KitaifaMakala/Tahariri

Viongozi wa SMZ mnabururwa!

Hivi kweli hii wizara ya Mambo ya nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Tanzania ama wa Tanganyika?
Kwani kila nikiangalia uwakilishi wa wazanzibari kwenye wizara hiyo muhimu ya muungano nashindwa kuona uiano wa karibu, maana ukienda kwenye wizara wenyewe Wazanzibari wapo wachache mno, na hata katika Afisi za Kibalozi basi kuna nyengine hakuna hata mzanzibari mmoja yaani hata wa dawa humpati.

Hukaa nikajiuliza hivi hizi Balozi ni za Muungano ama ni za Tanganyika? sasa ukiingia kwenye hizo Balozi zenyewe hata ile sehemu ya kukaribishia wanaokwenda huoni hata picha moja ya Zanzibar, yaani kilimanjaro, serengeti na kadhalika.

Ukiangalia local employers, ndio kabisa usiseme yaani wewe mwenyewe utacheka mambo ndio hayo kwa hayo.

Pia kuna baadhi ya maofisa pia huwa wakiona muda wao unakaribia kwisha basi hujidai kutafuta masomo na kuanza kwenda kusoma ili wapate kubaki na kazi za kibalozi huwa zinazorota. hali muradi mambo ni shaghala baghala.

Hili suala la katiba hili wala halitokuwa ndio suluhisho la Muungano bali litazidisha mazongano.

Suluhisho kama lazima tuwe na Muungano basi na uwe kama huu wa European Union.

Share: