Habari

Katiba Mpya: Kisheria, Kura ya Maoni Haitaweza Kufanyika Tena: JF

Katiba Mpya: Kisheria, Kura ya Maoni Haitaweza Kufanyika Tena
Sheria ya kura ya maoni (No. 3 /2014 ambayo ilianza kutumika tarehe 3/10/2014) inaweka masharti ya mambo ya lazima kufanyika katika mchakato wa kura ya maoni ambayo hayajafanyika hivyo kura ya maoni haitaweza kufanyika tena. Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo:-

(a) Kifungu cha 4(2)(c) kinampa mamlaka Rais kutangangazi kipindi cha kura ya maoni “period”.

Kifungu cha 5(1)(c) kinaipa Tume ya Uchaguzi mamlaka ya kutangaza tarehe ya kufanyika kura ya maoni. Cha ajabu kupitia tangazo la serikali No. 42 Rais ametangaza tarehe ya kura ya maoni badala ya “period” na Tume ya Uchaguzi bado haijatimiza matakwa ya kifungu cha 5(1)(c). Hivyo kisheria tarehe ya kura ya maoni haijawahi kutangazwa. Sheria inasema jambo analofanya mtu litakuwa na nguvu ya kisheria tu kama sheria inampa mamlaka mtu huyo ya kufanya jambo hilo. Sheria imempa mamlaka ya kutangaza tarehe ya kura ya maoni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na wala si Rais hivyo kwa kuwa mamlaka yametekelezwa na mtu asiye na uhalali wa kisheria, tarehe haijawahi kutangazwa.

(b) Tume ilipaswa kutoa elimu kwa umma kwa siku 60 kuanzia siku katiba inayopendekezwa ilipotangazwa. Katiba inayopendekezwa ilitangazwa kupitia tangazo la serikali No 382 tarehe 10/10/2014. Elimu kwa umma ilipaswa ianze tarehe 10/10/2014 hadi tarehe 10/12/2014. Kifungu hiki kinatumia neno “shall” , kwa kuwa haijafanyika inabatilisha zoezi zima la kura ya maoni. (c) Ibara ya 132 (2) ya Katiba ya Zanzibar inasema sheria iliyopitishwa na Bunge la Muungano haitaanza kutumika Zanzibar hadi iwasilishe katika Baraza la Wawakilishi. Sheria ya kura ya maoni haijawasilishwa Baraza la Wawakilishi hivyo “by-laws” zote zilizotolewa chini ya sheria hiyo kama vile swali la kura ya maoni, tarehe ya kura ya maoni nk havina nguvu ya kisheria Zanzibar na hivyo kisheria havijawahi kufanyika Zanzibar. Kwa kuwa Zanzibar ni moja ya muhimili wa kura ya maoni bila wao kushirikishwa hakuna kinachoiweza kufanyika. Hivyo kwa ujumla wake kura ya maoni haiwezi kufanyika tena maana sheria haijazingatiwa. Ikumbukwe kwamba kubadilisha sheria hii inahitaji 2/3 ya Zanzibar ambayo bila CUF haiwezi kupatikana.

Nilikuwa nahojiwa na Mlimani TV nilishauri na naomba nishauri tena ni vema Serikali ikatangaza kuwa kura ya maoni imeahirishwa hadi baada ya uchaguzi. Kuendelela na mchakato ni kupoteza bure fedha za walipa kodi kwani wazalendo wa nchi hii tutaenda mahakamani na hakika Mahakama itabatilisha zoezi zima maana halijazingatia sheria.

****************************** ****************************** *************
Kwa nyongeza UKAWA wana haki ya kugomea hili zoezi kwani ukiisoma sheria ya kura ya maoni utagundua serikali imepania kuipitisha hata kutumia nguvu. Hebu wanasheria tujadili maana ya section 34 (2) of the Referendum Act, 2013, thus,

34(2) For the purposes of subsection (1)(b), the votes to be counted for Zanzibar shall include:

(a) Votes of persons registered in the Zanzibar Electoral Commission register; and
(b) votes of persons residing in Zanzibar or Tanzania Mainland and registered under the National Electoral Commission register.

Note: The word “person” has not been defined by the Act.

Kwa tafsiri ni kwamba kura zitakazohesabika kuwa ni za Zanzibar ni zile kura za watu waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura la Tume ya Uchaguzi Zanzibar na pia kura za watu wanaoishi Zanzibar au Tanzania Bara ambao wameandikishwa katika daftari la Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa sheria ilivyo mtu yeyote wa Tanzania Bara anayeishi Zanzibar kura yake itahesabika kuwa ni ya Zanzibar lakini pia mtu yeyote anayeishi Tanzania bara hata kama si Mzanzibai kura yake itahesabika ni ya Zanzibar.

Sidhani kama ofisi ya AG iliyo na wataalam kibao wameshindwa kuona kuwa ” the law would lead to absurdity”. Nadhani wameweka kwa makusudi ili ikishindwa kupata 50+ 1 Zanzibar wakitumie kipengele hiki kuipitisha.

Again we have section 37 ambayo nayo inatia mashaka ya uchakachuaji.

37. The Commission may make special provisions for voting a referendum for voters who would not be able to vote on the voting day because of essential duties, being away for social and economic reasons, patients in hospitals, persons admitted at homes for the aged and similar institutions…………and expectant mothers.

Hiki kipengele kina maana kwamba watu hawa wanaweza kupiga kura siku zinazofuata baada ya kujua matokeo(who would not be able to vote on the voting day). Kuna uwezekano wa kuokoteza watu huko ili kupata nusu ya kura.

Kwa wale wanaounga mkono kura ya maoni wazingatie udhaifu wote huu wa kisheria watuambie kama kweli tunaweza kupata katiba halali kisheria

Naomba kuwasilisha
Onesmo Kyauke (Shule ya Sheria-Udsm)

Share: