Habari

Laa Hamad HR limalize haraka ili tuendele na safari yetu ya ukombozi wa Znz.

M/mungu hamfishi mnafiki na siki ikifika basi hukuazirisha tu mbele ya jamii, huyu jamaa HR Alisha pangwa na wanafiki wenzake kumuhujumu Maalim Seif kisiasa ili lengo nikuwa Maalim ndio kiungo Muhimu ktk harakati za ugombozi wa Zanzibar.

Lipi lifanyike nikumtowa aduwi wake ndani ya mifupa yake na sisi kukaa pembeni kuangalia mchezo ushezavyo, ndio tukashuhudia mambo haya ya huyu Hamad kulete choko choko hizi katika wakati huu.

Alichopangwa Hamad kukifanya nikumuhujumu Maalim kisiasa yani kumyoyoa mbawa kwa kumpokonya maamlaka ya uongozi wa chama na kumfanya Maalim a hang katika umakamo wa rais wa muda.

Hili lilikuwa ndio draft alilopewa Hamad alisheze ili kumbomowa Maalim na kumyoyoa mbawa, wana ukumbi nilini uliomsikia Maalim Seif kusema nifikapo kipindi Fulani nita ya hand-over madaraka yangu ya ukatibu hata HR kuja na hili la kumlazimisha kuyatowa ili yeye awe mrisi?.

Kama ni hoja zake za kuwa Maalim ana kofia mbili , jee yeye anazo ngapi kama Maalim ana mbili yeye ana tatu? Ni kiongozi katika kambi ndogo ya upinzani katika Bunge na ni Mbunge wa Wawi na ni Mfanya biashara marufu mkubwa.

Na hata katika mambo ya kijamii yeye Hamad Rashi ana wake wawili moja ni Mpemba na Moja ni Mbara huko aliko, sasa yupi mwenye majukumu mengi waungwana? Maalim au yeye? Maana hata mke Maalim ni moja tu Bi Awena.

Naikiwa kwa mtezamo wa kuvaa kofia zaidi ya mbili basi takribani viongozi wote hata Raisi mwenyewe ni kofia tatu kwa kuendelea, ni Raisi wa Muungano,Mwenyekiti wa Chama ,Amiri Jeshi mkuu etc.

Sasa point yangu hapa ndugu zangu wa Zanzibar

Kwa wakati huu tulionao kuelekea hio katiba mpya kutajitokeza vitimbi kibao ambavyo kama Wazanzibar hatukuwa makini lemga na mazumuni nikuondoshwa katika harakati za kujikwamuwa na kupelekwa deraction nyengine, ndio likafokonyolewa hili la HR.

Sasa chaumuhimu huyu nikumpiga zaruba huyu HR na tukaendelea na safari yetu Wazanzibar sihivyo hili litapaliliwa na itakuwa ndio gumzo la kila siku, huyu jamaa lengo nikukiyumbisha chama baada ya kucha kuhujumiwa Maalim Seif kwa kupokonywa nguvu za chama na hapo ndipo Wzanzibar tutakapo ona chama kikiyumba na Maalim akipiga kelele pembeni huku yuko powerless.

Nyerere hakuwa njinga aliposema nangwatuko, kikubwa alicho kifanya niku ji-(up date) zaidi tuliona alivyo jifanya Taminetor? Alijipa uwenyekiti wa chama na kukifanya chama ndio super power chenye nguvu zaidi kuliko chochote na matokeo yake ndio tunayaonsa?.

Sasa na Maalim akija akikubali kutowa mpini basi Wzanzibar tusubiri mizozo na kuvurukiga kwa chama, hili ndio lengo la Hamadi alilopangiwa kulifanya, mimi naweza kusema nibora Maalim kuashia nguvu za Umakamo R 1 kuliko ukatibu wa Chama.

Ukatibu wa Chama ni nguvu na Harakati za Uzalendo wa sauti za Wanyonge sasa ikiwa mipango yake Hamad ingekuwa basi Maalim angekuwa muflisi katika chama ndio ukaona cuf hili wamelishtukizia na kusema haraka Hamad awajibichwi .

Sihivyo akipewa muda huyu na ndicho anacho kichokora hivi sasa apewe muda ili apangiwe mipango mengine na wajiri wake, Bara kakataa kuhojiwa kwa mbinde na sababu ni hizo hizo zakawaida kuwa yeye hana imani na viongozi katika kamati hio yakuhoji yamadili?.

Na Zanzibar hivi sasa sababu ni hio hio kuwa hana imani na kiongozi mkuu(Maalim Seif) katika kikao hichi cha Zanzibar eti anasema kwa kukamata barua kuwa atolewe ilioandikwa na Maalim, sasa kama viongozi wote wa ngazi za juu huna imani nao basi jikate kiungwana unasubiri nini?.

Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote.

Share: