Kitaifa

Tunataka kiti chetu UN

MAKAO MAKUU UN
PlayPlay

 

MAKAO MAKUU UN

Balozi wa Jamhuri ya watu wa ZANZIBAR akifuailia kwa makini vikao vya Umoja huo

 

 

Kwa kweli huu ni wakati muafaka wa WAZANZIBAR kushinikiza viongozi na wawakilishi kudai kuitishwa KURA YA MAONI kuhusu kuwepo au kutoka kwenye MUUNGANO.

Hii ni kwa sababu balaa la kuimaliza zanzibar na rasilimali zake linazidi kuongezeka kutokana na ukweli kuwa wazanzibar sasa hivi wako kitu kimoja na hatari katika mjadala wa KATIBA MPYA wanaweza kuukataa muungano au wakadai serikali tatu jambo ambalo litahatarisha maslahi ya TANGANYIKA.

Kwa hiyo basi kwa habari za uhakika ni kuwa bado kiti chetu kipo UN hivyo basi kama tukivunja muungano basi wao watanganyika ndio itawalazimu waombe kiti chao.

Hivyo basi natoa wito kwa makundi yote wakiwemo wanasheria, waandishi wa habari, masheikh, wanafunzi, wasanii na watu wote waungane pamoja kuukoleza moto ili mapambano yashike kasi tayari hofu sasa imewajaa.

Share: