Habari

KAMA HUYAJUI ULIZA WENZIO

Nchi za kiafrika ikiwamo zanzibar nambari moja kuisaliti nchi yetu katika nyanja za kiuchumi na huku tunainyonya kuimaliza imalizike .
Uongo umekuwa itikadi za viongozi na wenye kipato kikubwa (matajiri feki)ili kujinufaisha bila kuwajali walala hoi kwamba wanasumbuka kimaisha na hakuna wa kutusaidia katika maisha ila kutudhalilisha na kutumaliza.
Leo hii makala yangu yatagusia mambo matatu ambayo ni ukweli mtupu na hakujitokeza hata mtu mmoja kugusia hali hii .
Sababu ni kwamba wale wanaomiliki mitandao ya internate ni watu wenye uwezo kwa hapa kwetu hivyo hawahitaji kujimaliza kwa kujitokeza na kuchambua mas-ala kama haya ninayokuja nayo leo. Mas -ala yenyewe ni kama yafuatayo.
1.Viongozi wote wa hapa kwetu wenye vipato kwa njia ya halali au haramu fedha zao wanaziweka katika mabenki ya nje.
2.Watoto wa viongozi ,matajiri na wenye vipato vikubwa wanaishi nje ya zanzibar na tanzania kwa ujumla.
3.Sasa imekuwa faradhi kwa viongozi ,matajiri na wenye vipato vikubwa wake zao huwa wanawapeleka nchi za ulaya au bara la marekani kujifungua ili watoto wao wawe na uraia wa nje kisha huwafanyia vyeti vya kuzaliwa zanzibar kama wamezaliwa hapa.

1Viongozi na matajiri feki kwa njia ya halali au haramu wote ambao wana kipato wamefungua akaunti za siri katika mabenki ya nje ili kujiwekea akiba pindipo ikitokezea fukunyuku yoyote wao wakapete nchi za nje na sio kama fedha zao zitabakia nchini ili ziweze kuzunguka na kuwafaidisha wananchi wa chini wakati wao hawapotezi chochote katika kuzizungusha huko.
Wako wenye akaunti nchi za ulaya ,arabuni ,india ,marekani na wengine japo kenya.
Nchi huwa inakumbazika kila siku kwani fedha hizo ingelikuwa zinawekwa katika mabenki ya hapa kwetu basi zingeliweza kufaidisha wale wenye kuchukua mikopo na kisha kuzirudisha baada ya kupata au kufanyia faida na umasikini utaweza kupungua kwa kiasi kikubwa.
Wengine wanaiba tu na kuweka nje lakini hata hawajui ni kiasi gani wameshaweka mpaka sasa.wengine wamewapa watu kuwawekea fedha hizo nje na kweli zimehifadhiwa katika benki lakini yeye mwenyewe hawasiliani na aliemkabidhi mpaka mkabidhiwa amtafute na kumjulisha kuhusu akaunti yake(jinsi walivyo wajinga wa kujua kadhia hii)wanazo mamilioni ya fedha lakini hakiwafai wao nawazalendo wenzao pia nchini ila zinawafaa watu wa njeeeeee.
Wengine fedha zao za nje wanatumia na mahawara zao lakini wake zao wa halali hawafaidiki kitu.
Wengine fedha zao wamezihifadhi akaunti ya siri hata watoto zao walio nje hawafaidiki nazo kwa masomo au kwa njia nyengine yoyote.
Wengine akaunti zao kutokana na za siri sana kufa kwao zitapotea kwani hakuna katika familia zao wanaojua kama baba yao au mume wake anayo akaunti nje.

2.watoto wa viongozi na wenye uezo wanaoishi nje ya zanzibar au tanzania kwa ujumla.
Asilimia kubwa ya viongozi wetu wa zanzibar ikiwa wazee wa chama ,wawakilishi ,wabunge na wenye vipato wanakula kidedea nje ya zanzibar au afrika .
Waliwasafirisha ati wanakwenda kutembea nao marekani,uingereza na nchi za ulaya tahamaki wamerudi wao tu watoto wamewabakisha huko.Asilimia zaidi ya 80 watoto wa viongozi hao wanaishi nje,sasa kama muungano mzuri au nchi ina amani na utulivu ni kwa nini watoto wenu hawaishi hapa kwenye amani na utulivu?Tena si hivyo tu wanakwenda nje na kuisaliti zanzibari yetu kwamba wanabughudhiwa na huku baba au mama yake ni mwakilishi au mbunge? Ama wale walala hoi wanastahiki kwani ni kweli wanabughudhiwa lakini wewe umo ndani ya baraza la wawakilishi kisha mwanao anaishi nje kwa kigezo cha ukimbizi tena umemsafirisha mguu kwa mguu kama si dhambi za kupindukia ni nini?

3.Sasa imekuwa faradhi kwa viongozi,matajiri na wenye vipate wastani kuwapeleka wake zao nchi za nje kama uingereza marekani na canada kwenda kujifungua ati watoto wao wapate uraia wa nchi hizo tena kwa gharama zozote zile kisha huwatengenezea waliozaliwa nje vyeti vya kuzaliwa kama kwamba wamezaliwa muembe ladu ,manazi mmoja,au nyumbani,hii imekuwa faradhi kwao.
Kisha CCM JUU ,CUF JUU na kudanganya wananchi.
Muulize muakilishi ana watoto wangapi?atakuambia wangapi mwambie leo nataka kuwaona basi bahati kama uwaweza kuwaona ikiwa anao sita waliopindukia miaka kumi na tano hatokuepo hata mmoja labda wawe chini ya umri huo.
Hii ndio zanzibari yetu kama hujui waulize wenzio.

Share: