Habari

Karume: Hatuna mamlaka kuivunja ZFA

May 29, 2018

NA MARYAM HASSAN

WIZARA ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imesema haina mamlaka ya kukivunja Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kutokana na kupeleka wachezaji nchini Burundi ambao hawakuwa na sifa za kushiriki mashindano ya Challenge kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17.

Kutokana na hali hiyo, Balozi Ali Karume, aliwataka viongozi wa chama hicho kujitathmini kwa kufanya marekebisho ya tatizo hilo na kuhakikisha halijirejei tena.

Akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wakilishi, alisema timu hiyo iliondolewa kwenye mashindano kwa kosa la kanuni na miongozo ya mashindano ambapo kila nchi shiriki ilitakiwa kwenda na wachezaji amabo wamezaliwa kuanzia 2002.

Alisema katika hatua hiyo ZFA, iliadhibiwa kutoshiki michecho yote ambayo itaratibiwa na CECAFA pamoja na kulipa dola za Marekani 15,000.

Aidha Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lulu Msham Abdalla, alisema uchunguzi unaonesha makosa yapo kwa ZFA na kueleza kuwa kabla ya mashindano hayo uongozi huo ulipatiwa barua ya kuonesha umri sahihi.

Alisema barua hiyo, imeonesha kuwa vijana wanaotakiwa kushiriki mashindano hayo ni vijana waliozaliwa 2002 na vijana waliozaliwa mwaka 2001.

Akizungumzia hati miliki, aliwaomba wawakilishi kuwafikisha waimbaji wa zamani katika ofisi husika ili kupata haki zao.

Zanzibarleo

Share: