Habari

Kauli inayodaiwa kumponza Diwani

MAY 31, 2018 BY ZANZIBARIYETU

Mwakilishi wa Jangombe juzi alivuliwa uanachama na kikao cha juu ya maamuzi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kwenda kinyume a maadili na miiko ya chama hicho, hapa nimewatumia Hansad ya kikao cha Saba cha tarehe 5/10/17 cha kujadili ripoti ya utekelezaji ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Utekelezaji wa Maagizo ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo kwa Mwaka 2016/2017. ambacho pamoja na mambo mengine inadaiwa kauli aliyoitoa barazani kuwa ndio chimbuko la ukosefu wake wa maadili na miiiko ya chama. bila ya shaka msomaji utapenda kujua kaongea nini huko nakuletea taarifa nzima lakini kwenye ukurasa wa 52 hadi 56 ndio kuna kadhia nzima ya majadiliano yake na baadhi ya wajumbe wenzake.

Hiki ndio kidokezo kidogo

Kwa kweli, hatugombi serikali isipokuwa sisi tunataka kusimamia Ilani ya Chama chetu kusimamia serikali yetu na ifanye kazi kwa umakini, ili kuturahisishia katika Uchaguzi 2020 kupata ushindi wa kishindo. Lakini kwa muelekeo huu mnarudisha kule kupata shida tena mpaka Bwana Jecha atuonee huruma.

Mhe. Mwenyekiti, nikiendelea mbele katika agizo nam. 4. Wizara inaendelea kutafuta muekezaji kwa ajili ya kuanzisha viwanda kuzalisha pembejeo za kilimo na mifugo tulikuwa na ZAPOCO hapa kuna kiwanda kinazalisha chakula cha kuku kiko wapi. Kwanini kimekufa. Sasa leo hii nashukuru kuna viwanda vidogo vidogo tu vya wananchi wenyewe wanazalisha Mhe. Mwenyekiti kama havijui Mhe. Waziri hivyo vipo kama vile Amani pale pana viwanda vinazalisha leo hii tunasema kwamba …

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum):

Mhe. Mwenyekiti, kwa ruhusa yako naomba Mhe. Mjumbe afute kauli yake, sisi hatujaonewa huruma na Jecha.

Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf: Mhe. Mwenyekiti, afuate utaratibu na ataje Kanuni…

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Mhe. Mwenyekiti, sisi hatujaonewa huruma na Jecha. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alishinda kwa asilimia 91. Afute kauli hiyo Zanzibar iliingia katika uchaguzi Zanzibar …(Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri,

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Naam Mhe.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri umesimama lakini hujanambia Kanuni gani imetumia kwa hiyo unasema….

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Kanuni ya 68 na kama siyo tafuta Kanuni wewe Mwenyekiti kakosea huyo..

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri….

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Serikali haijaonewa huruma hapa.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri, mimi nilikuwa nakusikiliza, lakini na Waheshimiwa Wajumbe wengine nao wamewasha microphones wanasema. Kwa hiyo, nilikawa nashindwa nifanye maamuzi gani. Kwa maana hiyo, nilikuwa nakusikiliza umesimama nimekuruhusu kuhusu utaratibu sikusikia umesema hivyo na umesema kwa Kanuni ya 68 nimekusikia sasa subiri nitoe mimi maamuzi.

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Ndio Mhe. Mwenyekiti ahsante.

54

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri, ndio maana nikakuuliza kwa Kanuni ya ngapi, taratibu gani aliovunjwa, ili tumwambie Mjumbe.

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Mhe. Mwenyekiti, Kanuni ya 68

Mhe. Mwenyekiti: Naam.

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Mhe. Mwenyekiti, Kanuni ya 68 tunamuomba Mhe. Mwanasheria Mkuu atusomee. (Makofi) Mhe. Mwenyekiti, tupo hapa katika mazingira ya kujenga na wala hatuharibu.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais: Mhe. Mwenyekiti kuna Mjumbe anazungumzia Kanuni ya 59 (8) inayosema ifuatavyo:

“Ni maarufu kwa Mjumbe yoyote:

(a) kutumia lugha ya matusi au kashfa;
(b) kutumia haki yake ya kusema kwa madhumuni ya kutaka kushelewesha shughuli za Baraza;
(c) kuzungumza mjumbe au mtu mwengine kwa nia mbaya au kumshambulia binafsi, isipokuwa kwa kutoa hoja halisi, inayohusu mwenendo makhsusi wa mjumbe huyo;
(d) kujiingiza katika mambo ya kuwasema wajumbe wenzake.

Sasa Mhe. Mjumbe hapa alichukulia lugha za kashfa na matusi kwa serikali ndio anayozungumzia Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum). (Makofi).

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,

nimekufahamu na nadhani Mhe. Abdalla Maulid Diwani kwa kitendo ulichosema kuwa

serikali imeonewa huruma naomba ufute hiyo kauli, ili tuendelee.

Mhe. Abdalla Maulid Diwani: Ahsante Mhe. Mwenyekiti. Nafikiri Mwenyekiti wa

Tume ya Uchaguzi Jecha na ndiye aliyeakhirisha uchaguzi, nafikiri sijatukana wala

sijazungumza lugha iliyokuwa siyo na kama anayebishana kama uchaguzi haujafutwa

sijui nani atakataa humu ndani. Naomba niendelee.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Mjumbe, kauli uliyosema kuwa serikali imeonewa huruma na

Mwenyekiti wa Tume. Sasa nadhani hoja ya Mhe. Mjumbe hili neno huruma ndio

anahisi kama umelizungumza sivyo, kwa sababu hatukuonewa huruma, labda kulikuwa

na makosefu katika uchaguzi, ndio maana Mwenyekiti akafuta matokeo. Kwa hiyo, wewe

55

ulitamka kuwa Mwenyekiti wa Tume ametuonea huruma. Hivyo, hii neno huruma nahisi

uifute hiyo kauli, ili tuendelee.

Mhe. Abdalla Maulid Diwani: Ahsante Mhe. Mwenyekiti, pamoja na maelekezo mazuri

uliyonipa natamka kwenye Baraza hili kufuta kauli yangu kwamba ile ilikuwa sio nzuri.

Naomba kuendelea. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Nakushukuru Mhe. Abdalla Maulid Diwani, naomba uendelee kwa

kumalizia dakika zako.

Mhe. Abdalla Maulid Diwani: Ahsante sana naomba muda unilindie. Mhe. Mwenyekiti

nilipozungumza agizo la 4 kuhusu kadhia kamba kutaka pembejeo tulikuwa na Kiwanda

cha Chakula cha Kuku Zanzibar. Sasa utekelezaji tunaambiwa wizara kushirikiana na

ZIPA inaendelea kufanya jitihada kutafuta muekezaji kwa ajili ya kuanzisha viwanda vya

uzalishaji pembejeo ya mifugo. Hichi kiwanda kilikufia nini. Naomba Mhe. Waziri

wakati atakapokuja anisaidie.

Lakini nikenda katika agizo nam 6 wizara iandae mpango wa kuanzisha Kituo cha

Utafiti wa Mifugo kufanya tafiti za aina mbali mbali. Mhe. Mwenyekiti, ninavyofahamu

Kituo cha Utafiti Zanzibar …

Mhe. Mwenyekiti: Waheshimiwa Wajumbe, naomba utulivu wenu, mchangiaji

anachangia minong’ono naona imekuwa mikubwa, kama ni ile hoja tayari tumeshaitolea

uwamuzi. Kwa hivyo, naomba Waheshimiwa Wajumbe tutulie tuendelee na shughuli

zetu. Mhe. Mjumbe endelea.

Kikao cha Saba – Tarehe 05 Oktoba, 2017

(Kikao kilianza Saa 3:00 asubuhi)

DUA

Mhe. Spika, (Zubeir Ali Maulid) alisoma Dua

TAARIFA YA SPIKA

Mhe. Spika: Waheshimiwa Wajumbe katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi cha tarehe

2 Oktoba, 2017, Mhe. Hidaya Ali Makame wa Nafasi za Wanawake aliuliza swali la

nyongeza kwa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi na Mhe. Naibu Waziri

Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi aliahidi kujibu kwa maandishi. Kwa Mujibu wa

Kanuni ya 40(4) ya Kanuni ya Baraza la Wawakilishi Toleo la 2016 sasa namuomba

Mhe. Waziri Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi asome jibu la nyongeza lililoulizwa na

Mjumbe huyo:

Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Mhe. Spika, kwa adhini yako

naomba kusoma majibu kama nilivyotowa taarifa, wakati nikijibu swali 50 ililoulizwa na

swali na nyongeza na Mhe. Hidaya Ali Makame alietaka kujua ni kiasi gani cha fedha

ambazo zitatumika kuwalipa watu wanaolipia mashamba jibu la swali hilo kama

ifuatavyo:-

Idadi ya wafanyakazi watakaohitajika katika kazi hiyo ni ishirini na tano (25) ni kiasi cha

fedha kitakachotumika katika kazi hiyo, ni Tanzania Shilingi milioni 15, kwa

mchanganua ufuatao:-

Idadi ya watu ni 15, siku sitini (60) kiasi elfu kumi (10) jumla kumi na tano elfu (15,000)

Mhe. Spika, nakushukuru.

Mhe. Spika: Ahsante Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili , Mifugo na Uvuvi , katibu kwa

shughuli inayofuata.

HATI YA KUWASILISHA MEZANI

Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Mhe. Spika, kwa idhini yako

naomba kuweka Mezani Hotuba ya Uwasilishaji wa Ripoti ya Wizara ya Kilimo,

Maliasili , Mifugo na Uvuvi ya Utekelezaji ya Maagizo ya Kamati ya Fedha, Biashara na

Kilimo kwa Mwaka 2016/2017. Mhe. Spika, naomba kuwasilisha.

Mhe. Spika: Ahsante Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi. Sasa

namwita Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ili naye awasilishe Hati

Mezani. Kwa niaba yake namuona Mhe. Hamad Abdalla Rashid.

2

Mhe. Hamad Abdalla Rashid (Kny. Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na

Kilimo): Mhe. Spika, kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mwenyekiti naomba kuweka

Hati Mezani Hotuba ya Maoni ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo kuhusu Ripoti ya

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Utekelezaji ya Maagizo ya Kamati ya

Mwaka 2016/2017 Mhe. Spika, naomba kuwasilisha.

MASWALI NA MAJIBU

Nam. 3

Ucheleweshwaji wa Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF)

Mhe. Mwanaidi Kassim Mussa: (Kny. Mhe. Abdalla Maulid Diwani): – Aliuliza:

Pamoja na Serikali kupitia mfuko wake wa CDF wa kutoa pesa za mfuko wa jimbo ili

kwenda sambamba na ahadi pamoja na ilani ya Chama, kwa bahati mbaya pesa hizi

zinachelewa kupatikana kwa wakati muafaka.

Ni lini Ofisi yako itaamua kubadilisha taratibu za utoaji wa pesa za mfuko wa Jimbo

mara tu baada ya kumaliza uchaguzi ili Wawakilishi waendelee kutoa huduma bora kwa

wananchi.

Mhe. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Alijibu:

Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Abdalla Maulidi Diwani

Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe swali lake Nam. 3 lakini kabla naomba kutanguliza

maelezo yafuatayo:-

Mhe. Spika, Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ni mpango maalum ulioanzishwa na Serikali

ya Mapinduzi ya Zanzibar Kupitia Sheria ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo Namba 4 ya

mwaka 2012 na Sheria ya Marekebisho ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo Namba 5 ya

mwaka 2016 ambazo zinaelezea uanzishaji na utaratibu wote wa uendeshaji na usimamizi

wa Mfuko huo kwa lengo la kusaidia wananchi katika Majimbo yao kupitia utekelezaji

wa Miradi midogo midogo waliyoibua wao wenyewe.

Mhe. Spika, baada ya maelezo hayo sasa kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe.

Abdalla Maulidi Diwani Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe swali lake Nam. 3 kama

ifuatavyo:-

Mhe. Spika, kwanza, nakubali kwamba fedha hizo ni kweli mara nyingi huwa

zinachelewa kupatikana kwa wakati muafaka. Sababu kuu ya kuchelewa kutolewa kwa

fedha hizo katika mkupuo wa awamu inayofuata ni ucheleweshaji wa marejesho kutoka

majimboni pamoja na kuchelewa kwa uwasilishaji wa majina na nambari za Akaunti

yaani Benki ya Kamati ya Maendeleo ya Jimbo.

3

Mhe. Spika, kwa masikitiko makubwa napenda kuliarifu Baraza lako Tukufu kuwa

uzoefu unaonesha kwamba mara zote baada ya uchaguzi majimbo yetu huwa

yanachelewa kuunda Kamati zao na pia Kamati zilizomaliza muda wake huwa

haziwasilishi marejesho ya matumizi ya fedha zilizotolewa awamu ya mwisho kama

ilivyoelekeza Sheria. Kutokana na sababu hizo Serikali imekuwa ikichukua hatua ya

kuzuia utoaji wa fedha za awamu nyengine baada ya uchaguzi kwa majimbo yote

ambayo yanashindwa kufanya marejesho ya matumizi ya awamu iliyopita na kuwasilisha

taarifa za majina ya Kamati za Jimbo na Nambari za Akaunti ya Benki iliyopangwa

kama ambavyo Sheria inavyoelekeza. Serikali itaendelea kutekeleza utaratibu wa

uendeshaji wa Mfuko huo kwa mujibu wa Sheria hizo ambazo zimetungwa na Baraza hili

Tukufu. Nakushukuru Mhe. Spika.

Mhe. Mwanaidi Kassim Mussa: Ahsante Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi hii kuweza

kuuliza swali la nyongeza.

Pamoja na majibu mazuri ya Mhe. naibu Waziri namuomba kumuuliza swali kama hivi

ifutavyo:

Je Mhe. Naibu Waziri, Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliwahi

kupata elimu katika suala zima la urejeshaji wa fedha za Mfuko wa Majimbo kwa wakati.

Mhe. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais: Ahsante sana Mhe.

Spika, kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mhe. Makamu wa Pili wa Rais naomba kumjibu

Mhe. Mwanaidi Kassim Mussa, Mwakilishi wa Viti Maalum kutoka katika Mkoa wa

Magharibi kama hivi ifuatavyo:-

Mhe. Spika, kabla ya kupitishwa kwa Sheria hii ndani ya Baraza hili Tukufu Wawakilishi

wote Baraza la Wawakilishi waliweza kupata Semina elekezi kuhusiana na Sheria hii ya

Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo wakati huo ilipopitishwa, hapa naizungumzia ile Sheria

Nam. 4 ya mwaka 2012, kupita Sheria hii ilifika katika Baraza hili Tukufu Waheshimiwa

Wawakilishi walipata fursa ya kujadili, wakapata semina elekezi mpaka wakaridhia

wakaweza kuipitia. Kwa hivyo tunaamini fika Mhe. Spika, katika Baraza hili wakati

Sheria hii inatungwa kulikuwa kuna semina iliyotolewa kwa Waheshimiwa Wajumbe,

lakini pia hata ukitizama marekebisho wa ile Sheria Nam. 5 ya 2016, nayo pia ilitoa fursa

kwa wajumbe kuendelea kujenga uwelewa wakati wanapitia marekebisho ya sheria hiyo.

Kwa hivyo Mhe. Spika, sisi tunaendelea kuamini kwamba semina ya awali ya kisheria

imetolewa lakini hata hivyo ofisi yangu imekuwa ikiwasisitiza Waheshimiwa

Wawakilishi wenye majimbo na kamati zao kufanya hivyo na kufika ofisini pale ambapo

wamekuwa wakihitaji maelekezo mengine na tumekuwa tukifanya hivyo kwa yale

majimbo ambayo yamekuwa yamefika. Lakini pia Mhe. Spika, ofisi yangu imeweza pia

kufanya semina maalum kwa wajumbe wa kamati hizi za maendeleo wa majimbo husika

katika majimbo yote ya Unguja na Pemba. Kamati zote hizi wajumbe wake wameweza

kupatiwa semina hii nakushukuru Mhe. Spika. (Makofi)

4

Mhe. Miraji Khamis Mussa: Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa nafasi ya kuuliza suali

dogo la nyongeza lakini nimshukuru sana Mhe. Waziri kwa majibu yake mazuri, lakini

katika majibu yake Mhe. Waziri alisema tatizo kubwa ambalo linawakabili Serikali

kutupa fedha Waheshimiwa Wawakilishi wa majimbo hizi za CDF ni kutorejesha kwa

wakati. Lakini yako majimbo yanarejesha kwa wakati sasa kutegeneza hukumu kwa wote

wakati si sahihi lakini naomba nimuulize yeye anijibu ni kwa nini serikali au wizara yake

isiweke utaratibu kwa wale ambao wamerejesha kwa wakati, wakapewa fedha hizi ili

waweze kuendelea na shughuli zao.

Lakini la pili Serikali kuendelea kufanya hivyo kwa kuwahukumu wote hawaoni kuwa

kuna majimbo ambayo yamerejeshwa kwa wakati, watakuwa hawajawatendea haki

inayostahiki kisheria.

Mhe. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais: Ahsante sana Mhe.

Spika, kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mhe. Makamu wa Pili wa Rais naomba kumjibu

Mhe. Miraji Khamis Mussa, Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni swali lake (a) (b) kama

ifuatavyo:-

(a) Mhe. Spika, kwanza nieleze furaha yangu kwa swali hili kuulizwa na Mhe.

Miraji Khamis Mussa kwa sababu Mhe. Miraji ni Mwenyekiti wa PAC

yeye alikuwa anayaona matatizo aliona wakati wa Kamati, lakini utaratibu

wa kutoa pesa hizi kwa serikali ni mfumo tunapoweza ku-release pesa hizi

tunatoa katika majimbo yote. Tabu inapotukuta pale ambapo tunapoweza

kutoa kwa awamu na changamoto inayotukuta inaikuta sisi tunaotoa pesa

hii. Kwa mfano, wakati tunatoa pesa kuanzia mwezi wa tatu 2017

tumejikuta mpaka jimbo la mwisho tunatoa pesa Mhe. Spika, kunako

mwezi wa saba.

Kwa nini tumefikia mwezi wa saba, tumefikia mwezi wa saba kwa sababu

kuna baadhi ya majimbo kuna matatizo ambayo nimeweza kuyaainisha

katika jibu langu la msingi, sasa matatizo yale yanapelekea wakati

mwengine usumbufu kwa wananchi husika ambao wanahitaji maendeleo

kupitia pesa za mfuko wa jimbo.

(b) Lakini pili tumepokea wazo lake tutatizama utaratibu mzuri itakapobidi

watu hawa kwa kuweza kuwa-categorize wale ambao watawahi kule

kurudisha mrejesho tutatizama, tunaweza tukatoa kipaumbele kwa ambao

wamewahi na wale ambao wamechelewa tutaendelea kuwastahamilia kwa

mujibu wa sheria, hasa ukisoma sheria ya section 25 ndani ya sheria yetu

ya Mfuko wa Jimbo nakushukuru Mhe. Spika. (Makofi).

Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf Al-Wardy: Mhe. Spika, nakushukuru sana mimi

nitaomba niulize maswali (a) na (b) kwa Mhe. Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa

Rais.

5

(a) Kwanza masuala yangu mimi mepesi sana, hizo fedha wanazoziongea za

mfuko wa jimbo wanazo au hawana tungependa kujua.

(b) Kwa kuwa Mhe. Miraji Khamis Mussa kauliza swali zuri sana kwa wale

ambao waliorejesha marejesho vizuri kabisa kwa wakati bado swali Mhe.

Naibu Waziri hajalijibu vizuri, sisi tunataka tujue tuliorejesha mapema kwa

vielelezo kamili fedha watatupa mapema au watasubiri mpaka wamalize

wote watupe mwisho.

Mhe. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais: Ahsante sana Mhe.

Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf Al-Wardy,

Mwakilishi wa Jimbo la Chaani swali lake la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mhe. Spika, Serikali pesa zakuzitoa katika majimbo haya inayo na mpaka sasa Serikali

kupitia Wizara ya Fedha, pesa kwa mwaka 2017/2018 katika bajeti hii tayari

zimeshatengwa. Tutaanza kulifanya hilo mara tu baada ya kupata lakini Mhe. Spika,

tunakichosema hili mpaka sasa katika zile pesa ambazo tumetowa katika mwaka

2016/2017 kuna majimbo manne tu ambayo yameleta mrejesho. Kwa tukianza kutoa

kidogo kidogo hivi Mhe. Spika, wakati mwengine inatupa wakati mgumu tunaendelea

kuwasisitiza Waheshimiwa Wajumbe tunaomba sana Waheshimiwa wajumbe tumepewa

pesa za maendeleo tumezitumia tulete return kwa mujibu wa sheria yetu sisi

tunachokifanya ni utekelezaji wa sheria iliyopitishwa na Baraza hili tukufu hatuwezi

kutumia njia nyengine. Kwa hiyo tunawaomba Waheshimiwa wa majimbo husika

watuletee mrejesho watakapoleta mrejesho sisi tutatizama katika majimbo yetu 54

tuliyokuwa nayo mpaka sasa Mhe. Spika, ni majimbo manne tu, sitaki kusema kwamba

la Chaani limo au halimo lakini Mhe. Spika, ni majimbo manne kwa hivyo tunawasisitiza

wenzetu watuletee hii pesa wafanye mrejesho tunawaingizia pesa katika mwaka wa fedha

2017/2018 nakushukuru Mhe. Spika.

Nam. 116

Nafasi za Ajira kwa Vijana Wanaomaliza Mafunzo ya JKU

Mhe. Salha Mohammed Mwinjuma – Aliuliza:

Serikali ya Jamhuri ya Muungano imekuwa na utaratibu wa kuwachukua vijana wake na

kuwaweka (JKT) na wakimaliza mafunzo yao huwaweka malezi na zinapotokea nafasi za

ajira Serikalini wao hupewa kipaumbele kwa mujibu wa sifa zao tofauti na Serikali yetu

kwa vijana wanaopitia JKU ambao huachiwa kurudi mitaani na kuchukuliwa wengine

wasiopita huko.

Je, Serikali ina mpango gani wa ziada kwa vijana wale tunaowaweka jeshini kwa miaka

miwili au zaidi na baadae kuwaruhusu mitaani bila ya kuwapa mtaji.

Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara

Maalum za SMZ – Alijibu:

6

Mhe. Spika, kwa idhini yako naomba kumjibu Mhe. Salha Mohammed Mwinjuma

Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia Vijana swali lake Nam. 116 kama ifuatavyo:-

Mhe. Spika, malengo makuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuweka vijana wa

kizanzibari katika Makambi ya JKU ni kuwafunza maadili mema pamoja na kuwa

wazalendo kwa nchi yao.

Mhe. Spika, hivyo vijana wanaomaliza elimu ya Sekondari na vyuo ni vyema

wakajiunga na JKU kwa kipindi cha miaka miwili, kwani vijana wanapokuwa makambini

wanapata fursa ya kuelimishwa mambo mbali mbali ya kizalendo ikiwemo somo la uraia

na mapenzi kwa kuipenda nchi yao. Aidha, vijana hufundishwa kazi za mikono kwa

mfano kilimo, useremala, ufundi na ushoni ili wapate kujiajiri mara wanapomaliza

mafunzo yao.

Mhe. Spika, kwa hivi sasa JKU haijaanza kutoa mitaji kwa vijana hao, isipokuwa

huwafundisha ujasiriamali na namna ya kujikusanya na kutafuta mitaji kutoka vyanzo

vyengine nje ya JKU.

Mhe. Spika, suala la ajira halina uhusiano wa moja kwa moja kwa vijana kujiunga na

JKU, isipokuwa ni miongoni mwa vipaumbele katika kuajiriwa. Kwa mujibu wa sheria

Nam. 2/2011 ya Utumishi wa Umma kifungu cha 57(3) (a) (b) na (c) kumewekwa

utaratibu wa ajira kuwa ajira zote lazima zitangazwe na kila mwenye sifa anastahiki

kuomba na kwa aliyekamilisha vigezo anastahiki kuajiriwa pasi na kuzingatia kama

amepita JKU au la kutokana na uwezo huo wa kisheria imepelekea kuwa JKU kukosa

nguvu ya kulisimamia suala hili.

Mhe. Spika, kwa msingi huo lengo la Serikali ni kuelimisha vijana na baadae vijana hao

waweze kujiajiri. Hata hivyo, ikitokea fursa ya kuajiri basi vijana hao huajiriwa, kwa

mfano mwaka 2015/2016 kati ya vijana 1200 waliomaliza mafunzo ya JKU ni vijana 162

waliopatiwa ajira katika Taasisi mbali mbali za ulinzi na usalama za SMZ na SMT.

Aidha, kuanzishwa kwa Shirika la Uwakala la Ulinzi la JKU, litawezesha kuajiriwa

vijana wengi wanaomaliza JKU. Pamoja na hayo, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa,

Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ inawasiliana na Wizara inayohusiana na

maendeleo ya vijana kutafuta uwezekano wa kuwasaidia vijana hao mara tu

wanapomaliza JKU ili waweze kujiajiri wenyewe. Ahsante.

Mhe. Salha Mohammed Mwinjuma: Ahsante Mhe. Spika, kutokana na majibu ya Mhe.

Waziri majibu mazuri ya kututia moyo na kutujenga imani vijana nilikuwa nataka

kumuliza swali dogo tu la nyongeza. Je Mhe. Waziri, wizara haioni kama sasa hivi ipo

haja ya kuweza kuwapatia mitaji vijana wale ili wakitoka waweze kujiajiri wenyewe.

Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara

Maalum za SMZ:

7

Mhe. Spika, kwa idhini yako naomba kumjibu Mhe. Salha Mohammed Mwinjuma, swali

lake la nyongeza kama ifuatavyo:

Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ inaona haja na

umuhimu wa kutafuta namna ya kuwapatia vijana mitaji na nilipokuwa nikijibu suala

langu mama nilisema hivi sasa tunawasiliana na Wizara ya uwezeshaji ili kuona jinsi

gani atunaweza kuwapatia mitaji vijana hawa.

Mhe. Rashid Makame Shamsi: Ahsante sana Mhe. Spika, na mimi kwa kunipa nafasi

ya kuuliza swali dogo la nyongeza kwa Mhe. Waziri, lakini awali nimpongeze sana kwa

majibu yake mazuri juu ya suala mama ambalo ameuliza Mhe. Salha.

Mhe. Spika, swali langu lina sehemu (a) na (b) pamoja na majibu mazuri Mheshimiwa

ameeleza kwamba vijana wanaokwenda JKT miongoni mwa mafunzo ambayo

wanayapata ni yale ya kuwajenga kiuzalendo, lakini sio vijana wote wanajengeka

kiuzalendo wengine wanamaliza miaka yao miwili lakini ule uzalendo haujajengeka.

a) Je, hatuoni vijana hawa kubaki mitaani kwa miaka mingi inaweza
wakashawishiwa na wakaweza kujiingiza katika vikundi vya ugaidi ambavyo

hivi sasa vimetanda katika nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki.

b) Amezungumzia juu ya suala la wakala wa ulinzi ambao zaidi amelenga wale
JKU, Je, kwa vijana hawa ambao wamemaliza JKT hatuoni nao waingie katika

suala hili la kupata ajira itakapoanza hii wakala wa ulinzi.

Mhe. Waziri Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara

Maalum za SMZ :

Mhe. Spika, kwa idhini yako naomba kumjibu Mhe. Rashid Makame Shamsi swali lake

la nyongeza lenye (a) na (b) kama ifuaavyo:

a) Kwanza msingi mkubwa kama nilivyosema vijana ni kuwafundisha uzalendo na
kazi nyengine za amali, sasa vijana kuwepo mitaani na kuanza kujihusisha na shughuli

nyengine zisizotarajiwa kama zile alizozitaja za ugaidi, hiyo ni akili ya mtu mwenyewe,

fikra na mawazo aliyonayo lakini lengo la kuwafundisha uzalendo maana yake ni

kujiepusha na mambo maovu kwa nchi na suala la ugaidi ni suala ovu kabisa na nchi

yao.

Kama nilivyosema Serikali ina lengo zuri la kuweza kuwafunza vijana hawa sasa kama

wapo ambao wanaingia katika mikondo hiyo basi si lengo la Serikali kuwafundisha

uzalendo na ukakamavu halafu mafunzo hayo wakenda wakayatumia kinyume na sheria

na taratibu za nchi. Wale ambao pengine watabainika kujihusisha navitendo hivyo basi

Serikali haitasita kuweza kuwachukulia hatua.

b) Tumeanzisha uwakala wa ulinzi na tunatarajia vijana waliopo JKU kuwachukua
katika kikosi hichi cha uwakala wa ulinzi, hatuoni kwamba na vijana Walioko JKT nao

8

wakapata fursa hii. Kwa kweli vijana wanaokwenda JKT na wanaokwenda JKU wote

wanakwenda kwa lengo moja na kusudio moja la Serikali zetu zote mbili, kwa hivyo

kama kuna kijana ambae amekwenda JKT au amekwenda JKU hawa wote wanayo haki

ya kuweza kupata fursa katika fursa ya ajira kwenye vikosi vya ulinzi na usalama.

Mhe. Ali Suleiman Ali: Ahsante sana Mhe. Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mhe.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za

SMZ kwa ruhusa yako naomba kuuliza swali moja la nyongeza.

Mhe. Spika, mimi kwanza niipongeze Serikali kwa azma nzima ya kuwaweka vijana

katika makambi na kujua wajibu wao kwa hatima ya nchi yetu na kuwa watarajiwa wema

katika kulinda nchi yetu na kujua ubaya wa uhalifu usitokee katika maeneo yetu. Lakini

kwa kuwa nia ya JKU ni kuwakusanya vijana kuwaweka pamoja kwa ajili ya kupata kazi

mbali mbali katika sehemu mbali mbali.

Je, kwa kuwa kuna huu uwakala wa ulinzi kupitia JKU nafikiri hii itakuwa ni

changamoto kubwa ya kuondoa matatizo ya ukosefu wa ajira katika sehemu za mahoteli

au ulinzi sehemu mbali mbali, Mhe. Waziri kwa kuliangalia hili kama kuna sera

imetungwa au inataka kutungwa sera hiyo imefikia wapi mpaka sasa hivi, ili vijana hawa

wawekwe pamoja na kuweza kupatikana pindi inapotokea sehemu ya ulinzi wawe rahisi

kuwapata.

Mhe. Waziri Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara

Maalum za SMZ: Mhe. Spika, kwa idhini yako naomba kumjibu Mhe. Ali Suleiman Ali

swali lake la nyongeza kama ifuatavyo:

Kwanza napenda nimfahamishe Mhe. Mwakilishi na Wajumbe wa Baraza hili katika

Baraza lililopita Serikali ilileta Mswada wa Sheria na tukatunga Sheria ya Uwakala wa

Ulinzi wa Uwekezaji na Utalii, Sheria ile inawataka waekezaji wote wa aina zote kufika

katika uwakala wa ulinzi na kupata walinzi wa uhakika kwa ajili ya kulinda ule

uwekezaji uliopo ndani ya nchi yetu, hivi karibuni tu Mhe. Rais amemteua Mkurugenzi

Mtendaji na tayari amemteua Mwenyekiti wa Bodi wa Uwakala wa Ulinzi na tayari wapo

wanafanyakazi si muda mrefu na mimi nitapata nafasi ya kuwateua Wajumbe wa bodi ili

zile process za Uwakala wa Ulinzi ziweza kufanya kazi ahsante sana.

Nam. 32

Umuhimu wa Sheria ya Ndoa

Mhe. Suleiman Sarhan Said – Aliuliza:

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajitahidi katika kuleta usawa, haki na kuondoa

uonevu wa kijinsia. Lakini katika jamii kumekuwa na uonevu kwa mke na watoto pindi

inapotokea kutokuelewana kwa wana ndoa na mwisho kuachana au talaka.

9

(a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuweka sheria ya kugawana mali baada ya

kuachana (talaka).

(b) Serikali ina mpango gani wa kuwapatia haki zao mke na watoto baada ya mume

au baba watoto kuwatelekeza kimaisha.

(c) Je, Serikali haioni chanzo cha watoto wa mitaani ni baba kutekeleza familia yake.

Mhe. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na

Utawala Bora – Alijibu:

Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake Nam. 32

lenye vipengele (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mhe. Spika, kama inavyoeleweka kwamba, Ndoa zote za Kiislamu, zinaongozwa

na sheria ya Dini ya Kiislamu (Qur-an na Sunnah). Aya ya 241 ya Suratul

Albakra inasema kwamba:-

“Wanawake waliopewa Talaka baada ya kuingia harusi wana haki ya kupewa

mali ya kuwaliwaza wapewe kwa kadri ya uwezo na umasikini wa mume huyo’’

Aidha, Mswada wa Sheria Mpya ya Mahkama ya Kadhi ya 2017, Mswada ambao

tumeujadili na kupitisha siku ya Jumatano tarehe 27/9/2017 imeipa uwezo

Mahkama ya Kadhi kushughulikia masuala yote ya kimadai na kesi zote ambazo

wadawa ni waislamu. Hivyo, Sheria zote hizo zinaruhusu mgawanyo wa mali

baada ya kuachana ilimradi tu utaratibu wa kisheria ufuatwe.

(b) Mhe. Spika, kama nilivyoeleza katika jawabu (a) kwamba masuala ya ndoa za

Kiislam yanaongozwa na Sheria za Dini ya Kiislamu, na iwapo Baba/Mume

ametelekeza familia yake, mlalamikaji anatakiwa aende katika Mahakama ya

Kadhi ili malalamiko yao yapatiwe ufumbuzi wa Kisheria. Sambamba na hilo

sheria ya kuwalinda wajane na watoto ya 2005 imeeleza wazi wajibu wa baba

kutoa matunzo kwa mjane na watoto.

(c) Mhe.Spika, kuna sababu nyingi zinazopelekea kuongezeka kwa watoto wa

mitaani ikiwemo hiyo aliyoisema Mheshimiwa Suleiman ya kwamba kutelekeza

familia yake. Mbali ya sababu hiyo zipo sababu nyengine ikiwemo,

mmong’onyoko wa maadili, kuwachana kwa wanandoa na kupelekea

kusambaratika kwa watoto, ugumu wa maisha na sababu nyingi nyenginezo.

Katika kulitafutia ufumbuzi suala hilo, wizara yangu kupitia Afisi ya Mufti

inaendelea kuelimisha jamii juu ya athari za Talaka na kuepuka ongezeko la

watoto wa Mitaani.

Mhe. Suleiman Sarahan Said: Nashukuru Mhe. Spika, na mimi nimshukuru Mhe.

Naibu Waziri kwa aya za Qur-ani alizothibitishia lakini pamoja na hayo hili tatizo

limekuwa kubwa sana la watoto wa mitaani na talaka ambazo hazishi sababu.

10

Sasa mimi namuuliza Mhe. Waziri kwamba kuna sheria za dini na kuna sheria za Serikali

katika nchi zetu, Je, kwani dini inakataa kutunga sheria ndogo ndogo au kanuni za

kukazia haki au kuweza kumpatia haki wale ambao wamefanyiwa dhulma.

Lakini (b) kuna watoto wanazaliwa nje ya ndoa wengine wanasema watoto wa haramu

wengine wanasema ni watoto wa nje ya ndoa, Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwapatia

haki zao watoto wale kwa kupitia DNA.

Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala

Bora:

Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake la nyongeza

lenye vifungu (a), (b) na (c).

a) Mhe. Spika, kama nilivyotoa maelezo yangu katika swali mama ni kwamba
kawaida dini ya kiislam huwa inatoa muangaza katika kutoa haki za watu zikiwemo haki

za watoto, tunapoisoma Qur-ani kuna aya mbali mbali ambazo inasisitiza kwamba watoto

wapewe haki zao. Kwa minajili hiyo niseme kwamba Qur-ani yenyewe haijakataza

kwamba zisiwepo haki za watoto kwa maana ya sheria ndogo ndogo zisiwepo, lakini

inasisitiza zaidi kwamba watoto walindwe kwa hivyo kulindwa kwa watoto kuna taratibu

zetu sisi wenyewe binaadam kutunga sheria mbali mbali. Kwa hivyo Sheria ya Kiislam

inasisitiza zaidi kwamba watoto walindwe kwa hivyo hakuna ubaya kwa maana hizi

sheria zetu kuwalinda hawa watoto na ndio maana tuna sheria mbali mbali ambazo

zinalinda watu mbali mbali, wakiwemo hao watoto.

b) Mhe. Spika, kidini au Dini ya Kiislam nadhani iko wazi imetoa maelezo mazuri
tu namna ya hawa watoto ambao wanazaliwa nje ya ndoa, kidini ya kiislam lakini

sambamba na hilo hakuna ubaya wewe baba ambae utakuwa umechangia suala lile

kutokezea kumsaidia kama binaadamu wa kawaida, hiyo iko wazi kama binaadamu wa

kawaida anatakiwa kumsaidia hilo. Lakini tukienda Kidini kuna utaratibu wake maalum

ambao naamini nyinyi Waheshimiwa Wawakilishi mnauelewa vizuri zaidi.

Nam. 82

Changamoto Wanazopata Waekezaji Zanzibar

Mhe. Jaku Hashim Ayoub – Aliuliza:

Pamoja na kazi nzuri wanayofanya Mamlaka ya Ukuzaji na Uwekezaji Vitega Uchumi

Zanzibar (ZIPA) za kuharakisha maendeleo ya uwekezaji Zanzibar, bado kuna

changamoto kadhaa waekezaji wanakumbana nazo kupitia Taasisi nyengine za Serikali

kama vile Ardhi na Mazingira n.k ambazo huwasumbua waekezaji na kurudisha nyuma

juhudi za Serikali kuu katika Sekta ya Uwekezaji.

11

(a) Je, kwanini Waekezaji wanasumbuliwa na baadhi ya Taasisi za Serikali kama

zilizotajwa hapo juu wakati suala la uwekezaji ni muhimu kwa nchi yetu.

(b) Je, Serikali inasaidia vipi Waekezaji wanaosumbuliwa na Taasisi hizo ili miradi

wanayotaka kuanzisha isikwame.

Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango – Alijibu:

Mhe. Spika, naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake Nam. 82 lenye vipengele (a)

na (b) kwanza naomba kutoa maelezo kama ifuatavyo:-

Mhe. Spika, kwanza, ni muhimu kuelewa kuwa ukiacha Sheria ya Uwekezaji, masuala ya

uwekezaji yanaongozwa pia na Sheria nyengine kadhaa ikiwemo zinazosimamia masuala

ya Ardhi, Mazingira, na mara kadhaa Sheria inayohusu Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji

Mkongwe. Taasisi zinazosimamia Sheria hizo nazo zinapaswa kusimamia vyema Sheria

hata pale inapohusu uwekezaji. Hata hivyo, kasoro zozote zinapojitokeza ni vyema

zikaratibiwa pamoja ili kufanikisha azma njema ya Serikali ya kuvutia uwekezaji nchini.

Mhe. Spika, baada ya maelezo hayo sasa naomba kumjibu kama ifuatavyo:-

(a) Mhe. Spika, Waekezaji hawasumbuliwi na Taasisi za Serikali. Kilichopo ni

namna tu Sheria zinazoongoza masuala mbalimbali zinavosimamiwa utekelezaji

wake ambao mara nyengine hauendani na matakwa ya Waekezaji na hivyo kuleta

dhana ya usumbufu.

(b) Mhe. Spika, Serikali imekuwa ikiwasaidia waekezaji kupitia uratibu wa ZIPA.

Aidha, inapobidi Serikali huunda Kamati au Timu za watendaji au hata Mawaziri

kushughulikia masuala tofauti yanapojitokeza kutegemea uzito wa jambo lenyewe

na utatuzi unaohitajika.

Mhe. Jaku Hashim Ayoub: Ahsante sana Mhe. Spika, pamoja na majibu ya kusikitisha

kwa mara ya kwanza kwa Mhe. Waziri leo ambaye sina mashaka na utendaji wake

nisikitike sana na ninaposema masuala yafanyieni kazi, ilikuwa nisi-declay interest lakini

kuna msemo shika shika na mwenyewe uko nyuma itabidi ni-declay interest niseme

maana yake nido yamenikuta mimi hata nilikuwa sitaki kutumia chombo hichi kwa kudeclay

interest.

Mhe. Waziri kama kuna mtu aliyeathirika katika Serikali mmoja ni mimi kuna waekezaji

ZIPA kibali dola 1000, hakuna kibali cha ujenzi kuliko ZIPA dola 1000 moja, ku-register

kampuni karibu 2000 na registation imefanyika na taasisi zote za Serikali ziliitwa pale na

Mkurugenzi Mkuu Salum, kama kuna mtu anastahiki kupata pongezi katika nchi hii

katika waekezaji Salum na nipelekee salam, kazi kwa Salum hailali ikafika siku ya pili

unapata jawabu.

Mhe. Jaku Hashim Ayoub: Mheshimiwa majibu haya hayakuridhisha mimi mwenyewe

nimeathirika nimechukuliwa pesa zangu hakuna kinachoendelea ….

12

Mhe. Spika: Mhe. Jaku swali lako ni nini?

Mhe. Jaku Hashim Ayoub: Swali langu lini Serikali itajipanga kuwa makini kwa

waekezaji kama nchi nyengine zilivyo, tukatumia mkono mrefu baada ya mkono mfupi

hilo la kwanza.

Lakini la pili. Mhe. Waziri kuna waekezaji watano wanatafuta vibali sasa hivi

vilipokuwa vinatoka ZIPA hakuna usumbufu sasa kufika huko Ardhi wanafanya mazoezi

bila ya kutaka ya kupanda ngazi na kushuka, Je, lini mtawapumzisha waekezaji hao

baada ya kulazimishwa kufanya mazoezi kwa nguvu bila ya hiyari yao.

Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango: Mhe. Spika, naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi

swali lake la nyongeza lenye vifungu (a) na (b) kama ifuatavyo:

Kama nilivyosema mwanzo uwekezaji nchini unasimamiwa na Sheria, Sheria ambazo

zimetungwa na kupitishwa na Baraza hili ni vyema sana Mhe. Spika, waekezaji wote wa

ndani na nje wakafuata sheria zilizopo, nasema kwamba pale yanapotokea matatizo

Serikali mara nyingi sana inafanya utaratibu wa kutatua matatizo hayo, ama huundwa

kamati kwa ajili ya kushughulikia lile tatizo linalohusika. Lakini la msingi la mwanzo

ambalo linahitajika ni kwa waekezaji kufuata sheria zilizopo ama ziwe za ardhi kuomba

vibali vya uhamiaji na kazi, masuala ya ulipaji wa kodi haya ni mambo ya msingi kwa

muwekezaji kuyafuata, sasa pale ambapo hayafuatwi ndio mara nyingi huwa yanatokea

matatizo yanayohitaji sasa Serikali kuyaingilia na kuyatafutia ufumbuzi.

Kwa hivyo mimi ningewashauri waekezaji wote wakasoma taratibu zetu, wakasoma

muongozo wa uwekezaji uliopo na hivi karibuni umepitishwa muongozo mpya ili

kuondokana na usumbufu huo. Lakini hili suala la kutoa huduma na kuwaepushia

waekezaji kwenda katika eneo moja na jengine kufuata huduma hizo, hivi sasa serikali

inaandaa utaratibu wa kuwa na kituo kimoja cha kutoa huduma kwa waekezaji, One Stop

Centre.

Hivi karibuni kama Mhe. Mjumbe alifuatilia tulikuwa na semina kubwa ya watendaji

wote wanaohusika wa taasisi zote, kulizungumza suala hili. Wizara tayari imeunda timu

ya kuweka vizuri ndani ya wiki mbili tunatarajia concept ya One Stop Centre

itawasilishwa serikalini kwa ajili ya kujadiliwa na kupata muongozo. (Makofi)

Mhe. Jaku Hashim Ayoub: Mhe. Spika, kuhusu utaratibu.

Mhe. Spika: Hapana Mhe. Jaku. Mhe. Hamza Hassan Juma, swali la nyongeza.

Mhe. Hamza Hassan Juma: Mhe. Spika, nakushukuru na mimi kwa kunipa nafasi hii ili

kumuuliza swali moja la nyongeza Mhe. Waziri. Mhe. Spika, mimi nampongeza sana

Mhe. Jaku Hashim kwa kuona hii kadhia iliyokuwepo katika suala la usumbufu kwa

wekezaji wetu wa ndani pamoja na wa nje. (Makofi)

13

Mhe. Spika, Mhe. Waziri alipokuwa kijibu swali alisema, waekezaji wanapaswa kufuata

sheria za nchi, sheria za mazingira, sheria za ardhi pamoja na sheria za ZIPA ili kuwekeza

uwekezaji wao. Mhe. Spika, nina ushahidi kuna waekezaji ambao wameshapata vibali

vya mazingira, lakini mpaka leo ZIPA wanashindwa kutoa certificate ili kuweza kupata

hati ya ardhi. (Makofi)

Lakini vile vile nina ushahidi kuna waekezaji hawana vibali vya mazingira, hawana lease

lakini wameruhusiwa kuwekeza miradi yao. Sasa huu ni ukiukwaji wa sheria, lakini vile

vile ni ubinafsi katika utendaji wa kazi. Mhe. Waziri nataka atuthibitishie je, tukimpa

ushahidi huo ataweza kuusimamia ili hao waekezaji waweze kupata haki yao ya

uwekezaji, ili kuondoa urasimu na usumbufu katika nchi yetu kwenye uekezaji?

Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango: Mhe. Spika, naomba kumjibu Mhe. Hamza

Hassan Juma swali lake la nyongeza kama ifuatavyo. Mhe. Spika, narudia kusema

kwamba upo muongozo na muongozo huo unahitaji kufuatwa na waekezaji wote.

Mhe. Spika, lakini mazungumzo au suala la Mhe, Hamza Hassan kidogo linapingana na

la Mhe. Jaku Hashim. Mmoja anasema ZIPA inafanyakazi vizuri, mwengine anasema

ZIPA hiyo hiyo ina kasoro. Kwa hivyo, ningeomba Waheshimiwa Wajumbe mkatupa

hasa, nini assessment yenu katika chombo hiki. Kwa sababu mawili yanapingana.

Nilitaka hilo niliweke wazi kwa sababu yamepingana. (Makofi)

Mhe. Spika, ninachoamini mimi ambaye ndiye msimamizi wa chombo hiki kwamba

ZIPA inafanya kazi zake vizuri na kwa mujibu wa sheria iliyowekwa. Pale inapotokea

tatizo, basi ni vyema Waheshimiwa Wawakilishi mkatuarifu kwa mapema kwamba hili

tatizo lipo, na nimesema kwamba serikali linapotokea tatizo basi haiachi kuchukua hatua.

Tutalichukulia hatua sasa, kama lipo tatizo ambalo mmeligundua, kuna watu wamepewa

vibali vya mazingira lakini ZIPA hawajatoa Certificate of Investment basi tuambieni,

lakini ndani ya utaratibu kwamba ZIPA inatoa Certificate of Investment tuambieni. Lakini

ndani ya utaratibu kwamba ZIPA inatoa Certificate of Investment ndani ya kipindi cha

wiki tatu, hiyo iko kwa mujibu wa muongozo ambao tumeuweka, sasa kama liko tatizo

tuarifuni tutalifanyia kazi hilo tatizo lilokuwepo. (Makofi)

Nam. 58

Maslahi Madogo ya Walimu Waliomaliza Diploma ya Elimu Mjumuisho

Mhe. Mwantatu Mbarak Khamis – Aliuliza:-

Mhe. Spika, baada ya Serikali kuanzisha elimu mjumuisho kwa lengo la kuwajumuisha

wanafunzi wote wale wenye mahitaji maalum na wale wasio na mahitaji maalum, walimu

wengi walikuwa na hamasa ya kujiunga na Chuo cha Kiislam ili kujiunga na cheti cha

“Inclusive” au Diploma. Hata hivyo, hivi sasa walimu wengi wamerudi nyuma kujiunga

na Diploma hiyo kutokana na Wizara kutokuzingatia maslahi ya walimu waliomaliza

Diploma Chuoni hapo.

14

Je, ni sababu gani zinazopelekea walimu waliomaliza Diploma ya “Inclusive”

kutokuongezewa posho kulingana na elimu yao.

Mhe. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali – Alijibu:-

Mhe. Spika, ahsante sana kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake

Nam. 58 kama hivi ifuatavyo:-

Mhe. Spika, kwanza naomba kutoa ufafanuzi kuwa, Chuo cha Kiislamu cha Mazizini,

kinatoa mafunzo ya elimu mjumuisho kwa ngazi ya Cheti tu, na Diploma ya Elimu

Mjumuisho inatolewa katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Katika

taratibu za Utumishi wa Umma hakuna taratibu za mtumishi kusoma cheti kwa mara ya

kwanza na baadae kujiunga na masomo ya cheti chengine na akarekebishiwa mshahara

wake kwa kupewa mshahara wa ngazi ya juu.

Hata hivyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, inalifanyia kazi suala hili kwa

kuwasiliana na Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, juu ya

namna ya kuwapatia haki zao. Ahsante sana. (Makofi)

Mhe. Mwantatu Mbarak Khamis: Ahsante Mhe. Spika, pamoja na majibu mazuri ya

Mhe. Naibu Waziri, ningependa kumuuliza swali moja la nyongeza lenye vifungu (a) na

(b). Je, ni lini mawasiliano hayo baina ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Ofisi

ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora yamefanyika, na ni hatua

gani za mawasiliano hayo yalivyofikiwa hadi sasa?

Mhe. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali: Ahsante sana Mhe. Spika, kwa

ruhusa yako napenda kumjibu Mhe. Mjumbe swali lake la nyongeza kama ifuatavyo.

Mhe. Spika, mawasiliano hayo yamefanyika kitambo na kwa sasa hatua iliyofikia na

kuweza kuzungumza zaidi na Mamlaka nyengine, kwa mfano Wizara ya Fedha na

Mipango ili kuona haki zao zinapatikana.

Mhe. Spika, niseme kwamba kwa mujibu wa taratibu za utumishi ziliopo, walimu hawa

wanastahiki kupewa haki yao, hasa katika kifungu cha 82(i)(ii) inaeleza wazi wazi,

kwamba mfanyakazi ambaye anakwenda masomoni na atakaporudi masomoni, kwa

mfano cheti, akirudi na cheti basi anapandishwa ngazi kwa mfano alikuwa hana.

Mfanyakazi wa digirii akienda kusomea Master halikadhalika. Sasa hawa walikwenda

katika masomo ya cheti na tayari wana cheti. Kwa hivyo, ina maana kanuni niliyoitaja

nukta mbili, inasema watu hawa hupewa, wanaita increment moja na nusu kila mwaka

wanasoma na hili linafanyiwa kazi hasa.

Nam. 60

Kutafuta Ajira za Ughaibuni Kwa Vijana

Mhe. Saada Ramadhan Mwendwa – Aliuliza:-

15

Kutokana na tatizo la ajira ambalo linaikabili Zanzibar kama zilivyo nchi zinazoendelea,

vijana wengi wamekuwa na utaratibu wa kuondoka nchini kwenda kutafuta ajira hasa

katika nchi za Arabuni. Hata hivyo, vijana hao wamekuwa wakipata matatizo makubwa

wanapokuwa katika nchi hizo za kigeni na katika siku za hivi karibuni raia kutoka

Tanzania, Kenya na Burundi wameripotiwa kufanyiwa vitendo vya kikatili na baadhi yao

kuteswa hadi kufa.

(a) Je, Serikali inazo habari za vitendo hivyo vya ukatili wanavyofanyiwa vijana hao.

(b) Serikali imechukua hatua gani katika kuwalinda na kuwasaidia vijana wetu.

(c) Kwa kuwa safari za vijana hao kwenda nchi za nje huratibiwa na mawakala, je

Serikali ina makubaliano yoyote na Mawakala hao.

Mhe. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto – Alijibu:-

Mhe. Spika, kwa heshima na tadhima naomba nichukuwe nafasi hii sana kumshukuru

Mwenyezi Mungu kwa kupata nafasi ya kuweza kukutana tena leo. Lakini pia nichukuwe

nafasi ya kuweza kumjibu Mhe. Mjumbe swali lake Nam. 60 lenye vipengele (a), (b) na

(c) kama ifuatavyo:-

(a) Mhe. Spika, serikali kupitia Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,

Wanawake na Watoto, imekua ikipokea habari kupitia vianzio mbali mbali

zinazothibitika na zisizothibitika, kuhusiana na vitendo vya ukatili

wanavyofanyiwa baadhi ya vijana hao. Kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 ni

kesi moja tu tuliyoipokea na kuthibitika ambayo ni mfanyakazi wa kike nchini

Dubai kwa tukio linalosemekana amegongwa na geti, tukio ambalo linaendelea

kufanyiwa uchunguzi. Matukio mengine yanayosambazwa na vyombo vya habari

hatuna uthibitisho rasmi.

(b) Mhe. Spika, serikali kupitia Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,

Wanawake na Watoto, inachukua hatua zifuatazo katika kuwalinda na kuwasaidia

vijana wetu.

Kuanzisha mtandao wa Mawakala wa Ajira waliosajiliwa na serikali baina
ya Tanzania na Oman, ambapo Mawakala hawa ndio wanakuwa dhamana

kwa vijana waliopata ajira.

Kuweka kumbukumbu za kila muajiri na mfanyakazi wake, ili ikitokea
tatizo taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa.

iii. Ofisi za Kibalozi za Tanzania hutuma kwetu taarifa zinazohusu muajiri,

muajiriwa, wakala waliopitia, namba ya simu ya muajiri, nambari ya

mkataba, pasipoti namba ya muajiriwa na nambari ya risiti iliyolipiwa

ubalozini ili tuweze kuhakiki na utambuzi na kuwaruhusu kwenda

kufanyakazi nje ya nchi.

16

Maofisa wa wizara kupitia Idara ya Ajira walishafanya safari kikazi, kwa
baadhi ya nchi za kiarabu kufuatilia wafanyakazi wetu na kujenga

mahusiano mema na nchi husika.

(c) Mhe. Spika, ndio maana serikali kupitia wizara ina mashirikiano na Taasisi za

Wakala binafsi wa ajira, ambazo zinafanya kazi hiyo kwa kuwapeleka vijana nje

ya nchi kufanya kazi.

Mhe. Saada Ramadhan Mwendwa: Ahsante Mhe. Spika, kwa majibu mazuri ya Mhe.

Waziri tegemeo la wanawake. Nilitaka kujua tu ni vikundi vingapi vya hao mawakala

ambao mmevisajili kwa hapa Zanzibar vinavyowapeleka vijana wetu nje.

Mhe. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto: Mhe.

Spika, naomba nilichukuwe swali hili, kwa sababu hivi karibuni kutokana na matukio

mbali mbali ambayo yamekuwa yakitokea, kuna baadhi tumeanza kuwafuta. Kwa hivyo,

naomba nilichukuwe hili ili niweze kuthibitisha ni wangapi sasa hivi ambao wamekuwa

register tena kwa mara nyengine, ili niweze kumjibu kwa uhakika zaidi. (Makofi)

Mhe. Amina Iddi Mabrouk: Ahsante sana Mhe, Spika, kwa kunipa nafasi ya kuuliza

swali moja la nyongeza. Pamoja na majibu ambayo hayaridhishi sana ya Mhe. Waziri.

Kwa kuwa katika jibu lake mama alisema kwamba kuna baadhi ya maofisa wamefanya

ziara katika baadhi ya nchi za Kiarabu.

Je, ni nchi ngapi ambazo wamefanya mpaka sasa. Pia ni nchi ipi na ipo wamefanya ziara

hizo?

Mhe. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto: Mhe.

Spika, naomba arejee kipengele cha mwisho Mhe. Spika.

Mhe. Spika: Kauliza kwamba ni nchi ngapi wamefanya ziara na ni nchi zipi, yaani

uzitaje hizo nchi. Hebu Mhe. Mjumbe naomba ulirudie hilo swali lako.

Mhe. Amina Iddi Mabrouk: Ahsante sana Mhe, Spika. Nilimuuliza swali kwamba kwa

kuwa katika jibu lake mama alisema kwamba kuna baadhi ya maofisa ambao wamefanya

ziara katika baadhi ya nchi za Kiarabu.

Je, ni nchi ngapi ambazo wamefanya hizo ziara. Lakini pia atuambie ni nchi ipi na ipi

ambazo wamefanya hizo ziara. Kwa sababu hili tatizo limekuwa kubwa sana.

Mhe. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto: Ahsante

Mhe. Spika, kwa heshima nipende kusema tu kwamba katika kufuatilia hizi shughuli,

maofisa pamoja na wizara wameweza kufuatilia katika nchi moja ya Qatar, ambayo kwa

makusudi kabisa tulikwenda kuangalia hali halisi za wafanyakazi waliokuwepo kule na

wanavyofanya.

17

Pia kwa sababu nchi nyengine zilikuwa hazina Mabalozi, hivi sasa Mhe. Rais wetu

ameteuwa mabalozi katika nchi ambazo zilikuwa hazina mabalozi, utaratibu wa

mawasiliano ya karibu unaendelea. Tunashukuru sasa hivi ndio maana kumekuwa hata

hili wimbi tulokuwa tunalisikia kila baada ya muda mfupi halisikiki tena.

Mhe. Salha Mohamed Mwinjuma: Ahsante Mhe. Spika, kutokana na majibu ya Mhe.

Waziri, ametuambia kuna taarifa mbali mbali zinazotolewa kutokupitia Ubalozini, na

taarifa nyengine zinatoka kwa waajiri wao, nilikuwa nataka kujua.

Je, wizara ina taarifa gani na ina taarifa ya vijana wangapi waliofuata utaratibu huo katika

nchi hizo. Ahsante.

Mhe. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto: Mhe.

Spika, nasikitika kwamba hapa kuna Echo kidogo haisikiki. Hilo swali la mwisho

ulilotaka kuuliza swali la mwisho, ulitaka kujua nini, hilo la mwisho.

Mhe. Salha Mohamed Mwinjuma: Kwa ruhusa yako Mhe. Spika, naomba kurejea.

Kutokana na taarifa ya Mhe. Waziri. Je, wizara ina taarifa ya vijana wangapi waliofuata

utaratibu kama alioueleza yeye katika jawabu lake mama. Ahsante?

Mhe. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto: Mhe.

Spika, mpaka sasa hivi kuna vijana zaidi ya 1,500 ambao wamesajiliwa na wamekwenda

na wanafanyakazi huko.

Nam. 57

Utafiti na Uzalishaji wa Zao la Minazi

Mhe. Omar Seif Abeid – Aliuliza:-

Mhe. Spika, na mimi nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali. Lakini kabla ya

kuuliza swali, naomba nifanye marekebisho kidogo yaliyojitokeza katika hilo swali langu

katika kipengele cha (b) ambapo mwandishi aliandika “dawa yoyote ambayo inazaa”.

Mhe. Spika, sikukusudia hivyo, kwa sababu najua dawa haizai. Lakini isomeke, je kuna

dawa yoyote ambayo inaweza kutumika. Ahsante sana, baada ya marekebisho hayo

naomba swali langu nambari 57 lijibiwe, ahsante sana Mhe. Spika.

Kwa kuwa Wizara ya Kilimo ina wataalamu na wafanyakazi ambao kwa kutumia

taaluma yao wanaweza kuongeza uzalishaji mkubwa wa nazi ambazo kutokana na

ongezeko la watu, na kwa sababu ya upungufu mkubwa wa zao hilo uliopo na bei ya nazi

imepanda hadi kufikia zaidi ya shilingi 1000 kwa nazi moja.

(a) Je, Wizara kwa kutumia wataalamu wake ina mpango gani wa kutafuta au

kufanya utafiti wa kupata mbegu za minazi ambazo inaweza kuzaa kwa muda

18

mfupi na kuwashajihisha wakulima kuipanda kwa wingi ili kupunguza upungufu

wa nazi uliopo hivi sasa.

(b) Je, kuna mbolea au dawa yoyote ambayo inaweza kutumika na kuifanya minazi

ambayo imeacha kuzaa kwa muda ikarejesha uzazi wake kama mwanzo.

(c) Je, ni aina gani ya miche ya minazi ambayo inaanza kwa muda wa miaka 3 na

kama ipo inapatikana wapi.

Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Alijibu:-

Ahsate sana Mhe. Spika, kwa ruhusa yako napenda kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake

Nam. 57 lenye vipengele (a), (b) na (c) kama ifuatavyo.

Mhe. Spika, kabla ya kumjibu Mhe. Mjumbe napenda kutoa maelezo mafupi kuhusiana

na swali hili.

Mhe. Spika, katika vipindi vya miaka 35 iliyopita utafiti wa minazi ulifanyika kwa

kiwango kikubwa kwa kujumuisha zaidi ya aina tano (5) za mbegu za kigeni pamoja na

mbili (2) za asili (East African Tall na Kitamli). Utafiti huu ulibainisha wazi kuwa mbegu

za asili ndizo zenye kustahamili mazingira ya Zanzibar, ambayo pindipo ikishughulikiwa

vizuri, yaani (kupaliliwa, kuwekewa mbolea na kukingwa na wadudu waharibifu hasa

mdudu bungu wa minazi), zinao uwezo wa kuzalisha nazi zisizipungua 50 kwa mnazi

mmoja kwa mwaka na kuishi miaka zaidi ya 75 ikiwa inazalisha. Minazi mifupi

ilionekana kuzalisha nazi nyingi (wastani wa zaidi ya nazi 100 kwa mnazi kwa mwaka)

lakini baada ya miaka michache (wastani wa miaka 15) huduma hushuka kwa kiwango

kikubwa cha uzalishaji wake.

Mhe. Spika, baada ya maelezo hayo mafupi naomba kujibu kama ifuatavyo:-

(a) Mhe. Spika, wizara inaotesha wastani wa miche 20,000 kwa mwaka. Lengo ni

kuisambaza kwa wakulima, kwa vile minazi yetu ya asili inao uwezo mkubwa wa

kuzalisha nazi kwa muda mrefu na zenye ubora, kwa kulinganisha na minazi

mifupi ambayo huzalisha kwa muda mfupi na nazi zisizo na ubora unaofanana na

mbegu ya asili.

(b) Mhe. Spika, minazi mingi ambayo inaonekana kuacha kuzaa kwa muda, kutokana

na mashambulizi ya wadudu ambao husababisha kudondoka au kukauka kwa

vidaka zaidi ya asilimia 50. Minazi inao uwezo wa kurejesha uzalishaji wake

pindipo wadudu hawa watadhibitiwa kwa mbinu za asili, ikiwemo kuchanganya

miti ya matunda kwenye shamba la minazi.

(c) Mhe. Spika, aina za mbegu fupi za minazi zinao uwezo wa kuanza kuzaa kuanzia

miaka mitatu tokea kupandwa, lakini kama nilivyoeleza katika maelezo ya

utangulizi, nazi zitokanazo na mbegu hizi hazina ubora kulinganisha na minazi

yetu ya asili, hususan katika kiwango cha mafuta. Mbegu fupi ambazo hivi sasa

19

zinapatikana hapa Zanzibar ni Kitamli, Malayan Yellow Dwarf (MYD), Malayan

Green Dwarf (MGD) na Cameroon Red Dwarf (CRD), na zinapatikana katika

mashamba ya wakulima na mbegu ya MGD inapatikana katika shamba la Utafiti

wa Minazi Kijichi.

Mhe. Omar Seif Abeid: Ahsante sana Mhe. Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya

kitaalamu ya Mhe. Naibu Waziri, nafurahi. Lakini naomba niulize tu swali moja dogo,

kwa sababu ilionekana kwamba hii ni vipindi vya miaka 35.

(a) Mhe. Spika, kwanza ningetaka nijuwe je, kipindi cha mwisho ambacho

mmefanya utafiti na kubaini haya mliyoyaeleza ilikuwa ni mwaka gani.

(b) Kwa kuwa umekiri kwamba miongoni mwa matatizo, kuna matatizo ya wadudu

wanaoababisha kukatika kwa vidaka na kupukutika na mambo mengine na mkatoa

maelezo kwamba kutumia kilimo mchanganyiko. Lakini ukiachia hicho kilimo

mchanganyiko ambacho wakulima wetu wanakilima kwenye nayo mashamba ya minazi.

(b) Je, dawa gani inayotumika kwa kuwauwa wadudu hawa wanaoshambulia hivyo

vidaka ambayo na taaluma yake mmeipeleka kwa wakulima ili wakulima wakaitumia

wakapata mazao zaidi. Ahsante sana.

Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Mhe. Naibu Spika,

ahsante sana Mhe. Spika, napenda kumjibu Mhe. Mwakilishi suali lake la nyongeza lenye

vipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:

a) Mhe. Spika, ulipomalizika utafiti huu ya minazi kama nilivyosema miaka 35
iliyopita mradi huu ulimalizika mwaka 2005.

b) Mhe. Spika, dawa ambayo inatumika kumuuwa mdudu huyu bungu inaitwa andro
lakini haishauriwi kutumia kwa sababu hii dawa inapigwa juu kwenye yale

matawi na unapopiga inaathiri pamoja na wale viumbe ambao wanaruka.

Inashauri zaidi kutumia hii dawa ya asili kuotesha miche ya matunda ndani ya

shamba la minazi ili kuweza kuwakimbiza wale sisimizi wanaoharibu, kwani

sisimizi na bungu ndio marafiki wanaokaa katika minazi hiyo. Nashukuru.

Mhe. Hidaya Ali Makame: Ahsante Mhe. Spika, kwa kuniona na mimi kuweza kunipa

nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mhe. Spika, kwanza nimpongeze sana Mhe. Waziri kwa majibu yake mazuri lakini

ningependa nimuulize suali dogo la nyongeza lenye kitoto (a) na (b).

a) Mhe. Spika, Mhe. Waziri ametwambia kwamba kuna miche 20,000 ambayo tayari
imeshatayarishwa ni wakulima wangapi ambao wamepatiwa miche hiyo ili

waweze kuendeleza kilimo hicho cha Minazi.

20

b) Je, ikiwa kama yale mashamba ya Serikali yana minazi peke yake na wakati hapa
umetwambia kwamba yachanganywe pamoja na miche ya matunda ili iweze

kusaidia wale wadudu ambao wanaharibu mbigu hizi za minazi. Je, ni utaratibu

gani mnaochukua nyinyi kama Wizara kwa haya mashamba yenu ya Wizara ili

kuweza kuhifadhi hizi mbegu za minazi yaweze kuzaa na dawa gani mnazotumia

kwa minazi ile ambayo imo ndani ya mashamba yale ambayo hamna miche ya

matunda. Ahsante.

Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Ahsante sana Mhe. Spika,

kwa ruhusa yako napenda kumjibu Mheshimiwa Mwakilishi swali lake lenye kipengele

(a) na (b) kama ifuatavyo:

a) Wakulima waliofaidika na miche hii zi zaidi ya 500 Unguja na Pemba.
b) Minazi ipo haizai sasa hivi tunaichukua kupandishia ile minazi ili kuweka
mengine na ile mikongwe kuifanyia utaratibu mwengine.

Mhe. Panya Ali Abdalla: Ahsante sana Mhe. Spika, na mimi nashukuru kwa kunipatia

fursa hii kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mhe. Waziri napenda na

mimi nimuulize nimuulize suali moja lenye (a) na (b).

Kwa kuwa mnazi ni zao tunalolitegemea sana katika visiwa vyetu vya Unguja na Pemba

kwa kupikia vyakula mbali mbali na pia tunapata mafuta yaliyobora katika mnazi.

a) Je, serikali inapotoa hii miche ya minazi kuwapatia wananchi kuna na wataalamu
ambao mnawafuatanisha nao ili waweze kupanda minazi hiyo kitaalamu ili

yaweze kupatikana mazao yaliyo bora.

b) Ni lini serikali itawafuatilia wakulima pale inapowapa miche wakapande ili kuona
ufanisi unapatikana na utunzaji bora wa miche hiyo.

Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Ahsante sana Mhe. Spika,

kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mheshimiwa Mwakilishi swali lake lenye (a) na (b)

kama ifuatavyo:

a) Wataalamu tunao wengi na tunapowapa miche hii tunajaribu kuwapa yale maneno
ya kitaalamu na ikiwa zaidi basi wanaambatanishwa na wahusika.

b) Serikali ipo tayari muda wowote kuwasaidia wakulima wetu hawa wa minazi ili
kuweza kulikuza zao hili tuweze kufaidika zaidi.

Nam. 45

Takwimu za Uzalishaji Mchele Zanzibar

Mhe. Omar Seif Abeid – Aliuliza:

21

Takwimu zinaonesha kwamba jumla ya tani 88,903.60 za mchele ziliagizwa na

wafanyabiashara wetu kutoka nje kwa kipindi cha mwaka 2016 na kwa sababu Wizara ya

Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi inacho kitengo cha uhakika wa chakula na

wataalamu wengi wa kilimo ambao wanaweza kufahamu ni kiasi gani cha mchele

unaohitajika kwa mwaka.

(a) Je, ni tani ngapi za mchele zinatosheleza kwa chakula bila ya kuwa na upungufu

hapa Zanzibar.

(b) Je, ni tani ngapi za mchele ambazo tunaweza kuzalisha hapa zanzibar na mahitaji

yalibaki ndio tukaagiza kutoka Nje.

(c) Je, ni kiasi gani cha Mchele kutoka Tanzania Bara unaoingizwa Zanzibar kwa

mwaka.

Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Alijibu:

Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali Nam. 45 lenye

vipengele (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mhe. Spika, tani za mchele zinazotosheleza kwa chakula bila ya kuwa na

upungufu hapa Zanzibar ni thamanini na tisa elfu na mia mbili (89,200) ambazo

zinatosheleza mahitaji ya nchi kwa mwaka mzima.

(b) Mhe. Spika, hizi sasa Zanzibar inazalisha wastani wa tani ishirini elfu mia tisa na

thamanini na tano (20,985) za mchele kwa mwaka. Hata hivyo Zanzibar inaweza

kuongeza uzalishaji wa mchele na kufikia tani sitini elfu (60,000) kwa mwaka

iwapo tutaendeleza kilimo cha mpunga wa umwagiliaji maji. Serikali kupitia

Wizara Kilimo bado inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya

umwagiliaji maji na matarajio yetu kwamba pindipo ujenzi ukikapokamilika,

tutaongeza uzalishaji wa mpunga. Hivi sasa kwa sehemu kubwa kinategemea

mvua na asilimia 98 ya eneo linalolimwa mpunga linategemea mvua.

(c) Mhe. Spika, kwa wastani Zanzibar inaingiza tani elfu tano mia tano na tisini na

sita (5,596) za mchele kwa mwaka kutoka Tanzania Bara na inaingiza tani tisini

na saba elfu mia sita kutoka Thailand na Vietnam.

Mhe. Omar Seif Abeid: Mhe. Spika, ahsante sana Mhe. Suleiman Sarahan kidogo

utaniwia radhi samahani. Mhe. Spika, nampongeza sana Waziri wka majibu yake mazuri,

sasa anaonekana kidogo mambo yake yameanza kuonyoka yapo vizuri, ahsante.

Mhe. Spika, pamoja na majibu mazuri ambayo Waziri umenipatia kwa ajili ya wananchi

wa Zanzibar na Wafanyabiashara kutaka kujua muelekeo wa biashara kwa sababu

chakula hichi cha mchele ndiyo chakula chetu kikubwa. Kwa kuwa Waziri umejibu

kwamba Zanzibar tunatoa hizo tani ishirini elfu na mia tisa na thamanini na tano na tano

elfu tano mia tano na tisini na sita zilizobaki ndizo huingizwa kutoka Tanzania Bara.

22

a) Mhe. Spika, sisi Zanzibar ni kisiwa na tuna milango mingi ya kuingilia hapa
kutoka Bara. Mimi nilitaka kujua je, Wizara imepataje kujua kwa uhalisia

kwamba hizi tani elfu tano mia tano na tisini na tisa tu ndizo zinazoingizwa

kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu ukiachilia mbali muda wa mavuno ukimaliza

wananchi wetu ndani ya kipindi cha miezi mitatu wamemaliza chakula chao.

b) Je, nijitihada gani za uhakika kwa Wizara itakazozichukua ili kuhakikisha hizi
tani elfu tano, mia tano tisini na sita zilizobakia kama zinazalishwa hapa hapa na

tunaachana na kuingiza mchele kutoka Tanzania Bara. Ahsante sana.

Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Mhe. Spika, ahsante sana

kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mheshimiwa Mwakilishi swali lake lenye vipengele

(a) na (b) kama ifuatavyo:

a) Mhe. Spika, Wizara ina wataalamu wake ambao inatumia kuchukua takwimu hizi,
kwa hivyo sisi tunatumia wataalamu hao kupata takwimu mchele unaingizwa tani

ngapi ndani ya Zanzibar.

b) Katika swali hili kuna mradi ambao wa ERPP mradi huu unaongeza tani zaidi
kwa ajili ya kupata mavuno zaidi, unatumia maji kidogo, mbolea kidogo, eneo

dogo lakini mazao yanakuwa ni mengi. Kutokana na mradi huu na miradi

mengine na mradi mwengine wa EXIM ambao tukikamilisha basi tunahakikisha

kwamba tani hizi zitazidi zaidi ya hizo efu ishirini.

Mhe. Suleiman Sarahan Said: Nashukuru Mhe. Spika, na mimi nimshukuru sana Naibu

Waziri kwa majibu yake mazuri. Mimi nilikuwa namuuliza Mhe. Naibu Waziri kwamba

tuna mabonde ya mpunga pale Kibirinzi yaliyofikwa na maji ya bahari na wananchi wale

mpaka leo hawapati tena kile kilimo, lakini serikali iliahidi kuwapatia maeneo mengine

au kuwafanyia utaratibu mwengine lakini mpaka leo hawajafanyiwa chochote nilikuwa

nauliza serikali.

a) Je, ni kauli gani au hatua gani zimeshukuliwa kuhusu wananchi wale.
b) Kwa kuwa wananchi wale hawapati sehemu ya kulima kupatia yale mazao yao.
Serikali imewatizamaje katika suala la kuwakimu kichakula katika muda huu

ambao hawajapatiwa eneo au ndiyo hawana mpangilio wowote.

Mhe. Spika: Mheshimiwa hilo ni suali jipya naomba ulilete kwa maandishi.

Mhe. Jaku Hashim Ayoub: Ahsante sana Mhe. Spika, Mhe. Waziri alipoingia Barazani

hapa mwanzo mwanzo alituahidi kipindi cha bajeti akasema hatutomaliza muda hapa

mchele hatutoagiza nje. Je, kauli ile anayo mpaka leo au akishindwa atajiuzulu kwa

kulidanganya Baraza.

Mhe. Spika: Mheshimiwa swali hilo nalifuta naliacha, tunaendelea Wizara inayofuata.

23

Nampongeza Waziri wa Kilimo leo majibu yalikuwa mazuri sana, mafupi yamekaa vizuri

sana. Ahsante sana hongera sana.

Nam. 77

Uingizwaji wa Dawa za Kupuliza Mbu Ambazo Hazina Kiwango

Mhe. Jaku Hashim Ayoub – Aliuliza:

Kumekuwa na kasi ya uingizwaji wa dawa za mbu za kupuliza ambazo zinaonekana zipo

chini ya kiwango ambapo dawa hizo zinapopulizwa zinaingia mikononi mwa mpulizaji

badala ya kusambaa kwa njia ya hewa.

(a) Je, Wizara imegundua tatizo la dawa hizo.

(b) Je, ukaguzi unafanywa kwa namna gani mpaka dawa hizo zinaingizwa katika

matumizi ya watu nchini kwetu.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya – Alijibu:

Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake Nam. 77 kwa

pamoja kama ifuatavyo:-

Mhe. Spika, kwa kawaida kupitia Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi, ukaguzi huwa

unafanywa kwa njia ya kuangalia dawa hizo pale zinapoingia nchini (Bandarini). Vipimo

mbali mbali huangaliwa ikiwemo tarehe ya kutengenezwa na kumaliza muda wa

matumizi ili kuhakikisha dawa hizo ni salama na zina viwango vinavyohitajika.

Mhe. Spika, kazi hii hufanywa kwa mashirikiano makubwa baina ya Wizara ya Afya na

Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kupitia taasisi husika ambazo zinahusika na

kulinda viwango na usalama wa dawa kwa matumizi nchini.

Mhe. Spika, inatokezea kidogo, wakati wakala inapofanya ukaguzi kwa kubaini bidhaa

zilizopitwa na wakati (Expired) katika maghala, kwa baadhi ya wakati hukuta pia bidhaa

ambazo ni nzima lakini hazikuhifadhiwa ipasavyo na kiuhalisia kutohifadhiwa ipasavyo,

hupelekea bidhaa hiyo kupotea ubora wake. Wakala anapokutana na hali hiyo hutoa

maelekezo kwa wahusika ili kunusuru ubora wa bidhaa hiyo kwa manufaa ya watumiaji.

Mhe. Spika, Wizara yangu inafatilia kwa kina taarifa juu ya kuwepo kwa dawa hizi, pindi

zikibainika na uwezekano wa kuleta madhara kwa binadamu, hatua za kudhibiti

zitachukuliwa mara moja. Ahsante.

Mhe. Jaku Hashim Ayoub: Ahsante sana Mhe. Spika, nilitegemea suala hili hasa

litajibiwa na Wizara ya Biashara. Sasa Mhe. Naibu Waziri utaangalia au kama Waziri

yeyote atasaidia si vibaya kwa mujibu wa Kanuni zetu za Baraza.

24

Mhe. Naibu Waziri mmepitisha Sheria ndani ya Baraza hili kuna Kampuni inaitwa

Kilimanjaro Dubai na Kampuni nyengine kukagua zile dawa, vyakula kutokana na

kiwango cha chake, lakini inatokana hizo Kampuni zilizokuwepo ni mzigo zinashindwa

kusimamia majukumu yake na wafanyabiashara kule hutozwa ada.

a) Je, serikali ina kauli gani kuhusu tukio hilo, tunaletewa dawa na nyengine
zinabadilishwa baada ya heat inaitwa hot baada ya hot inaitwa heat

zinabadilishwa majina tu, lakini kile kile chakula chenyewe ni mchele

unabadilishwa mapishi tu, unaweza kupika biriani, pilau, mseto.

b) Je, serikali haioni haja sasa baada ya kuumiza wafanyabiashara kutozwa ada vitu
hivyo huko nje ya kampuni ya viwango ambapo imeshindwa majukumu yake.

Lini serikali itatoa kauli kutafuta wakala wengine waweze kushindwa majukumu

haya.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya: Mhe. Spika, ni kweli kwamba serikali inayo wakala nje

ya nchi ambayo ni ZBF, Zanzibar Bureau Standard Wakala hii inafanya kazi katika nchi

tofauti ikiwemo Dubai, China na kadhalika. Wakala huyo wa viwango ana kazi ya

ukaguzi wa bidhaa mbali mbali za vyakula na vyombo vya moto na kadhalika. Lakini

bado naomba nirudi kwenye jibu langu la msingi kumjibu Mhe. Jaku Hashim Ayoub.

Mhe. Spika, inawezekana kwamba dawa hizi kule zilikaguliwa na ziliingia katika nchi

zikakaguliwa na zikawa zipo salama lakini zikaharibika au zikapoteza ubora kidogo

katika mazingira ya kuzihifadhi. Nilikuwa namuomba atupe muda ili wakala wa bodi ya

Chakula, Dawa na Vipodozi hapa Zanzibar ifanye utafiti wake baadae itatoa taarifa

kuhusu dawa hizo.

Mhe. Mohammed Said Mohammed: Mhe. Spika, ahsante kwa kuniona pamoja na

majibu mazuri sana ya Mhe. Naibu Waziri ningeomba kuuliza swali dogo sana la

nyongeza.

Kwa kuwa muuliza swali ameongeza juu ya kiwango cha dawa tofauti na alivyojibu Mhe.

Waziri cha ku-expire au laa, nataka kujua tu serikali ina mkakati gani wa kuunda

maabara ya kuona sasa tunapima vitu hivi hapa nchini vya viwango.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya: Mhe. Spika, naomba nimjibu Mhe. Mwakilishi swali lake

la nyongeza. Mheshimiwa suala hilo tunalichukua kama ni ushauri uliotupa Wizara

tutalifanyia kazi na naamini kwamba tutapata jawabu zuri la utekelezaji katika suala hilo.

Nam. 20

Kuondolewa Gari za Abiria Zenye Tairi Moja

Mhe. Suleiman Sarahan Said – Aliuliza:

25

Katika kulinda maisha ya wananchi wake, Serikali ilitoa agizo la gari za abiria zenye tairi

moja moja nyuma kama gari za HIACE kuondoka katika soko la usafirishaji abiria.

Lakini gari hizo bado zinashamiri kuletwa na kuendelea na biashara hiyo.

(a) Je, daladala za tairi moja moja nyuma hazina umuhimu tena wa kuziondoa katika

sekta ya usafirishaji abiria.

(b) Nini lengo la serikali kuhusu kuziondoa daladala hizo kwenye biashara hiyo. Na

kama bado lengo hilo lipo ni lini Serikali imeweka mwisho wa matumizi ya gari

hizo.

Mhe. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Alijibu:

Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba kumjibu Mhe. Mwakilishi swali lake Nam. 20

lenye vipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Umuhimu wa kuziondoa daladala zote zenye tairi mbili katika biashara ya

daladala upo palepale kama inavyoeleza kanuni ya 52 ya gari za biashara.

(b) Lengo kuu la serikali kuziondoa gari hizo ni kulinda maisha ya raia wake na

kuweka usalama wa abiria na mali zao na serikali tayari imesimamisha usajili wa

gari mpya za aina hii ila zile zilizokuwepo zimalizike wenyewe lakini kutokana

na ujanja unaotumiwa na wenye magari wa kubadilisha kila kitu katika “chasis”

za gari zilizokuwepo serikali inaandaa utaratibu mpya na utakapokamilika

itatangazwa rasmi siku ya mwisho ya matumizi ya gari za aina hiyo. Ahsante

Mhe. Spika.

Mhe. Suleiman Sarahan Said: Nashukuru Mhe. Spika, na mimi nimshukuru sana Mhe.

Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri lakini nina swali la (a) na (b) kama ifuatavyo:

a) Kwa kuwa serikali inajua kuwa kuna udanganyifu unaofanywa na baadhi ya
wamiliki wa gari hizo. Je, serikali imetoa elimu gani kwa wamiliki hao na

itawasaidiaje katika kuwasaidia kibiashara na kutokupata hasara.

b) Kwa kuwa serikali imeona gari za aina hiyo hazifai au pengine zina kasoro katika
suala la biashara hiyo. Je, serikali kwa gari hizo zitawabadilishia njia kuwatoa

mjini kuwapeleka mashamba au zitafuta leseni kabisa.

Mhe. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji: Ahsante sana Mhe.

Spika, kwa ruhusa yako napenda kuchukua nafasi hii kumjibu Mhe. Mwakilishi swali

lake la nyongeza lenye kifungu (a) na (b) kama ifuatavyo:

a) Kwanza napenda kumuarifu kuwa kwa mujibu wa sheria yetu ya Nam. 7 ya 2003
ya usafiri barabarani kifungu Nam. 14(2) (c) kinaelezea Wajumbe wa Bodi, katika

wajumbe wale wamo wajumbe kutoka watu wanaohusika na mambo ya usafiri

26

yaani daladala. Kupitia wale tunakuwa tunaelewesha namna gani ambapo

utaratibu watumie katika kuwaelimisha watu.

Kwanza si cheat, pili kwamba hizi gari tumeziondosha kwa sababu ya usalama

wao na abiria wetu, kwa sababu zile gari zinakuwa haziwezi kuhimili katika

mwendo mkubwa. Kama nilivyosema gari hizi nyingi asilimia zaidi ya 50 zipo

mjini zaidi. Sisi tunahakika kwamba hizi gari tutakapoziondoa moja kwa moja na

ndio lengo letu kuziondoa moja kwa moja basi wanaweza kuzitumia kwa

matumizi mengine, lakini kwa vile ajali ni nyingi tunaomba sana tuendelee

kukubali kwamba zile gari zisiendelee kufanya kazi tena. Ahsante Mhe. Spika.

Mhe. Ali Suleiman Ali: Mhe. Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mhe. Waziri wa

Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kwa ruhusa yako naomba kuuliza swali la nyongeza.

Mhe. Spika, mimi naipongeza serikali kwa kuwaza wazo hilo muhimu, juu ya kusema

kwamba gari zenye tairi moja ziondoke lakini swali langu liko hapa tunapotembea

pengine na Mhe. Waziri kapata nafasi hizo tumetembea katika sehemu mbali mbali

mfano Ethiopia, Zambia, Rwanda, Tanzania Bara pia ndani ndani zipo gari hizi bado

zinatumika na kwa hapa Zanzibar tunamini usalama wa maeneo yetu yapo karibu na hali

hiyo Mwenyezi Mungu anatuondoshea ajali hazitokei.

Je, hivyo Mhe. Waziri kwa kuzingatia ajira za watu wetu na huduma mbali mbali kwa

wanyonge gari hizi ziondoshwe wataofaidika si matajiri wenye uwezo wa kununua

magari makubwa.

Mhe. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji: Ahsante sana Mhe. Spika

kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mhe. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji

napenda kujuchukua nafasi hii Mhe. Ali Suleiman Mwakilishi wa wananchi Jimbo la

Kijito Upele swali lake kama ifutavyo:

Tunajua ni kweli lakini hata hivyo maisha ya binadamu nayo ni muhimu katika kipindi

cha Januari mpaka Agosti zimetokea zaidi ya ajali 387 za gari pamoja na pikipiki na vifo

zaidi ya 110. Kwa hivyo tunajua daladala hizi namna gani zinavyohatarisha usalama wa

watu wetu na vile vile mimi nina imani kubwa sana hawa watu ambao nitawaondoa kwa

utaratibu maalum wanalielewa hilo kwa sababu tayari tushatoa elimu kwa hivyo

watustahamilie lakini usalama wa watu wetu ni muhimu zaidi kuliko mali zetu. Ahsante

Mhe. Spika.

Mhe. Spika: Ahsante swali la mwisho linaulizwa na Mhe. Omar Seif Abeid Mwakilishi

wa Wananchi Jimbo la Konde.

Mhe. Omar Seif Abeid: Mhe. Spika, kwa ruhusa yako naomba nijibiwe swali langu

nambari 46 lakini kabla ya kunijibu niliomba Mhe. Waziri afanye marekebisho kwa

sababu swali langu mimi lilikuwa linahusiana na barabara ya Mtambwe sio Mtambile

ilikuwa ni Mtambwe Daya sio Mtambili Daya kwa hivyo baada ya hapo naomba swali

hili lijibiwe ahsante.

27

Nam. 46

Kumong’onyoka kwa Barabara ya Mtambwe – Daya, Pemba

Mhe. Omar Seif Abeid – Aliuliza:

Kwa kuwa Barabara ya Mtambwe-Daya katika eneo la Kinyasini kwa Yakob eneo hilo

lilimong’onyoka na kuanza kuonesha athari kubwa jambo ambalo lilipelekea kurejewa

matengenezo ya ujenzi kwa eneo hilo lakini hata hivyo muda mfupi tu baadae kutokana

na mvua kubwa zilionyesha za masika, eneo hilo limeshaanza kukatika tena licha ya

kujengwa kwa mawe na kutumia waya Maalum.

(a) Je, Wizara inafahamu kwamba eneo la barabara limeshaanza kukatika tena.

(b) Je, wataalamu watachukuwa hatua gani za dharura kulihami kabla athari kubwa

zaidi haijatokea.

Mhe. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Alijibu:

Ahsante sana Mhe Spika, kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mhe. Waziri wa Ujenzi,

Mawasiliano na Usafirishaji napenda kumjibu Mhe. Omar Seif Abeid suala lake Nam. 46

lenye vipengele (a) na (b) baada ya kufanya marekebishi ni kweli aliyosasema ni

kwamba.

Barabara ya Mtambwe-Daya ni miongoni wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilomita

32 zilizojengwa kupitia ufadhili wa MCC na kukamilika miaka minne iliyopita. Kutokana

na maumbile ya ardhi ya barabara ya Mtambwe-Daya, maeneo mengi yalijazwa udongo

na kifusi kwa kiwango kikubwa na baada ya mvua kunyesha baadhi ya maeneo hayo

likiwemo la Kinyasini kwa Yakob yaliaanza kukatika na hivyo kulazimika kumtafuta

Mkandarasi mwingine wa kuzifanyia matengenezo maalumu sehemu hizo kwa kujengwa

mawe yaliyopangwa kwenye nyavu maalum wenyewe wanaita (gabion) ili kuzuia

kukatika kwa barabara hiyo.

Mhe. Spika, baada ya maelezo hayo sasa naomba kujibu kama ifuatavyo;-

a) Ndio Wizara yangu inafahamu kuwa eneo hilo limeanza tena kukatika baada ya mvua
kubwa za masika zilizonyesha mfululizo mwezi April na Mei 2017, na juzi tarehe 22

mimi nilikwenda kuangalia athari hiyo.

b) Watalaam wa Wizara wanalifanyia kazi eneo hilo na mengineyo yaliyoathirika
kutokana na mvua zilizonyesha mfululizo mwezi Aprili na Mei 2017 ili kubaini

chanzo cha kukatika kwa maeneo hayo na kuyafanyia tathimini ambapo baadhi ya

maeneo ya barabara za Pemba yaliyoathirika tayari yameshafanyiwa tathmini ya

gharama kwa ajili ya matengenezo ambayo yatafanywa kwa awamu kulingana na

upatikanaji wa fedha. Ahsante Mhe. Spika.

28

Mhe. Omar Seif Abeid: Ahsante sana Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi ya kumuuliza

swali dogo la nyongeza Mhe. Waziri pamoja na majibu mazuri sana yenye kutia moyo

kwa ajili ya watumiaji wa barabara hiyo Watu wa Mtambwe na Wazanzibari wote kwa

jumla ambao wanatusikiliza.

a) Kwa kuwa wataalamu wameshakwenda na kuona hiyo athari iliyojitokeza na kwamba
hatua za dharura sasa zinahitajika kutokana na eneo lile kwamba tutakapoliwachia

linaweza likaendelea na kuingiza hasara zaidi mimi ningependa kujua ni kipindi gani

kinatarajiwa kulifanyia marekebisho ya kudumu tukapata ufumbuzi wa kudumu wa

eneo lile ambapo mara ya kwanza lishafanyiwa na mara ya pili lishafanyiwa na mara

ya pili lishajitokeza tena.

b) Ni kiasi gani cha fedha ambacho baada ya wataalamu kukagua kitahitajika kwa
kufanya haya marekebisho ambayo yatakuwa ya muda mefu ili kuhakikisha

halitaendelea tena kukatika eneo lile lilokuwa linakatika mara kwa mara. Ahsante

sana Mheshimiwa.

Mhe. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji: Ahsante sana Mhe.

Spika, kwa ruhusa yako napenda kuchukua nafasi hii kumjibu Mhe. Omar Seif Abeid

maswali yake ya nyongeza yenye kifungu (a), (b) kama ifuatavyo.

Kama ulivyosema yako maeneo mengi ambayo baada ya mvua kubwa hivi yameathirika

watalamu wetu wameenda kuchukuwa udongo ili kuchukuwa ufanywe test baada ya

kufanya udongo ule test basi tutajua ni kiasi gani tutataka kutumia katika kufanyia

marekebisho sehemu zile.

Kama ulivyosema kwamba kiasi cha fedha kitajulikana baada ya kufanya tathmini na

pale ambapo tutapata fedha basi haraka tutandelea kufanya marekebisho sehemu zile,

kwani kuna sehemu zilitokea athari hizo wakati wa mvua na takribani anazijua zikiwemo

Chamangwana na sehemu nyengine tofauti na kishatumia takribani milion 200,000,000.

kwa hili namuhakikishia kwamba baada ya kufanya tathmini tunaendelea kuhakikisha

kwamba tunazirekebisha zile sehemu ili barabara zile ziendelee kutumika kwa muda

mrefu zaidi. Ahsante Mhe. Spika.

Mhe. Maryam Thani Juma: Ahsante sana Mhe. Spika, na mimi kunipa nafasi ya

kuuliza swali moja la nyongeza lenye kitoto (a) na (b) kama ifuatavyo:

Pamoja na majibu mazuri Mhe. Waziri uliyotupa lakini nataka kuuliza swali hilo

kuhusiana na barabara ya Wete – Gando ambayo nayo imekatika. Jee Mhe. Waziri nataka

nijue kwamba Mhusika wa kuitengeneza barabara ile au eneo lile lilokatika ni Wizara

ama ni nani na kama ni Wizara ni sababu iliyofanya hadi leo eneo lile halijetengenezwa

hadi sasa.

Mhe. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji: Ahsante sana Mhe. Spika

kwa ruhusa yako napenda kuchukua nafasi hii kumjibu Mhe. Maryam Thani Juma

29

Mwakilishi wa wananchi Jimbo la Gando swali lake lenye kifungu (a) na (b) kama

ifuatavyo:

Ile barabara baada ya kujengwa na Mkandarasi wa MECO muda wake ambao unakuwa

mwaka mmoja ulipita hivi sasa dhamana wa kutengeneza barabara ile ni chini ya Wizara

yetu kupitia Idara ya UUB.

Kama nilivyosema kwamba tayari tumeshaanza kufanya marekebisho lakini tunataka

baadaye tuweke na lami kabisa, lakini kama nilivyosema mwanzo barabara ile kama

ilivyokuwa barabara ya Mtambwe Daya tunachukuwa udongo wake wa kufanyia test kwa

sababu kama ulivyosema baada ya kuathirika na mvua imeonekana kwamba ule udongo

unajivuta kwa hiyo kuifanya ile barabara isidumu. Ahsante Mhe. Spika.

Mhe Spika: Ahsante wakati wa maswali umekwisha Waheshimiwa Wajumbe kama

mtakumbuka kwamba inabidi sasa hivi tuahirishe shughuli zetu mpaka saa 11:00 kwa

hiyo hoja inayofuata itakuja kuingia kuanza kujadiliwa kuanzia saa 11:00 kwa maana

hiyo nachukua nafasi hii sasa kusitisha shughuli za Baraza mpaka saa 11:00 kamili jioni

ya leo.

(Saa 4:15 asubuhi Baraza liliahirishwa hadi saa 11:00 jioni)

(Saa 11:00 jioni Baraza lilirudia)

Mhe. Mwenyekiti, (Mwanaasha Khamis Juma) alikalia kiti

HOJA ZA SERIKALI

Ripoti ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya

Utekelezaji wa Maagizo ya Kamati ya Fedha, Biashara na

Kilimo kwa Mwaka 2016/2017

Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Mhe. Mwenyekiti, kwanza

kabisa naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na utukufu kwa

kutukutanisha hapa tukiwa wazima na afya njema na zaidi tukiendelea kuongozwa na

Mhe. Rais wetu mpendwa Dkt. Ali Mohammed Shein pamoja na wasaidizi wake wote.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu azidi kutupa amani na utulivu, ili hatimaye atukabidhi

kijiti 2020 Mwenyezi Mungu akitujaalia. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, naomba kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe binafsi kwa kunipa

fursa hii adhimu ya kuwasilisha Utekelezaji wa Maagizo ya Kamati ya Fedha, Biashara

na Kilimo ya Baraza lako tukufu, kama ambavyo walitupatia wakati walipokuwa

wakifanya kazi za kamati katika wizara yangu kwa lengo la kuimarisha utendaji na kuleta

ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya wizara.

Aidha, napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha,

Biashara na Kilimo, Mhe. Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni, Yussuf Hassan Idd, Makamo

30

Mwenyekiti ambaye ni wewe mwenywe Mhe. Mwenyekiti, nafasi ya wanawake Mhe.

Hamida Abdalla Issa pamoja na wajumbe wote wa kamati hiyo kwa ushauri, maelekezo

na mashirikiano waliyotupatia muda wote wakati wakitekeleza majukumu yao kwa lengo

la kuimarisha kazi zetu za kila siku. Ni imani yangu kuwa ushauri na maelekezo

waliyotupatia yamesaidia sana katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya wizara

yangu kwa ufanisi zaidi. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi inaendela kusimamia

na kutekeleza malengo ya Dira 2020 ya Zanzibar, Ilani ya Uchaguzi wa CCM 2015 –

2020, Mkakati wa Kukusa Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUZA), Malengo ya

Maendeleo Endelevu (SDGs 2015 – 2025), Mpango wa Mageuzi ya Kilimo (ATI),

Mpango wa Muda Mrefu wa Usimamizi wa Rasilimali za Misitu, Mpango Mkuu wa

Umwagiliaji Maji na Mpango Mkakati wa Kuimarisha Usimamizi wa Uvuvi. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo chini ya Mwenyekiti wake Mhe.

Yussuf Hassan Iddi ilipata fursa ya kupitia sekra zote za wilaya za wizara hii Unguja na

Pemba kwa lengo la kukagua na kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti kutoka taasisi na

idara tofauti za wizara, pamoja na kupokea taarifa za utekelezaji wa bajeti na majukumu

ya wizara.

Mhe. Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo mafupi sasa naomba niende moja kwa moja

kwenye maagizo ya kamati na utekelezaji wake uliofanyika.

Kwanza ni Idara ya Kilimo ambayo ilikuwa na mambo saba.

Agizo nam. 1. Kamati ilisema wizara iwasiliane na wazabuni wanaoleta pembejeo za

kilimo ili pembejeo hizo ziwafikie wakulima kwa wakati.

Utekelezaji. Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango tayari imepata

mzabuni Bajuta International (T) Ltd ya Arusha kwa ajili ya kuleta tani 700 za mbolea

(TSP). Tani 900 za Urea, mbegu tani 350, pamoja na dawa za kuulia magugu lita 15,000.

Serikali tayari imelipa mzabuni deni la nyuma la pembejeo la shilingi 600/= milioni.

Kupitia programu ya ERPP tani 306 za Urea na tani 152 za DAP mbolea zimenunuliwa

kwa ajili ya kuendeleza wakulima wa mpunga wa umwagiliaji maji.

Mhe. Mwenyekiti, taarifa ya ziada Kampuni ya Bajuta tayari imewasilisha tani 100 za

mbolea (Tani 65 Urea na tani 35 DAP), kwa ajili ya kilimo cha mpunga wa umwagiliaji

maji. Hivyo, wakulima kuanzia sasa wanapata mbolea bila ya matatizo yoyote. (Makofi)

Agizo nam. 2. Wizara kwa kushirikiana na Masheha na Serikali za Wilaya ihakikishe

mabonde yanayotumika kwa shughuli za kilimo na maeneo ya vianzio vya maji

hayavamiwi.

Utekelezaji. Wizara inashirikiana na masheha, Kamati za Kilimo za maeneo ya Serikali

za Wilaya katika kuhamasisha wananchi juu ya matumizi bora ya maeneo ya kilimo,

kutunza vyanzo vya maji na utunzaji wa mazingira, ili kuhakikisha mabonde yaliyo chini

31

ya usimamizi wa wizara yanatumika kwa kazi za kilimo. Aidha, wizara kwa kushirikiana

na FAO inatekeleza mradi wa kuhifadhi mito kama vile Mwanakombo, Chaani na

Kianga. Mpango huu pia unawafundisha wakulima na wana jamii juu ya utunzaji wa

vyanzo vya maji na mazingira.

Mhe. Mwenyekiti, taarifa ya ziada serikali imetuagiza tuanze kazi ya kuyapima maeneo

yote ya kilimo, ambapo kazi hii inatarajiwa kuanza robo ya pili ya mwaka wa fedha

2017/2018. Aidha, jumla ya shilingi 12, 377,200 zimetengwa kwa ajili ya upimaji wa

maeneo ya kilimo.

Agizo nam. 3. Wizara itoe elimu kwa wakulima juu ya mpango wa wizara kwa kununua

pembejeo za kilimo kutoka kwa wakulima, ili kuondoa malalamiko yasio ya lazima.

Utekelezaji. Wizara kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wakulima imeshatoa elimu katika

mabonde ya Tibirinzi, Weni, Mangwena na Dobi kwa mabonde ya umwagiliaji maji na

Kohowe, Msaani, Chanjaani kwa mpunga wa kutegemea mvua juu ya mpango wa

kununua mbegu kutoka kwa wakulima kwa ajili ya msimu wa mwaka 2017/2018. Aidha,

jumla ya tani 15.5 za mbegu ya mpunga tayari zimenunuliwa. Kazi hii imeanza vizuri na

wakulima wamelipwa kwa mujibu wa taratibu na hakuna mkulima yeyote aliyekopwa

mwaka huu.

Agizo nam. 4. Wizara itoe ushirikiano wa dhati kwa wawekezaji wote wanaowekeza au

wanaokusudia kuwekeza kwenye sekta zinazosimamiwa na Wizara ya Kilimo.

Utekelezaji. Wizara kwa kushirikiana na Tume ya Mpango na Mamlaka ya Uwekezaji

Zanzibar, inaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa wawekezaji. Aidha, wizara kwa

kushirikiana na ZIPA imesajili miradi ya umwagiliaji maji kwa kampuni ya NETAFIM ya

India na Kampuni ya ENCHELON kwa ajili ya uzalishaji wa sukari ya Stevia huko

Bambi.

Agizo Nam. 5. Wizara ishajihishe wananchi kulima kilimo cha spices, kwani kilimo hiki

kimekuwa na soko kubwa ulimwenguni.

Utekelezaji. Wizara kwa kushirikiana na Asasi Zisizo za Serikali, ikiwemo Zenj Spices ya

Zanzibar (Zanzibar Organic Spices Growers) na Kamapuni ya Lecon ya Ujerumani,

imewashijihisha vikundi vya wakulima, uzalishaji wa mazao ya viungo na

kuwaunganisha na masoko ya bidhaa huko Ujerumani. Aidha, wizara inaendelea kutoa

elimu pamoja na upatikanaji wa miche bora, wiara pia imekamilisha ujenzi wa jengo la

usarifu la Kizimbani na inaendelea kukamilisha ujenzi wa kituo cha usarifu wa mazao

Pujini, Pemba. Mpango wa Mkakati wa Mazao ya Viungo na Minazi umetayarishwa

kupitia Idara ya Misitu na Kilimo.

Agizo nam. 6. Wizara indelee na jitihada zake kwa kutumia fedha za OC kwa kufanya

ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji maji pale hali inaporuhusu, ili huduma hii

iwafikie wakulima wote kwa maeneo yao.

32

Utekelezaji. Kwa kutumia fedha za OC wizara imekarabati misingi ya umwagiliaji maji

katika mabonde ya Cheju mita 200, Kibokwa mita 300, Mwera 50, Bumbwi Sudi 180 na

Uzini mita 100 kwa Unguja. Kwa upande wa Pemba wamekarabati umefanyika katika

bonde la Mangwena mita 100 pamoja na bwawa la Kangagani kwa kushirikiana na

Costech. Kazi hii Mheshimiwa inaendelea. (Makofi)

Agizo nam. 7. Wizara indelee kufuatilia ili kuhakikisha Shirika la Umeme (ZECO)

linafanya matengenezo ya nguzo zilizoinama katika bonde la Cheju.

Utekelezaji. Wizara imewasiliana na Shirika la Umeme na tayari shirika limeshabadilisha

nguzo sita za umeme zilizokuwa zinahofiwa kuleta madhara. Aidha, wizara inaendela

kushirikiana na Shirika la la ZECO kwa kubadilisha nguzo nyengie saba zilizoanguka

hivi karibuni kufuatia mvua kubwa za masika.

Idara ya Maendele ya Mifugo ina hoja 12.

Agizo nam. 1. Serikali kupitia wizara iandae utaratibu maalum wa kudhibiti uingizaji wa

bidhaa za mifugo kutoka nje ya nchi hasa zile ambazo zinazalishwa kwa wingi hapa

ndani.

Utekelezaji. Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi itashirikiana na Bodi ya

Chakula na Vipodozi, Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha kuandaa kanuni ya udhibiti

wa uingiaji (Export/Import Regulation ) za bidhaa za mifugo.

Agizo nam. 2. Kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wafugaji.

Utekelezaji. Wizara imetoa elimu ya ufugaji bora wafugaji kuku, mbuzi, ng’ombe wa

maziwa kwa vikundi 131, Unguja 351 na Pmba 80. Vile vile kupitia Madaraka Mikoani

ugatuzi baadhi ya maofisa wa mifugo wa uzalishaji wamehamishiwa katika Halmashauri

za Wilaya ili kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa wafugaji. (Makofi)

Agizo nam. 3. Wizara iongeze ajira kwa wataalamu wa mifugo ili tuwe na wataalamu wa

kutosha.

Utekelezaji. Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kupitia Wizara ya Nchi (OR)

Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeomba nafasi za ajira 68 kwa

maafisa wa mifugo. Vile vile kupitia programu ya ASSP/ASPD-L, wizara imeteuwa na

kuwajengea uwezo wa kitaaluma na kuwapatia vifaa vya huduma binafsi na tiba kwa

jamii 204, Unguja 108 na Pemba 96 kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya mifugo

katika ngazi ya shehia. Wizara katika kipindi cha miaka mitatu imepeleka nchini China

jumla ya vijana 15 kwa ajili ya mafunzo ya udaktari wa mifugo. Vile vile kwa mwaka

fedha 2017/2018 wizara imesajili vijana 16 ambao watakwenda China kwa ajili ya

mafunzo ya udaktari wa mifugo.

Agizo nam. 4. Wizara iendelee kutafuta wawekezaji kwa ajili ya kuanzisha viwanda vya

kuzalisha pembejeo za mifugo na kilimo.

33

Utekelezaji. Wizara kwa kushirikiana na ZIPA inaendelea na jitihada za kutafuta

wawekezaji kwa ajili ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha pembejeo za mifugo na kilimo.

Agizo nam. 5. Serikali ianzishe mpango maalum wa kuhamasisha wananchi kula bidhaa

za mifugo kama vile mayai na maziwa ikiwemo na siku maalum ya kunywa maziwa.

Utekelezaji. Wizara itarejesha tena Siku Maalum ya Kunywa Maziwa Zanzibar kila

mwezi wa Juni. Vile vile kupitia Idara ya Uhakika wa Chakula na Lishe programu

maalum ya lishe maskulini inaendelea kutoa taaluma na uhamasishaji wa utumiaji wa

maziwa skuli.

Agizo nam 6. Wizara iandae mpango wa kuanzisha kituo cha utafiti wa mifugo ili

kufanya tafiti za aina mbali mbali.

Utekelezaji. Serikali tayari imeshaanzisha taasisi ya utafiti wa mifugo kwa lengo la

kuendeleza utafiti wa mifugo hapa nchini. Katika mpango kazi wa taasisi hiyo, mpango

wa utekelezaji wa utafiti unaandaliwa katika robo ya pili ya mwaka huu.

Agizo nam. 7. Kutokana na ongezeko kubwa la ukuaji wa Sekta ya Kilimo, sambamba na

ukuaji wa Sekta ya Mifugo, tayari yameanza malalamiko ya maeneo ya wazi kwa

wakulima na wafugaji, ili kunusuru migogoro ambayo inaweza kujitokeza hapo baadae.

Serikali ianzishe mpango maalum kwa kutengeneza maeneo ya mifugo.

Utekelezaji. Wizara inaendelea kuwashajihisha wafugaji kufuga ufugaji wa kisasa zero

grazing, ili waweze kutumia eneo dogo la ardhi kwa kufuga ng’ombe wachache wa kisasa

na wenye tija na kuacha kufuga ufugaji wa kizamani wa kutumia kamba. Jitihada zaidi

zinafanyika kwa wafugaji kupanda majani na kulisha masalia ya mazao.

Agizo nam. 8. Wizara itafute namna bora zaidi ya kuliimarisha na kuliendeleza Shamba

la Mifugo Pangeni kwa lengo la kuimarisha Sekta ya Mifugo.

Utekelezaji. Wizara inaendelea na jitihada ya kuliimarisha na kuliendeleza Shamba la

Mifugo Pangeni kwa kutumia kwa kazi za mifugo na kualisha mitamba ya ng’ombe wa

kisasa wa maziwa kwa ajili ya kuuziwa mifugo wafugaji wadogo wadogo. Kwa mwaka

2017/2018, wizara imejiandaa kuweka mbinu ya maji na kutekeleza njia ya kuelekea

Shamba la Mifugo Pangeni.

Agizo nam. 9. Wizara iandae mpango maalum kwa kuongeza idadi ya mifugo katika

shamba la mifugo Pangeni pamoja na kuzuwia kuuza mifugo inayozaliwa katika shamba

hilo kwa muda.

Utekelezaji. Wizara imechukua ushauri na mapendekezo yaliyotolewa kwa muda huu

ng’ombe 32 waliobaki wataendelezwa na kuimarishwa hapo shambani.

34

Agizo nam. 10. Wiara itafute suluhisho la maji katika Shamba la Mifugo Pangeni.

Kupitia Mradi wa Miundombinu na Kuendeleza Wafugaji Wadogo Wadogo.

Utekelezaji. Wizara imetenga fedha kutoka serikali, ambapo pamoja na kazi nyengne pia

kazi ya kuchimba kisima itafanyika ili kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji katika

Shamba hilo la Mifugo Pangeni.

Agizo nam. 11. Wizara ihakikishe upatikanaji hatimiliki wa shamba hilo.

Utekelezaji. Tangu miaka 60 eneo la Shamba la Pangeni limepimwa, limechorwa ramani

na limetengwa maalum kwa kazi ya mifugo. Aidha, suala la upatikanaji wa hatimiliki

linaendelea.

Agizo nam. 12. Wizara ianzishe mpango maalum wa kuifanyia matengenezo njia ya

kuelekea Shamba la Pangeni.

Utekelezaji. Wizara inaendelea na jitihada ya kuifanyia matengenezo njia ya kuelekea

Shamba la Mifugo Pangeni kupitia mradi wa miundombinu ya mifugo.

Idara ya Misitu na Mali Zisizorejesheka ina hoja 16

Agizo nam. 1. Wizara kwa kushirikiana na taasisi husika iendelee kukomesha matumizi

ya msumeno wa moto.

Utekelezaji. Wizara kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama inaendelea na

kampeni ya kuzuwia matumizi ya msumeno wa moto hapa nchini. Miongoni mwa juhudi

hizo ni pamoja na kufanya doria ya kuikamata na kuichoma moto misumeno hiyo. Jumla

ya misumeno 55 Unguja 31 na Pemba 24 imekamatwa na kuhifadhiwa na Idara ya

Misitu, kazi ya msako inaendelea kupitia masheha na vyombo vya ulinzi.

Mhe. Mwenyekiti, juhudi za kuelimisha wananchi juu ya umarufuku wa matumizi ya

msumeno ya moto zinaendelea, lakini bado hatujapata mashirikiano ya kutosha na

masheha ambao ndio walio karibu sana na wananchi.

Agizo nam. 2. Kuwe na usimamizi na utaratibu wa uchimbaji wa maliasili

zisizorejesheka.

Utekelezaji. Wizara inaendelea kukusanya taarifa kuhusu mahitaji na matumizi ya

maliasili zisizorejesheka (resource survey and/or assessment) kwa ajili ya kutayarisha

mpango mkakati wa matumizi endelevu ya maliasili hizo hapa nchini. Aidha, wizara

imetayarisha mpango kazi wa mwaka 2017/2018 kwa usimamizi wa matumizi ya mali

zisizorejesheka.

Agizo nam. 3. Serikali ianzishe sera maalum ya ‘Green Policy’ ili tuweze kupanda miti

kwa wingi katika nchi yetu.

35

Utekelezaji. Wizara tayari imeandaa mpango mkakati kwa ajili ya kutekeleza upandaji

miti mijini na vijijini kama ilivyoelekezwa katika sera na sheria za misitu Zanzibar.

Aidha, mpango huo unatekelezwa katika siku maalum ya upandaji miti kitaifa

unaofanyika katika mwezi wa Machi kila mwaka. Mkakati huu unahusu upandaji wa miti

ya minazi, mikarafuu, miti ya matunda na kivuli katika maeneo ya barabara na maeneo

yaliyopo matupu. Pia wananchi hupatiwa miti hiyo bure kupitia masheha.

Agizo nam. 4. Wizara itoe taarifa maalum mbele ya Baraza hili tukufu hali halisi ya

uchimbaji mchanga ili Wajumbe wa Baraza hili pamoja na wananchi waelewe dhamira

ya serikali juu ya matumizi ya rasilimali ya mchanga.

Utekelezaji. Wizara tayari imeshatoa taarifa serikalini na kwa wananchi kuhusu hali ya

upatikanaji wa mchanga hapa nchini. Wizara iko tayari kuwasilisha taarifa maalum

kuhusu hali halisi ya uchimbaji mchanga hapa Zanzibar mara baada ya kupata ridhaa ya

Baraza la Mapinduzi na hatimaye kuwasilisha hapa Baraza la Wawakilishi.

Agizo nam. 5. Wizara iangalie upya mgao wa mapato unaoingia katika Idara ya Misitu

kwa kupitia misitu ya Jozani. Je, idara inastahiki kupata mgao huo?

Utekelezaji. Wizara itafanya mapitio kuhusu mgao wa mapato yanayotokana na

makusanyo ya Jozani. Idara inastahiki kupata mgao huo kwa mujibu wa kanuni iliyopo.

Hata hivyo, mgao wa mapato ya Jozani upo kwa mujibu wa sheria Nam. 10 ya

Usimamizi wa Misitu ya mwaka 1996 kupitia Kanuni Nam. LN 26 ya mwaka 2009,

ambayo imeweka utaratibu wa mgawanyo wa mapato yanayopatikana katika hifadhi

hiyo. Utaratibu huo ni kama ifuatavyo:

Asilimia 40 ya mapato yote yanatumika kwa uendelezaji wa hifadhi yenyewe,
Asilimia 30 ni kwa ajili ya kulipa fidia kwa wenye mashamba eneo la Jozani,
ambao mazao yao yanaharibiwa na kimapunju.

Asilimia 20 ni kwa ajili ya Idara ya Misitu na
Asilimia 10 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jamii katika vijiji tisa
vinavyozunguka hifadhi ya Jozani.

Agizo nam. 6. Msitu wa Jozani unao mgao wake kwa ajili ya kuendesha shughuli za

misitu. Hivyo itumie fedha hizo kutatua changamoto zake zikiwemo kuunganisha

internet katika eneo hilo.

Utekelezaji. Fedha zinazopatikana katika mgao wa Jozani zimetumika kwa ajili ya

usimamizi wa maendeleo ya hifadhi ya Jozani. Wastani wa shilingi 15 milioni

zimetengwa kwa kazi ya ufungaji wa internet kupitia Kampuni ya Simu ya Halotel. Jamii

zinazozunguka hifadhi ya Jozani zinanufaika na mapato ya msitu huo, jumla ya shilingi

155 milioni zimegawiwa kwa wanajamii kwa kipindi cha miezi sita tu, Januari mpaka

Juni 2017.

Agizo nam. 7. Wizara iandae mpango wa kuongeza nafasi za ajira za misitu.

36

Utekelezaji. Wizara imetayarisha mpango wa rasilimali watu na kuwasilisha serikalini

ambapo unaonesha mahitaji ya wafanyakazi kwa kila sekta. Aidha, vijana watano, wanne

wa misitu na mmoja wa nyuki ambao wamesomesha na Mradi wa Hima waliomaliza

masomo ya Diploma wameajiriwa mwezi wa Septemba, 2017 na vijana saba waliomaliza

masomo ya Diploma mwezi waa Juni, 2017 kati ya fani ya misitu wanatarajiwa

kuombewa ajira hivi karibuni.

Agizo nam. 8. Wizara iendelee kutoa elimu ya kutosha katika maeneo mbali mbali, ili

kuhamasisha wananchi kutembelea katika misitu sambamba na kutangaza misitu hiyo

ndani na nje ya nchi. Hili agizoa la 8 na 9 yanakwenda pamoja Mhe. Mwenyekiti, yaani

wizara iongeze jitihada za kutangaza misitu ndani na nje ya nchi.

Utekelezaji. Wizara imeandaa mpango mkakati kwa Kitengo cha Uhamasishaji wa Misitu

ya Jamii na pia kupitia katika tovuti ya wizara. Idara inaendelea kutangaza misitu ya

Zanzibar ndani na nje ya nchi. Aidha, kwa kushirikiana na Kamisheni ya Utalii na

Kampuni ya watembezaji watalii katika kuitangaza misitu hiyo ndani na nje inaendelea.

Agizo nam. 10. Wizara iandae mpango wa kupatikana usafiri wa uhakika kwa ajili ya

usimamizi wa misitu.

Utekelezaji. Wizara imeaanda mpango wa upatikanaji wa usafiri kwa ajili ya maendeleo

ya msitu. Jumla ya gari tatu zenye thamani ya shilingi milioni 180 zitanunuliwa katika

robo ya pili ya mwaka wa fedha 2017/2018. Gari hizo zitanunuliwa kupitia mfuko wa

Jozani, gari moja kwa mapato yanayotokana na makusanyo ya mchanga gari mbili

milioni 120.

Agizo nam. 11. Uongozi wa misitu uendelee kutoa mashirikiano ya karibu na wanavijiji

wanaozunguka msitu, ili wawe walinzi wazuri wa misitu. Wizara imewawezesha

uundwaji wa kamati 57 za uhifadhi wa msitu wa jamii kwa Unguja na Pemba.

Agizo nam. 12. Wizara iendelee kutumia wataalamu watu ili kubuni vivutio vingine vya

watalii na wananchi wanaokwenda kutembelea kwenye misitu.

Utekelezaji. Wizara inaendelea kutumia wataalamu katika kubuni na kuwasajihisha

wanachi kutumia vituo vya utalii vilivyomo kwenye misitu ya Zanzibar, ikiwemo Misitu

ya Masingini, Jozani, Kiwengwa na Ngezi.

Katika msitu wa Masingini ujenzi wa mnara umekamilika na ujenzi wa miundombinu

mingine ya kuendeleza kituo hicho inaendelea kujengwa. Aidha, serikali imetoa shilingi

50 milioni kuendeleza hifadhi hiyo.

Agizo nam. 13. Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni,

iangalie uwezekano wa kujenga njia ya kuelekea msitu wa Ngezi. Wizara inaahidi

kwamba itashirikiana na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na

Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, ili kutafuta mbinu za kujenga barabara hiyo pale

ambapo uwezo wa kifedha utaruhusu.

37

Agizo nam. 14. Wizara kwa kupitia mapato yanayotokana na msitu wa Ngezi ijenge

majengo kwa ajili ya wafanyakazi. Wizara inakusanya wastani wa shilingi milioni 6 kwa

mwaka kutokana na mapato ya watalii katika msitu wa Ngezi, mapato hayo hayakidhi

ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wafanyakazi. Aidha, wizara inatayarisha mpango kazi

ambao utasaidia kuinua mapato katika hifadhi hiyo na kufanya mapitio ya bei ya

kuingilia kwa watalii. Jitihada zinafanyika za kuwasiliana na wafadhili ambao watasaidia

kuendeleza hifadhi hiyo ya Ngezi. Kwanza tunashukuru Shirika la Norway kwa

kuendeleza msitu huu wa Ngezi kwa nguvu zao zote. (Makofi)

Agizo la 15. Wizara iongeze juhudi ya kupanda miti ya asili katika eneo la msitu wa

Masingini. Wizara inaendelea na utaratibu wa kuongeza upandaji wa miti ya asili ili

kuongeza uhifadhi wa asilia katika hifadhi ya Masingini, ambapo msimu wa mwaka 2016

miti 30,100 ya asali na matunda hekta 26 ikiwemo mikungu, mikangazi, mifenesi, pilipili

doria, mifuu, mitufaa, mizambarau, miharita, mitondoo, mibirimbi, mishokishoki,

midoriani, miembe na miti ya ulaya imepandwa. (Makofi)

Agizo nam. 16. Wizara iangalie uwezekano wa kuanzisha mkahawa yaani Restaurant

katika msitu wa Masingini ambao utakuwa na vyakula vya asili, vikiwemo mihogo, viazi

na mashelisheli, ili uweze kujitangaza zaidi. Wizara imetayarisha mpango kazi wa

uendelezaji wa hifadhi ya msitu wa Masingini. Ujenzi wa mkahawa unatarajiwa kuanza

katika robo tatu ya mwaka 2017/2018. Jumla ya shilingi milioni 60 zimeombwa serikalini

kwa ajili ya ujenzi wa mkahawa huo.

Idara ya Utumishi Uendeshaji ina hoja 6

Hoja ya 1. Serikali itamke rasmi kwa yeyote anayemiliki shamba la serikali kinyume na

utaratibu, alirudishe na itowe tamko kali kwa atakayekataa kulirudisha.

Utekelezaji. Wizara kwa hatua ya kwanza imetoa tamko rasmi. Aidha, wizara kwa

kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vitamchukulia hatua za kisheria mtu

yeyote atakayekiuka tamko hili. Mhe. Mwenyekiti, pia wizara inaomba Waheshimiwa

Wajumbe wa Baraza lako tukufu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na

Masheha na wananchi wote watoe ushirikiano wa dhati kwa wizara, ili kuyatambua

mashamba yaliyobaki na yaweze kutumika kwa maslahi ya wananchi. Wizara itatoa

tamko rasmi kwa kupitia vyombo vya habari kwa kushirikiana na wizara zenye dhamana

ya biashara na tawala za mkoa.

Hoja ya 2. Utaratibu wa ukodishaji wa mashamba ya serikali, tuwe wazi ili kuepuka

malalamiko yaliopo. Ukodishwaji wa mashamba ya serikali yamefanyika kwa uwazi,

ambao zabuni zilitangazwa kwa kupitia vyombo vya habari vya ndani, ikiwemo redio

Zanzibar na gazeti la Zanzibar Leo.

Aidha, jumla ya mashamba 4 yamekodishwa kwa zabuni na mashamba 1460

yamekodishwa kwa mnada. Wastani wa shilingi bilioni 2.1 zilikusanywa kwa

38

ukodishwaji wa mashamba ya serikali ya mikarafuu, kinyume na hapo nyuma ambapo

hatuzidi kupata milioni 200 au milioni 300.

Hoja ya 3. Wizara kwa kushirikiana na wizara ya utumishi wa umma itowe vipaumbele

vya ajira kwa wataalamu wa kilimo, mifugo na uvuvi ili kuimarisha sekta hizo nchini.

Utekelezaji. Wizara kwa hatua ya kwanza imeajiri wafanyakazi 37 kwa Unguja na

Pemba. Hatua ya pili, wizara imewasilisha maombi 72 ya kujaza nafasi tupu. Wizara pia

imeorodhesha wahitimu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani kwa mazingatio ya ajira ya

mabibi shamba na mabwana shamba. Taarifa hizo zimewasilishwa Wizara ya Nchi Ofisi

ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mazingatio.

Hoja ya 4. Wizara ihakikishe watumishi wote walioondoka na vyombo vya moto vya

wizara vinarudishwa wizarani. Wizara imetekeleza agizo hilo ambapo hadi sasa

imekusanya jumla ya magari 13 na pikipiki 15 na kuweka katika utaratibu wa sheria.

Hoja ya 5. Wizara iandae mkakati na utaratibu maalum ili kuhakikisha kuwa wataalamu

wanaosomeshwa na wizara hawaondoki na wanazitumia taaluma zao kwa ajili ya

kuimarisha shughuli za wizara.

Utekelezaji. Wizara imeandaa mkakati wa mafunzo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais

Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa kuwataka watumishi wote

kujaza mkataba huu kabla ya kuanza masomo ili kuwadhibiti wanapomaliza masomo yao

kuendelea na kazi katika ofisi walizotoka. Kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka

2014 kifungu cha 76(1) kinafafanua.

Hoja ya 6. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya,

pamoja na Masheha na wananchi wote watowe ushirikiano wa dhati kwa wizara, ili

kuyatambua mashamba yaliyobaki na yaweze kutumika kwa maslahi ya wananchi. Kazi

hii imeanza kwa kazi kwa upande wa Masheha na Wakuu wa Wilaya, na jumla ya

Mashamba 174 yametambuliwa kwa kupitia kwa Masheha wa Pemba.

Chuo cha Kilimo Kizimbani kina maagizo 3.

Agizo la 1. Mara baada ya Mshauri Mwelekezi kuwasilisha maoni yake na kuangaliwa

kwa kina, wizara iandae mipango haraka kwa matumizi ya shamba hilo. Mshauri

Mwelekezi kwa kupitia mfumo wa zabuni hakupatikana kutokana na kukosa sifa za

kufanyakazi hiyo. Kwa hivyo, SMZ ilishauriana na SMT kuhusu namna bora zaidi ya

upatikanaji wa eneo la Makurunge. Baada ya mashauriano hayo SMZ imetoa muongozo

kwa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Mawasiliano na

Ujenzi ya Tanzania Bara, ili Shirika la Nyumba la Taifa litekeleze kazi ya upimaji wa

Shamba la Makurunge Bagamoyo.

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ilitekeleza agizo hilo na kwa kushirikiana

na NHC, tayari imeandaa makubaliano yenye kuonesha majukumu ya wizara, na

39

majukumu ya NHC katika utekelezaji wa kazi hiyo. Hatua inayofuata ni kukutana na

wataalamu wa pande zote mbili, ili kujadiliana njia bora ya utekelezaji wa kazi hiyo.

Kuhusu upatikanaji wa hati miliki, wizara imearifiwa na Halmashauri kuwa kwa mujibu

wa Sheria ya Mipango Miji ya Tanzania Bara ya mwaka 2007, endapo SMZ itasisitiza

kuendelea kupatiwa hati miliki ya shamba kwa matumizi asili. Halmashauri ya Wilaya ya

Bagamoyo kimsingi haina pingamizi na utoaji wa hati miliki kwa shughuli za kilimo na

mifugo kwa masharti yafuatayo.

Kwanza SMZ ilipie gharama za utengenezaji wa hati hiyo ambazo ni shilingi
za Kitanzania bilioni 1,255,399,115/=.

Kurejesha na kusarenda hati hiyo baada ya mpango wa mji mdogo wa
Bagamoyo kupitishwa rasmi. Kutokana na masharti hayo na kuepuka kwa

gharama kubwa isiyokuwa na lazima. Wizara imeona ni busara kuendelea

kuandaa mpango mpya wa matumizi ya Shamba la RAZABA kama

ilivyoelekezwa na SMZ

Idara ya Mpango wa Sera ya Utafiti ina hoja 18

Hoja ya 1. Wizara itafute njia bora ya kuhakikisha kuwa takwimu zinazotolewa na wizara

zinakuwa sahihi na tuondokane na utaratibu wa kimazoea wa kukusanya

takwimu.

Wizara imetayarisha njia zifuatazo za ukusanyaji wa takwimu sahihi.

Wizara, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu imetoa mfunzo
kwa wafanyakazi 30 juu ya ukusanyaji wa takwimu. Wizara imetayarisha

muongozo wa ukusanyaji, uchambuzi na uandishi wa ripoti ya taarifa za

takwimu kuanzia ngazi ya shehia hadi taifa.

Wizara, imetayarisha kalenda maalum ya ukusanyaji wa takwimu na aina
ya takwimu zinazopaswa kukusanywa.

Wizara, imefanya utafiti wa mazao ambayo yalikuwa hayarikodiwi
ipasavyo, zikiwemo embe, nazi na machungwa ambayo yatasaidia kujua

hali halisi ya uzalishaji wake.

Idara ya Maendeleo na Uvuvi

Agizo. Serikali ihakikishe kusimamia kuzuwia uvuvi haramu, unaofanywa na baadhi ya

wavuvi pamoja na kutafuta vyombo vya kutosha, kwa ajili ya kufanya doria za baharini

na kuwachukulia hatua za kisheria pale wanapobainika.

Utekelezaji. Wizara inashirikiana na vyombo vya dola KMKM na Polisi na jamii kufanya

doria za baharini. Watendaji wa wizara kwa kupitia vyombo vya habari wanatoa elimu ili

kudhibiti uvuvi haramu.

Wizara inazifanyia matengenezo boti zake za doria na ina mpango wa kuziongeza ili

ziweze kukidhi haja.

40

Vile vile wizara iendelee na utaratibu maalum wa usimamizi wa madiko, kwani baadhi ya

madiko yanaonekana hayatunzwi vizuri na yanatumika kinyume na malengo

yaliyokusudiwa.

Utekekezaji. Wizara imeyatathmini madiko na kugundua yafuatayo.

Jumla ya madiko 80 yametathminiwa kati ya madiko 8 yamepatiwa hati miliki ambayo ni

Fumba, Kendwa, Tazari, Nungwi, Matemwe, Pwani Mchangano, Uroa na Kikungwi.

Wizara imeshaomba nafasi za ajira 65 katika wizara husika kwa kufuatilia ufumbuzi

tatizo la wafanyakazi.

Wizara iunge mkono Wenyeviti wa Kamati za Wavuvi ili waweze kutekeleza majukumu

yao ipasavyo pasi na kuingiliwa na watu wengine. Wizara imeunda Kamati ya Wavuvi na

kuendeleza kutoa taaluma za usimamizi endelevu katika kazi ya uvuvi, kwa kupitia

kamati husika.

Aidha, wizara ipo karibu na Wenyeviti wa Kamati za Uvuvi, kwani wao ndio

wasimamizi wakuu katika Sheria husika. Wizara imewaelimisha Wenyeviti wa Kamati za

Wavuvi, ni kuwaelekeza kazi zao ipasavyo kwa kuzingatia sheria na kanuni za uvuvi.

Pia kwa kupitia Mradi wa SWIOFish, wenyeviti pamoja na wajumbe wengine wa kamati

walipatiwa mafunzo maalum, kuhusu utawala bora katika usimamizi wa uvuvi ambayo

yalikuwa na madhumuni ya kuwawezesha kutekeleza usimamizi mzuri wa kazi za uvuvi.

Vile vile, kwa kupitia vikao vya Kamati Tendaji za Wavuvi, wenyeviti hupata nafasi ya

kuelimishwa wajibu wao wa utekelezaji wa majukumu yao, zikiwemo sheria na kanuni

za uvuvi.

Wizara, imeanza mchakato wa kutayarisha muongozo wa utaratibu wa uendeshaji wa

Kamati za Uvuvi. Kwa kupitia muongozo huo wenyeviti watapatiwa mafunzo ya aina

mbali mbali ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Wizara, iendelee kutoa elimu kwa wavuvi ili wafahamu umuhimu wa kuwepo kwa

maeneo ya uhifadhi baharini. Wizara inaendelea kutoa elimu kwa wavuvi juu ya

umuhimu wa uhifadhi wa rasilimali za baharini katika maeneo yote ya bahari, kwa lengo

la kutunza rasilimali hizo na mazingira yake.

Wizara, ihakikishe kuwapatia vitambulisho wajumbe wa kamati za uvuvi ili waweze

kufanyakazi zao kwa kujiamini. Wizara imechapisha vitambulisho na imewachapia

wajumbe wote wa Kamati za Uvuvi. Hata hivyo, baadhi ya kamati zimefanya uchaguzi

hivi karibuni na kupata wajumbe wapya. Wizara pia inakusudia kutoa vitambulisho kwa

wajumbe wapya pamoja na wale ambao hawakupata hapo awali.

Mhe. Mwenyekiti, Kabla ya kuanza ujenzi wizara ijiridhishe kuwa eneo la ujenzi

halitakuwa na athari yoyote ya bahari kwa baadae katika eneo la ujenzi.

41

Utekelezaji. Utafiti wa hali ya bahari pamoja na thamani ya kimazingira zimefanyika, ili

kuhakikisha hakuna athari zozote zinazojitokeza baada ya ujenzi. Aidha, ujenzi wa vituo

vya utafiti na mabwawa utazingatia pia Sheria Nam. 3 ya Mazingira ya Zanzibar,

inayosisitiza kufanyika kwa tathmini ya mazingira.

Tukizingatia kuwa Zanzibar inaelekea katika uchumi wa bahari kuu, soko pia liendane na

ujenzi wa kisasa, ili kuimarisha uvuvi nchini na kuwavutia wawekezaji.

Soko la Samaki litakalojengwa Malindi kwa uhifadhi wa JICA na SMZ, litakuwa na

miundombinu na huduma zote muhimu ambazo zitasaidia kuimarisha sekta ya uvuvi

hapa nchini. Kuendeleza uchumi kwa kupitia rasilimali za bahari na kuongeza uhakika

wa salama wa chakula kwa wananchi.

Wizara ihakikishe kuwa mradi unasimamiwa vizuri ili kuhakikisha kuwa unamalizika

kwa wakati kama ulivyokubalika katika mkataba.

Utekelezaji. Wizara itahakikisha usimamizi mzuri wa mradi wa soko la kisasa la samaki

la Malindi, kwa kuunda timu maalum ya usimamizi wa mradi, ili kuhakikisha

unatekelezwa vizuri na unamalizika kwa wakati.

Aidha, kwa mujibu wa makubaliano na Shirika la JICA mkandarasi wa ujenzi atatoka

Japan na kusimamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na JICA yenyewe.

Wizara itoe mashirikiano mazuri kwa wavuvi wanaotumia eneo hilo, wakati utakapoanza

ujenzi huo wa kuwatafutia eneo jengine kwa kipindi chote cha ujenzi wa soko.

Serikali imeliangalia kwa kina suala hilo na tayari imeshawapangia wavuvi na watumiaji

wengine utaratibu mzuri utakaopunguza usumbufu wakati wa ujenzi.

Busara itumike ili kuhakikisha wananchi wanalitumia soko la Tumbe. Mazungumzo

yanaendelea na wanakijiji wa Tumbe tayari wameshawasilisha wizarani kamati yao ya

soko, na tunategemea baada ya muda mfupi wataanza kulitumia soko hilo bila ya

matatizo. (Makofi)

Serikali iangalie uwezekano wa kufanya matengenezo ya kasoro zilizopo, ili soko la

Tumbe liwe na mazingira mazuri kwa watumiaji wake.

Utekelezaji. Baadhi ya miundo ya maji tayari imetengenezwa na mingine inaendelea

baada ya makubaliano ya kamati ambayo tayari imeshaundwa.

Wizara ihakikishe inatafuta njia ya kuingiza mashine ya barafu katika chumba

kilichojengwa katika soko la Tumbe.

Utekelezaji. Wizara tayari imeshatafuta mtaalamu wa kuangalia mtambo wa barafu

ambao kwa kipindi kirefu umekaa bila ya kufanya kazi, endapo mtambo huo utakuwa

42

mzima utaingizwa sokoni kwa makubaliano na kamati ambayo tayari imeshaundwa.

Mtambo huo ulinunuliwa mwaka 2010, lakini haukuweza kufanyakazi hata siku moja.

Serikali imepanga kujenga Bwawa la Samaki katika eneo la Maruhubi kwa ajili ya

uanzishaji wa vifaranga vya samaki, ili wafugaji waondokane na changamoto ya ukosefu

wa vifaranga.

Utekelezaji. Ujenzi wa kituo cha kuzalisha vifaranga, yaani hatchery ya samaki, umeanza

rasmi mwezi Julai 2017, huko Beit-el-Ras na unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba

Mradi huo unaendelea kwa mujibu wa ratiba na utaratibu uliokubalika hapo awali.
Wizara iendelee kutoa elimu kwa wafugaji wa samaki ili watumie njia za kisasa za

kitaalamu katika kufanya shughuli zao kwa lengo la kuwa na uzalishaji mkubwa wa

samaki. Wizara inawawezesha wafugaji wa samaki kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji

bora wa samaki.

Aidha, kwa kipindi cha miaka miwili 2016/2017 wafugaji 60 wamepatiwa mafunzo ya

ufugaji bora wa samaki kutoka kwa wataalamu wa Kichina. Hadi hivi sasa Zanzibar ina

vikundi 144 vya ufugaji wa samaki.

Kutokana na kuimarika kwa shughuli za uvuvi na kuhamasika kwa ufugaji wa mazao ya

baharini, serikali iandae mpango wa kuanzisha kituo cha utafiti wa mazao baharini ili

kiweze kuwasaidia wavuvi na wafugaji wa mazao ya baharini.

Utekelezaji. Wizara kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Vietnam imeandaa andiko la

mradi wa kuanzisha kituo cha utafiti wa mazao ya baharini. Wizara kupitia mradi wa

SWIOFish. unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, imetenga wastani wa dola laki tatu za

Kimarekani kwa ajili ya kujenga kituo cha utafiti cha uvuvi katika eneo la Maruhubi.

Aidha, mshauri mwelekezi kwa ajili ya kuandaa michoro ya kituo hicho tayari

ameshapatikana.

Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika iangalie namna gani itaweza kuwasaidia

wafugaji wa mazao ya baharini kupata mikopo. Wizara imeanza mazungumzo na taasisi

za kifedha, Benki ya Maendeleo ya Kilimo, CRDB na NMB ili kupata mikopo ya

kuwapatia mitaji wafugaji wa samaki.

Aidha, jumla ya vikundi 119 vya wazalishaji wa sekta za kilimo, wamefanyiwa tathmini

kwa ajili ya kupatiwa huduma za fedha kwa kupitia benki hizo, hatua hiyo inasubiriwa ni

kuja kwa bei ya benki hizo kwa kuangalia tathmini ya mwisho iliyofanywa.

Kamati imeitaka serikali kuleta mbele ya Baraza la Wawakilishi Sheria ya Kuanzishwa

Mamlaka Uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania, ambayo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, ili kukidhi masharti ya kifungu cha 132 cha Katiba ya Zanzibar

ya mwaka 1984. Wizara kupitia Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania

imekamilisha utaratibu unaohitajika na ipo tayari kuwasilisha sheria hiyo wakati wowote

baada ya kupita kwenye Baraza la Mapinduzi.

43

Afisi Kuu Pemba Afisi kuu Pemba ina mambo tisa (9)

Wizara itakapotoa nafasi ya ajira iangalie upungufu uliopo kwa upande wa Pemba. Kwa

mwaka 2016/2017 jumla ya wafanyakazi 49 wameajiriwa kwa kada tofauti wakiwemo

Mbwanashamba na Mabibishamba, wahudumu mashambani, madereva, walinzi, mafundi

wa matrekta na mafisa wasaidizi uvuvi, mifugo na misitu.

Wizara ihakikishe inatoa ushirikiano katika kipindi chote cha uundaji wa bajeti kwa

mwaka huu kwa Afisi kuu Pemba. Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Wakuu wa Idara

zote kutoka Afisi Kuu Pemba wameshirikiana na wenzao waliopo Unguja kwa lengo la

matayarisho ya bajeti.

Afisi iendelee kutumia OC zake kwa ajili ya kupunguza madeni ya wafanyakazi, jumla

ya wafanyakazi 202 wanawake 107 na wanaume 95 wamelipwa fedha zao za likizo

shilingi 20, 200,000/= kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Wizara ihakikishe anapatikana mwanasheria katika Afisi Kuu Pemba kabla ya mwezi wa

Septemba, kwani zipo changamoto nyingi za kisheria ambazo zinahitaji uwepo wa

mwanasheria, wizara inatarajia wanasheria wawili Pemba katika nafasi mpya za mwaka

2017/2018.

Wizara iendelee kusomesha wataalam wake kwa kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti

zinazokwenda na wakati kwa upande wa Pemba. Mtaalam mmoja wa utafiti yuko

masomoni kwa ngazi ya PhD, wizara inaendelea kuwafundisha wataalam wake walioko

Pemba hatua kwa hatua kwa kuendana na uwezekano wa kibajeti na rasilimali watu.

Serikali iongeze bajeti ya taasisi ya utafiti Pemba ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Wizara imeanza kuchukua hatua kwa kulitafutia tatizo la bajeti kwa kuzingatia mgao wa

bajeti. Mwaka uliopita taasisi za utafiti zilikuwa shilingi milioni 25 mwaka huu

zimepewa milioni 63 sawa na ongezeko la asilimia 252 la ongezeko ya bajeti ya mwaka

uliopita.

Wizara iangalie uwezekano wa kujenga ukuta katika eneo la Kituo cha Utafiti ili kuliekea

eneo hilo uzio katika hali ya usalama, kazi ya ujenzi wa ukuta wa kuzunguka eneo la

kituo tayari imeshaanza kwa kujenga mita 50 kati ya 1600 za uzio wake. Matarajio ni

kuendeleza ujenzi huo hadi kukamilika mzunguko wote.

Serikali itafute vifaa vya maabara kwa ajili ya kuendeshaji wa shughuli za kituo hicho.

Wizara imekamilisha upatikanaji wa vifaa vya Maabara Kuu ya Utafiti iliyopo Kizimbani

Unguja kwa mwaka huu wa fedha, hii ni kutokana na ukomo wa bajeti kwa mwaka huu,

ambapo haiwezeshi wizara kupata vifaa kwa maabara zote mbili.

Wizara itenge fedha kwa ajili ya kuunganisha huduma za mtandao katika eneo hilo.

Juhudi za kupatikana huduma za mtandao zinaendelea kuchukuliwa tayari yamefikiwa

makubaliano baina ya Shirika la Simu Tanzania TTCL kufunga mitandao ya huduma za

44

internet kituoni hapo ufungaji wa mitandao hiyo inafanyika na fedha tayari

zimeshapatikana.

Mhe. Mwenyekiti, baada ya kusoma yote hayo naomba sasa kutoa hoja. (Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

Mhe. Mweneykiti: Ahsante sana Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi

kwa ripoti yako. Waheshimiwa Wajumbe, sasa naomba nimwite Mhe. Mwenyekiti wa

Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo.

Mhe. Hamad Abdalla Rashid (Kny. Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na

Kilimo): Awali ya yote, napenda kuelekeza shukurani zangu kwa Mtukufu wa

Ulimwengu na muumbaji wa viumbe vyote mbinguni na ardhini kwa kutujaalia uhai na

afya njema tukaweza kukutana katika Baraza hili Tukufu, kwa lengo la kuendelea

kuwatumikia wananchi wa Zanzibar, kwa kutekeleza majukumu yetu mbali mbali kwa

niaba yao, ambapo leo tupo hapa kupitia na kujadili Utekelezaji wa Maagizo ya Kamati

yaliyowasilishwa katika Baraza hili tukufu katika kikao cha mwezi wa Febuari, mwaka

huu.

Mhe. Mwenyekiti, ikiwa hii ni mara yetu ya kwanza kutumia utaratibu huu wa

kuwasilisha utekelezaji wa maagizo ya Kamati mbele ya Baraza lako hili tangu

kufanyiwa marekebisho kwa Kanuni ya Baraza letu, Toleo la 2016. Sina budi kuipongeza

Ofisi ya Baraza la Wawakilishi kwa kuona umuhimu wa kulifanya hili kwani hapo,

kuwepo utaratibu huu, mafanikio zaidi yatapatikana kwani baada ya uwasilishaji wa

utekelezaji wa maagizo ya Wizara, Baraza litakuwa na fursa nyengine ya kuweza

kuthibitisha yale yaliyoelezwa kupitia ziara zake mbali mbali za Kamati za Baraza.

Mhe. Mwenyekiti, Nachukua fursa hii kuthamini juhudi anazochukua Mhe. Rais wa

Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi za kutekeleza ipasavyo Ilani ya CCM

kwa kutimiza ahadi zake ambazo aliwaahidi wananchi wa Zanzibar katika Uchaguzi

Mkuu wa mwaka 2015. Kupitia juhudi zake, wananchi wa Zanzibar sasa wanafaidi

matunda mazuri kupitia yale aliyoyatekeleza na anayoendelea kuyafanya hususan katika

masuala mazima ya kikiimarisha Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi. Namuomba

Mwenyezi Mungu amzidishie uwezo huo na amjaalie maisha marefu yenye kheri na

yeye. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, nitakuwa sijatenda haki, ikiwa nitaacha kumshukuru Makamo wa Pili

wa Rais, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi kwa umahiri wake mkubwa wa kuyasimamia vyema

majukumu ya wizara zote za serikali, ambapo Zanzibar na wananchi wetu wananeemeka

na mafanikio yanayopatikana kutokana na utekelezaji wa wizara hizo. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, napenda kuelekeza salamu zangu za shukurani kwa Waziri wa Kilimo,

Maliasili, Mifugo na Uvuvi; Mhe. Hamad Rashid Mohammed, Naibu Waziri; Mhe. Lulu

Msham Abdalla kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoutoa kwa kamati ambao unapelekea

kupatikana ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu, Lakini pia, shukrani za dhati

45

zimuendee, Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo ndugu Joseph Abdalla Meza, Manaibu

Katibu Mkuu pamoja na watendaji wote wa Ofisi yake kwa kushirikiana nasi katika kazi

zote za kamati yetu. Kamati inamueleza Katibu Mkuu Meza kwamba Kamati ipo tayari

kufanya kazi nae na inamkaribisha sana katika harakati zote za kuwatumikia wananchi

wetu kwa kuhakikisha masuala yote ya kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi yanaimarika

ipasavyo Zanzibar. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, bila ya kupoteza muda, sasa naomba niwatambue kwa kuwataja

majina yao Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ambao

walitoa mchango na ushauri mkubwa katika utekelezaji wa kazi za Kamati hii, Wajumbe

wenyewe ni:-

Mhe. Yussuf Hassan Iddi

Mwenyekiti;

Mhe. Hamida Abdalla Issa

Makamo Mwenyekiti;

Mhe. Hamad Abdalla Rashid

Mjumbe;

Mhe. Moh’d Mgaza Jecha

Mjumbe;

Mhe. Ali Salum Haji

Mjumbe;

Mhe. Ussi Yahya Haji

Mjumbe; na

Mhe. Bihindi Hamad Khamis

Mjumbe.

Mhe. Mwenyekiti, kamati yetu pia inashirikiana ipasavyo na makatibu wawili (2) kutoka

Ofisi ya Bazara ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakitusaidia kutekeleza

majukumu yetu, kwa heshima naomba niwatambue makatibu hao ni:

Ndugu Asma Ali Kassim

Katibu

Ndugu Said Khamis Ramadhan

Katibu

Mhe. Mwenyekiti, pamoja na mambo mengine, kamati yetu inalo jukumu la kupitia,

kuchambua na kujiridhisha na majibu yaliyowasilishwa na wizara hii kuhusu utekelezaji

walioufanya wa maagizo yaliyotokana na ziara zilizofanywa na kamati yetu katika

kipindi kilichopita na kuwasilisha ripoti yetu hapa Barazani katika mwezi wa Februari,

Leo hii, Kamati yetu inawasilisha hotuba hii ikiwa ni utekelezaji wa Kanuni ya 108
fasili ya (15) ya Baraza la Wawakilishi, Toleo la mwaka 2016.

Mhe. Mwenyekiti, katika ripoti hiyo, kamati yetu iliwasilisha Maagizo 72 ambayo

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ilitakiwa kutoa majibu majibu katika

kikao hichi cha mwezi wa Septemba au Oktoba. Napenda kulieleza Baraza kwamba

kamati yetu ilipokea, ilipitia na kujadili ipasavyo utekelezaji wa maagizo hayo. Kiujumla,

46

kamati yetu ilikubaliana na majibu yaliyotolewa na watendaji wa wizara na kuyaunga

mkono kwa asilimia mia moja. (Makofi)

Mhe Mwenyekiti. kamati inaipongeza sana wizara kwa kukamilisha ipasavyo utekelezaji

wa maagizo ya kamati kwa kuanzisha Taasisi Maalum ya Utafiti wa Mifugo, ambayo

itatumika kufanya tafiti za mifugo hapa nchini. Kamati inaimani kwamba kuwepo kwa

taasisi hiyo kutaiwezesha wizara na wananchi wetu kutambua matatizo yanayowakabili

wafugaji na kuyatafutia ufumbuzi.

Mhe. Mwenyekiti, kamati yetu imeridhishwa sana na hatua iliyochukuliwa na Wizara ya

Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa juhudi zake za kuanza utekelezaji wa agizo la

kamati kuhusu uanzishwaji wa Bwawa la Kufugia Samaki (hatchery) kwa ajili ya

uzalishaji wa vifaranga vya samaki ili wafugaji waondokane na changamoto ya ukosefu

wa vifaranga.

Kamati ilipata fursa ya kutembelea katika eneo la Beit-el-Ras ambapo mradi unafanyika

na kujiridhisha hatua iliyofikia ujenzi huo unaoendelea huko na kutarajiwa kumalizika

mwezi wa Novemba mwaka huu. Hivyo, kamati inasisitiza kwamba Wizara iongeze bidii

katika kusimamia vizuri wajenzi pamoja na kuhakikisha maendeleo endelevu ya

kuuimarisha mradi huo, ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuiletea tija Serikali yetu

ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mhe. Mwenyekiti, kamati yetu hainabudi kuipongeza Wizara hii ya Kilimo, Maliasili,

Mifugo na Uvuvi kwa utekelezaji wa agizo la kukamilisha upatikanaji wa vifaa vya

Maabara Kuu ya Utafiti iliopo Kizimbani Unguja. Maabara hizi zitatusaidia kufanya

utafiti mbali mbali na kupata ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili sekta yetu ya kilimo

Zanzibar. Pamoja na mafanikio hayo, jitihada za makusudi zinahitajika kwa ununuzi wa

vifaa hivyo kwa upande wa Pemba.

Mhe. Mwenyekiti, kamati yetu kwa kiasi kikubwa ilikubaliana na utekelezaji wa agizo la

uimarishaji wa Msitu wa Hifadhi wa Masingini kwa kuendelea kupanda miti mbali mbali

ikiwemo mikungu, mifenesi na miharita. Hivyo, kamati inaipongeza sana wizara kupitia

Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka kwa kuwa na azma nzuri ya kuuendeleza

Msitu wetu wa Masingini. Lakini kamati yetu imeishauri wizara kuongeza katika orodha

ya miti ambayo imekusudia kuiimarisha katika msitu huo ikiwemo miti ya asili ya

Mivule na Misaji. Hili linatokana na uasili wake wa kuwepo na kuoteshwa hapa Zanzibar

pamoja na umuhimu wake kiuchumi, kimatibabu na kiutalii.

Mhe. Mwenyekiti, kuhusu agizo la kuliimarisha Shamba la Mifugo Pangeni. Kamati

iliarifiwa kuwa kupitia mradi wa miundombinu ya mifugo wizara itachimba kisima ili

kuondoa tatizo la maji sambamba na kuifanyia matengenezo njia ya kuelekea shamba

hilo. Kwa kuwa agizo hili halijatekelezwa, kamati yetu itaendelea kulifuatilia agizo hili

kwa karibu zaidi ili kuongeza kasi ya utekelezaji na yale malengo yaliyowekwa na

serikali kwa Shamba la Pangeni yaweze kutimia kwa asilimia kubwa.

47

Mhe. Mwenyekiti, Kamati yetu ilipokea utekelezaji wa agizo la kuusimamia ipasavyo

Mradi wa Soko la Kisasa la Samaki la Malindi, ili kuhakikisha mradi unatekelezwa vizuri

na unamalizika kwa wakati. Kamati iliarifiwa kuwa wizara kupitia Idara ya Maendeleo

ya Uvuvi wataunda timu maalum ya kusimamia utekelezaji wa mradi huo ambao utaanza

mwaka huu. Kamati yetu itazidi kuufuatilia mradi huu kwa karibu, ili soko hili la Malindi

liweze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa na serikali. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, katika kutaka kujua kwa kiasi gani wizara inaimarishaje Mpango wa

Rasilimali watu katika idara zake hususan kwa upande wa Pemba, ili kutatua changamoto

ya ukosefu wa wafanyakazi. Kupitia utekelezaji uliowasilishwa, wizara ilieleza kwamba

wafanyakazi walioajiriwa kuwa ni 49 kwa kada tofauti kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Kamati inapongeza juhudi hizo ila inasisitiza apatikane mwanasheria, ili awe mwarubaini

wa changamoto zinazojitokeza kwa upande wa Pemba.

USHAURI WA KAMATI

Mhe. Mwenyekiti, mbali na maelekezo ambayo kamati yetu ilitoa ushauri kwa Wizara hii

ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa nia njema waliyonayo ya kuhimiza na

kusisitiza utekelezaji wake. Miongoni mwa mambo hayo ni:

1) Pamoja na kwamba Zanzibar haiwezi kujitosheleza katika uzalishaji wa mifugo

ya kutosha kwa ajili ya nyama na maziwa. Hivyo ni vyema wizara ikawa na

mpango mkakati maalum wa kuwasaidia mitaji wafugaji wetu wa ndani ili

waweze kuzalisha zaidi na kutatua changamoto hiyo.

2) Pamoja na kutatuliwa kwa Chinjio la Kisakasaka, kuna haja ya chinjo hilo

kuimarishwa na kupatiwa miundombinu imara, ikiwemo kuiwekea lami barabara

iliyoelekea eneo la chinjio, kwa vile chinjio hilo ni rasilimali kubwa katika

upatikanaji wa mapato ya serikali na mahitaji ya nyama kwa matumizi ya kila

siku kwa wananchi wetu.

3) Pamoja na kuwa na Sera ya Kijani (GreenPolicy). Wizara inatakiwa kuhimiza

upandaji wa miti kwa kuwatumia watumiaji na wakaazi katika maeneo husika.

Kwa mfano, Idara Maalum zote na Serikali na Skuli za Zanzibar zipande na

kuiimarisha miti katika maeneo yanayowazunguka.

4) Pamoja na serikali kumiliki Shamba liliopo Makurunge. Juhudi za makusudi

zinahitajika kuchukuliwa, ili kuliimarisha shamba hilo lipate kuwa na tija na

serikali. Kamati inaipongeza wizara kwa jitihada walizofikia ya kuandaa rasimu

ya makubaliano (MoU) baina ya Shirika la Nyumba la Taifa na Wizara yetu ya

kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.

HITIMISHO

Mhe. Mwenyekiti, mwisho kabisa, napenda kuwashukuru Waheshimiwa Wajumbe wa

Baraza lako Tukufu kwa kunisikiliza kwa utulivu wa hali ya juu wakati wote nilipokuwa

48

nikiwasilisha hotuba hii. Aidha, salamu zangu za pongezi pia zimwendee Mwenyekiti

wangu wa Kamati hii ya Fedha, Biashara na Kilimo pamoja na Wajumbe wake wote kwa

kukubali kuniteua mimi kuwasilisha hotuba hii kwa niaba yao kwenu Waheshimiwa

Wajumbe. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, sasa naomba nichukue fursa hii kwa mara nyengine nikuombeni

Waheshimiwa Wajumbe muijadili, mutoe ushauri pamoja na mapendekezo yenu na

hatimae muunge mkono utekelezaji wa Maagizo haya.

Mhe. Mwenyekiti, baada ya kusema hayo machache, kwa niaba ya Kamati ya Fedha,

Biashara na Kilimo. Naomba kuwasilisha. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante Mhe. Hamad Abdalla Rashid kwa niaba ya Mwenyekiti wa

Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo. Waheshimiwa Wajumbe, majadiliano yanaendelea

na mchangiaji wetu wa mwanzo naomba nimwite Mhe. Ali Suleiman Ali, akifuatiwa na

Mhe. Abdalla Maulid Diwani na Mhe. Miraji Khamis Mussa ajitayarishe.

Mhe. Ali Suleimam Ali: Ahsante sana Mhe. Mwenyekiti, awali ya yote nimshukuru

Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama hapa kuichangia Wizara ya Kilimo,

Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa taarifa yake ya kamati ya mwaka 2016/2017.

Mhe. Mwenyekiti, nimpongeze Mhe. Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu

Mkuu, Wakurugenzi na watendaji wote wa Wizara hii kwa kazi nzuri ambazo wanafanya

kuhakikisha kwamba mambo mbali mbali tunafanikiwa kwenye chakula cha aina mbali

mbali.

Lakini Mhe. Mwenyekiti, nampa pongezi za pekee Mhe. Waziri, kwa kazi zake nzuri na

juhudi yake ambayo tunamuona, kwa sababu mimi husema kila siku Mhe. Waziri, Katibu

nani wote haki yao ya kutembea katika maeneo kujua mazingira ya shida za watu, sio

kukaa ofisini na kupulizwa na vipoza hewa au mafeni wakati huo umepitwa na wakati

Mhe. Mwenyekiti.

Mhe. Mwenyekiti, Mhe. Waziri ana bidii ya peke yake na bahati nzuri na Naibu Wake

sasa hivi kabadilika sana mimi nampongeza sana Mhe. Lulu Msham Abdalla najua ulezi

kazi, lakini bado kaleleka vizuri na sasa hivi anafuata kwenye muelekeo ambao

unatakiwa, pia katika majibu yake anayojibu sasa hivi tunasema ka-improve sana katika

mambo yake ya maendeleo katika shughuli zetu, hongera sana. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu na kilimo ndio roho ya nchi

yetu, bila ya kilimo tutaharibikiwa sana katika maendeleo mbali mbali katika nchi yetu

kilimo kina mambo mengi kuna kilimo cha mwani, kilimo cha mpunga, kilimo cha

mihogo, mboga mboga na mambo mengineyo. Lakini pia tunategemea kwamba Zanzibar

ni sehemu moja ambayo tunategemea sana chakula cha mchele kwa asilimia 90% ya

Wazanzibari wanapenda chakula cha mchele.

49

Safari hii kwa mara ya kwanza nilipata taarifa tu namuomba Mhe. Waziri aje atupe jibu

kuhusu taarifa hiyo. Kwa kweli, uliuzwa mchele kule Wizara ya Kilimo, Maliasili,

Mifugo na Uvuvi mchele huo ulikuwa unauzwa lakini una foleni kubwa sana tuliambiwa

bei yake kuanzia 1,600/-, 1,800/- na 2,000/- lakini kama huna ubavu huupati, nasikia

mbegu hiyo tamu sana na nzuri na watu walikuwa wanashinda hapo kwa foleni

wanagombania. Kwa hivyo, Mhe. Waziri namuomba akija atupe maelezo na tuelewe

wapi unapatikana na kiasi gani tani ngapi tulipata na wananchi wamenufaika kiasi gani.

(Makofi)

Bahati mbaya Mhe. Mwenyekiti sikubahatika kuuonja mchele huo au wali wake, lakini

waliouonja waliokula wanasema ni wali mzuri wa ajabu. Hivyo, namuomba Mhe. Waziri

sana katika utafiti wao waiongeze hiyo mbegu kwa wakulima mbali mbali, ili wananchi

wetu wafaidike na mchele huo mpya wa kisasa kabisa.

Jengine Mhe. Mwenyekiti, uvuvi ni sehemu moja kubwa katika nchi yetu, ambayo

kisiwa chetu narudi kila siku tumezungukwa na bahari juzi nimeziona meli ya uvuvi za

Kichina, na meli zile tunaambiwa hivi sasa hivi vijana wetu wengi wachaanza kupata

ajira katika meli hizo. Naomba nimuulize Mhe. Waziri na hili, je meli hizi zipo hapa kwa

muda gani na zitafanya kazi katika maeneo gani, lakini pia vijana wetu kwa bahati

mbaya wengi lugha ya Kichina hawana wanasaidiwa na nani katika kuendelea

kushirikiana na Wachina ambao wanavua katika bahari kuu.

Tumesikia kwamba juzi wameanza Dar-es-Salaam na hapa wamekuja na wamepokelewa

vizuri. Kwa hivyo, hiyo ni changamoto ya mafanikio na naamini kwamba itaongezwa

mipango basi vijana wetu wengi watapata faida ya ajira katika sehemu ya uvuvi.

Mhe. Mwenyekiti, bado wavuvi wetu wengi ni masikini na wavuvi wetu wana nyezo

duni katika kufanya kazi zao za uvuvi. Kwa hiyo, namuomba sana Mhe. Waziri pamoja

na kuona kwenye taarifa hii, kuna mipango kadhaa imeandaliwa kupatikana vyombo vya

kisasa vya uvuvi lakini huko nyuma tunapotoka vilikuwepo vyombo vingi sana

viligawiwa katika madiko mbali mbali, sijui vipo wapi. Kwa kweli, hatujui kama

viliuzwa au watu wamegawana wakafanya wanavyotaka lakini azma ya serikali ilikuwa

vyombo vile visaidie wananchi wetu wapate ajira na kusaidia nchi yao katika upatikanaji

wa kitoweo cha samaki, lakini chombo vile vimetoweka kabisa. Mhe. Mwenyekiti,

namuomba Mhe. Waziri na kwa mpango huu namuunga mkono mzuri, lakini usimamizi

uwe bora, ili kuvilinda vyombo hivyo na kuvijua faida yake visipate hasara.

Mhe. Mwenyekiti katika suala jengine ambalo nitalizungumza Zanzibar tuna rasilimali

ya misitu, lakini misitu yetu kwa asilimia kubwa inapotea na kuna misitu yetu ambayo

tunaitizama kama misitu ya kitaifa Ngezi na hapa Masingini tumeambiwa inaanzishwa

rasmi sasa hivi na zimetengwa pesa kama milioni 60 kwa kuanzia ujenzi wa mkahawa

utakuwa mzuri kama kivutio cha watalii au wananchi tu wa kawaida kwenye kutembea

kwenye maeneo hayo ya misitu wa asili wa hapa Masingini. Kwa maana hiyo,

namuomba Mhe. Waziri autangaze rasmi, haidhuru unatangazwa lakini wananchi wengi

hawauelewi, kwa sababu katika sehemu ya Masingini hapa sikukuu kubwa, au siku za

50

sikukuu tunajua wananchi wetu au vijana wetu au watoto wetu wanakwenda kutembea

katika sehemu ya wanyama pale.

Sasa labda tuseme kwa kuwa watoto wanakwenda pale na patakuwa na sehemu ya

mazingira ya kwenda kusoma au kujivunza. Kutokana na hali hiyo, ingekuwa ni vyema

ukatangazwa rasmi msitu ule fedha naamini zitapatikana vizuri na wananchi watajua

faida ya ule msitu uko vipi na maumbile yake, ili wananchi wapate kusoma na kuelewa

na kuhifadhi.

Suala jengine Mhe. Mwenyekiti kwa wenzetu Tanzania bara ufugaji wa nyuki, ufugaji wa

nyuki ni pato kubwa sana kwa nchi yetu, kwa sababu wenzetu Tanzania bara

wanasafirisha na kwenda nchi za nje, lakini kwetu Zanzibar sijaona. Je hawa wafugaji

nyuki wamepotea hawapo au mazingira ya misitu yetu haitoshi. Kwa hivyo, Mhe. Waziri

akija hapa atupe maelezo tujue huu ufugaji wa nyuki unakasoro gani au una faida gani

tulikoanzia na hapa katikati ukapotea. Lakini naamini wafugaji wako wengi na

wanaamini kufanya kazi nzuri, ili tupate faida kwa ajili ya maendeleo ya vijana wetu na

serikali kupata pato lake.

Mhe. Mwenyekiti, la mwisho kabisa namuomba sana Mhe. Waziri pamoja na kilimo

kizuri kilichotokea safari hii au mavuno yaliyopatikana bado tunahitaji matrekta,

matrekta ni kilio kikubwa na matrekta ni sehemu moja ya uzalishaji rahisi lakini

venginevyo wananchi wetu wanapata shida, kijembe kongoroka kimepita na wakati.

Kwa hivyo, nimuombe sana Mhe. Waziri matrekta kila eneo yakiwepo Cheju,

Kilombero, Pemba sehemu mbali mbali basi wananchi wetu watafaidika na watalima

vizuri na faida itapatikana.

Mhe. Mwenyekiti, baada ya haya machache kwa heshima kabisa nampongeza tena Mhe.

Waziri na Naibu wake na watendaji wote wa wizara, lakini nawatakia kheri na mafanikio

yetu ya kilimo, ili mchele mpya tuupate na Waheshimiwa Wajumbe wajue wapi

unakwenda kununulia, ili wananchi wote wafaidike.

Mhe. Mwenyekiti, naunga mkono kwa asilimia mia moja. Ahsante.

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante sana Mhe. Ali Suleiman Ali kwa mchango wako. Sasa

naomba nimwite Mhe. Abdalla Maulid Diwani, akifuatiwa na Mhe. Miraji Khamis Mussa

na Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf ajiandae.

Mhe. Abdalla Maulid Diwani: Ahsante sana Mhe. Mwenyekiti kwa kunipa nafasi hii na

mimi kuchangia katika Taarifa ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kuhusu

utekelezaji wa maoni. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kunijaalia uzima

nikafika katika Baraza la lako tukufu.

Lakini haraka haraka kwa michango yangu kwanza niipongeze serikali kwa azma nzima

wa kuleta utaratibu huu mpya ambao kwa mara ya kwanza unapitia maelezo ya

kusimamia namna gani Baraza la Wawakilishi inayofanya moja ya kazi yake ya Kikatiba

kuisimamia serikali nashukuru sana kwa hilo. (Makofi)

51

Vile vile, nimpongeze sana Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti na Baraza la

Mapinduzi, kwa namna ambavyo anavyotoa maelekezo yake kupitia wasaidizi wake,

mawaziri kwa namna gani kuona Zanzibar tunapiga hatua katika kuwaletea maendeleo

wananchi wetu wakwezi, wakulima na wanyonge wa nchi hii namshukuru sana.

Sambamba na hilo, ikapelekea mpaka dakika hii imekuwa hata kilio cha mawizara

kuhusu upatikanaji wa fedha zao zile za bajeti kuweza kuvuka asilimia 70% na 80%

niipongeze sana. Hali hiyo, inaonesha wazi kabisa watu makini aliowachagua Dkt. Ali

Mohamed Shein wanasimamia makini zile sera na maamuzi ya Mhe. Rais wa Zanzibar

na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, hilo nampongeza sana. (Makofi)

Nikiendelea mbele katika mchango wangu mimi nitaangalia sana katika hili buku lenye

taaarifa hizo. Naomba kwenda kwenye agizo nam. 1 naomba nisome halafu nitoe

maelezo yangu. Agizo nam. 1 wizara iwasiliane na wazabuni wanaoleta pembejeo za

kilimo, ili pembejeo hizo ziwafikie wakulima, utekelezaji inakwambia wizara

ikishirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango imepanga na tayari imeshapata. Je, huyu

mtu aliyeshinda hii zabuni si yule ambaye aliyerudishiwa mbegu zile ambazo zilikuwa

pembejeo zilizokuwa na matatizo.

Mhe. Mwenyekiti, lilikuja swali kwenye Baraza hili hili na baadae tukaambiwa

imerudishwa. Sasa je, inakuwaje tena katika utekelezaji huu, wa mwaka 2016/2017

kwamba tena anapata nafasi yule yule kuhusu kutuletea mbegu zile, napata shaka na

hapo. Kwa kweli, Baraza hili lilikuja swali la Mhe. Masoud Abrahman Masoud kuhusu

pembejeo au kuhusu mbolea isiofaa na wizara ikaamua kuirudisha, leo hii kwenye hichi

kitabu yule yule yumo.

Mhe. Mwenyekiti, hapa Mhe. Waziri kidogo napata ukakasi kutokana kwamba hichi

kitabu wamekitengeneza wenyewe na wamekipitia wenyewe na leo hii wametuletea sisi

humu ndani tena. Wakati suala la huyu huyu sasa tulizungumza humu kwenye Baraza hili

na kwamba akarudishia zile pembejeo zake tukaambiwa gharama gani, leo hii tunamuona

kwamba kapata tena. Nadhani wakati atakapokuja Mhe. Waziri atakuja kutoa maelezo

zaidi namna gani kinachoendelea nataka moja nisimamie hapo.

Lakini mbele nikiendelea Mhe. Mwenyekiti, katika kifungu cha tano (5) juu ya

utekelezaji agizo limetoka, limetoka kwamba wizara ishajihishe wananchi kulima kilimo

cha spices, kwani kilimo hicho kimekuwa na soko kubwa ulimwenguni. Mhe.

Mwenyekiti, ni kweli soko kubwa ulimwenguni sio leo tu toka zamani spices tunajua

mpaka Zanzibar imekuwa Spices Island, kwa sababu ya wakulima hivyo viungo, lakini

chakusikitisha bado tukishatoka karafuu hatuna sisi kiungo chengine tunachojivunia.

Kwa mfano, leo hii tukitaka pilipili manga container moja hatupati hapa na watu

wanahitaji hizo container, tukitaka mdalasini leo container moja hatupati.

Sasa hapa tunaambia kwamba eti serikali majibu yake ya wizara, wizara ikishirikiana na

Asasi Zisizo za Kiserikali ikiwemo Zenj Spices, Zanzibar Organic Spices Growers na

Kampuni ya Lecon ya Ujerumani imewashajiisha vikundi. Je, Mhe. Waziri ni vikundi

52

vingapi vilivyoshajihishwa, kwa sababu hapa tuko katika utekelezaji wa bajeti ya

2016/2017 na wala sio 2017/2018.

Hivyo, angalau basi angetwambia baada ya hayo Waheshimiwa Wajumbe

tumevishajihisha vikundi kumi na tano (15) Charawe, Mwakaje, Uroa na sehemu

nyengine wapi na impact yake ishapatikana, lakini leo hii ndio kwanza unatwambia

kwamba eti imeshirikiana na Asasi Zisizo za Kiserikali inawashajihisha, nini impact yake

kushajihisha tuone kwamba mazao yanapatikana ndio jibu tunalolitaka sisi, na wala sio

vyenginevyo kwenye maandishi wametuandikia wameshajihisha ni mwaka mzima kwa

mujibu ya bajeti hii.

Huu utekelezaji huu ni wa mwaka 2016/2017 sio 2017/2018, tuko nje sisi ya muda, sasa

ingelikuwa ungetujibu aa baada ya kushajihisha 2016/2017, leo hii 2017/2018 tumeanza

kupata impact hii, vikundi hivi na hivi tayari vimevishajihisha na tunazo spices kiasi

hichi, tunawakaribisha wanunuzi au wasafirishaji kupeleka nje ya nchi, ili kuzipeleka

kule na kusema Zanzibar Spice Island watu wakubali, lakini sio haya ambayo

yameandikwa hapa. Kutokana na hali hiyo, ndio napata shaka kama kweli ripoti hii

kutoka maagizo ya Baraza la Wawakilishi wamekaa wakajadili kuisoma vizuri, leo hii

tukaja tukaipitia tena humu. Mhe. Mohamed Said Mohamed alisema anapata ukakasi

kuzipitia hizi ripoti, kwa sababu hazina kitu.

Mhe. Mwenyekiti, sisi bajeti iliyopita 2016/2017 tuliidhinishiwa Wizara ya Kilimo,

Maliasili, Mifugo na Uvuvi shilinigi 48,977,300,000/-. Je, aliweza kupata kiasi gani

katika bajeti yake, nusu na robo ya bajeti ameipata, sasa je utekelezaji wake uko wapi

ndio huu wakusajihisha bado mpaka dakika hii hakuna kitu.

Nikiendelea mbele Mhe. Mwenyekiti, nakwenda kwenye agizo nambari 7, wizara

iendelee kufuatilia kuhakikisha Shirika la Umeme (ZECO) linafanya matengenezo ya

nguzo zilizoinama katika bonde la Cheju. Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi

(ZECO) ni Shirika la Serikali lililo chini ya Wizara ya Ardhi, Maji na Nishati. Agizo

mwaka mzima jibu lake tumetwambia kwamba wizara imewasiliana na Shirika la

Umeme tayari shirika limebadilisha nguzo 6. Aidha, wizara inaendelea kushirikiana na

Shirika la ZECO kubadilisha nguzo 7 zilizoanguka narudia tena.

Mhe. Mwenyekiti, wizara inaendelea, yaani kubadilisha nguzo za umeme Mhe. Waziri ni

siku moja tu. Sasa sijui uendelevu huu wa siku ngapi hizo nguzo 7 ziwe mpaka leo

wizara inaendelea na ZECO kuhakikisha kwamba inabadilisha nguzo, nguzo ya umeme

inabadilishwa siku moja tu na tena ndani ya saa moja nguzo imeshahamishwa. Kwa

kweli, tulitegemea hapa tuambiwe kwamba ZECO washakamilisha zoezi lile tunaangalia

jambo jengine, sio leo 2017/2018 tunazungumza Wizara ZECO inaendelea come on

nguzo moja inabadilishwa si chini ya saa moja, leo hii tunaambia.

Kwa hiyo, naona hizi ripoti zenyewe kwa kweli zinatia hata msisimko kuzisoma kwa sisi

muliotuletea, jambo tukisema wengine tutaambiwa kwamba tunakuwa wakali

tunaigomba sana serikali. Kwa kweli, hatugombi serikali isipokuwa sisi tunataka

kusimamia Ilani ya Chama chetu kusimamia serikali yetu na ifanye kazi kwa umakini, ili

53

kuturahisishia katika Uchaguzi 2020 kupata ushindi wa kishindo. Lakini kwa muelekeo

huu mnarudisha kule kupata shida tena mpaka Bwana Jecha atuonee huruma.

Mhe. Mwenyekiti, nikiendelea mbele katika agizo nam. 4. Wizara inaendelea kutafuta

muekezaji kwa ajili ya kuanzisha viwanda kuzalisha pembejeo za kilimo na mifugo

tulikuwa na ZAPOCO hapa kuna kiwanda kinazalisha chakula cha kuku kiko wapi. Kwa

nini kimekufa. Sasa leo hii nashukuru kuna viwanda vidogo vidogo tu vya wananchi

wenyewe wanazalisha Mhe. Mwenyekiti kama havijui Mhe. Waziri hivyo vipo kama vile

Amani pale pana viwanda vinazalisha leo hii tunasema kwamba …

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Mhe. Mwenyekiti,

kwa ruhusa yako naomba Mhe. Mjumbe afute kauli yake, sisi hatujaonewa huruma na

Jecha.

Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf: Mhe. Mwenyekiti, afuate utaratibu na ataje Kanuni…

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Mhe. Mwenyekiti,

sisi hatujaonewa huruma na Jecha. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la

Mapinduzi alishinda kwa asilimia 91. Afute kauli hiyo Zanzibar iliingia katika uchaguzi

Zanzibar …(Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri,

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Naam Mhe.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri umesimama lakini hujanambia Kanuni gani imetumia

kwa hiyo unasema….

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Kanuni ya 68 na

kama siyo tafuta Kanuni wewe Mwenyekiti kakosea huyo..

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri….

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Serikali haijaonewa

huruma hapa.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri, mimi nilikuwa nakusikiliza, lakini na Waheshimiwa

Wajumbe wengine nao wamewasha microphones wanasema. Kwa hiyo, nilikawa

nashindwa nifanye maamuzi gani. Kwa maana hiyo, nilikuwa nakusikiliza umesimama

nimekuruhusu kuhusu utaratibu sikusikia umesema hivyo na umesema kwa Kanuni ya 68

nimekusikia sasa subiri nitoe mimi maamuzi.

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Ndio Mhe.

Mwenyekiti ahsante.

54

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri, ndio maana nikakuuliza kwa Kanuni ya ngapi, taratibu

gani aliovunjwa, ili tumwambie Mjumbe.

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Mhe. Mwenyekiti,

Kanuni ya 68

Mhe. Mwenyekiti: Naam.

Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum): Mhe. Mwenyekiti,

Kanuni ya 68 tunamuomba Mhe. Mwanasheria Mkuu atusomee. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, tupo hapa katika mazingira ya kujenga na wala hatuharibu.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais: Mhe. Mwenyekiti kuna

Mjumbe anazungumzia Kanuni ya 59 (8) inayosema ifuatavyo:

“Ni maarufu kwa Mjumbe yoyote:

(a) kutumia lugha ya matusi au kashfa;

(b) kutumia haki yake ya kusema kwa madhumuni ya kutaka kushelewesha

shughuli za Baraza;

(c) kuzungumza mjumbe au mtu mwengine kwa nia mbaya au kumshambulia

binafsi, isipokuwa kwa kutoa hoja halisi, inayohusu mwenendo makhsusi

wa mjumbe huyo;

(d) kujiingiza katika mambo ya kuwasema wajumbe wenzake.

Sasa Mhe. Mjumbe hapa alichukulia lugha za kashfa na matusi kwa serikali ndio

anayozungumzia Mhe. Said Soud Said (Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum).

(Makofi).

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,

nimekufahamu na nadhani Mhe. Abdalla Maulid Diwani kwa kitendo ulichosema kuwa

serikali imeonewa huruma naomba ufute hiyo kauli, ili tuendelee.

Mhe. Abdalla Maulid Diwani: Ahsante Mhe. Mwenyekiti. Nafikiri Mwenyekiti wa

Tume ya Uchaguzi Jecha na ndiye aliyeakhirisha uchaguzi, nafikiri sijatukana wala

sijazungumza lugha iliyokuwa siyo na kama anayebishana kama uchaguzi haujafutwa

sijui nani atakataa humu ndani. Naomba niendelee.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Mjumbe, kauli uliyosema kuwa serikali imeonewa huruma na

Mwenyekiti wa Tume. Sasa nadhani hoja ya Mhe. Mjumbe hili neno huruma ndio

anahisi kama umelizungumza sivyo, kwa sababu hatukuonewa huruma, labda kulikuwa

na makosefu katika uchaguzi, ndio maana Mwenyekiti akafuta matokeo. Kwa hiyo, wewe

55

ulitamka kuwa Mwenyekiti wa Tume ametuonea huruma. Hivyo, hii neno huruma nahisi

uifute hiyo kauli, ili tuendelee.

Mhe. Abdalla Maulid Diwani: Ahsante Mhe. Mwenyekiti, pamoja na maelekezo mazuri

uliyonipa natamka kwenye Baraza hili kufuta kauli yangu kwamba ile ilikuwa sio nzuri.

Naomba kuendelea. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Nakushukuru Mhe. Abdalla Maulid Diwani, naomba uendelee kwa

kumalizia dakika zako.

Mhe. Abdalla Maulid Diwani: Ahsante sana naomba muda unilindie. Mhe. Mwenyekiti

nilipozungumza agizo la 4 kuhusu kadhia kamba kutaka pembejeo tulikuwa na Kiwanda

cha Chakula cha Kuku Zanzibar. Sasa utekelezaji tunaambiwa wizara kushirikiana na

ZIPA inaendelea kufanya jitihada kutafuta muekezaji kwa ajili ya kuanzisha viwanda vya

uzalishaji pembejeo ya mifugo. Hichi kiwanda kilikufia nini. Naomba Mhe. Waziri

wakati atakapokuja anisaidie.

Lakini nikenda katika agizo nam 6 wizara iandae mpango wa kuanzisha Kituo cha

Utafiti wa Mifugo kufanya tafiti za aina mbali mbali. Mhe. Mwenyekiti, ninavyofahamu

Kituo cha Utafiti Zanzibar …

Mhe. Mwenyekiti: Waheshimiwa Wajumbe, naomba utulivu wenu, mchangiaji

anachangia minong’ono naona imekuwa mikubwa, kama ni ile hoja tayari tumeshaitolea

uwamuzi. Kwa hivyo, naomba Waheshimiwa Wajumbe tutulie tuendelee na shughuli

zetu. Mhe. Mjumbe endelea.

Mhe. Abdalla Maulid Diwani: Ahsante sana. Kituo cha Utafiti Zanzibar kipo muda

mrefu nchi hii, kipo Kizimbani kama sikosei. Katika utekelezaji wake tunaambiwa

serikali tayari imeshaanzisha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo kwa lengo la kuendeleza

utafiti wa mifugo hapa nchi katika mpango wa taasisi hiyo, mpango wa utekelezaji

unaoandaliwa katika robo ya pili.

Kwa mujibu wa bajeti hii robo ya pili imeshapita zamani, tuko 17, 18, robo ya pili

ilitakiwa iwe Septemba ya 17 yaani hii Bajeti 16/17, robo ya pili baada ya Julai,

Septemba pale 16 ndiyo robo ya pili, kwa sababu robo hizi ni nne katika mwaka miezi

mitatu mitatu. Sasa wanaposema kwamba inaanzia kwenye robo hii kwa bajeti gani

iliyopitisha hii, wakati Bajeti yake hii ni 2016/17. Mhe. Mwenyekiti, naomba ufafanuzi

katika hicho.

Mhe. Mwenyekiti, kwa kweli tuna mambo mengi ya kusema katika hizi ripoti ambazo

tumeletewa humu ndani ya Baraza. Lakini tunashindwa kuzisema nyengine ambapo

ndiyo yale unaweza kuja kuambiwa kwamba unakiuka taratibu naomba Mwenyezi

Mungu asijujaalie tukafika huko. Lakini kwa kweli tunaletewa ripoti imani yangu

kwamba hata hao Mawaziri pengine hawaziangalii kwa umakini mpaka wakatuletea sisi

humu ndani tuzichangie ripoti hizi. Kwa kweli acha tuendelee ahsante sana.

56

Mhe. Mwenyekiti: Nakushukuru sana Mhe. Abdalla Maulid Diwani. Sasa naomba

nimwite Mhe. Miraji Khamis Mussa na atafuatiwa na Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf na

Mhe. Hamza Hassan Juma ajiandae.

Mhe. Miraji Khamis Mussa: Ahsante Mhe. Mwenyekiti, kwa kunipa nafasi jioni ya leo

kuchangia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na

Uvuvi. Kwanza nianze kuwapongeza viongozi wa Wizara hii, Mawaziri, Naibu Waziri,

Makatibu Wakuu na watendaji kwa hatua nzuri ya majibu ya utekelezaji, kila tukipitia

tunaona mambo yamekwenda vizuri, baadhi ya sehemu tu ndivyo ambavyo tunaweza

tukachangia tukapata ufafanuzi wa ziada. Kwa ujumla mimi naanza kwa kuwapongeza na

niipongeze kamati kwa uwasilishaji wao mzuri.

Mhe. Mwenyekiti, naomba niende kwenye agizo Nam. 1 ukurasa wa 7 ambalo wizara

iliagizwa na kamati iwasiliane na wazabuni wanaoleta pembejeo za kilimo. Katika

majibu ya utekelezaji wameeleza vizuri lakini kuna maeneo wametaja tani ambazo

zinapatikana lakini hasa wakazielekeza katika majibu kuwa watapatiwa wakulima wa

umwagiliaji maji. Shida iliyopo eneo lote hili mpaka maelezo ya ziada wametajwa

wakulima wa umwagiliaji maji. Tulichokuwa sisi tunapata mashaka tunawakulima wengi

zaidi kuliko hawa wa kilimo cha umwagiliaji ambao wanahitaji pembejeo, wanahitaji

mbolea hizi, lakini hawakuingizwa katika katiba hii yaani wale wakulima ambao

wanategemea mvua.

Kwa kweli, ikawa tunapata mashaka maana ndiyo wananchi nchi pia, sasa katika

utekelezaji huu umewalenga kundi moja lakini kundi kubwa halikulengwa hapa. Sasa

sijui katika utekelezaji wa namna hii hawa wakulima wa kawaida wanaotegemea mvua

tunawapeleka wapi. Sasa kama walikuwemo katika mpango huu kwa nini katika

utekelezaji tusiwaainishe. Kwa hiyo, kidogo tu nilikuwa napata mashaka lakini sina tatizo

sana waziri atakapokuja pengine kibinaadamu tumesahau lakini atupe maelezo ya ziada

ya hawa wenzetu ambao ni kundi kubwa vipi tunawasaidia.

Mhe. Mwenyekiti, niende kwenye ukurasa wa 9 agizo nam. 5, wizara ishajihishe

wananchi kulima kilimo cha spices, kwani kilimo hichi kimekuwa na soko kubwa.

Maelezo hapa kwanza tushukuru angalau tu kuwa wizara inashughulikia na inashirikiana

na asasi tofauti. Kwa kuwa wizara ina jukumu la moja kwa moja la kuandaa nursery zake

kwa kuandaa miche lakini pia kuandaa mashamba yake ambayo yatakuwa ni sehemu ya

kutoa msaada, yaani nazungumzia mashamba darasa, kutoa msaada kwa wakulima wetu

hawa.

Mhe. Mwenyekiti, hapa hatujaona mpango ule katika ukelezaji lakini tunaona katika

maendeo mengine hasa katika kilimo cha migomba tunaona nursery zao, kilimo kama

cha mikarafuu kunautekelezaji ule tunatoa miche bure, lakini kunako eneo hili la spices

wizara hatujaona ikajipanga kuelekea huko. Lakini, bado inashirikiana na asasi

nashukuru ndiyo hatua ya awali, lakini azma iwe endelevu ya kuonekana tunatia nguvu

katika eneo hili.

57

Mhe. Mwenyekiti, namuomba Mhe. Waziri atakapokuja atwambie kuna mkakati gani wa

kuelekea huko, angalau sasa tunashirikiana na asasi lakini mbele sisi wenyewe kama

wizara tuwe tumeweka mpango maalum wa kuwa na nursery zetu au mashamba darasa

ambayo yanaweza yakatusaidia katika kukuza kilimo hichi.

Mhe. Mwenyekiti, naomba niende katika ukurasa wa 11 kunako agizo nam. 3. Wizara

iongeze ajira kwa wataalamu wa mifugo, ili tuwe na wataalamu wa kutosha. Kwanza

niipongeze wizara kwa hatua hii ya utekelezaji, inaonekana wazi wameshawasiliana na

wizara ambazo inasimamia huu utoaji wa vibali vya ajira na wameweka hapa wameomba

ajira 68. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, baada ya pongezi hizo Mhe. Waziri labda nishauri tu. Mara nyingi

tunapowaajiri mabwana shamba hawa, tunawaajiri watu ambao makazi yao makubwa

inakuwa mjini, sasa inakuwa usumbufu mkubwa wa kuwapatia usafiri au vipando, wakati

mwengine inakuwa tunapata mashaka. Lakini na ile dhamira hasa ya serikali ya kutimiza

yale mahitaji inakuwa hayapatikani tunatimiza upatikanaji wa ajira lakini malengo hasa

hayafikiwi. Kwa kweli, sitaki tubague lakini serikali ijipange kidogo katika kuona ile

dhamira kubwa ya kuwatafuta wataalamu hawa basi angalau watoke katika maeneo

ambayo tunawapeleka ya vijijini. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, naomba niende ukurasa wa 14 katika Agizo la 11, ambalo linasema

Wizara ihakikishe upatikanaji wa hatimiliki katika shamba hilo. Shamba hili ni Shamba

la Pangini na katika utekelezaji hili shamba lina miaka 60 ambalo limeshapimwa na

ramani zimeshatolewa lakini kuna tatizo la upatikanaji wa hati. Sasa napata mashaka

kidogo kwa sababu Wizara mbili hizi, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Ardhi kunaukaribu

mkubwa sana, kwa sababu hata kuna mashamba mengine mnapoyajadili ya mikarafuu na

mmeshaanza kuyatambua na kuyapima, kwa nini ndani ya miaka 60 mpaka leo hatujafika

pahala tukaivumbua hii hati.

Mhe. Mwenyekiti, hapa kidogo Mhe. Waziri mimi sina mashaka lakini wasi wasi upo.

Kabla ya hili shamba kuanza kumegwa hebu tuone utekelezaji au upatikanaji wa hii hati

na kuliendeleza hili shamba upatikane. Mhe. Mwenyekiti, namuomba Mhe. Waziri

atakapokuja anisaidia hapa mkwamo hasa katika upatikanaji wa hii hati ni nini ndani ya

hiyo miaka 60, angalau wananchi na wao wafaidike na taarifa hizi. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, naomba niende ukurasa wa 15 katika agizo nam. 2, linalosema kuwe

na usimamizi na utaratibu wa uchimbaji wa maliasili zisizorejesheka. Kwa kweli,

niliposoma hapa pia napo naipongeza wizara. Mhe. Mwenyekiti, naomba katika kipindi

kirefu hizi maliasili sizorejesheka tunazo, lakini tunaona hapa wizara yenyewe imekiri

kuwa inataka kutayarisha mpango mkakati kwa muda mrefu au muda wote ambao

tunaishi katika utaratibu wa kuwa na maliasili zisizorejesheka. Sasa hivi kuna taarifa

hapa kuwa wizara ndiyo kwanza inataka kuanza kuandaa mpango wa mkakati wa

matumizi endelevu ya maliasili zisizorejesheka hapa nchini.

Mhe. Mwenyekiti, Mhe. Waziri hivi mpaka leo kuwa hatuna mpango mkakati katika

kufanikisha eneo hili la kulinda mali asili zetu, hapa nataka mashaka sana. Najua

58

unaweza ukakosa kutayarisha mpango mkakati lakini ukawa na mpango kazi lakini

hautoshi lazima mpango mkakati uwepo. Sasa kuna changamoto zipi mpaka leo

zinapelekea kuwa tumekosa kuwa na mpango mkakati katika eneo hili muhimu sana hapa

nchini. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, naomba niende sasa katika eneo la agizo nam. 4 katika ukurasa wa 17

ambalo wizara itoe taarifa maalum mbele ya Baraza hili, kuhusu hali halisi ya uchimbaji

wa mchanga ili Wajumbe wa Baraza hili pamoja na wananchi waelewe dhamira ya

serikali juu ya matumizi ya rasilimali ya mchanga. Nikushukuru sana Mhe. Waziri

maelezo yako yametosheleza lakini kuna faida tu kwa wananchi wetu ili tuweze kuipata.

Mhe. Mwenyekiti, maelezo ya utekelezaji wizara yatari imetoa taarifa serikalini kwa

wananchi kuhusu hali ya upatikanaji wa mchanga. Lakini wizara iko tayari katika

maelezo yanayofuata, kuwasilisha taarifa maalum kuhusu hali ya uchimbaji wa mchanga

Zanzibar katika Baraza hili. Sasa mpaka leo hatujaona katika ile ratiba ya ndani ya

Baraza tumeona taarifa za ZAWA zinakuja lakini taarifa hii haipo.

Mhe. Mwenyekiti, naomba nimuulize Mhe. Waziri katika eneo hili kunachangamoto gani

hivi ameshawahi kuwasiliana na kiongozi wa Baraza, ili kuleta taarifa ya ikakwama au

mpaka sasa hivi hajawa na dhamira ya kuomba hicho kibali cha kuingiza taarifa hii ndani

ya Baraza hili. Nafikiri ni vyema atupe taarifa tufaidike Wajumbe wa Baraza, ili tuone

kama hatukupata ndani ya Baraza hili tutapata lini au kibali hichi amekwama wapi ili na

sisi tufaidike katika kupata taarifa muhimu za eneo hili.

Mhe. Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kuwapongeza viongozi wa wizara wamefanya

kazi nzuri, niipongeze kamati maagizo yao yamekwenda vizuri, naomba nishukuru sana

kwa kupata nafasi jioni ya leo. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante sana Mhe. Miraji Khamis Mussa, Mwakilishi wa Jimbo la

Chumbuni kwa mchango wako. Sasa naomba nimwite Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf,

akifuatiwa na Mhe. Hamza Hassan Juma na Mhe. Suleiman Makame Ali wa Ziwani

ajiandae.

Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf: Bismillahi Rahmani Rahim. Mhe. Mwenyekiti

nakushukuru kwa kunipatia nafasi na nitajitahidi kuchangia Wizara hii ya Kilimo,

Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa kuwa sina uzoefu nayo sana mambo haya lakini

nitajaribu kuchangia ninavyofahamu kwa mujibu wa ripoti hii ilivyokuja.

Mhe. Mwenyekiti, naomba nianze na suala moja ambalo lipo katika page Nam. 5

ningetaka kujua kuhamasisha wafugaji wa samaki chaza, kaa na kamba ili kuendeleza

uzalishaji wa mazao haya, pia juhudi zitachukuliwa katika kutafuta masoko kwa mazao

ya baharini.

Mhe. Mwenyekiti, Mhe. Waziri ningependa kuja kujua ufugaji wa samaki na vitu

vyenginevyo ambavyo vimetajwa hapa kazi yangu havina athari au labda ladha yake

59

inakuwa tofauti au vipi katika vitu kama hivi, samaki, chaza, mlivyotaja na vitu vyengine

vyo hawa wa kufuga. Tofauti yake haileti athari yoyote katika masuala ya afya au vipi.

Mhe. Mwenyekiti, tukienda kwenye ukurasa nam. 6 vile vile kusomesha wanafunzi 104

waliopo diploma 47 na cheti 57 na kuchukua wanafunzi wapya 100, diploma 50 na cheti

50 kupitia Chuo cha Kilimo cha Kizimbani. Mhe. Mwenyekiti, ningependa kutoa ushauri

kwa sababu tumeona wanaopewa elimu hapa ni wanaotoka kwenye Chuo cha Kizimbani

na sehemu nyenginezo ambazo wanazoona wao wanafaa kupewa elimu. Lakini je, katika

vile vikundi ambavyo vinahusisha wakulima, ikiwa wafugaji na wengineo, wamejipanga

vipi kuweza kuwatoa watu hata kama hawana elimu ya shule kubwa kwenda kuwapa

elimu kama hizi wanazokwenda kuwapa watu ambao wamewataja hapa. Sasa kama

wamefanya hivyo ni wangapi tayari wameshawapa elimu hiyo au kuna utaratibu gani

ambao wameuwandaa.

Mhe. Mwenyekiti, vile vile ukurasa huo huo nam. 6, kushajihisha na kuwaunganisha

wakulima, wafugaji na wavuvi katika masoko ya ndani na nje ya nchi kwa

kuwaunganisha pamoja na kuwapatia mikopo kutoka taasisi za kifedha. Hapa Mhe.

Mwenyekiti, hadi hivi leo kama masoko tumeegemea zaidi kwenye masoko ya Unguja na

Tanzania Bara. Lakini vipi wamejipanga zaidi kuweza kuwatangazia hawa wakulima,

wafugaji, wavuvi, vitu vyao ambavyo wanavitengeneza katika ku-create kutoka kwenye

akili zao kama masuala ya mbolea, wale wanaotengeneza pilipili nmeona kama karafuu

na vitu vyenginevyo. Kwa hiyo, vipi wamejipanga kuhusu masoko ya nje zaidi ili

kuitangaza Zanzibar nje kuliko soko la ndani ya nchi.

Mhe. Mwenyekiti, mimi kabla ya yote ningempongeza sana leo Waziri wa Nchi, Afisi ya

Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud kwa kumsaidia Mhe. Said Soud Said

(Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum) kwenye Kanuni za Baraza la Wawakilishi na

kuweza kufanikisha, nampa pongezi sana.

Mhe. Mwenyekiti, suala la uvuvi ambalo nitalizungumzia mwanzo lenye page 30, 31, na

32 ambalo limezungumzia masuala ya uvuvi kwa ujumla. Wizara iandae utaratibu

maalum wa usimamizi za madiko, kwani baadhi ….. samahani ukurasa Nam.7 ugawaji

wa kilimo wa dawa.

Mhe. Mwenyekiti, wizara iwasiliane na wazabuni wanaoleta pembejeo za kilimo, ili

pembejeo hizo ziwafikie wakulima kwa wakati. Mhe. Mwenyekiti, naomba Mhe. Waziri

wakati atakapokuja anisaidie hivi vitu vyote vilivyoletwa mbolea na vitu vyenginevyo

ujagawaji wenu mmejikita kwenye njia gani, kila wilaya wanagawa vipi au wanagawa

kila jimbo ama wanagawa kwa kikundi ambacho kinalima au vipi. Hivyo, napenda kujua

ugawaji wenu uko vipi na wepi hasa ambao wamenufaika zaidi na ugawaji wa dawa hizi.

Mhe. Mwenyekiti, nikiendelea naomba nende kwenye page nam. 9 ambayo

inazungumzia masuala ya viwanda, kwenye wizara itoe ushirikiano wa dhati kwa

wawekezaji wote wanaowekeza au wanaokusudia kuekeza kwenye sekta zinazotumiwa

na Wizara ya Kilimo.

60

Mhe. Mwenyekiti, naomba kumuuliza Mhe. Waziri hapa wanatafutwa wawekezaji wa

vitu tofauti kuhusiana na wizara yake kwa kushirikiana na ZIPA, tukiangalia kwenye

page nam. 10 naona ZIPA ipo hapa kuna sehemu ambayo wametaka washirikiane kwa

ajili ya kutafuta investors. Je, tayari wanapokuja kupata investors wameshajitayarisha na

feasibility study zetu ambazo zitaonesha kitu gani wanachotaka mtu a- invest labda

kwenye masuala ya mifugo, afunguwe kiwanda cha nyama, au kwenye masuala ya uvuvi

kifunguliwe kiwanda cha samaki, wameshajitayarisha na plan zao mtu anapokuja tayari

wanamuonesha au wanataka mtu aje na maoni yake sio maoni yao. Ningependa kujua

njia hizo ambazo wanazozitumia.

Mhe. Mwenyekiti, vile vile page ya 10 inazungumzia serikali kupitia wizara iandae

utaratibu maalum wa kudhibiti uingizaji wa bidhaa za mifugo kutoka nje ya nchi hasa zile

ambazo zinazalishwa kwa wingi ndani na mambo ya dawa. Mhe. Mwenyekiti, naomba

kujua Mhe. Waziri uletaji wa hizi dawa zinazokuja Zanzibar ni ngapi ambazo

wameshawahi kukamata kwamba hazina kiwango au labda mtu kadanganya au kuna

kampuni imeleta vitu ambavyo havipo kwenye kiwango zikaweza kuathiri wale

watumiaji.

Mhe. Mwenyekiti, jambo jengine nitakwenda kwenye page nam. 13 ambalo linahusiana

na wakulima na wafugaji kwa mambo ya kisasa wanavyotaka Wizara. Wizara indelee

kutafuta wawekezaji wa ajili ya kuanzisha ….Sorry page nam 13.

Katika suala la ukuwaji wa sekta ya mifugo tayari yameanza malalamiko ya maeneo ya

ardhi kwa wakulima na wafugaji, ili kunusuru migogoro ambayo inaweza kujitokeza

hapo baadaye serikali ianzishe mpango maalum wa kutenga maeneo ya mifugo waweze

kutumia eneo dogo la ardhi kwa kufuga ng’ombe wachache wa kisasa na wenye tija na

kuacha ufugaji wa kizamani.

Kwa kweli, suala hili Mhe. Waziri liko very open. Kwa hiyo, naamini wizara itapokuwa

tayari kuwasaidia wananchi kuwapa elimu kuwasaidia na kuwafundisha, basi nafikiri

idea hii hawatoikataa, ambayo wameipendekeza kutaka kuwapelekea kwao kufata ufugaji

wa kisasa hata kilimo cha kisaa watapojiandaa na wao wananchi watakuwa wako tayari

lakini wakisema wawaachie wananchi peke yao suala hili hawataliweza, kwasababu hivi

vitu vinataka capital vinataka elimu vinataka nguvu. Sasa pindipo wizara itakapokuwa

itapokuwa ishajidhatiti kuwasaidi wananchi kwenye suala hili, basi naamini wananchi

waatakuwa tayari na hii idea sio mbaya ni nzuri.

Mhe. Mwenyekiti, naomba nende kwenye idara namba 14 kuna Idara ya Misitu na

Maliasili Zisizorejesheka hapa imesema wizara kwa kushirikiana na Taasisi husika

iendelee kukomesha matumizi ya misumeno ya moto. Mhe. Mwenyekiti, naomba kutoa

ushauri au kama nafikiri inawezekana wanalitumia tayari. Kwa kweli, suala la ukataji wa

miti na mambo mengineyo Zanzibar hasa minazi, ambayo tulikuwa tunaringia sasa hivi

imepungua hata madafu fedha nyingi sana, nazi hainunuliki na hasa nchi kama hii

kununua nazi shilingi 1500/= ni pesa nyingi sana au dafu shilingi 1000/=.

61

Lakini ninachotaka kusema andaeni mfuko maalum kwa kuweza kuwapa watu ambao

watatoa information kwa wale wanaokata minazi, wanaokata miti ambayo hawataki

ikatwe waweze kuwapa bonus watoe information na yule watakayemkamata atapigwa

penalty pesa zao zitakuwa zimerudi na watamuweka ndani kukomesha suala hili. Mhe.

Mwenyekiti, hili ni wazo ambao najaribu kulitoa kama linakuwa halipo basi naomba

walizingatie.

Nitaendelea kwenye page namba 17 Mhe. Mwenyekiti, page namba 17 inazungumzia

suala la mchanga. Wizara itoe taarifa maalum mbele ya Baraza hili kuhusu hali halisi ya

uchimbaji mchanga, ili Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza hili pamoja na wananchi

waelewe dhamira ya serikali.

Mhe. Mwenyekiti, hakuna anayetaka kubishana na wala anayetaka kwenda kinyume na

serikali lakini tuangalie athari ni ipi. Mhe. Mwenyekiti, kwa kweli serikali imezuia suala

la mchanga Mhe. Waziri kutoka kule kwa mwanzo kwenda sasa hivi katika njia ambayo

ya ku-save na kuweza ku protect labda masuala mengine ambayo wanajua wao kuweza

mchangza kuwepo labda mambo mengineyo.

Lakini tatizo tunaloliongelea sisi sio kama hatutaki kuzuiliwe au hatutaki serikali ifanye

maamuzi yake, tatizo mchango umekuwa pesa nyingi mara nne gari ambalo tumekuwa

shilingi 180,000/= la tani kumi la mchanga sasa hivi tunalinunua kwa laki 750,000/=

hichi ndicho kitu ambacho tunapigania nacho. Mhe. Mwenyekiti, naiomba serikali

kwamba iendelee kuweka vikwazo inavyovitaka kwenye masuala yale ili kudhibiti haya

masuala lakini mchanga uweko bei ya mwanzo, kwa nini mchanga upande wakati

mchanga wakati mchanga utakapopanda tofali limepanda bei, saruji imepanda bei hapa

hapa utakuja kukuta tunaumizi wananchi wa chini, waliokuwepo juu hawataadhirika sana

kwa sababu uwezo wanao lakini watoathirika ni masikini wa chini ambao kipato chao

kidogo.

Mhe. Mwenyekiti, lengo letu sisi kwamba Mhe. Waziri afanye anavyotaka anavyoona

yeye anaweze kuona nchi kuiweka katika hali nzuri hakuna tatizo, lakini suala la

mchanga liwe bei kama ya mwanzo au hata kama imepanda kutoka laki 180,000/= iwe

angalau basi iwe laki 250,000/=. Lakini sio tunvyonunua sasa hivi mchanga shilingi

750,000/= kutoka shilingi 180,000/=.

Nikiendelea na mchango wangu Mhe. Mwenyekiti, naomba niende kwenye green policy

mambo ya masuala ya kuotesha miti page namba 16. Mhe. Mwenyekiti, naiomba wizara

kwa sababu hapa wameweka kila mwezi wa Juni wanasema ni siku ya kupanda miti

lakini. Lakini nashauri suala la kupanda miti katika nchi au katika sehemu muhimu lisiwe

la kila Juni la mwaka kila mwezi wa Juni, isipokuwa liwe la kila siku angalau kwa

mwezi watafuta siku tatu kuweza kuotesha miti sehemu tofauti tusingejee Juni kwa ajili

ya kuotesha miti.

Kwa kweli nchi nyingi ambazo ndogo mkama hizi tukienda zina green kubwa miti mingi

kila design ya rangi na kivuli na mambo mengineyo. Sasa naomba hili suala kwamba kila

62

Juni liondoke naiwe mazoea kwamba tuoteshe miti kila tunapopata muda katika mwezi

angalau mara tatu kwa siku.

Mhe. Mwenyekiti, niende page nam. 19 ambayo inazungumzia Msitu wa Jozani. Msitu

huu unao magao wake kwa ajili ya kuendesha shughuli za msitu na itumike fedha hizo

kama inavyoeleza. Mhe. Mwenyekiti, naomba kumuuliza Mhe. Waziri eneo la Jozani

kwa sababu ni eneo la utalii na sehemu nyingi duniani tunaenda tunakuta kama

Ngorongoro National Park na sehemu nyenginezo Tanzania kuna mahoteli je mtu

atakayekuwa tayari ku invest hoteli ikiwa ndogo ikiwa kubwza ndani ya msitu wa Jozani

yuko tayari kama wizara kushirikiana mtu ku invest ndani ya Jozani Forest ama kwenu

kuna vikazo.

Kwa mfano, tukichukulia Tanzania bara kwenye parks kubwa kubwa za wanyama Wild

Park hizo National Reserve hizo wana mahoteli makubwa makubwa na hoteli ndogo sasa

ningependa kujua kwa upande wa Jozani muko tayari mtu kuweza ku invest hotel yoyote

kwza mujibu wa uwezo ambao atataka kufanya.

Lakini vile vile ningeenda kwenye page namba 20. Wizara iandae mpango wa kupatika

usafiri wa uhakikia kwa ajili ya usimamizi wa misitu. Mhe. Mwenyekiti, hapa wizarza

ikajibu inatumia milioni 180,000,000/= kununua gari tatu kwa ajili ya Msitu wa Jozani.

Mhe. Mwenyekiti, naomba kujua Mhe. Waziri hivi haiwezekani kutumika milioni

70,000,000/= kwa gari tatu instead of milioni 180,000,000/= kwa sababu milioni

180,000,000 ni fedha nyingi sana kwa kuzipitisha misituni kwenye ukaguzi, zipo gari

ambazo used Nissan yake Hilux ya juu milioni 30,000,000/= mazuri tuu ambayo

yametumika.

Kwa kweli, hapa tunakuta milioni 180,000,000 wakati income yenyewe ya Jozani Forest

sio kubwa ya hivyo. Mhe. Mwenyekiti, naomba kutoa ushauri fedha hizi zingepunguzwa

zingetafuta gari ambazo zitakuwa kidogo bei yake ya chini hata wanunue tano sita lakini

kuliko gari tatu kwa milioni180,000,000 kwa sababu tu ya doria ya Jozani au kuingia

kwenye vichochoro vya Jozani.

Mhe. Mwenyekiti, naomba kutoa ushauri wangu wa mwisho kwa masuala ambayo hili

suala la page namba 25 kuna watendaji waliondoka na vyombo vya moto. Lakini wizara

ikaeleza kwamba virejeshwe na inaeleza kwamba kuna vyombo karibu 15

vimesharejeshwa na watendaji ambavyo waliondoka navyo pikipiki 15 na magari 13.

Kwa kweli, nafikiri Mhe. Waziri haya mambo hayana haja kusubiri order kutoka kwenye

kamati hii iweko kwamba kitu kiwepo official kuwepo open kabisa kwamba mtendaji

hana haki kuondoka na kitu cha wizara au kitu cha serikali.

Suala hili ni zuri wamefanya. Lakini mengine kwamba nitakachoomba kwamba wizara

inahusisha zaidi watu wanyonge, wavuvi tungeomba watafutiwe maboti mazuri waweze

kupewa kwa kila kikundi, kama ikiwa Zanzibar kuna vikundi wakaanza basi kikundi

kimoja kikapewa boti moja kuweza kwenda kuvua deep sea….

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Nadiri naomba umalizie muda wako umekwisha.

63

Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf: Ahsante sana Mhe. Mwenyekiti.

Kwa hiyo, wakaweza kwenda kuvua deep sea mukawapatia meli za kisasa, na vile vile

wale watu ambao wanaotaka kuwakamata basi huko off shore ndio wanaofanya mambo

ya wizi wa samaki, na wale ambao local wanaovua kwa kiboti naomba sana waachiliwe

kwa sababu uvuvi wenyewe uko taabani vitendea kazi hawana, washughulike zaidi na

watu ambao wanavua off shore na meli kubwa.

Vile vile, wakulima wangu wa Jimbo la Chaani asiwasahau Mhe. Waziri naomba twende

pamoja tuhudhurie tukutane nao tuwasikilize shida zao, kwasababu washaniomba sana

Mhe. Waziri wa Kilimo aje na mimi leo nakupa tarifa hii kwamba ukipata muda twende

zetu pamoja tukamalize mambo.

Mhe. Mwenyekiti, nakushukuru sana kama nilivyosema wizara hii sina udhoefu nao ndio

maana nikajaribu kupiga piga kidogo na nashukuru sana na ripoti hii naikubali asilimia

mia moja ahsante sana.

Mhe. Mwenyekiti: Ahante sana Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf Mwakilishi wa Chaani

kwa mchango wako. Sasa naomba nimwite Mhe. Hamza Hassan Juma akifuatiwa na

Mhe. Suleiman Makame Ali na Mhe. Omar Seif Abeid ajiandae.

Mhe. Hamza Hassan Juma: Mhe. Mwenyekiti, mimi nikushukuru kunipa nafasi hii

nikaweza kuzungumza machache katika kumsaidia Mwenyekiti wetu wa Kamati kutia

nyama Ripoti ya Maagizo waliyotowa kwa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na

Uvuvi.

Mhe. Mwenyekiti, nataka kama walivyotangulia wenzangu kumpongeza sana Mhe.

Waziri pamoja na Naibu wake na kama alivyosema Mhe. Ali Suleiman Ali kweli Mhe.

Waziri wetu wa Kilimo ni mwalimu na anajua kulea namini Mhe. Waziri siku za mwanzo

kidogo naibu wetu alipokuwa anajibu maswali kidogo yalikuwa yanamkanga. Lakini kwa

kuwa amekaa na mwalimu sasa hivi tunashukuru tunapata majibu kutoka kwa Naibu

Waziri majibu ambayo yanaturidhisha tunapongeza sana. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, moja kwa moja nataka ninze katika ukurasa wa tisa katika kifungu cha

5 Ripoti inayosema Wizara ishajihishe wananchi kulima cha spices, kwani kilimo hiki

kimekuwa na soko kubwa ulimwenguni.

Mhe. Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Mhe. Waziri namna gani wizara

inavyoshirikana na Asasi ambazo Zisizo za Kiserikali yaani NGO’s katika kuhamasisha

uzalishaji wa hivi spices. Mhe. Mwenyekiti, naomba Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili,

Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Mhe. Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko.

Kwa kweli, nilihudhuria Maonesho ya Sabasaba pale viwanja vya Dar-es-Salaam.

Kimsingi ukiingia katika lile banda la Zanzibar na mimi kwa bahati nzuri miaka yote

huwa ninakwenda kuna improvement kidogo imeanza kujitokeza hasa katika vile

64

vifunganishi, kwa kweli wanajitahidi sana katika kuwasaidia. Lakini kuna kilio cha wale

wajasiriamali wetu na moja katika kilio chao wasema kwamba Wizara ya Kilimo,

Maliasili, Mifugo na Uvuvi inawapa mashirikiano pamoja na Wizara ya Biashara,

Viwanda na Masoko kuwapeleka kwenye yale maonesho.

Lakini kuna changamoto moja kubwa ambayo inayowakwanza hasa katika

kuzitengenezea ubora, yaani kuziweka katika ile standard ambayo nafikiri hapa inaitwa

ZBS. Sasa kitu ambacho wanalalamika wale wanasema ukiangalia wajasiriamali wetu

wanaoshughulika na hizi spices kwanza ni wadogo, yaani mitaji yao midogo. Sasa hizi

spices zao wanapokwenda kuzipeleka kwenye ukaguzi, yaani kila spice moja

wanalipishwa kile kima cha fedha nimekisahau lakini wanalipishwa kidogo fedha nyingi.

Kwa hivyo, wanasema kwamba sisi biashara zetu wanauza spices kama tano. Kutokana

na hali hiyo, kitu ambacho wanakiomba hawa kwamba zile spices zao wanapokwenda

kule ZBS basi alau watengenezewe kama package ya pamoja, ili waweze kupata unafuu

wa ile ada. Kwa kweli, wanasema ada inapokuwa kubwa ndio wakati mwengine

wanakimbia kwenda kule ZBS na matokezeo yake wanakwenda kule kwenye maonesho

super market zinakuja zinataka bidhaa, lakini inapofika pahala hebu nioneshe ile ZBS

yako utakuta wengine wanao ZBS nyengine hawana sasa hii inatokana na mitaji yao

midogo.

Sasa Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi pamoja na Waziri wa Biashara,

Viwanda na Masoko. Kwa kweli, miongoni mwa mawaziri ambao nawapongeza sana

kwa jitihada za kufanya utafiti na kutafuta namna gani yakuweza kuinua kiwango cha

bidhaa zetu wanajitahidi sana. Mhe. Mwenyekiti, ushauri wangu wangejaribu kutafuta

funds, pengine kupitia kwa mabenki mbali mbali, na sasa hivi tuna Benki ya Maendeleo

ya Kilimo kwa wenzetu Bara kule, nafikiri na hapa mjaribu ku invite, ili kuwasaidia hawa

hasa katika hizi gharama za kupimisha zile bidhaa zao ili ziwe na kiwango vizuri.

Mhe. Mwenyekiti, kwa mfano kuna mmoja yeye aliniambia tayari amepata soko kubwa

sana kwenye super market, na kwa kweli hata ule uwezo wake wa ku- supply katika

super market unakuwa ni mdogo, lakini sasa wengine hawa wachanga wachanga

wanashindwa katika hiyo. Nadhani Mhe. Waziri naomba katika jitihada zake za

kuhangaika huku na kule, basi wakae nao hawa, ili kuangalia hii changamoto ya kuweza

kuwasaidia hasa hizi gharama.

Lakini jenine Mhe. Mwenyekiti, ukurasa wa 12 hii paragraph ya 5. Kamati imesema

serikali ianzishe mpango maalum wa kuhamasisha wananchi kula bidhaa za mifugo kama

vile mayai, maziwa ikiwemo Siku Maalum ya Kunywa Maziwa. Mhe. Mwenyekiti,

jawabu ya Mhe. Waziri imeeleza hapa kwamba kuna Siku Maalum ambayo imewekwa

ya Mwezi Juni, lakini vile vile kupitia Idara ya Uhakika wa chakula na Lishe Program

Maalum ya Lishe Maskulini inaendelea kutoa taaluma.

Mhe. Mwenyekiti, kwa kweli naomba Mhe. Waziri anajitahidi sana katika kuhamasisha

kilimo cha uvuvi yaani ufugaji wa samaki, lakini naomba ajikite zaidi katika

kuwahudumia au kuwasimamia hawa wafugaji hasa katika suala zima la maziwa.

65

Kimsingi kipindi cha nyuma tulikuwa tunapata yale maziwa zamani tunaita maziwa ya

vibandani, lakini sasa hivi soko la maziwa kidogo wananchi wamekuwa wakiuza tu

kienyeji enyeji kwenye chupa hivi kunakuwa hakuna hasa ile package nzuri ya maziwa

ambayo wakulima wetu au wafugaji wetu wanaelekezwa.

Nadhani Mhe. Mwenyekiti, sasa hivi tunae muwekezaji wa Kiwanda cha Maziwa ndugu

yetu Bakhresa tunamshukuru, lakini bado support yake kwa wakulima hawa wa maziwa

haijakuwa nzuri na kiwanda kile sasa hivi tunaambiwa kinaagiza maziwa ya unga, ili

kuweza kutengeneza maziwa ya kunywa. Kwa hivyo, maziwa ya unga sitegemei kama

ubora wake yatakuwa sawa sawa na maziwa ya mifugo.

Kwa hivyo, Mhe. Mwenyekiti naomba Mhe. Waziri akae na muwekezaji yule aangalie ni

namna gani anaweza akasaidia kununua maziwa kutoka kwa hawa wafugaji, au wafugaji

hawa waweze kusaidiwa katika kutengeneza package nzuri ya kuhifadhi yale maziwa, ili

yaweze kutumika katika kiwango ambacho kilicho bora. Kwa kwali, hili naliomba Mhe.

Mwenyekiti, na wenzetu hawa wakulima au wafugaji wakiweza kusadiwa katika njia

hiyo naamini wataweza kupata moyo wa ufugaji, ili kuweza kuendeleza maisha yao.

Mhe. Mwenyekiti, vile vile ukurasa huu huu wa 12 kifungu No. 7 kinasema kutokana na

agizo linasema kutokana na ongezeko kubwa la ukuwaji wa sekta ya kilimo sambamba

na ukuwaji wa sekta ya mifugo tayari umeanza malalamiko katika maeneo ya ardhi ya

wakulima na wafugaji, ili kunusuru migogoro ambayo inaweza kujitokeza hapo baadaye

serikali ianzishe mpango maalum wa kutenga maeneo ya mifugo.

Mhe. Mwenyekiti, hili nashukuru kwamba serikali wamejibu jawabu nzuri. Lakini hapa

kitu ambacho nataka niseme zaidi katika kuyalinda hasa maeneo ya kilimo. Mhe.

Mwenyekiti, hivi sasa hivi kama tunavyojua population Zanzibar inazidi kuongezeka na

hili neno nitaendelea tena kulisema kwamba wakati tayari tuna dalili za uwekezaji wa

sekta ya mafuta na gesi Zanzibar, basi tutegemee immigration itakuwa kubwa watu

wataingia kwa wingi nchini.

Sambamba na hilo tena kwa bahati hapa Zanzibar bado Shirika letu la Nyumba

halijaweza kuwa na uwekezaji mkubwa katika kujenga nyumba, ambazo zitakazoweza

kuja ku-afford wale wahamiaji kuja kukaa katika nyumba zile. Kutokana na watu wetu

pengine na unyonge wao na umasikini wao mtu akitokezea na pesa yake ndogo basi mara

nyingi wako tayari kuuza ardhi zao kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi. Kwa kweli

hali hii, itapelekea sana haya maeneo ya kilimo ambayo yaliyobakia yataendelea

kuvamiwa kwa ajili ya kujengwa nyumba matokezeo yake wakulima wetu wataanza

kupoteza maeneo ya kulima.

Mhe. Mwenyekiti, hili naliomba kupitia Shirika la Nyumba ambayo Kamati yangu

inasimamia inajitahidi, lakini vile vile Mhe. Waziri, waweze kuyatambua Wizara ya

Kilimo hawezi kuyatambua maeneo ya kilimo na yalindwe maalum, ili kuhakikisha

kwamba yasivamiwe katika ujenzi wa makazi ya watu.

66

Mhe. Mwenyekiti, suala No 14 wizara kushirikiana na taasisi ukurasa wa 14 Idara ya

Misitu, Maliasili Zisizorejesheka, agizo linasema wizara kushirikiana na taasisi husika

iendelee kukomesha misumeno ya moto.

Mhe. Mwenyekiti, tumeona jitihada ya wizara katika suala zima la kuzuia misumeno hii

ya moto na katika jawabu la Mhe. Waziri humu ameeleza zaidi ya misumeno 55, Unguja

31, na Pemba 24 imeshakamatwa. Kwa hiyo, tunawapongeza sana serikali kwa jitihada

hii kwa sababu ni kweli kwamba hawa watumiaji wa misumeno ya moto wakati

mwengine wanaitumia vibaya, wanakata miti ya watu miembe michanga na miti mingine

ambayo inasababisha kuwavunja moyo wakulima lakini bado jitihada hizi ziongezeke.

Nadhani tungeliwashirikisha zaidi masheha kwa sababu masheha wao ndio wanaokaa

katika maeneo mbali mbali na hii misumeno ya moto inatumika katika shehia zao. Kwa

mfano, tukiangalia kama sasa hivi zao la minazi, yaani minazi mingi kwa kweli inakatwa,

kuna viwanda vingi vya mbao za minazi na kwa kweli minazi yetu inakuwa inaangamia

hasa kupitia hii misumeno ya moto. Lakini tunaipongeza jitihada ya wizara, lakini vile

vile wasipunguze kasi. Kwa hiyo, misumeno hii inaweza ikaangamiza miti yetu kwa kiasi

kikubwa.

Mhe. Mwenyekiti, ukurasa wa 16 katika eneo hili la Wizara ya Kilimo, kifungu Nam.3

agizo la kamati linasema serikali ianzishe sera maalum ya Green Policy, ili kuweza

kupanda miti kwa wingi katika nchi yetu. Tumeona hapa Mhe. Waziri wa Kilimo,

Maliasili, Mifugo na Uvuvi amesema kwamba kuna Siku Maalum ya Upandaji wa Miti

Kitaifa katika mwezi wa Machi ya kila mwaka. Mwenzangu amezungumza hapa Mhe.

Nadir Abdul-latif Yussuf, lakini na mimi vile vile nataka kuongezea, hili zoezi Mhe.

Mwenyekiti nadhani kwa kila mwaka mara moja kwa kweli bado kasi inakuwa ni ndogo,

na watu inafika pahala wanasahau. Unajua hewe hewe Waswahili wanasema inasaidia

kumfanya mtu aharakishe mwendo.

Nitachukulia mfano mdogo Mhe. Mwenyekiti, tunashukuru Baraza letu kupitia ziara

mbali mbali za kutupeleka kwenye kujifunza kwa vitendo, Baraza limeweza mimi

mwenyewe limenisafirisha nimekwenda China. Wakati ule nilipokwenda China

niligundua kwamba ndani ya barabara za ndani ya miji, yaani unakuta miti barabara zote

zimezungukwa na miti, yaani ile miti inafuata zile barabara. Sasa sisi tukajaribu

kuwauliza wale wenyeji wetu, hii miti mbona iko mingi mpaka mjini. Kwa kweli, wao

wakasema kwamba kuna mwaka kulikuwa kumefanyika mkutano mkubwa kule nchini

China, ambao ni mkutano wa Siku ya Mazingira Duniani, lakini vile vile mkutano

unazungumzia masuala ya kuondoa hewa chafu, pamoja na suala la kuhifadhi ile wanaita

tabianchi.

Kwa hiyo, kwa kuwa siku ile iliadhimishwa nchini China, kwa hiyo kupitia azimio katika

mkutano ule wenyewe wenyeji nchi ya China wakasema kuanzia leo tutahakikisha katika

kutekeleza huu mkutano au azimio la mkutano huu, tutahakikisha China nzima

inapandwa miti. Kwa maana hiyo, utakuta kule wenzetu hawasubiri siku moja kwa

mwaka wanashirikiana na Mabaraza ya Miji kuhakikisha kwamba wanapanda miti

67

maeneo ya mbali, yaani kama kwenye nursery halafu miti ile inang’olewa mizima

mizima inakuja kupandwa mjini, kama walivyofanya hapa Forodhani.

Mhe. Mwenyekiti, sasa imesaidia sana ile China kuifanya kwamba iko green, na hili

nilikuwa naomba sana Mhe. Waziri najua hakujipanga kwa bajeti hii, lakini tunashauri

katika bajeti inayokuja kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za

Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, basi tuhakikishe kwamba

tunaziboresha barabara zetu lakini pia tunapanda miti kila mara, ili kuhakikisha kwamba

nchi yetu inakuwa green. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, ukurasa wa 17, kifungu kidogo cha 4 wenzangu wamezungumzia hapa

suala hili la Kamati ilishauri kwamba wizara itoe taarifa kuhusu hali ya uchimbaji wa

mchanga. Kwa kweli, hili suala ni kweli ni muhimu Mhe. Waziri nafikiri iko haja hii

taarifa iletwe, ili tuipate kuichangia, kwa sababu wananchi wanalalamika upande wao

lakini na wale wadau ambao na- declare interest Mhe. Mwenyekiti na wao vile vile

wanalalamika upande wao. Sambamba na hilo, kama hivi karibuni kuna zoezi ambalo

linafanyika ambalo sisi tulilishauri kwenye vikao mbali mbali vya wizara kwamba

magari haya lazima yajuulikane hasa capacity yake ni tani ngapi.

Mhe. Mwenyekiti, hili zoezi Mhe. Waziri limeanza lakini naomba alisimamie kwa

karibu, kwa sababu kama nilivyosema mwanzo mimi na-declare interest kwa sababu ni

mdau katika sekta hiyo. Kuna wawekezaji hapa tulikuwa tunawasafirishia mchanga

katika maeneo yao, hao ndugu zetu wa China wakapima gari, gari ni tani kumi na moja

na nusu lakini sasa hivi gari imepigwa na Wizara ya Kilimo na Misitu inaambiwa ni tani

kumi na nusu, sasa which is which. Mhe. Mwenyekiti, nadhani Mhe. Waziri hili suala

ajaribu kulisimamia kwa karibu kwa sababu tusiangalie tu katika kupata mapato, kwa

sababu mfano gari hiyo ambayo ilikuwa inasomeka tani kumi na nusu, ilikuwa inalipiwa

shilingi elfu 78,100/= sasa hivi imepimwa tena inasomeka tani kumi na nne na nusu

inalipwa shilingi 94,500=.

Sasa watendaji wetu wakichukulia zaidi kuangalia kwenye kupata mapato matokeo yake

ile cost ina-reflect kwenda kwa wananchi vile vile. Tukiangalia magari haya yana

gharama kubwa sana running cost zake ni kubwa. Kwa hiyo, unaweza ukakuta kwamba

wananchi wanalalamika lakini vile vile ukiangalia na running cost vile vile zinaenda

sambamba na hizo gharama. Sasa mimi nadhani wizara ingeliangalia namna gani ya

kuweza kupunguza baadhi ya charge ili hii gharama isiweze kuongezeka.

Mhe. Mwenyekiti, lakini pia tunakushukuru sana Mhe. Waziri uko karibu sana na hili

suala tunashukuru mara zote unapopata ushauri unauchukulia hatua haraka haraka, kwa

hiyo tunakushukuru vile vile kwa mashirikiano yako.

Mhe. Mwenyekiti, la mwisho kabisa nilikuwa naangalia ukurasa wa 21, kifungu cha 12

kinachosema wizara iendelee kutumia wataalamu wake ili kubudi vivutio vyengine vya

watalii na wananchi wanaokwenda kutembelea kwenye misitu. Sasa Mhe. Mwenyekiti,

naendelea tena kulishukuru Baraza la Wawakilishi kuna mkutano mmoja nilihudhuria

kule Geneva na ile siku ambayo tuliyopata mapumziko tulipata nafasi ya kutoka kidogo

68

tukenda sehemu za mapumziko beach kule kama ilivyo Forodhani. Wenzetu kule

wamejaribu kuweka yale mabango ambayo yana-display usiku zinawaka taa ambazo

ukienda unaweza kusoma. Wameweka species kila species ya ndege aliyekuweko katika

nchi ile kwa hivyo wanaandika…

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Hamza naomba umalizie.

Mhe. Hamza Hassan Juma: Haya ndio namalizia.

Mhe. Mwenyekiti: Muda wako umekwisha malizia.

Mhe. Hamza Hassan Juma: Haya ndio namalizia Mhe. Mwenyekiti, sasa ndio najaribu

kumuhamasisha Mhe. Waziri tuandae ziara mimi na yeye kwenda Geneva ili

nikamuoneshe vile vivutio ambavyo vinaweza kusaidia utalii wetu. Mhe. Mwenyekiti, na

kwa sababu mfano ambao nautoa tena wenzetu wa China wanaweza wakakuelezeni

kwamba kuna jiwe liko hivi, liko hivi lakini matokezeo yake ukienda ukisema ah jiwe

lenyewe hili kumbe Zanzibar tuna mawe zaidi ya mia moja kama yale lakini tunashindwa

kuyatangaza.

Kwa hiyo, nadhani Mhe. Mwenyekiti eneo letu la Forodhani sasa hivi limejengwa vizuri

linapendeza tungeliweza ku-display maeneo hayo, tukaweka species zinazopatikana

Zanzibar tukaeleza historia zake ingesaidia wageni wale kwenda kuwapeleka katika

vivutio vya utalii bila ya wenyewe kukusudia.

Baada ya hayo machache Mhe. Mwenyekiti, nakushukuru kunipa nafasi hii naunga

mkono ripoti hii ya kamati, lakini vile vile utekelezaji wa Mhe. Waziri katika ripoti ya

kamati. Ahsante sana.

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante sana Mhe. Hamza Hassan Juma kwa mchango wako.

Waheshimiwa Wajumbe, nina wachangiaji kama wanne waliobakia na tukiangalia muda

wetu unatuacha mkono, sasa niwaombe wajumbe nitakaowapa nafasi wachangie Mhe.

Suleiman Makame Ali umeniomba dakika tano nitakupa dakika tano halafu atafuata na

Mhe. Omar Seif Abeid ili tupate tumpe nafasi Mhe. Waziri atoe majumuisho. Lakini

kabla ya Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi nitampa pia nafasi Mhe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed

na baadaye Mhe. Waziri atatupa ufafanuzi kwa zile hoja zilizotolewa. Mhe. Suleiman

Makame Ali.

Mhe. Suleiman Makame Ali: Ahsante sana Mhe. Mwenyekiti, na mimi nashukuru kwa

kunipa nafasi hii ya kuweza kuchangia taarifa hii ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo

na Uvuvi kuhusu utekelezaji wa maoni ya kamati.

Mhe. Mwenyekiti, niende kwenye ukurasa wa 15 kamati walisema kwamba kuwe na

usimamizi wa utaratibu kuhusu masuala ya misumeno ya moto. Mhe. Mwenyekiti,

kwanza niipongeze sana kamati pamoja na wizara kwa kuliona hili na kuhakikisha

kwamba wanaidhibiti misumeno ya moto, kwa sababu kusema la ukweli misumeno ya

69

moto inaathiri sana na inatusababishia ukame na ndio ukaona jua hili linawaka kutokana

na kwamba miti haipo kila siku inakatwa.

Mhe. Mwenyekiti, jambo la kusikitisha kwamba wizara imesema kwamba kuna baadhi

ya masheha hawatoi ushirikiano. Sasa naomba kusema hapa kwamba huyu sheha

anafanya kazi kwenye Serikali hii ya Mapinduzi, ikiwa kama hawezi kutoa ushirikiano

kwenye wizara hii basi huyo hafai aondoke Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala

za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ yupo.

Kwa kweli, kama sheha hawezi kutoa ushirikiano na anajua kwamba fulani na fulani ndio

wanaodhibiti msumeno wa moto ndani ya shehia yake, lakini hawezi kutoa ushirikiano

kwa sababu ni kwamba hawezi kukabiliana na kazi yake, kwani pamoja na majukumu ya

kazi na hilo nalo ndilo. Kwa hiyo, sheha huyo itakuwa hafai na Mhe. Waziri nakuomba

sana kwamba masheha hawa wote wakibainika basi ni kwamba waondoshwe kwa

utaratibu na kisheria kama inavyojuulikana.

Mhe. Mwenyekiti, nikiondoka hapo niende kwenye ukurasa wa 24 kuhusu masuala ya

ukodishwaji wa mashamba.

Mhe. Mwenyekiti, kwanza niipongeze serikali sana, sana kwa kuliona hili lakini pia

nimpongeze huyo aliyepeleka wazo hili kuhakikisha kwamba mashamba yote ya serikali

lengo ni kujuulikana ili kudhibitiwa. Mhe. Mwenyekiti, kuna baadhi ya watu kwa sababu

tayari ile adhma ya muasisi wa Mapinduzi Mzee Abeid Amani Karume wengine

hawakufahamu, tayari kuna baadhi ya wengine wameshayauza mashamba haya na ndio

serikali ikaona kwamba ipo haja ya kuyatambua. Sasa maoni yangu kwa wizara pamoja

na kamati na serikali kwa ujumla kuhakikisha kwamba mashamba haya yaliyotambuliwa

na kama kuna mengine yawekwe wazi na ya juulikane lakini na kama kutakuwa kuna

watu wanayaficha makusudi kama ilivyokusudia wizara wayarudishe kwenye serikali

basi wachukuliwe hatua watu hao.

Mhe. Mwenyekiti, naiomba wizara kwamba ikeshahakikisha basi wale wakulima ambao

mashamba haya wanayashughulikia wakati ilikuwa lengo ni kuyajua, warejeshewe

wenyewe kwa sababu wao ndio waliokuwa wakiyatunza mashamba yale. Kwa kweli,

nina imani wakati ilikuwa kama wao ndio waliokuwa wakiyatunza mashamba yale, basi

wakirejeshewa kwa utaratibu uliokuwa mzuri nina imani kwamba hawatuthubutu

kufanya tena kitendo hiki ambacho walikuwa wanakifanya wengine.

Kwa hiyo, naomba sana Mhe. Waziri badala ya kuhakikiwa mashamba haya wale wote

ambao kwamba walikuwa wakiyatunza mashamba haya warejewe kwa utaratibu mzuri na

tayari wapewe kumiliki lakini isiwe kama kupewa kwa sababu kuna wengine huwa ni

watarazakuna wakiwepa tawi wanachukua na lile shina kwamba ndio hao waliokuwa

wakiuza mashamba. Hivyo, imani yangu ni kwamba wakifahamishwa wataweza kujua na

wataweza kukaa na mashamba haya vizuri, ili kuhakikisha kwamba serikali inapata

mapato yake.

70

Mhe. Mwenyekiti, mkulima wa karafuu kwa tunavyodhibiti magendo nina imani

hatathubutu kuchuma karafuu halafu akaiuza kinyemela, kwa sababu tayari atachuma

karafuu na atapeleka ZSTC kila sehemu sasa hivi kuna vituo vya kununulia karafuu. Kwa

hivyo, naiomba sana wizara kwa sababu lengo ni kuyajua mashamba haya na si kama

wanavyopotosha huko mitaani, kwa sababu kuna waliokuwa hawaitakii mema nchi yetu,

wanasema kwamba mashamba ya mikarafuu wakulima wamenyanganywa.

Kwa kweli, hilo sio lengo hawakunyanganywa mimi naunga mkono kwa sababu Mhe.

Rais wa Zanzibar pia alisema mpaka kule Makonyo kwamba hawakunyanganywa, lengo

ni kuyatambua ili yajuulikane lakini nina imani kwamba mashamba haya yatarejeshwa.

Kwa hiyo, naomba sana Mhe. Waziri kupitia wizara yako badala ya kuyahakiki

mashamba haya wale wenyewe warejeshewe, ili waendelee kuyaenzi na kuyatunza.

Mhe. Mwenyekiti, nikitoka hapo niende kwenye ukurasa 30 kuhusu suala la wafugaji

samaki.

Mhe. Mwenyekiti, kwanza niipongeze sana wizara kwa kuhakikisha kwamba wafugaji

samaki wamepewa taaluma na mimi hilo nathibitisha ni kweli, kwa sababu ndani ya

jimbo langu Shehia ya Ndagoni wanafuga samaki na walikuja pale Maruhubi, Nyangumi

House wakapata mafunzo pale kama mwezi mzima. Kwa hiyo, naiomba sana wizara

kuhakikisha kwamba ufugaji samaki uendelezwe kwa sababu tayari watu wapo tayari

kuhakikisha kwamba wanafuga samaki, pweza, chaza na mambo mengine. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, lakini niende kwenye suala la uvuvi haramu imeelezewa hapa suala la

uvuvi haramu. Mhe. Mwenyekiti, kuna uvuvi haramu unatuathiri kama vile utupa, nyavu

za kukokota na mambo mengine. Lakini Mhe. Mwenyekiti, huyo mvuvi lengo ni kufika

bahari kuu, bahari kuu atafikaje apate chombo cha uhakika cha kuweza kufika bahari

kuu. Mhe. Mwenyekiti, kuna uvuvi unaitwa dhulmati pengine wengine hawaufahamu

humu, lakini uvuvi ule wa dhulmati unavuliwa bahari kuu. Kuna uvuvi wa nyavu za

jarufe unavuliwa bahari kuu.

Kwa maana hiyo, wale wavuvi wakipatiwa vyanzo hivi vya kuvua kwa bahari kuu basi

mimi nina imani wataondokana na uvuvi haramu. Kwa hiyo, naiomba sana wizara

wahakikishe waweze kuwapatia wavuvi vyombo vya uhakika ili kuweza kufika kule

bahari kuu na waache kuvua kuvua uvuvi haramu wa mabomu na mambo mengine.

Mhe. Mwenyekiti, naunga mkono ripoti hii asilimia mia kwa mia. Ahsante sana. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante sana mheshimiwa kwa mchango wako sasa naomba nimpe

dakika tano Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi na baadae atafuatiwa Mhe. Waziri wa Nchi,

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na baadae nitampisha Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo,

Maliasili, Mifugo na Uvuvi na mwisho kabisa atatumalizia Mhe. Waziri wa Kilimo,

Maliasili, Mifugo na Uvuvi.

Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi: Ahsante sana Mhe. Mwenyekiti, kwa kunipa fursa hii ya

mwisho mwisho na mimi kuchangia kwenye mada hii iliyowasilishwa na Wizara ya

71

Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, inayohusika na chakula, ndio maana chakula chote

kinatokana na uzalishaji wa kilimo dunia nzima hii.

Kwanza kabisa kidogo niseme jambo lilonigusa kwamba mwenzangu hapa alichangia,

alikuwa anachangia vizuri baadaye akaja akatoa maneno ambayo kwa kweli si ya

kuridhisha. Kwa kweli, yamenivunja moyo sana nasema lakini namuomba Mwenyezi

Mungu na mimi asinielekeze nikasema maneno kama yale hata nikiwa na jazba za aina

gani. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, sasa kwa kuanza kuchangia nimesema kwamba kilimo ndio uti wa

mgongo wa uchumi wa dunia nzima, kilimo ndio kinachotupa chakula. Ukitizama hapa

mavazi tuliyovaa, chakula tulichokula chote kinatoka kwenye kilimo, hata hivyo viwanda

vinavyotayarisha vyakula vinapata raw material kutoka kilimo chenyewe. Kwa hiyo,

kilimo ni muhimu sana.

Mhe. Mwenyekiti, hapa nimeangalia haya maagizo takriban yote kabisa halafu

nikaangalia na mikakati yote iliyoelezwa humu ambayo wameleta malengo malengo 18,

yote yanalenga kwenye kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula ambayo ni nzuri sana.

Nasema uzalishaji hauwezi kuwepo wa kutosha kama hakuna jambo la kwanza kabisa

utafiti. Jambo la pili elimu ya ugani, la tatu ambalo ni la maumbile mazingira yetu. Haya

mazingira haya kuwe na misitu ilete mvua, kuwe na nini mambo yote yanayohusika na

mazingira ambayo yatakuwa ni rafiki kwa mazao kuota vizuri, basi hayo mazingira hayo

yanatakiwa.

Mhe. Mwenyekiti, sasa tukiangalia uzalishaji wetu unavyokwenda na vile unavyokuwa

kidogo haujaenda kwa ile kasi ambayo itatuwezesha tujitosheleze kwa chakula kwa

kipindi pengine cha miaka mitano au kumi ijayo tuna muda mrefu sana. Sasa kwa sababu,

ili tuzalishe lazima kuwe na utafiti wa kutosha, na utafiti wa kilimo unaambatana na

mambo ya kujaribu mazao mbali mbali, mbegu mbali mbali kuzijaribu ukaona ipi inafaa

kumpelekea mkulima.

Mkulima anafanyiwa demonstration plot, sasa hivi demonstration plot zinamvutia

mkulima anaoneshwa labda hapa pawekwa mbolea kiasi fulani, hapa panawekwa dawa

kiasi fulani halafu anaona matokeo pamoja na huduma zote zile za mbolea. Sasa sidhani

kama kuna demonsration plot zinazoendelea kwa sasa kama zipo zinaweza kuwa zipo

lakini zinahitaji kuongezwa kasi ya demonsration plot, ili uzalishaji uongezeke.

Mhe. Mwenyekiti, jengine ni training wakulima wetu, ili wazalishe lazima wafundishwe

hiyo elimu ya organ tunaita. Kuna mabwana shamba wengi sana nafikiri kila shehia

takriban kila shehia kuna bwana shamba kwa hilo tumefanikiwa vizuri sana. Kwa hivyo,

sasa kinachotakiwa hawa mabwana organ wapewe teknoloji ya kisasa ambayo ni

innovation tunaita, ili waweze kusambaza kwa wakulima kwa wakati inavyotakiwa na

wakulima.

Vile vile, hizi pembejeo zetu ambazo siku zote tunatumia mbolea na madawa, lakini

mbolea siku zote ni NPK yaani ile mbolea ya ammonia upate nitrogen, kuna ile ya

72

calcium na ile ya potassium siku zote na inaitwa blanket recommendation,yaani popote

hatuangalii udongo wa aina wala wa aina gani. Kwa kweli, weka gunia moja la mbolea

chumvi chumvi, weka robo gunia ya mbolea ya potassium, weka nusu gunia ya mbolea

nyengine hivyo tunakwenda. Sasa utafiti hautaki hivyo, utafiti unatakiwa kila aina ya

udongo una recommendation zake a mbolea, ili uweze kufanikisha pamoja na hiyo

irrigation ambayo mimea ipate maji ya kutosha ili iweze kuzalisha mazao ya kutosha.

Mhe. Mwenyekiti, sasa hivi sidhani kama kuna tafiti za kutosha nasema tafiti za kutosha

za udongo, zipo tafiti za udongo zinafanywa lakini sijui kama zinatosha kabisa kukidhi

haja ya kutuwezesha na sisi tukaweza kuzalisha. Wenzetu wa sasa hivi wanaweza

kuzalisha hekta moja tani 20 pengine na zaidi, lakini tuseme tani 20 za mpunga. Hivi sasa

sisi nadhani kama tumefikia labda tani 8 au 10 average, bado tuko chini sana. Hivyo, ili

tujitosheleze tunahitaji kuongeza bidii, kuongea tafiti nyingi sana ili tuweze kupata

mazao mengi na bora.

Sasa nikiingia kwenye mazingira yetu ukiangalia historia ule msitu wa Jozani na wa

Kiwengwa ulikuwa umekwenda moja kwa moja mpaka Nungwi.

Mhe. Mwenyekiti: Mhe. Mjumbe, dakika tano tayari.

Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi: Ahsante sana Mhe. Mwenyekiti. Kwa kweli,

nilichokusudia kusema ni kwamba misitu sasa hivi tunahifadhi vizuri lakini bado

inakatwa, tujaribu sana kuhifadhi misitu yetu tuwaelimishe wananchi wasikate misitu

tuwatafutie njia mbadala za kupikia ili hii misitu yetu isikatwe. Vile vile na sehemu

ambamo si lazima kujenga wanaweza wakapewa sehemu nyengine, basi wapewe sehemu

za kujenga muzuri misitu yetu iendelee kuota.

Mhe. Mwenyekiti, baada ya kuzungumza hayo muda tutakuwa nao huko mbele kuja

kuchangia Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi. Kwa hiyo, nakushukuru sana

kwa kunipa nafasi hii leo, ni nafasi ya mwisho lakini ni nafasi nzuri.

Ahsante sana Mhe. Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante sana Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi. Lakini kwanza nimuombe

radhi Mhe. Omar Seif Abeid nilikutaja kabla ya Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi. Kwa hiyo,

naomba radhi kwa hili kutokana na muda, hivyo naomba mchango wako upeleke kwa

maandishi. Sasa naomba nimwite Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa

Rais kwa dakika tano. (Makofi)

Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais: Mhe. Mwenyekiti,

nakushukuru nitajitahidi niseme kwa dakika tano. Mhe. Mwenyekiti, Baraza lako tukufu

hili ni chombo kikubwa sana. Sisi Waheshimiwa Wajumbe tuliomo humu wananchi

wanatusikiliza kwa makini maelezo yetu, tunavyochangia kwa maslahi yao na maendeleo

ya nchi yetu. Kwa hiyo, lazima tuwe waangalifu sana na kauli zetu, hasa pale

tunapowazungumza wenzetu ambao wao hawana nafasi ya kuingia humu ndani wala

73

hawana nafasi ya kujitetea. Kwa hivyo, ni vizuri sana maneno yetu yawe yana misingi ya

kufuata kanuni na taatibu zetu tulizojiwekea katika Baraza hili.

Mhe. Mwenyekiti, ni hivi juzi tu, wakati ukimaliza mjadala wa Wizara ya Mawasiliano,

Ujenzi na Usafirishaji Mhe. Naibu Spika, alituwaidh na kututaka sana Waheshimiwa

Wajumbe tujikite katika kuchangia taarifa zinazowasilishwa, ili tuweze kutoa mchango

wetu vizuri kwa kufuata taratibu zetu za kikanuni, lakini kwa kusaidia wananchi wetu na

maendeleo yetu. Kwa hiyo, tunapotamka baadhi ya maneno yanaweza kabisa kutuondoa

katika mstari ambao umekusudiwa.

Mhe. Mwenyekiti, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo kwa mujibu wa Katiba na

Sheria. Tumefanya hivyo kwa kupitia misingi ya kidemokrasia mpaka kufikia hatua hii

ambayo leo sote tupo hapa ndani na si kwa njia nyengine yoyote, lakini kwa sababu ya

katiba na sheria ndio iliyoweka serikali kwenye mamlaka. Tulishindana vyama vingi

Chama cha Mapinduzi ndicho kilichokubalika na wengi kwa wananchi kikachaguliwa na

serikali yake inafanya kazi ya kutekeleza Ilani hiyo na kwa umakini mkubwa mawaziri

wote wanafanya kazi zao vizuri kwa misingi ya katiba, sheria, kanuni na maelekezo

yanayotolewa na serikali. (Makofi)

Naamini wajumbe wengi humu ndani wanaridhika na utendaji kazi kwa mawaziri na

serikali kwa ujumla wake, na ndio maana taarifa zetu tunazoleta hapa, kwa kiasi kikubwa

Waheshimiwa Wajumbe wamezipitisha vizuri sana na ahsanteni sana. (Makofi)

Sisi tutaendelea kushirikiana vyema na Baraza hili tukufu, ili kutekeleza kazi zetu kwa

umakini mkubwa na kufuata misingi na taratibu zilizowekwa na kuhakikisha kwamba

tunatoa huduma bora kwa wananchi. Lakini tungewaomba sana Waheshimiwa Wajumbe

baadhi yetu tuangalie sana kauli zetu, kwa sababu maelezo mengine yanaweza kutoa

tafsiri tafauti na yakaharibu sura nzima ya nchi yetu. Kwa hiyo, hiki ni chombo kikubwa

tuna wajibu sote kwa pamoja kutekeleza majukumu yetu vizuri.

Mhe. Mwenyekiti, sisi kwa upande wa serikali tunawahakikishia chombo hiki kitukufu

na wananchi wote wa Zanzibar kwamba mambo yetu yatakwenda kwa kufuata katiba ya

nchi, sheria na kutekeleza wajibu wetu kama unavyoelekezwa na serikali. Kwa msingi

huo, tutaendelea kufanya kazi zetu kwa umakini mkubwa, kwa busara na kutekeleza yale

yote yenye maslahi ya wananchi na nchi yake.

Mhe. Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,

sasa naomba nimwite Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi na uzingatie

muda kwa sababu nitakupa dakika tano na dakika kumi zilizobaki tutamuachia Mhe.

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.

Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Mhe. Mwenyekiti ahsante

sana. Nimpongeze sana Mhe. Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo kwa

74

mashirikiano yao katika utekelezaji wetu wa kazi hizi za Wizara ya Kilimo, Maliasili,

Mifugo na Uvuvi. Moja kwa moja niende katika masuala ya kilimo kuhusiana na mchele.

Mhe. Mwenyekiti, mchele unapatikana katika wizara yetu kuna duka letu pale, mkulima

huyu ana uwezo wa kuzalisha tani 5 itategemea na mpunga jinsi vile anavyoupata.

Tumpongeze sana Mhe. Naibu Katibu anayehusiana na mambo ya kilimo kwa kutoa

msaada mkubwa kumsaidia kijana huyu kuweza kupata mashine hii ya kukobolea

mpunga.

Mhe. Mwenyekiti, moja kwa moja niende kwenye wakulima ambao wanamwagilia maji.

Kuna Mhe. Mjumbe alisema kwamba labda tumewasahau wale ambao wanatumia mvua.

Hatukuwasahau lakini hawa wa umwagiliaji maji kilimo chao kinaanza mwanzo halafu

ndio wanafuata hawa wa mvua. Kwa hiyo, mwanzo tunawapa wao halafu baadae

watafuata wale wa mvua. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, niondoke hapo kwenye kilimo niende moja kwa moja kwenye mifugo.

Vijana ambao tumewapatia elimu hii ya mifugo ni vijana 204 kwa kupitia mradi wa ASP,

ASPDL, vile vile vijana hawa wanajisaidia binafsi kwani ni ajira zao wenyewe na kuwa

kama wamejiajiri kupitia wizara hii.

Mhe. Mwenyekiti, niondoke hapo niende kwenye maliasili. Maliasili bado tuna

changamoto kubwa sana kuhusiana na misitu, bado wananchi hawataki kukubaliana na

zile taratibu ambazo tumewawekea, bado uharibifu wa misitu ni mkubwa sana. Kwa

hiyo, nitoe wito kwa wananchi pamoja na Wawakilishi wa Baraza hili tuweze kusaidiana

katika kutunza misitu hii ambayo inazunguka katika nchi yetu ya Zanzibar.

Mhe. Mwenyekiti, niende moja kwa moja kwenye uvuvi. Uvuvi tuna vyombo ambavyo

tumevisajili, mnamo tarehe 28/9/2017 tulizindua rasmi ukaguzi wa vyombo vya Bahari

Kuu ambavyo vitavua hapa. Vijana wetu ni kweli wamebahatika kupata nafasi za kazi

mule na hawa Kichina hawajui lakini wanasaidiwa na yupo mmoja ambaye anajua

kuzungumza Kiingereza kwa hivyo wanasaidiwa katika lugha ya Kiingereza.

Mhe. Mwenyekiti, napenda kumtaarifu Mhe. Mjumbe kwamba, kuhusiana na samaki wa

kufuga. Samaki hawa hawana athari yoyote kiafya ikiwa watafugwa kwa utaratibu

unaofaa. Vile vile wana taste kama samaki ambao tunawavua baharini.

Mhe. Mwenyekiti, jengine Mhe. Mjumbe aliomba lini nitakuwa na nafasi ya kwenda

naye ziara katika jimbo lake la Chaani. Mimi niko tayari muda wowote yeye tu,

nitakwenda na wataalamu wangu wa kilimo, ili tuweze kuona tunasaidia vipi wananchi

hawa wa Chaani.

Mhe. Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja ripoti hii ya Kamati ya

Fedha, Biashara na Kilimo ahsante. (Makofi)

75

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante sana Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na

Uvuvi. Sasa naomba nimwite Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa

ajili ya kutoa ufafaunuzi juu ya hoja zilizowasilishwa na Waheshimiwa Wajumbe.

Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi: Mhe. Mwenyekiti, kwanza

nikushukuru na niwashukuru Waheshimiwa Wajumbe waliopata fursa ya kuchangia na

wale waliopata nafasi ya kusikiliza.

Mhe. Mwenyekiti, waliochangia kwanza nimshukuru sana na naomba niwatambe kama

ifuatavyo:-

Mhe. Hamad Abdalla Rashid kwa kazi nzuri aliyoifanya kuwasilisha ripoti kwa
niaba ya kamati.

Mhe. Ali Suleiman Ali
Mhe. Abdalla Maulid Diwani
Mhe. Miraji Khamis Mussa
Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf
Mhe. Hamza Hassan Juma
Mhe. Suleiman Makame Ali
Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi
Mhe. Masoud Abrahman Masoud
Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi na
Mhe. Naibu Waziri wa Afya amechangia kwa maandishi na kama kuna mtu
nimemsahau naomba radhi sana. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, kwa sababu ya muda hoja zilizotolewa ni za msingi sana nataka

niseme tu kwamba kwa niaba ya serikali ambayo tunaiwakilisha hapa tunazipokea.

Lakini nataka niseme mambo matatu. (Makofi)

La kwanza, sote tunafanya kazi hapa zaidi tukitizama Ilani ya Uchaguzi wa CCM

ambayo ndio iliyoingia madarakani kwa kupitia ilani hiyo ya uchaguzi, na anayesimamia

ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nataka niseme kama kuna mtu anafanya

kazi kwa uadilifu mkubwa sana kwa moyo wa kujituma na upenzi mkubwa sana, na

Mwenyezi Mungu ndiye aliyemchagua kushika madaraka, si tume, si chochote

Mwenyezi Mungu ndiye anayepanga nani ashike madaraka. Mimi na wewe tuko hapa

lakini Mwenyezi Mungu aliyepanga kushika madaraka, uki-question hiyo una-question

authority ya Mwenyezi Mungu. (Makofi)

Mhe. Mwenyeikiti, sisi tumepitia Mwenyezi Mungu ametuteuwa tufanye hiyo kazi yake,

tumeifanya kwa uadilifu, tumepata kiondozi muadilifu anafanya kazi kwa uadilifu

pamoja na yule ambaye yumo humu ndani, basi mchakato ni huo huo. Kwa kweli,

naomba sana hili jambo tuliheshimu sana ni jambo linatokana na Mwenyezi Mungu

wenzetu wengine wanatangaza kuapishwa kila siku asubuhi hawajaapishwa, kwa sababu

Mwenyezi Mungu hakuwachagua, hilo tu Mwenyezi Mungu hajawachagua. Uongozi

unatokana na Mwenyezi Mungu someni aya za Qur-an ziko very clear. (Makofi)

76

Kwa hivyo, mimi nasema Mhe. Mwenyekiti, tusichanganye maneno. Lakini tujue

wenzetu wengine mnatokana na vyama vyenu na mimi natokana na chama changu,

huwezi ukakibeza chama chako kilichokufikisha kwenye madaraka, mana unapoquestion

uteuzi wowote ule ambao na wewe ni sehemu yake maana yake una-question

legality ya chama chako na authority ya chama chako si sahihi hata kidogo. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, naomba Waheshimiwa Wajumbe tuwe na tahadhari, tumeingia kwa

sababu ya nafasi za chama tulichokipata ambacho tumekikubali wenyewe. Nataka niseme

hili kwa sababu kwa uzoefu wangu nafaa kutoa wasia wakati mwengine kwa mambo

kama haya makubwa yanapotokea. (Makofi)

Pili Mhe. Mwenyekiti, niseme kwamba Waheshimiwa Wajumbe wamesema mambo

mengi sana na ya msingi, mengine ni ushauri mzuri sana. Tumepata ushauri wa Mhe.

Dkt. Makame Ali Ussi hapa mambo ya mbolea kwamba tuangalie udongo na kadhalika,

tumepata ushauri wa namna gani zero grazing tufanye na kadhilika, ushauri wa kila aina.

Kwa dakika 20 Mhe. Mwenyekiti, nafikiri nitakuwa siufanyii haki ukumbi huu, ila

niseme mambo mawili makubwa ambayo yameguswa sana.

Kwanza ni suala la mchanga. Mhe. Rais wa Zanzibar amelitolea maamuzi, amelitolea

msimamo wa serikali. Makamo wa Pili Rais hapa ndani ya Baraza hili amefanya kazi hii,

mimi nimefanya kazi hii, ndiyo tukasema katika exercise tunayoendelea nayo sasa hivi

bado serikali itaendelea kutoa taaluma na kuelimisha. Waheshimiwa Wajumbe tukimaliza

processes ya kupeleka kwenye Baraza la Mapinduzi tutakuja tena kwenye Baraza hili

tutakuelezeni latest position juu ya mchanga wala msiwe na wasi wasi kama kamati

ilivyoagiza. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, la msingi tujue tu kama rasilimali hii haipo, hili neno nataka nilirudie

na Mhe. Rais wa Zanzibar alilisema vizuri katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini.

Alisema na akatoa mifano kwamba hata Mombasa leo hawana mchanga, Ghana hawana

mchanga, duniani kote ukenda kwenye mitandao unakuta kuna crises kubwa sana ya

mchanga, kwa sababu matumizi ya mchanga yamebadilika sasa wanatumia hata kwenye

kuchimbia mafuta.

Mhe. Mwenyekiti, kwanza tukubali kwamba (resource) rasilimali haipo, tunahitaji

kujipanga na serikali imejipanga itakuja itatoa maelezo ya kina namna gani ilivyojipanga

katika suala zima la kuendelea na sekta ya mchanga. Hilo naomba tukubaliane kabisa

wala msiwe na wasisi wasisi wowote Waheshimiwa Wajumbe tutakuja hapa tutakaa

pamoja tutalitatua. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, matatizo ambayo yanatokea ndani ya utekelezaji kama alivyosema

Mhe. Hamza Hassan Juma tuko tayari wakati wowote njooni ofisini tukae pamoja, kama

kuna kasoro ya kiutekelezaji ni kasoro za kibinaadamu tutazitatua kwa pamoja hilo

nimesema niliseme.

77

Mhe. Mwenyekiti, kuhusu mbolea kwamba kampuni iliyokuja pale wakati ule ikaleta

mbolea, siyo mbolea ilikuwa ni mbegu mbovu na kampuni inaitwa Hanzwaa. Kampuni

ya Bajuta tunataka tuishukuru sana kwa miaka minne mfululizo imeikopesha serikali

mpaka inadai serikali 3,069,000,000/=, ilivumilia muda mrefu sana.

Mhe. Mwenyekiti, kwa mara ya kwanza nataka nimshukuru sana Mhe. Rais wa Zanzibar

kwa mara ya kwanza tulikuwa tunapata mbolea asilimia 15 mpaka 20 ya mahitaji. Kwa

mara ya kwanza Mhe. Rais wa Zanzibar mara hii ameagiza tupate mbolea na pembejeo

zote kwa asilimia isiyopungua 50. Kwa kweli, hiyo imetokana na wale waliowahi kuonja

mchele mara hii na nawakaribisha waje pale kwenye duka la kilimo wanunue mchele

ambao ni mtamu sana unashinda wa Mbeya, waje waone kazi ambayo aliyoifanya Mhe.

Rais wa Zanzibar kwa kusimamia wizara hii tukahakikisha wakulima wetu wanazalisha

vizuri, wanazidisha chakula vizuri sana. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti, leo nilikuwa nawakulima kutoka Tumbatu, wanasema kwa mara ya

kwanza wana magunia matano, sita, kumi ya mpunga ndani ya nyumba zao ni mafanikio

makubwa sana. Kwa hivyo, nasema serikali imejipanga vizuri katika hili jambo la

kusimamia kilimo na mimi nataka niwakaribishe Waheshimiwa Wajumbe hapa muje

tarehe 10 kwenye siku ya Chakula Duniani kwenye Maonesho ya Kizimbani, muone hizo

mnazosema pilot project tunazozifanya demonstration farm tunazozifanya, lakini kazi

kubwa tujue ni sisi wananchi kazi yetu kufanya sio wizara kufanya.

Kazi ya wizara kubwa ni kusimamia policy, taratibu na taaluma kwa wananchi wafanyaji

ni wananchi wenyewe siyo sisi hata kidogo, kwanza hilo tulielewe. Lakini serikali vile

vile ilijiondoa katika kufanya biashara. Maana tumekuwa questioned hapa ooh! kwa nini

hamjatekeza ZAFICO na nini. Tulikubaliana kabisa Mashirika ya Umma yamalizike

muda wake twende katika sekta binafsi kuziimarisha. Mhe. Mwenyekiti, wasome vizuri

kwenye Ilani ya Uchuguzi ya CCM inasema nini.

Hivyo, ndio maana serikali kwa kuona kwamba baadhi ya maeneo mengine hatujafanya

vizuri tukaanzisha Kampuni ya Uvuvi sasa hivi, ni kwa sababu pale ambapo tunaona

bado sekta binafsi haijachukuwa role na mahitaji ya wananchi ya yapo serikali ndio

inachukua hatua ku-intervene. Itakapofikia pahala ZAFICO tumekosa chakula cha mifugo

hapatikani mtu serikali itachukuwa jukumu ya kufanya hivyo, ili kuhakikisha kabisa

chakula cha kuku na mifugo kinapatikana.

Kwa hiyo, nasema serikali kwa upande mmoja inaendelea na kushajihisha kufanya sekta

binafsi ishiriki pale inaposhindika serikali itatunza wajibu wake, ili kuwaondolewa

wananchi shida ambazo wanazo.

Jengine Mhe. Mwenyekiti, niseme ni kweli mahitaji ya mchele ni makubwa lakini nataka

niwashukuru sana wakulima. Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia baadhi ya wakulima

wamevuna si chini ya tani 3,5,6 mpaka 8 wengine kwa kutumia taalum ya Shadid. Jambo

la msingi lililopo ni kwamba wananchi lazima wabadilike wakubali kutumia teknolojia za

kisasa, wakubali kusikilizam taaluma ili waweze kupiga hatua na nina mfano ulio hai.

78

Mhe. Mwenyekiti, tulikwenda kwenye bonde la Bumbwisudi na Mhe. Mwakilini hapa

mmoja, jirani yao walikubali kufata taalum wamevuna vizuri, jirani hakufanya utaalamu

kavuna vibaya, mashamba ya sehemu moja. Kwa hivyo, kama mkulima akikubali kufuata

utaalam nahakikisha kabisa mambo haya yataweza kubadilika.

Jengine ambalo Mhe. Mwenyekiti, niseme haraka haraka ni suala la mifugo. Kweli kweli,

kabisa katika Sekta ya Mifugo bado hatujenda vizuri sana, lakini tumefanya programu

moja nzuri sana kopa ng’ombe, lipa ngombe. Pale tulipozungumzia Zero Grazing tayari

tuna wafugaji wasiopungua 300 ambao wako katika ufugaji wa lipa ng’ombe, fuga

ng’ombe wako katika Zero Grazing. Huu mradi bahati mbaya ulimalizika kati kati. Hata

hivyo, hivi sasa kwa kushirikiana na Benki ya Kilimo tunaurudisha tena badala ya

mkulima kukopa ng’ombe, akalipa ng’ombe, atakopa pesa anunue ng’ombe, alipe pesa na

atapewa na grace period ndani yake.

Mhe. Mwenyekiti, najua muda wako unaniandama sana. Lakini nataka niseme haya

makubwa la mchanga tutalishughulikia na taarifa itakuja mradi tuende kwenye process

zile za serikali. Suala la mbolea kama nilivyosema Mhe. Rais wa Zanzibar amejitahidi

sana tuweza angalau sisi kupata nusu naamini mazao yataonekana na asubuhi liliulizwa

swala kama je, ahadi yangu ile la kujiuzulu ipo? Mhe. Mwenyekiti, narudia tena mimi

namuani sana Mwenyezi Mungu na naamini kabisa Mwenyezi Mungu anasimama na

uongozi ulio imara, meena mnazoziona zipo hizi hapa ni uadilifu na utiifu kwa Mwenyezi

Mungu kwa Dkt. Ali Mohammed Shein na wafuasi wake. (Makofi)

Tuna kila sababu ya kujivuna mazao ya pembeleo ya chakula mara hii mengi, mazao ya

matunda tulikuwa tunaagizia asilimia 80 kutoka Bara sasa tunaagizia asilimia 20, mazao

ya karafuu mara hii hata hayasemeki. Kila neema Mwenyezi Mungu katupa iliyobakia ni

hasada ambayo ipo na Inshaallah Mwenyezi Mungu ataijaalia itashindwa hivi karibuni.

Mhe. Mwenyekiti, naomba kutoa hoja. (Makofi)

Mhe. Mwenyekiti: Ahsante sana Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili Mifugo na Uvuvi.

Sasa niwahoji wale wanaokubaliana na ripoti ya Mhe. Waziri wa Kilimo, Maliasili,

Mifugo na Uvuvi wanyanyue mikono, wanaokataa, wanaokubali wameshinda. (Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

(Hoja iliamuliwa na kuafikiwa)

Mhe. Mwenyekiti: Waheshimiwa Wajumbe, namshukuru sana Mwenyezi Mungu lakini

pia nimpongeza Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi na watendaji wake wote

pamoja na Wenyeviti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi kwa ripoti zao. Lakini pia

niwashukuru Waheshimiwa Wajumbe kwa utulivu kwa muda wote tuliokuwepo hapa

naomba niakhirishe kikao mpaka kesho saa 3 asubuhi.

(Saa 1:45 usiku Baraza liliakhirishwa hadi tarehe 6/10/2017 saa 3: 00 asubuhi)

79

Zanzibar Yetu

Share: