Habari

Karume boys yazidi kusomba vigogo

May 31, 2018

Makamu wa rais ajiuzulu

NA AMEIR KHALID

SIKU chache baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha soka Zanzibar ZFA Abdulghani Msoma, hatimae Makamu wa rais Unguja Mzee Zam Ali naye amebwaga manyanga.

Katibu Mkuu wa chama chicho Mohammed Ali Hilali (Tedy) amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa kiongozi huyo, kufuatia sakata la timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana (Karume Boys) kuodoshwa katika mashindano ya CECAFA yaliyofanyika nchini Burundi Mwaka huu.

Tedy alisema Mzee Zam amewasilisha barua hiyo mapema juzi huku akikiri kupokea taarifa kutoka kwa CECAFA, inayofafanua kuhusu umri wa mashindano ambapo amewaomba msamaha kwa kusema alipitikiwa.

Alisema kweli walipokea ufafanuzi wa umri kutoka CECAFA kupitia ‘email’ ya Mzee Zam na mwenyewe alikiri huku akisema alisahau, hivyo kutokana na kadhia hiyo ameamua kuomba kujiuzulu.

Zanzibar iliondolewa katika mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo walikwenda kinyume na kanuni ya Mashindano.

Kutokana na makosa hayo Karume boys imepewa adhabu tatu ikiwemo kuondolewa mashindanoni, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa kulipwa na Chama cha Soka la Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia gharama za tiketi, malazi na chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa Burundi.

Zanzibarleo

Share: