Habari

Kangi Lugola: Wanaotaka kuleta vurugu Zanzibar watakamatwa kama Kuku

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuwa kuna watu wamejipanga kuvuruga amani ya Zanzibar na kuvuruga amani ya Tanzania watakamatwa mmoja mmoja kama Kuku.

Waziri Lugola amesema kuna watu ambao wanaamini kuwa ni Vyama vya Siasa kumbe ni magenge ya wanasiasa.

“Kuna watu wamejipanga kuvuruga amani ya Zanzibar kuvuruga amani ya Tanzania, lazima tuwaambie kuwa hiyo mipango waliyoipanga watakamatwa mmoja baada ya mwingine kama kuku kabla mipango yao haijatekelezwa,” alisema Kangi akiwa Zanzibar.

“Kuna watu ambao sisi tunaamini kwamba vi Vyama vya siasa kumbe ni magenge ya Wanasiasa ambao wanapanga mipango ya kukaidi na kufanya mikutano ya hadhara ambayo imezuiwa nirudie kufanya mikutano ya hadhara ikiwemo maandamano ilhali imekatazwa ili wananchi kufanya shughuli za kimaendeleo wameanza kuonekana kule maeneo fulani fulani kule Pemba.”

Jamii Forums

Share: