Habari

Kwanini Lipumba hakubaliki Tabora sawa na Shein Mkanyageni

Elbattawi
Jumamosi, Juni 9, 2018

DK Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyeykiti wa Baraza la Mapinduzi, ni kwanini watu wengi wa kwao Mkanyageni, Pemba hawamkubali?. Dk Shein, anaelezwa kuwa ana asili ya Pemba.

Kadhalika, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa watu wengi wa Tabora, hawamkubali?.

Dk Shein, ni wapi alipokosea. Kwa tabia machoni anaonekana ni mpole, mtaratibu na muungwana. Ni kweli hiyo ndiyo hulka ya Dk Shein?. Maswali tunayo mengi kuliko majibu.

Inaelezwa kuwa aliwahi kugombea mara mbili mfululizo nafasi ya Ubunge/Uwakilishi jimbo la kwao la Mkanyageni, wananchi walimkataa.

Watu wengi wanahoji kuwa Dk Shein, kuna siku aliyowahi kushindana, akashinda?. Si ubunge wala si uwakilishi aliyoshinda kwao, iweje ashinde Urais wa Zanzibar nzima!.

Aidha, inaelezwa kuwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 baada ya ishara kujitokeza za kushindwa alifanya mbinu kurejea tena madarakani kwa hila za kufuta na kubuni uchaguzi wa marejeo.

Baya zaidi kwa kiongozi huyu, inadaiwa kuwa katika Ikulu ya Zanzibar, ametengeneza taasisi ambayo kazi yake ni kuhakikisha watu wenye asili ya Pemba, hawaajiriwi kazi serikalini.

Pia, kiongozi huyu akiwa ukingoni kumaliza muhula wa pili wa uongozi wake, imeelezwa ameshindwa kuwaunganisha Wazanzibari kuwa wamoja.

Kuhusu Profesa Lipumba;
Wanyamwezi, Wasukuma na Wamanyema ni moja katika makabila ya jamii ya Wazanzibari tangu dahari. Lipumba kuwa mnafiki kwa Wanyamwezi wa Zanzibar ni sawa kuwa mnafiki kwa Wanyamwezi wa kwao Tabaro.

Swali lilikuwa, ni kwanini watu wengi wa Tabora hawamkubali Lipumba?. (jibu) Binafsi, kwanza naona ni bora hata wasimtake (wasimkubali) ni aibu kuwa na mtu kama huyu…ni shida, mnafiki aliyebobea.

Watu wa Tabora, wanaogopa kusalitiwa kwa kuwa wao ndiyo wanaomfahamu vizuri zaidi kuliko mtu yeyote kwa kuwa ni mtoto wao. Tabia zake za usaliti wanazijuwa tangu akiwa mtoto kwa wazazi wake.

Kwa hakika watu wanamjuwa Lipumba kama Mnyamwezi wa Tabora, lakini hadi leo hii sijui ni kwanini Wanyamwezi wameshindwa kumuunga mkono ndugu yao. Nadhani, wanahofu kuwasaliti.

Profesa Lipumba ni msomi aliyekosa bahati na mapenzi kutoka kwao Tabora na ndani ya jamii nyingi za Tanzania. Hapana shaka kuwa Lipumba kapoteza dira, jahazi la kuaminika limeshaenda mrama.

Hatuwezi kumshangaa kumuona leo yupo na akina Dk Shein, Said Soud, Juma Ali na wenzao wengine kwenye visebule vya Ikulu ya Zanzibar, wakishikana mikono na fisadi/dhalimu wa Wazanzibari Dk Ali Mohamed Shein. Maalim Seif, alikataa kuguswa mkono wake na dhalim.

Musukuma (Joseph)
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma (CCM), alimsifu sana Lipumba kwa kuwa na hulka ya usaliti na alidai kuwa anafaya juhudi kubwa kuvifarakanisha CHADEMA na CUF, ili umoja wao (UKAWA), usambaratike.

Musukuma alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na EATV baada ya kuulizwa ni kiongozi gani wa upinzani anayemvutia.

“Mwanasiana wa upinzani anayenivutia ni Profesa Lipumba anajua namna ya hesabu za kuvuruga vyama nampenda sana,” alisema na kuongeza.

“Lipumba yeye na Sakaya ni mabingwa wa kutibua siasa wanajua kupiga hesabu za kuchekecha vyama, hata ikitokea kufarakana kwa CHADEMA na CUF zitakuwa ni juhudi za Lipumba,” alisema Musukuma.

Pamoja na hayo, Musukuma ameendelea kwa kusema “Lipumba nampenda kwa sababu ni mvurugaji wa hivi vyama vya upinzani, anaifanyia kazi nzuri sana CCM, yule ni ‘master’ wa kuvuruga”.

Kwa upande mwingine, Joseph Musukuma alisema katika maisha yake anatamani awe fundi wa hesabu za siasa za kuvuruga vyama kama alivyo Profesa Lipumba.

Watu wanaposema, wanapomfananisha Lipumba na msomi mjinga (mjinga aliyesoma) hawakosei. Kila dalili zipo kwamba Lipumba kapoteza dira jahazi limeshaenda mrama kama nahodha wa CUF na siasa za upinzani kwa jumla. Tayari amebugi.

Kwa hadhi ya kisiasa aliyokuwa nayo ndani na nje ya Tanzania, haikufikiriwa kuwapo kwa matukioa ya sasa yanayonasibishwa na usaliti wa Lipumba. Mwenyezi Mungu ‘AMUHIDI’.

Hebu tuwaangalia watu/viongozi wa upinzani akina Mbowe, Lema na Lowassa (CHADEMA), kila wanapogombania kwao wanakubalika kila uchaguzi. Tumwaangalie Zitto (ACT-Wazalendo) kwa Waha wa Kigoma.

Maalim Seif kwao Mtambwe na Pemba yote na Urais wa Zanzibar, kila uchaguzi anashinda. Lipumba, kwa Wanyamwezi hatujui tatizo nini?. Kadhalika, Dk Shein na watu wa Mkanyageni, hawamtaki kabisa, hawamkubali.

Habari mpya ilioko Zanzibar

Dk Ali Mohamed Shein amekutana na viongozi wa vyama vya siasa (venye mrengo wa CCM) kwa ajili ya kushauriana namna ya kuwapata wajumbe wawili watakaoteuliwa katika Tume mpya ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutoka vyama vya upinzani/CCM.

Dk Shein alikutana na viongozi hao Jumamosi, Juni 9, 2018 Ikulu ya Zanzibar, ambako viongozi wa vyama 17 vya siasa walihudhuria wakiwemo wenyeviti na viongozi wengine wa ngazi za juu wa vyama hivyo vya upinzani (upinzani bandia).

Hatua hiyo imekuja kwa ajili ya kutekeleza maelekezo ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 katika kifungu chake cha 119 (1)c, kuhusiana na kuwapata wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Mkutano huo unafanyika baada ya Tume ya uchaguzi chini ya Mwenyekiti Jecha Salim Jecha, kumaliza muda wake. Tume hiyo ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano kilichoanzia Aprili 30, 2013 mpaka Aprili 29, 2018.

Dk Shein alieleza kuwa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 katika kifungu chake cha 119 (1)c, kimeweza kutoa maelekezo mazuri ambayo ndio njia moja wapo iliyowakutanisha viongozi hao wa vyama vya siasa.

Dk Shein, tunaweza kumwita mkuu wa madili tayari amewaita viongozi wa upinzani bandia akina Lipumba, Hamad Rashid na Said Soud na wenzao ili kuweka mazingira mazuri kwa CCM kuendelea na dhuluma zake hapo 2020.

Said Soud, hivi karibuni ndani ya Baraza la Wawakilishi, alisikika akisema kuwa CCM Zanzibar, itashinda milele kwa sababu ndicho chama kinachopendwa Zanzibar.

Hivyo, ni mpinzani gani wa kweli anaweza kutoa kauli hiyo , ilhali anajuwa kuwa CCM Zanzibar, haipo, wala haijawahi kushinda uchaguzi wowote katika mazingira mazuri ya uchaguzi wa haki, wazi na huru?.

Share: