Habari

MA-CCM Na Utawala Wa Kubebana

Naibu Speaka wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Tulia

Naibu Speaka wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Tulia

Assalamu alaikhum Warahmatullah wabarakatuhu Ndugu wazanzibari wenzangu Mulioko Ndani na Nje ya Visiwa Vyetu Adhimu. ama mimi sina budi ila kumshukuru Allah kwa Mtihani wa Uchaguzi Aliotupa na Shida ya Maisha ilioanza kuwakamata Wananchi Wa Zanzibar. Hii Yote nikwasababu Ya Utawala Tuliobnao Wa CCM kuwatia Adabu Wananchi wa Zanzibar kwasababu Tu Wametumia Haki Yao Ya Kidemocrasia. Ili Wabadilishe Mfumo wa Utawala kutoka wa CCM Kwenda Wa CUF.

Bila yakupoteza Muda na kuwakera Wasomaji ni Bora niandike haya niliokusudia katika kichwa cha Habari. Makala hii inaweza ikatuvuta nyuma kidogo ili tuweze kukumbuka historia ya CCm. Katika Campeni zetu za Uchaguzi zilizopita ni Viongozi Wachache wa UKAWA au Upinzani Wameweza Kuwaeleza Wazanzibari Au Watanganyika juu ya Mfumo wa Utawala huu Wa CCM ulivojengeka na Nani aliekuwamo na nani aliekuwa hayumo ndani ya Chama hichi.

Nikisema hivo ninakusudia kwamba CCM kwa muda wote Uliotutawala kwa Mabavu na Ghilba yauibaji wa Kura Imekuwa ikiota Mizizi Mirefu na Kujijenga katika Utawala wa KITABAKA. Katika Ndani ya Chama hichi moja ya IDEA zao ukiacha zile Idealogy za MABAVU, FITNA, UBAGUZI wa Dini, Asili na Rushwa basi kuna hii ya Kujijengea Uzio wa Utawala Wa MATABAKA. Yaani Anaanza baba kuwa kiongozi akeshaingia tu ndani ya System ya Uongozi wa CCM hapo kiongozi Huya atavuta kila aliekuwa karibu naye kutoka kwenye Family na kujizungushia Uzio wa Tabaka la Uongozi.

1. Tabaka la Watawala: Hili nitabaka Ambalo Ndani yake Kuna Viongozi waliokamata au wanaoshikilia Nafasi Nzito ( Nyeti). Lakini hawataki Kumuona Mtoto wa Kimasikini yaani Mtanzania wa Kawaida anakamata nafasi Nyeti. Hivo Watawala hawa Wa CCM huchukua Watoto Wao, Ndugu zao, Marafiki wao wa karibu sana na Hata Mahawara Wao huingizwa katika JOPO la Uongozi sio kwa Sifa utendaji Bora wa kazi zao au Kielimu; bali Ni KUBEBANA ili wapate wajilinde na makosa au Uharamia wanaoufanya kwa Wananchi. Mfumo Huu umekuwa ukitayarishwa Makusudi Ili Nchi ya Tanganyika na Zanzibar Iendelee Kutawaaliwa na CCM. Akitoka BABA akamate MTOTO, MJUKUU, Kitukuu na hata Mahawara wao.

Mifano ni hii:

MA-KUFULI tokea amepata Uraisi badala ya kumchagua Waziri Mkuu ambae hafungamani na uhusiano wake au Wa RaISI ALIEPITA; badala yake amekwenda kumchagua MAJAALIWA ambae ni Rafiki yake wa karibu. Spika Wa Bunge Jobu Ndugai na yeye Amemchaguwa HAWARA Wake ili TULIA awe naibu Spika. Waziri Mkuu MAJAALIWA katika Utawala wa Kikwete yeye ( Nafikiri) alikuwa Naibu Waziri ndani ya Serikali ya Jakaya Kikwete. Hebu tujiulize Masuali ni Kwanini Majaliwa alibebwa na Jakaya Kikwete?

Kwasababu Mkewe Jakaya Kikwete, Salma Kikwete na Mkewe Majaaliwa kama sio Ndugu basi ni Marafiki wa Karibu na Picha zao zipo wakati wakiwa Wasichana huko Kwao Mkoa wa LINDI. Ukiingia Katika JOPO la Waliokuwa MaRaisi. Mzee Ruksa (Mwinyi) ana watoto Wake wanafanyakazi BOT na Mmoja alikuwa anataka kupenyezwa kuwa Spika wa Bunge kwasababu Uluwa wa Mtoto wa Mwinyi katika nafasi ile alionayo sasa ya East Africa, unamalizika karibuni. Hivo hapa palikuwa na mpango madhubuti wakutaka mtoto wa Mwinyi Mwinyi apatiwe FUPA jengine la Kungongona – NA kuMtayarisha kuja kugombea Ubunge au Uraisi hapo baadae.

Viongozi Wengine Ni Joseph Sinde Warioba ana mtoto wake Ni Mbunge wa CCm kama hakuangushwa. Samuel Sitta, Jakaya Kikwete ana watoto BOT na mmoja Riziwani ni Mbunge, na yeye anatayarishwa kuja kugombea nafasi za Uraisi huko Mbeleni. jOHN POMBE ANA MTOTO WAKE KATIKA OFISI ZA MAMBO YA NDANI, na viongozi wengi Wengine Kutoka Unguja na Bara wanachukuwa watoto wao na kuwaweka katika Nafasi Nyeti za Uongozi.. Kama mtu hataki kuniamini na atembelee TRA, BOT, ZRB, Wizara ya Fedha Zanzibar, Baraza la Wawakilishi aone kwamba humu hamuna watoto wa Magwigwi ya CCM.
Utawala wa Kubebana huwa hauna uwajibikaji Mzuri katika Utendaji wa kazi, siohivo tu pia unakuwa na upendeleaji mkubwa wa nafasi za masomo au mikopo. Humu. Kwasababu Watu wenye urafiki, Udugu au Wapenzi hamuwezi kuiongoza Nchi au Kuwaongoza Wananchi kwa Insafu Njema na mukafuata Sheria za Nchi bila ya Upendeleo

..Na hii Ndio iliopelekea Kwa Uongozi Huu wa CCM, licha yakuwa na Fedha nyingi sana ambazo huchotwa na Wakubwa. Lakini maendeleo ya Wananchi hasa wa Vijijini huzorota. Hawa Wananchi wa Vijijini ambao Wengi Wao Wanaona CCM ndio Mungu Wao huwa wanaishi maisha duni zaidi kuliko Wananchio wengine. Kutokana na Mfumo Huu wa TABAKA Tawala na Tabaka Tawaliwa, CCM huendelea kutudanganya na Kuwadhulumu Wananchi haki Zao za Msingi kama vile Huduma za Jamii. Ushahidi wa Kila Kiongozi ndani Ya CCM kulinda Maovu yake ni ule Ulaji Mkubwa wa Targeter Ecrow, Richmond, Misaada inayotoka Mellenium Challenge n.k. Hivo hata mtu akifanya Makosa hawezi kushitakiwa wala kufunguliwa kesi kwasababu huwezi kwenda step moja au mbili usimkute kiongozi huyo amejijengea Uzio wa Tabaka Tawala.

2. Tabaka la Malofa, Mabwege, Wapuuzi na Waongo kama tunavoitwa na Watawala Wetu. Tabaka ila ni tabaka linalotawaliwa kwa Hiari katika Upande wa Tanganyika na Kule Zanzibar Tabaka hili Wanatawaliwa kwa Nguvu za Dola, Fitna za Uunguja na U-Upemba, U-Hizbu na U-Afro. Tabaka hili limejazwa Sumu Za Ujinga kwa raia Huku Viongozi Wa CCM Wakiendelea Kututawala Wao na Familia Zao na kujizungushia Uzio wa Hariri za Marafiki zao au Marafiki za Wake Zao.

Kwanini nimeandika makala hii kwasababu nataka Niwajuilishe Watanzania Au Watanganyika na Wazanzibari kwamba Wakati umefika wakuchambua kwa kina utawala huu na Kuweza Ku-Ukataa kwa Nguvu zetu Zote. Kila tunapoendelea kuwakubali CCM Watujengee Utawala wa Kitabaka Chance ya Wananchi Kujitawala wenyewe na Kuepukana na Umasikini Itakuwa ina didimia kila siku zikienda mbele.

Share: