Habari

Kumbukumbu ya MV Spice 9 September

Leo ni tarehe 9 September 2018. Tarehe na mwezi kama wa leo miaka saba nyuma, Zanzibar ilipatwa na janga kubwa la kuwapoteza maelfu ya raia wake waliokufa maji, kutokana na uzembe wa maofisa wa bandari na wamiliki wa meli.

Serikali haikujali, ili uamini kuwa serikali haikujali mwaka mmoja baada ya ajali ya Mv Spice Islander kuua maelfu ya wananchi wakiwemo watoto. Mv Skagit nayo ilikuja kuzama kwa uzembe. Misiba hii miwili yote ni misiba ya kitaifa, lakini taifa lenyewe liko wapi?

Sahau kuhusu Mv Fatihi ambayo ilizama bandarini nayo pia iliua ndugu zetu wachache. Basi Katika tukio kubwa kama la Mv spice vp serikali haina habari nalo? Ndipo muandishi Mohammed Khelef akasema “Taifa lisilo waomboleza wahanga wake haliwezi kuwakumbuka mashujaa wake.

Taifa lisijali wananchi wake haliwezi kuthamini machungu yao” Kiini cha puuzo hili ni nini? (kwa maoni yangu) ni kule serikali kukosa ridhaa za wananchi na kuyatwaa madaraka kwa kwa mtutu na damu za wananchi.

Ewe Mola wetu mtukufu tunakuomba uwasemehe, uwarehemu maiti wetu na ndugu zetu wengine waliokwisha kutangulia mbele ya haki.

Share: