Habari

Kamati Maalum CCM Zanzibar yateua wakuu wapya wa Idara

WAJUMBE wa Kamati maalum ya halmashauri kuu ya CCM Zanzibar iliyokutana chini ya Mwenyekiti wake Dk. Ali Mohamed Shein imeteua na kupitisha majina ya wajumbe wa sekretarieti na Kamati ya maadili ya chama hicho itakayodumu kwa miaka mitano ijayo.

Akito taarifa kwa waandishi wa habari, naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Abdallah Juma Sadallah ‘Mabodi’ amewataja wajumbe hao ambao pia watakuwa ni wakuu wa Idara ni pamoja na aliyewahi kuwa Katibu wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja na alikuwa ni Afisa wa Idara ya Organazesheni Catherine Peter nao alieteuliwa kuwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar.

Dk. Mabodi amewataja wajumbe wengine kuwa ni Bakari Hamad Khamis anaekuwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Oganaizesheni,Kombo Hassan Juma kuwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Afadhali Taibu Afadhali anaekuwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Fedha na Uchumi Zanzibar.

Kikao hicho pia kimeridhia majina ya wajumbe wa kamati ya maadili ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar itakayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali mohamed Shein, naibu katibu mkuu wa ccm Zanzibar Dk. Abdallah juma sadallah ambae ni katibu wa kamati hiyo.

Wajumbe katika kamati hiyo ni pamoja na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi, mjumbe wa sekretarieti Kombo Hassan Juma, Yasmin Aloo na Ramadhan Shaib Juma ambao pia ni wajumbe wa halmashauri kuu na Kamati Maalum ya CCM.

Aidha Dk. MABODI alieleza kuwa kikao hicho kimepokea taarifa ya mwelekeo wa chama kwa kipindi cha miaka 10 ijyo na kuwahimiza wajumbe wa mkutano huo na vingozi wengine wa chama kusimamia utekelezaji wa ilani ya ccm katika maeneo yao ya utendaji.

Kikao hicho ni cha kwanza toka kukamilika kwa chaguzi za ngazi mbali mbali za uongozi ndani ya chama uliofanyika mwaka uliopita ambao uliwachagua Mwenyekiti wa ccm taifa dk. John pombe magufuli na makamu wenyeviti wa chama hicho Tanzania Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Tanzania bara Philp Japhet Mangula.

Zanzinews

Share: