Habari

kwa hali kama hii kweli tutafika salama?

Hali ya kwetu zanzibar hivi sasa iko katika njia panda.na kuna haja ya kutafakari zaidi namna ya kuiokowa ili tuweze kufika salama bila ya umwagaji damu. tuna kila ya sababu ya kusema kuwa Zanzibar hakuna demokresia ya kweli. ni udanganyifu wa kisiasa tu, ambao unatudanganya.

Ikiwa kweli kuna demokresia, iweje kutokee kundi ambalo linatamka wazi mbele ya hadhara ya kuwa nchi hawaitoi kwa vikaratasi? wakati demokresia inatamka wazi kuwa kutakuwepo chaguzi ambazo zitaruhusu wale ambao watashinda kupitia chaguzi hizo kupewa haki ya kuongoza nchi? ingefaa tujiulize ikiwa katika siasa za haki na usawa kunaruhusiwa kutamkwa maneno ya aina hii, kweli kuna haja ya kutumia fedha za wananchi kutayarisha chaguzi ambazo zinazotakiwa kuwa huru na haki? na kuwepo watu wanaotamka maneno ya aina hii? na ikiwa ni kinyume chake, kuna haja gani ya kutayarisha chaguzi za aina hio na kuhatarisha maisha ya wananchi wasio na hatia yoyote kama hali yenyewe ndio kama hii? Ingekuwa kweli Zanzibar kuna demokresia, la kwanza ilikuwa ni kuwachukulia khatuwa kali watu ambao wanatamka maneno ya aina hii na kuwafikisha mahakamani ili sheria iwahukumu!! sasa matamko ya aina hii yamejenga ushindani hatarishi, kwani kuna na wale waliotamka ya kwamba wasipopewa ushindi wao ikiwa watashinda, basi watanganganuwa ushindi wao kwa nguvu !! kwa misimamo hii miwili inahakikisha ya kwamba pande hizi mbili zote zinajitayarisha vita visivyokuwa na haja!!

Pande hizi mbili killa mmoja anajitayarisha kivyake. na la ajabu zaidi yakuwa wale ambao wametamka kuwa hawatoi serikali kwa vikaratasi, ndio ambao wanapita kwa njia hio hio ya vikaratasi kwa kuwaandikisha katika daftari hilohilo la karatasi majina ya watu ambao kisheria hawana haki ya kupata vitambulisho vya Zan ID, na wala kupata haki ya kuandikishwa katika daftari halali ya wapiga kura, ili waje kutumia haki hio kwa vikaratasi hivyohivyo ambayo wanavikataa kuwa ndio njia ya kupatia ushindi katika njia ya demokresia inayotambulika na kukubalika kuwa ndio njia halali ya kuthibitisha ushindi kidimoresia!! sasa tunajiuliza, kuna haja gani ya kupoteza na kugharimu fedha zote hizi kutayarisha uchagzui huu ikiwa kuna washiriki wa uchaguzi huu waliokuwa si tayari kuukubali ushindi huu wa vikaratasi?

kwa mitazamo hii miwili kuna ishara ya kuhatarisha na kuitia Zanzibar katika hali ya hatari na isioridhisha!! ingefaa hali hii ingewahiwa mapema, kwa kutayarishwa kikao ambacho kitawakutanisha pande zote mbili hizi na kujaribu kuyatatuwa mamatizo yaliopo mapema, kabla ya mambo hayakufikia kuharibika zaidi na kuleta khasara na kuitia dowa Zanzibar!!

Bila ya shaka kuna ushahidi kamili ya wale ambao wamepandikizwa katika kushiriki uchaguzi huu wasio na haki nao!! wawekwe hadharani, mmoja baada ya mwengine, ili ijulikane wanaostaki na wasiostahiki haki hio ili wachukuliwe khatuwa za kisheria!! na wale ambao wananyimwa haki zao zitafutwe njia za kuwapatia haki zao kihalali, na killa upande uridhike yakuwa sasa waliokuwa na haki ya kupiga kura inaridhisha kwa pande zote mbili ili kuepusha majanga yanayotukabili yasitokee!! halafu ndipo tuendelee na huo uchaguzi ambao hatuna budi kuufikia na kuweza kupata uamuzi wa halali na wa kuridhisha pande zote mbili. kwani popote panapokuwa na ushindani wa aina yoyote ni lazima mmoja wapo ashinde, na alieshindwa akubali kuwa kashindwa na kuendelea na yajayo!! kinyume na haya tunachelea kusema kuwa huko tuelekeapo kwa hali hii si kuzuri na hakuna maslaha na Zanzibar na watu wake.

Inawezekana kuwa wako ambao kwa makusudi wanataka mambo haya yawe kama yalivyo, hwenda kukawa na maslaha nayo. lakini hatufukiri ya kuwa yatakuwa ni maslaha na Zanzibar na watu wake!!

jamani mti na machoooo!!! hili si la mzaha !! kuna roho za watu zitapotea, nani wa kulaumiwa? kweli tutafika salama ????????????????? Sidhani .

V99!!

Share: