Habari

LIPUMBA AISHIWA PUMZI MAHAKAMANI;

TAARIFA KUTOKA MAHAKAMA KUU-
DAR ES SALAAM:

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)

TAREHE 7 SEPTEMBER, 2018

LIPUMBA AISHIWA PUMZI MAHAKAMANI;

 Wakili wake Mashaka Ngole akacha kufika mahakamani kama mbinu ya kuchelewesha maamuzi ya mahakama kwa hofu ya kupata kipigo cha kisheria.

 Asingizia kuwa mgonjwa, mahakama yataka kujua hospitali alikolazwa na kuamuru awe amepatikana ifikapo saa 8.00 mchana. Yagundulika kuwa amejificha Arusha na kuzima siku yake ya mkononi.

 Mahakama yatupilia mbali mapingamizi yake.

SHAURI KUHUSU WABUNGE VITI MAALUMU KUAMULIWA TAREHE 5 OKTOBA, 2018

TAARIFA KWA UMMA

Alkhamis Tarehe 6/8/2018 yaliitwa mashauri matatu yafuatayo;
1) Shauri Na. 248/2018 (Joran Bashange/Nassoro Mazrui dhidi ya Lipumba na wenzake 15)
2) Shauri Na. 84/2018 (Joran Bashange/Nassoro Mazrui dhidi ya Lipumba na wenzake 15)
3) Shauri la Wabunge wa CUF (Abdallah Mtolea na wenzake 19 dhidi ya Lipumba na wenzake)

Mashauri Na.248/2018 na Na. 84/2018 yaliitwa mbele ya Mheshimiwa Jaji Magoiga wakati shauri la Wabunge 19 liliitwa mbele ya Mheshimiwa Jaji Arufani.

1) Shauri Na.248/2018 ni shauri dogo linalotokana na shauri la msingi Na. 84/2018 (linaloomba zuio la kuitishwa Mkutano Mkuu wa Taifa feki wa Lipumba) shauri hili lilikuja kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali za pingamizi (Points of Preliminary Objection) zilizowasilishwa na Mashaka Ngole (mshitakiwa Na. 2) akipinga kusikilizwa kwa shauri hilo na kuiomba mahakama ilitupilie mbali. Amri ya kusikilizwa hoja za awali ilitolewa na mahakama tarehe 27/8/2018 kufuatia ombi la Mashaka Ngole mwenyewe. Katika hali ya kushangaza Mashaka Ngole hakufika mahakamani akituma taarifa ya kuuguliwa. Mahakama iliamuru apigiwe simu kutaka kufahamu lini anaweza kupatikana ili kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza hoja zake za awali, lakini simu yake ilikuwa imezimwa. Mahakama imepanga kusikilza hoja za awali tarehe 3/10/2018.

2) Shauri Na. 84/2018 litaitwa tena kwa kutajwa tarehe 3/10/2018.

3) Shauri la Wabunge wa majimbo 19 la mwaka 2017 linahusu ombi la kupata kibali (leave) kuomba marejeo Mahakama ya Rufaa kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu katika shauri Na.21/2017 la wabunge wa majimbo 19. Hoja za awali zilizokuwa zimewasilishwa na Mashaka Ngole ZIMETUPILIWA MBALI kutokana na Mashaka Ngole kuikimbia kesi kwa kutofika mahakamani bila sababu za msingi kwa mara kadhaa.

Uamuzi huo ulitolewa na mahakama baada ya jitihada zote za kumpata kushindikana hata baada ya kuhairisha shauri mpaka saa 8.00 mchana. Katika hali ya kustaajabisha, wakati katika shauri Na. 248/2018 ilitolewa taarifa kuwa amesafiri kwenda Arusha kwa matatizo ya kifamilia, hapa mtoa taarifa alisema Mashaka Ngole ni mgonjwa tangu mwezi Julai, 2018 na alikuwa amelazwa. Mahakama ilipotaka kufahamu anatibiwa hospitali gani ndipo, mtoa taarifa alipobabaika hali ilyodhihirisha kuwa hakuwa anatoa taarifa sahihi mbele ya Mahakama.

Washitakiwa katika mashauri Na. 248/2018 na Na. 84/2018 ni hawa wafuatao;

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Mashaka Ngole (Mwenyekiti Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Mungiki kinyume na Katiba ya CUF Ibara ya 92(1)(c), Magdalena Sakaya, Abdul Juma Kambaya, Jafari Mneke, Thomas D.C.Malima, Omar Muhina Masoud, Salma Masoud, Haroub Mohamed Shamsi, Khalifa Suleiman Khalifa, Mohamed Habib Mnyaa, Nassoro Seif Amour, Thiney Juma Mohamed, Rukia Kassim Ahmed, Kapasha H. Kapasha, Na Maftaha Nachuma.

Hoja za awali za mashaka Ngole kupinga shauri Na. 248/2018
a) Shauri Na. 248/2018 lisisikilizwe kwa kuwa linapingana na kifungu Na. 21 cha sheria ya vyama vya siasa sura 258 ikisomwa kwa pamoja na ibara ya 98(4) ya Katiba ya CUF-Chama cha Wananchi.

b) Shauri Na. 248/2018 lisisikilizwe kwa kutomuunganisha mdaawa mahsusi.

c) Waleta maombi hawana mamlaka (locus stand) kuleta shauri Na. 248/2018 mahakamani dhidi ya wajibu maombi.

Ratiba ya mashauri mengine italetwa kwa kadri Majaji watakapokuwa wakipangwa.

HAKI SAWA KWA WOTE

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI
maharagande@gmail.com
+255 715 062 577 / +255 767 062 577

Share: