Habari

Kampuni ya Rafiki Network matatani kwa wakimbiza upepo Pemba

July 29, 2018 – by Manager

Imeandikwa na Mwandishi wetu, PEMBA

WAKIMBIAJI wa mbio za Marthoni kisiwani Pemba, wamesikitishwa na maandalizi hafifu yaliyofanywa na kampuni ya Rafiki Network, katika mashindano ya mbio hizo zilizoanzia Konde hadi Chakechake.

Wakiambiaji hao ambao walishika nafasi ya kwanza katika mbio refu za kilomita 42 na mbio fupi zilizoanzia Konde hadi Madenjani, wamesema kuwa kampuni hiyo mara nyengine inapatoka kuandaa mbio hizo inapaswa kutafuta ushauri kwa wanamichezo husika ambao wanaoshiriki.

Beatus Stevin ambaye aliibuka mshindi wa kanza katika mbizo refu zilioanzia Konde hadi Gombani za Kilomita 42, alisema hakufurahishwa na maandalizi ya mbizo hizo, hali ambayo imepelekea kuhatarisha maisha ya wakimbiaji.

“Kampuni ilipaswa kutoa ‘skoti’ kuanzia mtu wa kwanza hadi wa mwisho, hata kwa wale ambao pia wako katikatika lazima iweze kuwaskoti, lakini leo imeweza kuwaskoti mtu wa kwanza hadi wa nne, waliobakia hawakuwa na ulinzi kama mtu atagongwa au kuanguka njiani wao watajuaje,”alihoji.

Alisema kushiriki katika mashindano hayo kwa Pemba ndio mara yake ya kwanza, huku suala la mazoezi ndio lililoweza kumsaidia kuibuka na ushindi.

“Mazoezi ndio kitu pekee cha kuhakikisha unaweza kufanya vizuri, ikizingatiwa michezo ni afya ambao humjenga mkimbiaji kuwa na hali nzuri na kuondokana na maradhi nyemelezi,”alisema.

Philipo Jacob Mambo ambaye ni mshindi wa kwanza katika mbio fupi, zilizoanzia Konde hadi Madenjani, aliwataka waandaaji kujipanga kikamilifu, kama wanataka kufanya mashindano hayo.

Alisema lengo la mashindano hayo ni kukuza na kuinua sekta ya utalii, lakini yameweza kukosa hamasa pamoja na wawekezaji aktika utoaji wa zawadi kwa washiriki.

“Mimi nimeweza kushiriki mashindano mbali mbali, yakiwemo yale ya dunia yaliyofanyika Uengereza mwaka 2002 na kushika nafasi ya 42, Uholanzi, Duabai, Jamaica, lakini mkimbiaji anafuatwa mwanzo hadi mwisho,”alisema.

Mshindi wa kwanza upande wa wanawake mbio refu za kilomita 42 kutoka Konde hadi Gombani, Upande wa wanawake Adelima Traseas alisema hakuna mashindano ya Marathona ambayo wanawake wanaweza kushindana na wanaume duniani kote.

Alisema kitendo kilichofanywa na Rafiki Network ni jambo la ajabu sana, kuwachanganya wanawake na wanaume katika mashindano hayo, hata ikiwemo katika utoaji wa zawad.

Alisema zawadi ya mshindi wa kwanza mwanaume na mashindi wa kwanza wa kike ni sawa sawa kitu ambacho kimemshangaza sana kuona mshindi wa kike mpaka kufikiriwa.

“Mimi nimeshiriki mashindano mengi duniani hichi walichokifanya wao ni kitu cha ajabu kabisha, mashindano yoyote yanayofanyika wanawake wanawekewa zawadi zao kwa kuwa hawaweze kushindana na wanaume, leo wao wanasema ati hawakuwa na utaratibu huo, kwanini wakataka sisi wanawake tushiriki”alisema.

Kwa upande wake Afisa habari wa Rafiki Netwark Kisiwani Pemba, Ali Othman alisema hawakuwa na uwelewa huo kama mwanamke anatengewa upande wake na zawadi zake katika marathano.

Alisema changamoto zilizojitokeza watahakikisha mwaka ujao hazitokei tena, ili kufikia lengo lao la kuazishwa kwa mbio hizo za marathoni.

Pembatoday

Share: