HabariMatangazo

Latest news : Press Conference kesho in shaaAllah live saa 4 asubuhi

Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma ya The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi)

Inawatangazia wazanzibari wote kuwa kesho, jumatatu tarehe 04/04/2016 kitafanya Press Conference (Mkutano na waandishi wa Habari) kutangaza Azimio la Baraza Kuu la Uongozi la CUF kwa lengo la kutoa msimamo na mwelekeo wa Chama katika harakati za kuendeleza vuguvugu LA kudai haki ya wazanzibari kutokana na maamuzi waliyoyafanya tarehe 25/10/2015.

Mkutano huo utakaojumuisha viongozi wote wa kitaifa utarushwa live na kituo cha radio cha 102.9 SWAHIBA FM kuanzia saa nne kamili asubuhi.

Unaweza Kusikiliza Matangazo ya Redio moja kwa moja kwa kubonyeza hapa na bonyeza Swahiba FM

Share: