Habari

kuazima machine za usajili wa wapiga kura kwa jirani ni sawa na kuazima msuwaki wa mwezio,

Hakuna asiejuwa kwamba utayarishaji wa usajili wa daftari la wapiga kura si jambo dogo. na ni jambo ambalo linagharimu fedha nyingi sana, na lina ulazima wa daftari hilo kuwa hai kwa wakati wote.

kwetu Tanzania jambo hili halikupewa umuhimu na ulazima unaostahiqi kuwepo katika jambo kama hili.
kulipozuka utafutaji wa kura ya maoni juu ya katiba mpya, kulilazimu utaratibu wa kupatikana usajili uliobora na utakaokubalika ili hatimae kuwezekane kupigiwa kura katiba itakayopendekezwa hapo itakapokuwa tayari.

Juu yakuwa jambo hili halikutekelewa kwa dhamira njema toka lilipoanzishwa kwake, lakini ninaweza kusema yakuwa hata kusudio lenyewe la kadhia hii lina walakin wake.

Tumeishi na muungano wa Tanzania uliobuniwa na waasisi wetu kwa miaka zaidi ya khamsini bila yakuwa na uhalali na viashirio vya kukubalika, ila kwa ubabe wa hali ya juu, kwa wale watakaothubutu kuuhoji muunngano huu kwa miaka hii yote ilikuwa ni ukhaini!!

leo tupo wengi tunajiuliza, hivyo kwa miaka yoote hii, juu yakuwa walijitokeza wapinzani kudai katiba mpya itakayokwenda na wakati na kukataliwa, iweje hii leo ghafla kujitokeze shamrashamra za kukubalika pawepo na katiba ya muungano mpya? kimezidi nini? na nini sababu zake? Ndugu zangu suala hili ni muhimu sana kujiuliza ili tupate jawabu sahihi ya kuturidhisha.

Tuna uzowefu wa kuona kwamba jambo lolote kubwa ambalo linahitajia kutekelezwa nchini kwetu huwa linahitajia kuombewa fedha au kukopewa ili litekelezeke. khasa linapokuwa linahitaji gharama kubwa kutekelezeka.na haya hayatekelezwi isipokuwa kuwe na ulazima wa kufanya hivyo. sasa ulazima wa kufanya hivyo unatokana na nini? na kwanini haya yasifanywe kabla ya hapo, kukingojwa nini?

Sasa ukijiuliza mambo kama haya utagunduwa yakwamba liko jambo ambalo limesabibisha haya yote yagharimiwe ili liweze kutekelezeka!! kinyume na sababu hii kungekuwa hakuna ulazima wa jambo hili kuzinduliwa na kugharimiwa ili liwepo!! jee jambo lenyewe ni lipi? mzanzibari umejiuliza? Zinduka !!

Hili jambo ni la gharama kubwa sana. na gharama hizi zimetokana na misaada kutoka kwa wafadhili wetu. Mfadhili hatoi misaada bure, ila nyuma ya misaada hii awe ana maslaha nayo. na ama atakusaidia au atakukopesha kwa gharama nafuu kwa maslaha yake zaidi. kwa bahati mbaya jambo hili limechukuliwa kwa wepesi mno. lakini kumbe lina uzito wake ambao haukupimwa kabla , ila tumeshitukia tuko ukingoni. pesa zimekwisha tumika, na si hashaa nyengine zimetumika vibaya na si kwa nia hii iliokusudiwa, na hwenda zimekwisha hazipo tena !! sasa ikiwa hazipo zimekwisha na jambo lenyewe lililokusudiwa halikukamilika na sisi tumefadhiliwa au kukopeshwa na sababu yenyewe ni hii ya kutekeleza katiba ipite na ikubaliwe ili wanufaike hao waliokusudiwa itakuwaje? ndio haya tunayoyashuhudia hivi sasa!!

Kura ya maoni bado, daftari halikukamilika, pesa zimekwisha tushatia matumboni kwetu au zitatusaidia kwa kampeni tusizimalize!! wapinzani wamesusia kupiga kura ya maoni,na huku tukidandia mashine za usajili kwa majirani zetu? sasa huu ni utamaduni wa aina gani tujiulize? Hili ni kama binaadamu kwenda kuazima msuwaki kwa jirani ili uweze kuja safisha meno yako!! jee hili linawezekana? pesa zilizokusudiwa kukamilisha jambo hili ziko wapi? haya ndio masuala ambayo wafadhili wetu ndio watakayokuja kutuuliza. jee tunalo jawabu lake? hatunaaaaaaaaa !!!

V99!!

Share: