Habari

KUZIDISHA DUA SIKU YA TAREHE 26/04/2012

Asslamau alaykum,

Nakuombeni ndugu zangu waislamu na wengine wote wenye kuitakia mema nchi ya Zanzibar itakapo fika siku ya tarehe 26/04/2012 kila mja na kunyoosha mikono juu kumuomba Allah atuhurumie na kutuondolea hili jinamizi la Muungano.

Huu sio muungano ni dhulma kwa masikini wananchi wa Zanzibar kwa kizazi cha leo na kitakacho fuata kesho na kesho kutwa.

Nakuombeni waja waislamu popote pale duniani wenye kupenda haki na heshima ya utu wa Zanzibar siku hii ya Tarehe 26/04/2012 kuomba dua ya aina yoyote ile unayoijua kwa Allah kuuondoa huu Muungano na vile vile kuwabadilisha nafsi zao wale wote wenye kuutetea huu muungano usiyokuwa na haki kwa pande 2 zinazojidai kuungano.

Allah tunakuomba, hakuna mwengine wa kumuomba, ni wewe mwenye kuomba na mwenye kupokea maombi yetu.

Allah ni wewe uliyotufikisha hapa tulipo leo tunakuomba kwa usiku na mchana utuondolee hii dhulma na utawala wa kikoloni wa Tanganyika kwa wananchi wa Zanzibar.

Allah ni wewe pekee uliojabari na hakimu na mpangaji wa usiku na mchana tunakuomba utuondolee huu ushirikina wa Muungano. Tunafahamu Allah wewe ni pekee mwenye mamlaka na maamuzi kwa kila binaadamu, Tunakuomba utumie mamlaka yako kuwashinda washirikina wa huu Muungano wa Tanganyika.

Allah wewe ndio mjuzi na mtaalamu, Allah wewe ndio mwenye kuwapa viburi na ujasiri wa utawala hawa madhalimu tunakuomba utuondoshee hii dhulma ya miaka 48 katika visiwa vya Zanzibar.

Allah tunakuomba utuzidishie nguvu na maarifa, utupe ujasiri wa kutetea haki za wanyonge wa Zanzibar.

Allah  tunakuomba kwa rehma na uwezo wako uwashinde wale wote wenye kutetea Muungano huu usiokuwa na heri kwa Zanzibar.

Allah tunakuomba uwashinde wale wote wenye kulinda maslahi yao binafsi ndani ya huu Muungano na wenye kupitisha dhulma za usiku na mchana kwa waja wako wananchi wa Zanzibar.

Allah tunakuomba uwashinde makafiri wenye kutumia hadaa, vitisho, na dhulma kwa kutumia jina la Muungano.

Allah wewe ndiye uliyemtia  Nabii Yussuf ndani ya tumbo la samaki na ni wewe uliyemuokoa Nabii Yussuf ndani ya tumbo la samaki na ni wewe utakaye waokoa Wazanzibar ndani ya tumbo la Muungano huu wa dhulma.

Allah ni wewe uliyemuokoa Nabii Ibrahim A.S katika moto na ukaufanya kuwa baridi na salama. Hakuna kilicho juu yako kinachoweza kutumia ufalme wako.

Wale wote wenye kusema kwamba Muungano ukivunjika Wazanzibar watapata shida, Hawa ni wanafiki na washirikina ambao wakuamini wewe Allah.

Hawa ndio katika kundi lile la Abu jahel, wanajidai ni waislamu kumbe wanafiki na Allah tuoneshe zaidi na zaidi hawa wanafiki.

Laana Tullwah kila mwenye kuutetea huu Muungano wa dhulma.

Share: