud Media) ambazo zilikuwa mstari wa mbele kuipigia kampeni Katiba ya CCM CHENGE na Muungano haramu zilifanya hivo. Lakini media hizi hizi zilishindwa kupigia kampeni haki ya Wazanzibari dhidi ya CCM- Wana habari wamekuwa kama makasuku au makinda ya ndege, wanangoja mounth feeding. na hawawezi ku create ambiguas question dhidi ya mfumo mbaya wa uendeshaji kesi au mahakama au utawala. Mimi sikujuwa kama ile Cloud Media inatumiliwa na CCM na ni moja katika mfumo. Acha mungu awape mitihani mikubwa yakuondokewa na watu wao 2. Media wamekuwa woga hata kuandika kile walicho kikopi and past. Na utawala ukiwa mbovu na wa kiupendeleo kama huu wa JMP ndio media hawa hupata sababu yakugeuka makinda ya ndege Mnana.

Ili democrasi iendelee kukuwa ni lazima wapinzani, Media na mfumo system ya chama tawala na viongozi wake waweke Siasa pembeni inapokuja wakati wa kufanya kazi na kuwatumikia wananchi wanyonge. Na sio atoke mtu mmoja mmoja amuandikie Magufuli barua ya kutaka amsaidie kama yeye ndie Mungu. Mfumo ungekuwa na systen za kesi na kukata appeal na ingekuwa inawapa uhuru mawakala wakujitegemea. Tumeweza kumsikia dada yetu Fatma karume anasikitika sana kukosa kufanya kazi zake vizuri yakuwatetea wadau wake kwasababu mfumo wa Utawala hautaki mtu mwengine awe na futraha kama sio CCM au mzazi wake ni mkereketwa.

# Raisi anatakiwa awe Baba asiependelea.

Nduguzangu wananchi tumeona ile kesi ya kijana wa Kigoma, aliasingiziwa kesi ya mauwaji na polisi na DPP kumtupa jela bila yakufanya uchunguzi na kumuhukumu. Kijana huyu ana rafiki ndani ya Ikulu natumai amemsaidia kupeleka kilio chake huko na kumuandikia Raisi. Raisi ameamua kuchukua hatua ya kesi hii mara moja na kila mtu ameona nini kilitokea. Huyu naweza kumpa credit yakuwa raisi kwa tukio hili. Magufuli kajigeuza baba na katoa maamuzi bila ya kuogopa au kumuonea haya mtu au kundi jengine. Masikitiko yangu kwamba, Magufuli aalikuwa ni matumaini ya Wazanzibari na ukandamizaji wa mfumo wa CCM SMZ hasa siku ile uchaguzi wa Wazanzibari ulipofutwa na baadae kuvamiwa kwa Jeshi. Magufuli alifeli kutoa uamuzi wa haki na kuheshimu katiba ya Zanzibar . alifanya hivo kwasababu ya upendeleo wake dhidi ya Vyama na Nchi. Wazanzibari wanajuwa sasa kwamba Muungano na kila raisi anaekaa anakaa na utawala wakuimaliza Zanzibar.

Pale raisi anapofanya haki basi  wananchi wanaweza kuwa na furaha licha yakuwa ni masikini, furaha hii inaleta upendo ndani yake na pakiwa na upendo wa kweli kweli ndani ya jamii zetu basi Nchi hunaza kunawiri na uzalendo huzaliwa. Magufuli huyu badala yakugeuka baba katika suali zima la Uamsho yet again amekuwa blind eyes na anaona uhamisho kwavile ni Waislamu basi waacheni waozee ndani. Mwisho anapita akisema ati masuali ya Zanzibar yataamuliwa na Wazanzibari.

SISI tunasema Hewellah na alioko juu mgojee chini.

 

Share: