Habari

KISIWANDUI IMEITIKA JINA: Jussa Facebook

KISIWANDUI IMEITIKA JINA

Katika SURA AT-TAUBAH, aya ya 119, Allah ametuusia tumche Mwenyezi Mungu na tuwe pamoja na watu wakweli. Wasia huu hautaki ufafanunuzi kwa sababu maisha yanasherehesha tafsiri na sababu za wasia huo.

Watu wasipokuwa wakweli wataanza kudanganya watu lakini wakishtadi katika upotofu huo huanza kujidanganya wenyewe na kuwataka watu sasa waamini uongo wao. Haya ndio yanayojitokeza kwa uwazi katika utawala wa sasa wa Kisiwandui. Kujidanganya na kutaka watu waamini uongo wao.

Mswada uliopitishwa hivi karibuni na Baraza lisilo na Wawakilishi umezaa kioja cha ajabu na Mwenyekiti wa Wenyeviti Bwana Hamza Hassan Juma akiamini ana hoja timamu ya kutungua hata roketi ikiwa angani alisema kwa kinywa kipana hoja zumbukuku hoja tatu za kituko.
Hapa tunaangazia kwa ufupi hoja zake hizo na kutoa majibu kwa ufupi.
a) Hoja ya Baraza la Wawakilishi Kuidhinishwa Kutunga Sheria ya Mafuta ya Zanzibar.

Alisema kuwa Bunge la JMT kwa kutumia mamlaka yake ya kutunga sheria za Muungano limeidhinisha Baraza la Wawakilishi kutunga sheria ya mafuta ya Zanzibar. Alisema haya kwa kinywa kipana, kadamnasi akiwa live katika redio Swahiba FM.

Majibu aliyopewa yaliakisi hoja pofu na potofu aliyotoa. Kwanza ni kanuni ya Sheria yoyote duniani kuwa Sheria haiwezi kukasimu mamlaka ya kutunga sheria nyengine. Sheria siku zote inakasimu uwezo wa kutunga kanuni yaani sheria ya kukasimiwa (delegated legislation). Bwana Hamza hakuweza kujibu hoja hiyo kwamba hivi kwa kuruhusiwa na Bunge, vipi Baraza litatunga Sheria? Baraza litakuwa limetunga Kanuni. Hoja hiyo pia iliambatana na ile ya masharti ya Ibara ya 64 ya Katiba ya JMT inayosema kwamba endapo Baraza la Wawakilishi litatunga sheria kwa jambo ambalo limo mikononi mwa Bunge, Sheria hiyo itatenguka. Wanasheria wanapenda kusema “void ab initio”…yaani hii ni sawa na noti feki, batil tokea nasabu yake, batili tokea mimba yake illipotungwa…batil zaidi ya haram. Mnajua majibu ya Hamza? .. Mhh yanachekesha. Anasema mbona sisi Zanzibar tumeshazoea kuvunja Katiba na hakijatokea chochote???
Majibu ya ziada aliyopewa ni kuwa hata hiyo sheria ya Bara mloisoma kinyumenyume mbona haijawapa mamlaka ya kutunga sheria ya mafuta mbona haijasema hivyo? Akauliza kwa sauti ya chini imesemaje??? Akajibiwa kakaeni muisome tena labda mlipoisoma mwanzo mlihadaliwa na gilligilani ya siasa na kicheko cha wizi cha Kikwete na maneno ya kifedhuli ya Magufuli… mkadhani mmepata kumbe mmepandwa mgongoni!!! Sheria ya Mkoloni inasema hivi:

“2. This Act shall, subject to subsection (2) apply to Mainland Tanzania as well as Tanzania Zanzibar-
(2) The regulation of petroleum upstream operations, midstream and downstream activities and matters incidental thereto to which this Act apply shall-
(a) where such operations or activities are undertaken within Mainland Tanzania, be governed and administered by institutions established or referred to under this Act; and
(b) where such operations or activities are undertaken within Tanzania Zanzibar, be governed and administered by institutions in accordance with the laws of Tanzania Zanzibar.

Sheria ya Mkoloni inasema wazi kuwa Sheria itayotumika ni moja tu nayo ni ile ya Mkoloni. Zanzibar inachoruhusiwa ni “devolution” katika kuisimamia tu sheria hiyo ya Mkoloni, sio kutunga ya kwake.

Mkoloni hajafanya hivyo kwa bahati mbaya. Ni kwa kuidhibiti sekta hii. Kwani mamlaka ya kugawa vitalu yanabaki kwa Waziri wa Mkoloni na hata mamlaka ya kutangaza eneo la utafiti yanabaki kwao.

b) Hoja ya Mipaka

Bwana Hamza anasema kuwa wamepitisha sheria ili wapate nguvu ya kudai mipaka kwani mipaka ni katika mambo madogo madogo ya kushughulikiwa baadae.
Alipewa majibu ya kina kwamba kwanza hoja ya mipaka ndio ilokwamisha suala la jambo hili kutolewa katika Muungano na Mkoloni ndio mana amesubiri mpaka Zanzibar walipoingia vipofu ndio akawadanganya kuwa kawaruhusu kumbe anawadhibiti zaidi.
Kwanza, Mkoloni ameshakivamia rasmi kisiwa cha Fungu Mbaraka ambacho ni cha Zanzibar kabla hata Mkoloni hajazaliwa. Na ametangaza hata katika makongamano ya kimataifa pale Chatham House, tarehe 26 Februari, 2013.

Pili, Mkoloni anadai kuwa katika kugawa mipaka itumike kanuni ya equidistance line. Hii ni hoja ya kichekesho lakini Mkoloni wetu hana haya. Kanuni hiyo haiwezi kutumika kwa sababu mpaka wetu wa kaskazini baina ya Tanganyika na Zanzibar ndio huo huo wa Kenya na Tanzania ambao umetumia mfumo wa “parallel of latitude”. Aidha, kwa upande wa Kusini Zanzibar haina mpka wa nchi kavu na Tanganyika, hivyo kinachoangaliwa ni wapi territorial waters za Zanzibar zimeishia kwa upande wa Kusini. Bila shaka ndio maana Mkoloni anadai Latham kwa sababu itaipunguzia Zanzibar urefu wa kilomita 60 ndani ya Bahari. Watu wetu wa Kisiwandui hata hilo hawalioni? Wanacheza siasa katika uwepo wa nchi???

OTHMAN MASOUD OTHMAN ☆MWANASHERIA☆

Tagsslider
Share: