Habari

Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani UN afariki dunia

Picha: Kofi Annan, Katibu Mkuu wa UN kuanzia tarehe 1/1/1997 – 31/12/2006

Bern, Switzerland
Saturday, August 18, 2018

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan amefariki dunia akiwa hospitali mjini Bern, Switzerland baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Annan ambaye ni mshindi wa ‘Nobel Peace Prize’ inayohusiana na kazi maalum za kuhudumia binadamu, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Alishika cheo cha Katibu Mkuu wa Umaja wa Mataifa kuanzia Januari 1, 1997 hadi Desemba 31, 2006 alikuwa ni Katibu Mkuu wa saba wa umoja huo.

Former UN Secretary General Kofi Annan has died aged 80 after battling a short illness.

Mr Annan, who won the Nobel Peace Prize for humanitarian work, died in hospital in Bern, Switzerland this morning with his wife and three children by his side.

The family confirmed the tragic news on his Twitter account, writing: “It is with immense sadness that the Annan family and the Kofi Annan Foundation announce that Kofi Annan, former Secretary General of the United Nations and Nobel Peace Laureate, passed away peacefully on Saturday 18th August after a short illness,” read a post on his Twitter account.
“His wife Nane and their children Ama, Kojo and Nine were by his side during his last days.”

Annan, mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambaye alifanya kazi hiyo kwa mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.

Baadaye alipoondoka katika nafasi hiyo aliteuliwa na umoja huo kuwa Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Syria katika kutafuta suluhu ya amani nchi humo.

Katika taarifa iliyotangaza kufariki kwake, wakfu wa Kofi Annan ulimtaja kama mtu aliyejitolea sana katika masuala ya kimataifa ambaye katika maisha yake yote alipigania kuwepo ulimwengu wenye amani.

Annan akiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, uongozi wake ulikumbwa na matukio mazito na makubwa hasa vita vya Iraq pamoja na janga la ugonjwa wa ukimwi (HIV).

1938: Alizaliwa tarehe 8 Aprili, Kumasi ambao sasa ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Ghana
1962: Alianza kufanya kazi kwennye Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswiss
1965: Akamuoa Titi Alakija, amabye walizaa watoto wawili mwanamke na mwanamme
1984: Alimuoa Nane Lagergren, baada ya kumtaliki Titi Alakija, mwaka 1983
1991: Dada yake ambaye ni pacha Efua, alifariki
1993: Akawa mkuu wa oparesheni wa UN za kulinda amani
1997: Ateuliwa kuwa katibu mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa – UN
2001: Alishinda tuzo la amani kuhusu huduma za binadamu
2006: Aondoka ofisini kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa baada ya kufanyakazi kwa miaka 10

Kofi Atta Annan na dada yake Efua Atta Annan, walizaliwa kwenye mji wa Kumasi, Ghana nchi ambayo wakati huo ilikuwa inajulikana kama Gold Coast, Aprili 8, 1938.

Majina ya pacha hao yaliamaanisha kuwa walizaliwa siku ya Ijumaa, huku majina yao ya kati yakimaamisha kuwa waliukuwa ni pacha.

Alikulia kwenye familia ya kitajiri, mababu zake walikuwa ni viongozi wa tamaduni na baba yake alikuwa ni gavana wa mkoa wakati nchi bado ilikuwa chini ya utawala wa ukoloni wa Uingereza

Alisoma chuo kikuu wakati Ghana ndiyo kwanza ilikuwa imepata uhuru na baadaye alisoma Macalester College, Marekani. Annan aliajira kwenye Umoja wa Mataifa, Taasisi ya WHO.

Kazi yake alikuwa ofisa wa bajeti wa Shirika la Afya la Dunia (WHO) alifanyakazi hiyo kwa zaidi ya miongo minne hadi alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UN, mwaka 1997.

Mwaka 1993 Annan alikuwa amepanda cheo baada ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu na Mdhamini Mkuu wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya usimamizi wa amani.

Mwaka mmoja baadaye kulitokea mauwaji ya kimbari nchini Rwanda, ambako idadi ya watusi na wahutu 800,000 waliuawa katika kipindi cha siku 100 nchini humo.

Kisha mnmo mwaka 1995 waislamu 8,000 wa Bosnia, wakahamishwa na vikosi vya Serbia katika kile kilichotajwa kuwa kuwapatia eneo salama kwa usimamizi wa Umoja wa Mataifa nchini Bosnia.

Kufuatia matukio hayo mawili mabaya sana, Umoja wa Mataifa, kupitia Annan, ulilaumiwa vikali baada ya kuelezwa kuwa idara yake ilikuwa imepuuza taarifa walizokuwa wamepewa ikionya kuwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalikuwa yamepangwa.

Mwaka 2003 Marekani wakatangaza kuwa wangeenda vitani nchini Iraq. Mwishowe Marekani wakaupuuza zuio lililotolewa na Umoja wa Mataifa na kuivamia Iraq.

Hatua hii ilileta uhasama kati ya Annan na Marekani. Akizungumzia uvamizi huo, baadaye aliiambia BBC kuwa “kwa maoni yetu sisi uvamizi huo ulikuwa kinyume cha sheria.’

Tofauti hizo kati ya Annan na Marekani zilimletea matatizo baadaye kuhusu sakata lililojulikana kama “mafuta kwa chakula” iliyoibuka mwaka 2004.

Miezi 18 kabla hajastaafu, mwezi Disemba mwaka 2006 aliondoka ofisini. Akiwa na karibu miaka 70, ulikuwa ni umri ambapo watu wengi wanataka kupumzika.

Kofi Annan pamoja na mke wake wa pili, wakili raia wa Sweden, Nane Marie Lagergren, waliofungua ndoa mwaka 1984, walikwenda nchini Italy kwa likizo la wiki sita.

Kulingana na Gazeti la The Guardian, baada ya wiki moja akiwa kwenye likizo aliamua kutoka kwenda kununua gazeti dukani lakini akajikuta amezingirwa na kundi la vijana waliyokuwa wanahitaji kupata sahihi yake.

Kwa bahati mbaya walikuwa wamemfananisha Annan na mchezaji filamu Mmarekani Morgan Freeman. Hakukataa, aliweka sahihi kwa kuandika jina Freeman na kukimbia.

Kofi Annan na mcheza filamu huyo wa Marekani, Morgan Freeman wanashabihiyana sana kwa umbo, sura na kimo. Kofi Annan endepo ataonekana kwa ghafla, hawezi kutofautishwa na Morgan Freeman.

Baadaye mwaka 2007, alifungua Wakfu wake ‘Kofi Annan Foundation’ (kofiannafoundation.org) ofisi zake kuu zipo mjini Geneva, Switzerland kwa minnajili ya kusaidia maendeleo, usalama na amani.

Share: