Habari

Kama Wangenisikiliza Nigewambia (Muamsho) Mihadhara Waliotoa Imetosha

Assalamu Alaikhum warahmatullah wabarakatuhu ndugu Wazanzibari wote wa kike na kiume na wa ndani au nje ya Nchi yetu adhimu. Ama sina budi ila kuchukua nafasi hii kumshukuru (Allah) Muumba wa mbingu na ardhi na kunipa uzima wa afya na akili timamu. Yakuweza kutafuta rizki za halali na kumubudu yeye Muumba wa Mbingu na ardhi.

Kabla sijawapeleka wasomaji kwa Mungu au kuwachosha, kusoma nataka nichukue nafasi hii niwaonye  au kwa lugha nyengine (waombe) nduguzetu wa MUAMSHO. Kwamba Mihadhara walioitoa yote imefika katika vijiji na miji ya Maziwa Makuu ya Nyasaland, seuze Visiwani?Wazanzibari wote wameshapata Ujumbe wao. Hivyo haina haja tena yakuendelea kutoa mihadhara hiyo, haswa kwavile  Kuna WAKURYA Wanatamani DAMU za Wazanzibari hao.

Pili Watu wote Wameshafahamu juu ya Uzalendo wao, Elimu zao za Dini na Dunia. Na jinsi gani Muislamu anatakiwa ailinde Nchi yake kwa vitendo, maneno au kuchukia. Tukumbuke kama familia bila ya Baba au Mama haiwi familia, hivyo Usalama wao (Muamsho) ni muhimu kwao wenyewe na familia zao.

Najua kuna watu wanaona bora Akhera kuliko kuishi Zanzibar ukatawaliwa na mtu ambae  ana chuki na jamii fulani au nchi fulani. Na hivi ndivyo ulivokua utawala huu wa Serikali ya Tanzania/ Tanganyika kwamba wanakejili, dharau na ubaguzi juu ya wazanzibari.  Kuna viongozi wengi  Wakristo au nchi nyingi World-Wide tokea September 11 wamejawa na chuki juu ya maendeleo ya Waislamu na nchi zao. Lakini tunatakiwa tutumie Hekma, tujenge hoja ikiwa na mifanopamoja  na imani yetu ya kile tunachokidai kama tutakipata ndio tutaweza kuondoa udhalimu huu.

Mimi kama Active Member wa AMNEST International nimeona reporti nyingi sana juu ya shutuma za waislamu kubaguliwa. Lakini hili lisitufanmye Wazanzibari tukawa Ma-Foundementalistic. Zanzibar ni visiwa ambavyo vimechanganya Dini na ni Cosmopolitern Culture.  Tuna Nduguzetu  Wahindi W Magoa na kabila nyengine amabao wamezaliwa hapa karne na karne na wanadini nyengine. Hivyo tunaposimama kudai haki zetu nilazima tudai kama Wazanzibari wamoja. Na sio U-muslim au u- kristo na u-pagurn.

Nachukua nafasi hii vile vile, kukumbusha tu (mimi) au Wazanzibari wengi hawako tuyari kuikosa AMANi na Utulivu tuluionayo sasa. Sio kwamba na maanisha MUAMSHO  ndio wavunjaji wa Amani? Laa hasha.

Wavunjaji wa Amani ni Vyombo vya Dola ambavyo vimekua Vinuka Damu za Wazanzibari.  Wazanzibari hatuna Alie yoyote wala hatuwezi kupigana na Wakurya waliokaribishwa na Viongozi wetu wa CCM SMZ.  Hivo tujaribu kutafakari kabala hayajatufika tena  (allah atuepushe mbali Amin.)

Fikra zangu zinanambia Pindipo Muamsho wataendelea NA MIHADHARA INAWEZA KUHATARISHA MAISHA YAO NA YA WATU WENGINE NA TUKAKOSA YALE AMBAYO TUMEYAKUSUDIA.  Na kwavile Population yetu ni ndogo kitu kidogo tu kinaweza kuathiri mpango mzima na kupungua idadi hiyo, hapo itajazwa na hao hao tunaowakataa. Vile vile Serikali ya Tanganyika so call (Muungano) ndio itapata sababu yakusema wamezima fujo hilo kwasababu za UDINI, kumbe ni uongo mtupu.

Wazalendo tutizame mifano hii ni mikutano Mingapi imefanyika na wala Redio za Tanganyika hazijatangaza? Hii nikwasababu wao wanalolitaka ni Muungano kudumu milele na Zanzibar kupotea. Si tumeona ile kesi ya Nduguyetu aliambaiwa aliisaidia Al- aqaida? Tuinunue Amani Umoja na Utulivu kwa Bei yoyote ile Zanzibar.Na kwavile MUAMSHO yetu ni Vikundi vya Dini inaweza ikafahamika hivyo.

Hivyo tunatakiwa Wazanzibari wote tuliojumuika na Muamsho tuache Jazba na kuwakejeli watu wengine ambao wana Mawazo tofauti na sisi au wana dini tofauti. Na badala yake tupeleke madai ya hoja za Kimaendeleo za kiuchumi, kijamii na utamaduni wetu ili tuwafunge wale wanaokataa kama Zanzibar inanyimwa hakki za Uchumi. Wanaotufikiria sisi ni Islamic Foundemetalisim they will prove wrong.

Tuchukue Misemo ya wazee wetu “Hala Hala Mti na Macho”. Hatuko tayari kuwaona baadhi ya Viongozi wa Muamshio wanaishia Jela au wanamwaga damu zao kwa so calll Katiba. Nilazima tutumie Imani ya Dini yetu, ustaarabu na tuende nao sambamba. At the end of the day we would archiave what we want to.

Waswahili Wasema ” Uji Moto Hupembwa kwa Ncha ya Ulimi”.

Na sisi tujaribu kuchukua mifano hii na kuitumia kwa vitendo hadi tufike pale tunapotaka.Wazanzibari  tukumbuke kwamba hatuwezi kupata kila kitu kwa wakati mmoja. Mambo huenda Aste aste (pole pole). Kuna faida gani yakuomba hakki yako na kupoteza Damu au kuhatarisha Amani ya nchi yako Uipendayo?Na baadae ukakosa Hakki ile unayoidai kwa muda mrefu, na ile fursa Ndogo Uliokua nayo ukanyanganywa kabisa kabisa?

Viongozi wa CCM wanatumiliwa na Tanganyika kuchafua Amani ya zanzibar kwa ku waprovock Wazanzibari na madai yao.Na sasa wanatafuta sababu tu kuvunja Amani na Umoja kwa Visingizio vya Sheria. Kwanini tusijenge hoja MOJA tu kama Wazanzibari  na tukaitumia hii Amani na Utulivu tulionao ikatufikisha Hoja yetu  kule tunakotaka?

Kwanini tusitumie Umoja wetu tukawa na sauti moja na Mataifa yakatusikia kwa mifano na Vielelezo vya Maendeleo baina yetu na hiyo Nchi tunayoambiwa Tumeungana nayo? Hivyo tunatakiwa ndugu Wazanzibari tuendelee kuwa wastahamilivu na tuwe na kauli moja tu ya lile tunaloamini kwamba tukilidai linaweza kupatikana bila ya Vita wala kupoteza Amani, Umoja na Heshima ya Nchi yetu. Jambo hilo sio jengine ila kuwe na Muungano wa Mkataba kama ilivyo EU countries.

Ni kweli Muungano ni Batil, lakini tumeshika Makali na wao wameshika Mpini. Ni Kweli Muungano unatudhulumu juu ya Maendeleo ya Kijamii, Uchumi na culture data tunazo. Lakini Wenyewe tuliridhia kwani ni sisi Wazanzibari ndio tunawachagua Viongozi wasiokua na Vission na kuwakataa Vingozi waliokua na Elimu kwasababu ya Ubaguzi wa mtu anakotoka. Muungano wa Mkataba liwe chaguo letu tutakapokataliwa kura ya Maoni.

Hili linaweza kuthaminiwa na hata Mataifa ya Nje kuliko kuonyesha chuki za kidini na kuhubiri Islamic Government. Kwanini ulilonalo hulihifadhi kwanza.

Samahanini kama nitawakera wasomaji au kwa maandishi mengi.

Mungu Ibariki Zanzibar na Utulinde Amin.

Wabilahi Taufiq

Share: