Habari

Kashfa ya pembe za Ndovu China/TZ zakanusha wauzaji wathibitisha

Tanzania elephant population from 1976 to 2013

Waziri wa Mambo ya Nje Benard Membe amekanusha vikali shutma zinazoikabili serikali ya Tanzania na China kuwa imejihusisha na biashara haramu ya Pembe za Ndovu.
Waziri huyo akithibitisha Bungeni amesema kwamba ”Ninapenda kupitia Bunge lako tukufu kuutaarifu umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kwamba madai yaliyotolewa na NGO hiyo ya Marekani ya kuihusisha ziara ya kihistoria ya Rais wa China kutembelea Tanzania kama nchi ya kwanza toka aingie madarakani na biashara ya pembe za ndovu hayana ukweli wowote. Vilevile, madai ya kwamba Serikali ya Tanzania haijali na wala haichukui hatua dhidi ya wanaojishughulisha na biashara haramu ya pembe za ndovu sio kweli. Taarifa za EIA ni za kupikwa na kuungwa kuungwa ili kuchafua heshima ya nchi yetu, pamoja na kuchafua heshima ya rafiki zetu Taifa la China. Ni taarifa iliyoandaliwa na kutolewa wakati huu ili kukidhi ajenda mahususi ambayo tunaifahamu fika.

Hata hivo kwa mujibu wa shirika la kuchunguza biashara haramu za wanyama pori EIA lenye makao yake makuu nchini Uingereza katika ripoti yake limethibitisha kuwa Tanzania imekuwa ikipoteza Ndovu kwa kasi kuliko nchi yoyote ya Africa ,Tembo wa Tanzania wanakadiriwa kufikia 17,000 kutoka 70,000 tokea mwaka 2006 hadi 2013.

Wandishi maalum (undercover agency) wamethibitisha biashara hiyo inayohusisha viongozi wa juu wa nchi mbili hizi baada ya kuongea na wauzaji watatu waliohusika na biashara hizo za ndovu .

Wachunguzi hao wakiongea na Mmiliki wa Kampuni ya usafirishaji Bwana Suleiman Mochiwa, na Bwana. Paulo Gavana Ambae ni muuzaji wa bidhaa hizo walisema kuwa ” Bei ya Meno ya Ndovu hupanda kufikia kilo kwa Dola 700 za kimarekani viongozi hao wanapokuja.

Mfanya biashara mwengine wa tatu ambae hakutaka jina lake litajwe amesema ziara ya Bwana Hu Jintao ambae alikuwa rais wa China kutoka mwaka 2002 hadi 2012 alipotembelea Tanzania na ujumbe mkubwa ulisababisha biashara hiyo kupanda tena zaidi kama ilivopanda hivi karibuni alipotembelea tena Tanzania.

” Wanakuja kuchukua vitu vingi tu ” aliendelea kusema “lakini si vya Hu Jintao tu peke yake,bali ujumbe mzima,kisha huenda moja kwa moja Uwanja wa ndege kwa vile VIP huchekiwi basi hutumia njia hiyo kusafirisha bidhaa hizo.”

(chanzo The guardian UK,Michuzi TZ)

Share: