Habari

Kangi Lugola: Sharubu na ndevu ndio ishara za ujana dume

Jaribu nawe kufuga ndevu.

Bahati ya kusikiliza clip ya video ya Waziri wa Mambo ya ndani, Bw Kangi Lugola iliyoitowa hapo jana.

Bw Kangi Lugola ametishwa na sharubu pamoja na ndevu zake kiasi ya kushindwa kuzuwia povu mdomoni mwake. Hii ni kutokana na uwoga wake kwa ndevu na sharubu.

Turudi nyuma kidogo, mwanzoni baada ya kuteuliwa kushika nafasi hii, Bw Lugola alikuwa akitembea na ilani ya CCM mkononi kama vile kavikwa hirinzi mikononi mwake. Jana Bw Lugola anazungumza bila ya kuwa na hirinzi hiyo.

Baadae Bw Lugola alianza kuvaa mashati na masuti yenye bendera mifukoni, mikononi, mabegani, nk. Jana kashindwa au kasahau kuyavaa.

Hivi kulikoni kwa Lugola, mtu aliyekuwa na style mpya leo ghafla bin vup zinabadilaka. Au ni woga wake juu ya ndevu na sharubu.

Time itatwambia kama Lugola alikuwa yuko Sawa siku ya jana, kwanza kilicho mleta Zanzibar kitajulikanwa, pili maneno yake aliyosema yatapambanuka. Sidhani kama katika muda wake wote ameshawahi kufika Zanzibar.

Labda aambiwe Lugola “This is Zanzibar, you will never walk alone”. Kwamba kama huijuwi Zanzibar ndio mara yake ya mwanzo, unapofika Zanzibar hutokwenda peke yako.

Zanzibar ni nchi nyengine, usishangae yote uliyosema yakakurudia mwenyewe. Majini yetu hata ujifiche wapi yatakufika na yatatekeleza maagizo, kaa ukijuwa. Huwezi kuletea fitna au kuwatisha Wazanzibar wanayo madai yao.

Kwa vile Una nguvu zote ni wakati wa kutumia nguvu hizo. Hakuna sababu ya kuomboleza. Wangapi wamepita Waziri wa Mambo ya ndani na bado Zanzibar na Wazanzibar wanaendelea na marai Yao.

Ishara ya udume ni kufuga ndevu, Lugola anza sasa nawe kufuga ndevu ili watu waanza kukuogopa

Share: