Habari

Juma Duni ndio mgombea wa Urais wa Zanzibar 2020

Mengi yamesemwa hivi karibuni baada ya Mjumbe wa Baraza kuu la uongozi wa Chadema kutoa kauli ya kumkaribisha Maalim Seif kujiunga na Chadema hivyo kumuhakikishia kuwa atapewa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar 2020.

Kila mmoja atakuwa na muono wake, ila muono wangu nikuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Chadema ni JUMA DUNI HAJI. Huu ndio muono usiohitaji miwani wala makengeza.

Nimesema mgombea Urais wa Zanzibar kuwa ni JUMA DUNI HAJI, ndio yeye sikuweka ushabiki na wala sitanii. Sababu zangu ni ni hizi:

1. JUMA DUNI ni mwanachama hai/mstaafu wa Chama cha Chadema. Hivyo anazo haki zoote za kuwa mgombea wa Urais bila kupingwa.

2. JUMA DUNI alikuwa mgombea mwenza wa Chadema katika Uchaguzi wa mwaka 2015, hivyo kuonyesha kuwa anatimiza vigenzo na masharti yote yakuwa mgombea.

3. JUMA DUNI uwezo wake unajulikana sio kwa Wazanzibar tu bali hata kwa Watanganyika. Pamoja na makala, hotuba na umakini wake wakati wa kuzungumza jukwaani.

4 JUMA DUNI ni msomi kati ya wasomi mahiri GIC, wengi wa classmates wake wanalijuwa hilo.

5. Kufuatia msimamo wa CUF kususia Uchaguzi chini ya mgombea Maalim Seif huku akiwasilisha madai yake, haiyumkin kwake yeye kuingia kwenye Uchaguzi 2020 akiwa mgombea. Kwavile hakuna kilicho badilika. Atakuwa anakwenda kinyume na msimamo wake.

6. CUF sasa hivi imebakiwa na muda mfupi wa kujipanga huku CCM kwa miaka 3 iliyopita imekuwa ikijitayarisha vya kutosha.

7. Maalim Seif asitoke CUF, abakie CUF aendeleze mapambano na Lipumba. Kutoka kwake CUF kutaipa team Lipumba kuongeza nguvu zake.

Nadhani nimeeleza sababu za kutosha kutokana na muona wangu. Akili ni nywele kila mmoja ana zake. Vile zitakavyo chipua ndio zinatakavyomea.

Mwisho kwa nafasi ya mgombea mwenza inamfaa sana Ismail Jussa, kuwa mgombea mwenza kupitia Chadema.

Share: