Habari

Jumuiya ya Maimamu Zanzibar yapinga madai ya wanaharakati wa kutetea haki za wanawake

Na Fatma Makame na Miza Kona Maelezo

Jumuiya ya Maimamu Zanzibar ( JUMAZA ) imepinga madai ya wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wanaotaka mwanamke kupewa nafasi ya kadhi katika Mahakama ya Kadhi Zanzibar jambo ambalo halikubalikia katika dini ya kiislamu .

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi ya JUMAZA Majestiki, Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Sheikh Muhidin Zuberi Muhidin amesema hakuna sheria katika dini ya kiislamu inayoruhusu mwanamke wa kiislamu kupewa nafasi ya ukadhi.

Alisema uislamu ulikuja kumkomboa mwanamke na kumpa heshima na sio kumnyima haki zake za msingi na kumwekea mipaka ili kuweza kutekeleza majukumu yake yanayokubalika bila kwenda kinyume na maamrisho ya dini.

“Katika kipindi cha Mtume hakukuwa na kadhi mwanamke katika Mahkama ya Kadhi, mwanamke ameekewa mipaka maalum katika dini ya kutoa maamuzi, hawezi kutoa idhini katika ndoa hivyo akishika nafasi hiyo atalazimika kuozesha jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria ya dini ya kiislam”, alifahamisha Shekh Muhidin.

Katibu Muhidin aliwataka wanaharati wanaotetea haki za wanawake Zanzibar kuachana na mambo yanayokwenda kinyume na dini na kushughulikia harakati zao ili waweza kuinusuru jamii kuingia katika mfarakano na kupelekea uvunjifu wa amani.

“Serikali inatakiwa kuwa makini sana na masuala yanayohusu sheria za dini ili kuiepusha jamii kuingia katika hatari uvunjifu wa amani”, alisisitiza Katibu Mtendaji.

Nae Mwenyekiti wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa JUMAZA Nassor Hamad Omar amewataka Wanaharakati hao kutumia nguvu zao kuiokoa jamii katika kupinga vitendo vya udhalilishaji na sio kuibua mijadala isiyokubalika.

Hata hivyo amevitaka vyombo vya habari kufanya utafiti wa kina kuhusu masuala ya dini kabla ya kuzitoa habari ili kuwa na uhakika wa taarifa yenyewe kwa lengo la kuepuka upotoshaji kwa jamii.

Zanzinews

Share:

2 comments

  1. shawnjr24 13 Novemba, 2017 at 21:24

    Masheikh ubwabwa ukisikia ndio hawa, hili nakubaliana na Jumaza. Lakini Jumaza mbona mpo kimya kwa wale ndugu zetu wa uamsho? Na waislamu wote ni ndugu. Au wale ndio mnawaogopa kuwatetea msije mkakosa ubwabwa na kuletewa mazombi kukucharazeni mikwaju?. Kama leo waislam wa Tanzania wanapaza sauti kama wale wakristo wa bara wallahi waislamu tusingelikuwa tunaonewa kama hivi. Lakini leo tumekuwa na sauti kama ya panya aliebanwa na mlango au mbwa koko alietia mkia katikati na kukimbia mbio kwa uoga.

  2. Papax 14 Novemba, 2017 at 13:50

    Kama mwana mke atakizi vigezo, vya kuwa kadhi, uislam, hauja kataza, kusema kweli uislam, umetao surusa kubwa kwa vimbe wa allwa, kwenye uongozi mdogo kama huu ukazi , uislam, haujakataza, kwanza hii nchi ,c, yakidi hii ni huruma tu ya watawala ili na wao wapate hii ajira, sasa nyie wenye kilimbo za sisa za kigaini ndio ntapinga

Leave a reply