Habari

KIPI BORA:Nguvu za Dola au Watu wanaolilia haki zao???

Once upon Time

Alikuwepo marehemu CUF: Innalillah Waina Ilaihi Rajighuun

Marehemu CUF, alizaliwa munamo 1992. Baba yake CUF ni merehemu Kama Huru na mama yake kwa bahati alikuwa ni Bismilah, lakini Bismilah alikufa mapema na mzee Kama Huru kumuoa mwanamke mmoja wa Kitanganyika aliekuwa akiitwa Vuguvugu la watu (Civic movement).  Tokea marehemu azaliwe, amekuwa mwiba kwa mfumo kandamizi wa utawala wa kijana CCM na babu yake  Popobawa Muungano, hasa kwa upande wa Zanzizibar. Mwiba na wasi wasi huo uliwakumba watawala wa mfumo mbovu wa Siasa za Kikoloni mambo leo pale siku mtoto CUF alipompindua kwa mabondia kijana CCM katika uchaguzi wa mwanzo wa Vyama vingi October 1995. CUF alikuwa na umri wa miaka 3 tu  alipo mbwaga kijana CCM ambae alikuwa ana  nguvu, kiburi na jeuri kubwa. Jeuri hii inakuja kwa sababu anabebwa na  vyombo vya dola pamoja na babu yake Popobawa Muungano. Hata hivo nuru  ya CUF ilianza kumtia kiwewe Popobawa Muungano na kijana CCM nakuanza kufanya mbinu kwa kuwatumia Wazanzibari ili kijana  CUF asije kupata uongozi katika Visiwa vya Zanzibar.

Hata hivo nguvu ya CUF haikutokana na pesa wala Material Goods bali ni uzalendo uliojengwa na imani na uungwana wa watu wengi wanyonge ambao wanaendelea kudhulumiwa, subira na matumaini yakumpenda CUF na wale waandamizi wake. Hivo kijana CUF aliwavutia Wazanzibari  na baadhi ya Watanganyika wanyonge nakuanza kuwa na matumaini  na kumpenda. Kwa  njia nyengine tunaweza kusema  CUF alikuwa na umma uliomfuata nyuma na kumuona ni muokozi wa kulivua au kulijadili  “Popobawa jeusi la Muungano  na kumuondoa kijana CCM. Popobawa la Muungano limekuwa likiwanyanyasa hata Watanganyika wanyonge kwakuchota rasilimali zao na kuufaidisha mfumo wa watu wachache wanao mlinda kijana CCM na babu yake Popobawa Muungano. Kwa upande wa Zanzibar popobawa hili limekuwa  kitanzi  au tambara chafu linalo kugubika nakuwamaliza puumzi Wazanzibari kwa miaka mingi sasa.

CUF amefariki akiwa mdogo sana mwenye umri wa miaka 27½, na  kifo chake kimesababishwa na walezi  wake (jamaa zake wa Umamani  kutokaTanganyika). Hawa ndio chanzo cha husda na choyo dhidi yake, ambao wamekubali kununuliwa kwa fedha nyingi sana za walipa kodi; ili wamtowe roho CUF. Hata hivo kifo cha marehemu CUF kilitabiriwa rasmi mwaka 2015 pale alipombwaga tena Kijana wa makamo CCM, ambae sasa utawala wake kijana huyu umekuwa wa khofu, vitisho, dhulma na vilio  kwa watu wa Tanganyika na Zanzibar.

 

Kwanini CUF achukize kwa Utawala wa CCM na Mfumo wa Dola??

Wakati CUF alipozaliwa 19 93 alikubalika moja kwa moja kule Visiwani Zanzibar, kwasababu kama nilivosema hapo juu. Tokea mapinduzi haramu ya Zanzibar ya 1964,  Wazanzibari wamekuwa hawana raha wala furaha kwa Popobawa jeusi  la Muungano. Popobawa Muungano ni mfumo ambao baba yake CCM na mama yake wanautumia kuwanyanyasa Wazanzibari na kuwagombanisha wenyewe kwa wenyewe ili wapate kuwaibia ardhi yao ndogo ambayo ina hazina ya utamaduni, dini na imani kutoka 1200.  Hivo basi kuzaliwa kwa CUF Wazanzibari waliona kuna chombo mbadala ambacho kinaweza kusimama na kuwatetea Wazanzibari hao. CUF huyu alipozaliwa alilelewa na maalim Sefu pamoja na kundi lake la wana siasa waliofungwa na CCM.  CUF alipitia misuko suko mikubwa na na kusalitiwa na walezi wake wengi wa umamani hadi kuja Profesa Lipumba, ambae huyu ndie aliekamilisha kifo chake siku ile ya 2016 aliposema anataka arudishiwe kijana wake CUF. Malezi ya Lipumba kwa CUF yalikuwa yana utata na wasi wasi huku kwa upande wa Wazanzibari CUF alienziwa kwa uvumilivu wake, Wazanzibari wakimtegemea sana kuikomboa Zanzibar. Hio ndio historia ya CUF

Rambi rambi kwa CUF na uzalendo aliotuachia Wazanzibari.

Nakumbuka wakati wa 1998, maalim alipotiwa ndani  yeye na Mh. Ali Haji Pandu, marehemu Sudi Yussuf Mgeni, Haji Mgwali,  na wengine (nimewasahau majina). Nakumbuka Wazanzibari vijana wakiwemo akina Nassor Sefu, Marehemu Bahorera walipo fanya maandamano ya amani kupinga kauli ya Sofia Kawawa kuhusiana na Quran au  Sheria za dini za kiislamu juu ya urithi. Kauli zile ziliwafanya Wazanzibari wengi waanze kumuona kijana CCM kumbe ni kijana aliekuwa na  msimamo mkali wa dini yake ya Kikristo aliofundishwa kwa umahiri na baba yake Popobawa Muungano.  na katika dini hio Popobawa Muungano anakuwa pembeni mwa CCM. Licha ya kwamba wazazi wake walisema yeye  CCM hana dini yoyote  lakini . Wananchi wengi walianza kuuchunguza Utawala wa CCM wa ndani na nje nakuziangalia nyanja zote za kiuchumi ni jinsi gani nyanja hizi zilikuwa zina dhibitiwa na watu wenye Dini ambayo CCM ndio anaiyabudu. Marehemu CUF kwa upande wa Zanzibar ameacha waombolezaji wapatao 1.5 milion na kule Tanganyika idadi hatuijuwi. Waombelezaji hawa wamelia tokea 2016 pale mlezi wa marehemu CUF Profesa Lipimba alipoanza kumshambulia kwa Mapanga kijana CUF.

Nakumbuka nikiwa teenager nilikuwa nyuma ya maandamano yale, hadi polisi walipoaingilia kati nakuanza kupiga watu viboko in retaliation, wananchi waliwarushia mawe polisi hao na maandamano kufanikiwa kuzimwa. Kilichofuata ni kamata kamata ilioletwa na m Polisi mawe. “Nakumbuka! Nakumbuka! Nakumbu hii itabakia kuwa historia.

Baada ya CUF kufariki dunia, Kijana CCM amekuwa akitumia baadhi ya vyombo vya dola kama vile Jaji Litungi nakutoa maneno ovyo dhidi ya Wazanzibari ambao wamepata kijana mwengine mdogo ACT wakuwaliwaza na  “Pengine” kuwasaidia safari yao ya mabadiliko. Hakuna asiejuwa kwamba kijana huyu CCM amekuwa akimtumia Lipumba ( aliekuwa mlezi wa marehemu CUF) nakufanya Sanamu la CUF -Lipumba nakuliabudu.  CCM amefanya haya sio kwa utani bali nikutaka kuhakikisha kwamba dhamira ya kumsaidia babu yake Popobawa Muungano kuimeza kabisa kabisa Zanzibar. Lipumba kwa upande wake kule Tanganyika anajuwa wazi kama hana watu  wakumfuata yeye kuabudu Mzimu wa Marehemu CUF kwa faida ya kupewa ruzuku. Lakini aanatumia vyombo vya Dola ambavo vinamilikiwa na CCM pamoja na babu yakePopobawa Muungano ili awadanganye Watanganyika na Wazanzibari.

Masuali yetu tunamuuliza CCM, Popobawa Muungano na Mtumishi wao Lipumba. Ni kipi kizuri kuwa na umma wa watu wanaokupenda nakukuamini kwa uungwana wako?

AU

Pesa na mfumo kandamizi ambao unawatumilia wale watu wenye imani ndogo ya kidini na kimila na watu wenye Umimi?

Lipoumba ajuwe kwamba Wazanzibari hasa hao Wapemba alio wataka wasikubali ACT bali wakijenge kivuli cha marehemu CUF, watu hawa wanajuwa kwamba CUF ni umma wa watu wenye matumaini yakupata mfumo mzuri na wa haki wa uongozi na sio kundi la Makuhani wavhache wanaotumia fedha za Umma na kuendelea kuwakandamiza Watu hao.

Share: