Habari

JPM: Watakaochezea Muungano kukiona

April 27, 2018

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amesema mtu yeyote atakaejaribu kuuchezea muungano atashughulikiwa vikali hata kama atakuwa nje ya nchi.

Aliyasema hayo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo alisema kuna watu ambao hawapendi muungano uwepo lakini ni wa kupuuzwa.

Alisema muungano ni kitu kikubwa cha kujivunia hivyo Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na serikali.

“Muungano wetu ni mfano wa kuigwa duniani, kwa sababu ni muungano wa kihistoria, ndio muungano ambao ni mfano katika mataifa mengine, lakini kuna watu ambao hata kama mkifanya vitu vizuri wenywe kazi yao ni kubeza tu, sasa nasema kwa yeyote atayejaribu kuuchezea muungano huu atachuliwa hatua kali haijalishi yuko ndani ya nchi ama nje ya nchi” alisema.

Katika hatua nyengine, Magufuli ametangaza kuipandisha hadhi manispaa ya mji wa Dodoma kuwa jiji kuanzia jana.

Aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Zanzibarleo

Tagsslider
Share: