Habari

LIPUMBA AMSHAURI KIKWETE KUUNDA SEREKALI YA UMOJA WAKITAIFA.

DAR-ES-SALAAM.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WANANCHI CUF, PROFESA IBRAHIM HARUNA LIPUMBA AMEMSHAURI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA MRISHO KIKWETE KUCHUKUA MAAMUZI YA BUSARA YA KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA HIVI SASA,KAMA ILIVYO ZANZIBAR ILI KULINUSURU TAIFA. PROFESA LIPUMBA AMETOA USHAURI HUO LEO WAKATI AKIFUNGUA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA KUU LA UONGOZI LA CUF, UNAOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MAKAO MAKUU YA CHAMA HICHO BUGURUNI MJINI DAR ES SALAAM.

AMESEMA KUWA KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA KUTALETA MARIDHIANO NA KUIEPUSHA NCHI NA MADHARA MAKUBWA YANAYOWEZA KUJITOKEZA KUTOKANA NA HALI ILIYOPO SASA.

KIONGOZI HUYO WA CUF AMETOA RAI HIYO KUFUATIA SEREKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUKUMBWA NA MSUKOSUKO MKUBWA WA KIUONGOZI .

AMESEMA KUWA MSUKOSUKO HUO UNAONEKANA WAZI KUFUATIA TAARIFA YA RIPOTI YA KAMATI YA BUNGE YA MALIASILI, ARDHI NA MAZINGIRA, HALI YA KUKOSEKANA KWA UWAZI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA NA HATMA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015, PAMOJA NA MALALAMIKO NDANI YA CCM KWAMBA KUNA MAWAZIRI WENGI NDANI YA SERIKALI NI MZIGO.

MWENYEKITI HUYO WA CUF AMEBAINISHA KUWA HALI ILIYOPO INAONESHA KUWA SERIKALI YA CCM INAYOONGOZWA NA RAIS KIKWETE HIVI SASA IMEKOSA KUSIMAMIA UADILIFU NA UTAWALA BORA NA KWAMBA NI VIGUMU KUWEZA KUSIMAMIA HAKI NA UTAWALA BORA KWA WANANCHI WAKE. AMESEMA RIPOTI YA KAMATI YA BUNGE YA MALIASILI, ARDHI NA MAZINGIRA ILIYOTOLEWA JUZI BUNGENI NA KUSABABISHA MAWAZIRI WANNE KUPOTEZA NYADHIFA ZAO, INATHBITISHA KUWA HALI SI SHWARI NA KWAMBA NCHI IMEKUMBWA NA UVUNJIFU MKUBWA WA HAKI ZA BINAADAMU NA KUKOSEKANA UTAWALA BORA.

AMESEMA WATU WALIOKWENDA KUTOKOMEZA UJANGILI, BADALA YAKE WAMEKUWA WAVUNJAJI WAKUU WA HAKI ZA BINAADAMU KWA KUTESA WATU WASIOKUWA NA HATIA NA KUSABABISHA BAADHI YA WATU KUPOTEZA MAISHA NA MALI NYINGI ZA WANANCHI IKIWEMO WAFUGAJI KUPOTEA.

 

AKIZUNGUMZIA MCHAKATO WA KATIBA NA HATMA YA UCHAGUZI MKUU UJAO, AMESEMA, WAKATI INAONESHA WAZI KATIBA MPYA HAITAWEZA KUPATIKANA KATIKA MUDA ULIOPANGWA AWALI IFIKAPO MWEZI APRIL MWAKANI, BADO WANANCHI HAWAELEWI UTARATIBU UTAKAOTUMIKA KUWAWEZESHA KUPIGA KURA YA MAONI NA KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2015. AMESEMA TANGU MWAKA 2010 ULIPOFANYIKA UCHAGUZI MKUU DAFTARI LA WAPIGA KURA HALIJAFANYIWA MAPITIO, WAKATI UTAFITI UNAONESHA KATIKA KIPINDI HICHO HADI SASA KUNA WATANZANIA WAPATAO MILIONI NNE WATAKUWA WAMETIMIZA MIAKA 18 NA KUWA NA HAKI YA KUPIGA KURA.

Share: