Habari

KAMPENI YA VIJANA NI WAKATI WETU YAZINDULIWA RASMI PANGANI

Na Fatma Ally

KAMPENI YA VIJANA NI WAKATI WETU YAZINDULIWA RASMI PANGANI.

KAMPENI ya (Vijana ni Wakati Wetu) Pangani kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani akishirikiana na Ofisi ya Mbunge na Halmashauri leo imezinduliwa rasmi katika viwanja vya Bomani ambapo mwitikio umekua mkubwa sana kwa vijana wengi kuweza kujitokeza.

Aidha katika kampeni hiyo,Mkuu wa Wilaya hiyo, Zainab Abdallah alidhamiria kukutana, kuhamasisha, kuzungumza, kutambuana na vijana wote wa Pangani kwa lengo la kuwasapoti na kuwaleta pamoja ambapo kwa kutumia kanzi data wataweza kujua idadi hali ya Vijana wasio kuwa na kazi.

“Tumeamua kuwasapoti kuandaa mipango ya miradi, kuwapa uwezeshi wa miundombinu ikiwemo kutumia asilimia za vijana ambayo ni haki yao, kurudisha karakana zilizokufa, kuwapa sapoti kuwaunganisha na miradi ya halmashauri, ufuatialiaji na usimamizi chini ya Idara ya Vijana ” amesema DC Zainab.

Ameongeza kuwa, Vijana ambao wameshapiga hatua wametambuliwa na kua mfano kwa wengine ambao hawajaanza kabisa, huku akidai wao kama viongozi bila kutambua hatma ya vijana ambao hawana kazi.

“Hii ni awamu ya kwanza ya program hii, awamu ya pili itaambatana na kuwatengenezea mazingira wezeshi na mafunzo rasmi kulingana na malengo yao, na kwa awamu ya tatu tutakamilisha kwa kuhakikisha hakuna kijana ambae atakaa mitaani hana shughuli maalum ya kufanya ” amesema

Kampeni hii imezinduliwa na Mkuu wa Wilaya leo 03 Sept 2018 na itahitimishwa 06 Sept.2018 na itapita Tarafa zote 4 za Pangani kuanzia Pangani Mjini tarehe 3 kuelekea Mwera Tarehe 4 Madanga tarehe 5 na itamalizia Mkwaja Tarehe 6 Sept.2018.

Share: