DIRAKitaifa

Bandari zetu Zanzibar na Bara

Bara mizigo imepungua tokea Magufuli aingie madarakani na ziara za kushtukizia,sasa wafanya biashara wameamua kurudi tena Zanzibar kushushia mizigo..Bara wameshtukia hili,wakatoa kwanza sababu ya kupungua mizigo Bara eti uchumi wa China umedorora,ndio maana na mizigo imepungua Bara..

Pili,wakaona mizigo inashushwa Zanzibar kisha inapelekwa Bara,Wakaamua kupitisha bajeti yao juzi kuwa,mizigo yote destination Bara hata kama itashushwa Zanzibar basi ushuru ulipiwe Bara ( imagine kwanza hii ni nchi moja lakini mishuru miwili)

Tatu,Ushuru wa mizigo inotoka Bara kuelekea Zanzibar ilipiwe Zanzibar, mazao yanayozalishwa Tanzania yasamehewe ushuru,na utalii uongezewe kodi ( nimeona mashirika ya watalii wameandika barua kulalamika kodi zimepanda mno kwa nchi za Kenya na Tanzania).. hapa judge mwenyewe.. kitu gani kinachotoka bara kuja Zanzibar saivi? asilimia ngapi itatoka kule kuja ZNZ,na hata ukilipa ZNZ TRA ndio wakusanyaji.

Nne, Juzi Ijumaa ya tarehe 16 nimesikia Rais kazindua kreni mpya ya mizigo kutatua tatizo la makontena msongamano,na Bwana Manji kakubali kuwapa miezi 6 kutumia uwanja wake walomuzia kuweka empty containers walozisababisha wenyewe kwa ucheleweshaji wao.

Tano,Bandari haina hata Ramp ya kushushia magari kwenye container tena ya chini tu,nimeona juzi gari zinashuka kwenye container zimepangiwa mipira chini zinakanyaga,gari moja ikavunjika hapo hapo bumper la nyuma,TRA wanaambiwa wanaharibu, basi wakaanza kuwaka eti hawalipi kosa sio lao, sasa kosa la nani na sheria wao wanasema gari huruhusiwi kuendesha hadi wakutolee nje ya bandari…basic things zinakosekana na watu wanalipa mapesa kibao.

Sita, Baadhi ya kampuni zimegoma kuleta mizigo Zanzibar wanasema destination ni bara kisha ufanye maarifa mwenyewe kupeleka Zanzibar,na nyengine wamesema kuna charge ya ucheleweshaji saivi container kushushwa Zanzibar.

Hivi mambo haya yataisha lini?

Share: