Kitaifa

Al Bashir: Sudan haitaanzisha uhusiano na Israel ‘ Zanzibar inaikumbatia Israel

Rais wa Sudan ametangaza kuwa nchi yake kamwe haitakuwa na mahusiano na utawala haramu wa Kizayuni. Rais Omar al Bashir amesema kuwa Sudan haitaanzisha uhusiano na Israel kwa hali yoyote ile.

Rais huyo amesema Marekani na nchi nyingine nyingi zinaiwekea mashinikizo nchi yake ili ianzishe uhusiano na utawala wa Kizayuni, lakini akasisitiza kuwa Khartoum haitasalimu amri mbele ya mashinikizo hayo. Ameongeza kuwa nchi hizo zinasema kuwa zitaisaidia Sudan kumaliza mgogoro wake wa kiuchumi iwapo itaanzisha uhusiano na Israel, lakini akasema kwamba wananchi wa Sudan hawahitaji msaada wa aina hiyo.

Share: